Mashabiki Wamshambulia Irene Kisa Ugonjwa wa Dogo Janja

Mwanadada Irene uwoya amejikuta katika wakati mgumu baada ya mashabiki zake na mashabiki wa mume wake Dogo janja kumshambulia kwa maneno katika ukurasa wake wa instagram kutokana na kuumwa kwa Dogo janja.

Dogo Janja ambae alionekana akiwa hospitali wikiend hii  lakini inavyosemekana ni kwamba mwanadada huyo hakuwa anaonekana maeneo ya hospitali huku akipost picha yuko sehemu nyingine kabisa ikionekana ni sehemu ya starehe.

Hata hivyo wawili hao wameonekana kuwa hawako karibu sana kama zamani, lakini kila mmoja anapooulizwa kuhusu mahusiano yao wamekuwa wakisema kuwa kila mtu ana ratiba na kazi zake hivyo hawawezi kuharibiana ratiba.

Dogo Janja ambae anasemekana kusumbuliwa na matatizo ya kupumua  kwa shida na pia kupungukiwa na maji anasema kuwa hakuna watu wanaojua zaidi ya ndugu zake huku akisherekea sikukuu yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini hapo.

mpaka sasa hakuna mtu anaejua zaidi ya watu wangu wa karibu tu, lakini pia naomba mashabiki zangu waniombee tu niwahi kupata nafuu na kutoka humu maana wala sitamani kukaa humu.

Hata baada ya kuweka post yake akiwa anaumwa watu mbalimbali wameenda katika ukurasa wa Irene uwoya na kumsema kuwa hamjali kabisa mume wake ambae yuko hospitali ana kazi ya kufanya mambo mengine tu Binafsi.

Dogo Janja Ajibu Tetesi za Kuachana na Mkewe

Msanii wa bongo fleva Dogo Janja amefunguka na kuwajibu mashabiki walikuwa wanasambaza na kutukana katika mitandao kuhusu mahusiano yake a kindoa na mkewe Irene uwoya.

Wiki iliyopia mwanadada Irene alionekana katiak safari na rafiki yake mwingine wa kiume tofauti na mumewe Dogo janja huku wawili hao wakionekana kula raha huko Dubai na kusababisha watu kuanza kuhoji na wengine kusema kuwa mwanadada huyo ameachana na Dogo janja na ndio maana hawajaenda wote Dubai lakini pia ameamua kwenda na mwanaume wingine.

Dogo janja alitafutwa na Team ya XXL na kuuulizwa kuhusu swala la kuachana kwao kama ni kweli na Dogo janja aliwajibu “hatujaachana lakini na isis tumeamua kuweka mambo yeu wazi, na ndio maana unakuta hakuna picha  nyingi tunazopiga pamoja siku hizi”

Baada ya hapo waliamua kumtafuta Irene ili kuthibitisha kauli ya mume wake nae pia aliwajibu kwa kusema “nimerudi juzi na sijaenda na dogo janja kwa sababu na yeye ana ratiba zake, na sioni haja ya kuongozana ane kila sehemu wakati kila mtu ana ratibza zake.Watu wafanya mambo yao na waache kufuatilia mambo ya watu”

 

 

Alichoandika Dogo Janja Kwenye Picha ya Uwoya Iliyoleta Utata Mtandaoni

Baada ya picha za Uwoya kusambaa katika mitandao ya kijamii na kusababisha watu kuongea sana juu ya picha hizo huku wengine wakisema kuwa mwanadada huyo na mke wa mtu na mwezi wa Ramadhani umeisha hivi karibuni hivyo hakupaswa kuweka picha hizo katika mitandao ya kijamii  mume wake na msanii huyo hajaonyesha ku-mind chochote kuhusu swala hilo zaidi ya kuendelea kumpa kichwa ju ya picha hizo.

Katika picha hiyo aliyoweka irene katika ukurasa wake wa instagram na kulalamika kwanini watu wamekuwa wakimsema kila anapoweka picha katika ukurasa wake Dogo Janja nae alionngezea upande wa maoni na kusema ‘usicheze karibu hii midoli kwa sababu hii  midoli hawang’ti”

Picha hizo za uwoya alizopiga akiwa ufukweni zilisambaa katika mitandao ya kijamii huku baaadhi ya wasanii wenzake kama mwijaku akisema kuwa swala hili linamfanya irene kupoteza kabisa heshima yake.

Dogo Janja Akubali Kumuita Mtoto wa Uwoya Mdogo Wake

Msanii wa muziki bongo Dogo Janja ambae mwaka jana alifunga ndoa na mwanadada Irene Uwoya na watu wamekuwa wakimsema sana tangu wao kuwa katika mahusiano kutokakna na ukweli kwamba wawili hawa hawalingani kiumri na kwamba watu wamekuwa wakimlinganisha Dogo Janja na Irene kama mtu na mtoto wake.

Katika siku ya kuzaliwa ya mtoto wa uoya wa kiume anaejulikana kwa jina la Krish, Dogo Janja aliamua kuwaridhisha walimwengu baada ya kumuita Krish kuwa ni mdogo wake na kwamba irene uwoya ni mama yao na kumshauri mdogo wake huyo kuwa msikivu kwa mama yao na kwamba anamshauri kutulia na kumheshimu mama yao.

katika ukurasa wake wa instagram, Dogo Janja aliandika” happy birthday mdogo wangu Krish , mungu akupe maisha marefu sana.mama anatupenda  watoto wake wote tusimuangushe.

Posti hiyo ilizua maswali na maneno engi katika kursa za instagram lakini wawili hao wamekwa wakionekana kuwa na mapenzi yaliyoshibaban kuliko hata vile ambavyo watu wengi walikuwa wakisema kuwa ndoa hiyo haitachukua muda mrefu kwa sababu wawili hao wamependana kwa kimaslahi na sio mapenzi.

 

Agness Alinifanya Nikutane na Dogo Janja:-Irene Uwoya

Mwanadada Irene Uwoya wikiendi iliyopita alifunguka na kusema kuwa kama isingekuwa rafiki yake Agness Masogange ambae kwa sasa ni marehemu basi asingeweza kukutana na Dogo Janja ambae kwa sasa hivi ndio mume wake wa ndoa.

Akiongea na Clouds e , katika sherehe ya ufunguzi wa sehemu ya kuoshea magari iliyofunguliwa na Perfect Chrispin , irene uwoya alisema kuwa mume aliekuwa nae sasa ni agness ndio aliemuunganisha nae na mara nyingi alikuwa akimuongelea sana na ndipo hata yeye aliapoanza kuwa karibu na Dogo Janja.

Irene uwoya na marehemu agness masogange walikuwa marafiki sana  kwa muda mrefu na hata msiba wa mwanadada agness irene alionekana kuumizwa sana na kutokwa na rafiki yake huyo na kuamua kuchora tatoo katika mwili  wake kama kumbukumbu ya kumuweka rafii yake huyo moyoni.

Irene na Dogo Janja walifunga ndoa mwaka jana mwezi wa na ndoa ambayo ilizua mgongano mkubwa sana wa mawazo baina ya watu lakini wao tayari walikuwa wameshaamua kufanya hivyo.

Penzi la Uwoya na Janjaro Linavyowakosha Watu Mtandaoni.

Penzi la mwanadada Irene Uwoya na  Dogo Janja limezidi kuwa chachu katika mitandao ya kijamii baada ya wawili hao  kuwa wanawarusha watu roho kwa kuwaonyesha kile wanachokuwa wanakifanya katika maisha yao ya ndoa.

Katika ukurasa wake wa instagram, dogo janja aliwekanpicha ya mkewe irene uwoya na kuandika “tunza cha ndani, hawara hana shukrani #abdulfamily

katika uwanja wa comments irene uwoay akajiu kwa bashasha kuhusu maneno ,achache ya mumewe na kuandika”nakupenda sana sijawahi kukutana na mwanaume ana akili kamaa wewe na muelewa kama wewe…mdogo lakini mmmhh achaa tu mimi ndo najua ..ndo maana wakiongeana na mimi huwa nawanagalia tu nasema iiiii@ dogojanjatz”

Wiki iliyopita Irene aliwaonyesha mashabiki kuwa ametoka kuchora tatoo yenye jina la abdul ambalo ni jina la mume wake Dogo Janja na hivi karibuni amekuwa akionekana akiwa amevaa necklace yenye herufi A kumaanisha Abdul.

Madee Afunguka Usiri Wa Ndoa ya Dogo Janja.

Msanii mkubwa na maarufu bongo ambae amekuwa ni kama baba mlezi wa msanii Dogo Janja,Madeee amefunguka na kusema kuwa waliamua kufanya usiri aktika ndoa hiyo kwa sababu waliona kuwa endapo wangewashirikisha watu wengi inewezekana hata ndoa iyo isingefungwa kabisa kutokana na maneno ya watu.

Madee alisema kuwa alikuwa anajua kuwa wawili hao ni maarufu hivyo endapo wangetangaza ndoa hiyo ingeleta utata mkubwa na hata kuharibu kabisa mipango ya ndoa hiyo.

Nilijua ni habari kubwa, ni habari ambayo ingeleta purukushani kwa wanahabari hata ndoa yenyewe isingefanyika, na hata wale ambao tumewaalika tulijua hawa wana marafiki zao ambao ni wana habari, hivyo tulichokifanya ni kutengeneza usiri wa ile shughuli, hata tuliowaalika tuliwaambia mnakuja hapa lakini simu zenu wekeni hapa, unangia unashuhudia tukio lakini hauna ushahidi wa kupeleka kwa wengine”, amesema Madee

Madee anasema kuwa waliona hata haina haja ya kuwaalika watu wengi kwa sababu  inawezekana kila mtu angekuja na neno lake la kuwashauri na kutia doa ndoa hiyo.

Tungesema tuanze kuwaalika watu wangeanza kuwashauri ,ooh usikubali kuolewa na huyo au   kuoa huyo  ile ndoa ingekufa na tungepata dhambi.