“Sijawahi Kuchanwa na Viwembe Kisa Mume Wa Mtu

Mrembo anayetikisa Mitandao ya kijamii kwa umbo lake matata Jane Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kudhihirisha kuwa hajawahi kuchanwa na viwembe kisa kuiba mume wa mtu.

Siku za nyuma kuna stori zilisambaa kwamba Sanchi aliwahi kuchanwa chanwa na viwembe Baada ya kukamatwa na mume taarifa ambazo Sanchi amethibitisha kuwa ni uongo Baada ya kuanika mwili Wake hadharani ukiwa hauna makovu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Sanchi alisema tangu azushiwe kuwa alichanwa na viwembe baada ya kufumaniwa na mume wa mtu hivi karibuni, hajawahi kuwadhihirishia watu kuwa hana kovu hata moja kwenye mwili wake bali watu walikuwa wakijifurahisha kwa kuongea.

Wale wote waliokuwa wakidai nimechanwa mwili, sitamaniki, basi waangalie halafu wakiona kama nina kovu lolote, waniambie maana watu wanaweza kukuzushia kitu bila sababu“.

Siku mbili hizi Sanchi ameonekana akiwa anajiachia na mavazi ya kuogelea katika visiwa vya Zanzibar alipoenda na Mpenzi Wake kujiachia.

Mimi na Poshi ni Kama Mafuta na Maji:-Sanchi

Mwanadada Jane Lyimo amefunguka na kusema kuwa  mwanadada anaetamba sana katika mitandao ya kijamii kwa sasa anaejulikana kama poshi wala hamtii jamba jamba kwa sababu haweiz kujilinganisha nae hata kidogo.

Sanchi ambae amekuwa akitamba kwa muda mrefu kutokana na kupiga picha za kujiachia lakini pia mwenye umbo zuri la kuvutia watu katika  mitandao ya kijamii,

Sanchi anasema kuwa pamoja na kwamba kuna watu wamekuwa wakianza kumfananisha na mwanadada huyo kwa umbo na baadhi ya vitu lakini ukweli ni kwamba watu hao wamekuwa wakijidanganya kwa sababu wamekuwa watu tofauti sana.

Sanchi anasema kuwa pamoja na yote ukweli ni kwamba yeye na poshi ni kama maji ya mafuta huweiz kuwafananisha hata kidogo.

Sanchi Afungukia Biashara Ya Mbwa Inayomuweka Mjini

Mwanamitindo maarufu kwenye mitandao ya kijamii anayezidi kutesa na umbo lake matata Janey Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kuweka wazi Jinsi biashara yake ya kuisaliti mbwa inavyomuweka mjini.

Sanchi amedai kuwa anashukuru anamaliza mwaka akiwa anaendelea na maisha yake vizuri huku madili yake ya biashara ya mbwa aina ya bull yakiendelea kumfanya atanue kinoma mjini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Sanchi alisema kuwa watu wengi wamekuwa hawamuelewi anapokuwa akipiga picha na mbwa, lakini ni kwa vile hawajui mbwa hao wanampa madili kwa kiasi gani.

Maisha yangu yanaenda kama kawaida kwa ajili tu ya hao mbwa wanaowaona kwenye ukurasa wangu wa Instagram. Mimi ni balozi wa biashara hiyo hivyo riziki yangu ya kila siku inapitia hapo”.

 

Sanchi Aanika Siri Nyuma Ya Msambwanda Wake

Mrembo anayekimbuza hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii Jane Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kuweka wazi Siri ya kuwa na shepu Kama yake.

Kwenye interview yake na Gazeti la Risasi Jumamosi, Sanchi alisema kuwa, madafu yana mchango mkubwa sana kwenye shepu yake kwani hupendelea kunywa maji yake badala ya maji ya kawaida au kimiminika kingine.

Mimi nitawapa siri yangu leo, madafu ndio kila kitu kwangu na hii tangu niko mdogo. Mama alikuwa akipenda sana kunywa maji ya madafu, nikawa namuuliza kwanini.

Lakini pia Sanchi anaweka wazi kuwa maji ya madafu yanafanya tumbo kuwa na mfumo mzuri kwa sababu yanasafisha kila kitu, hadi mkojo unakuwa safi.

Kuanzia wakati huo kila nikisikia kiu, labda dafu lisiwepo lakini likiwa lipo karibu maji yake ndiyo ya kuniondolea kiu, najua pia yananifanya nionekane mrembo zaidi”.

Sanchi amefunguka hayo Baada ya Kuwepo kwa tetesi kuwa umbo hilo matata alilokuwa nalo huenda likawa ni fekero jambo ambalo amelikana na kuweka wazi kuwa mama yake mzazi amejaaliwa msambwanda Kama Wake.

Sanchi Adai Anapiga Picha Za Uchi Ili Kutafuta Pesa Sio Wanaume

Mrembo anayekamata headlines kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili umbo lake matata Janey Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kutoa sababu za kupiga picha za utupu.

Sanchi amedai kwamba  watu wengi wanaoweza kumfikiria kwamba anapiga picha utupu ili apate Wanaume  lakini sio kweli yeye anapiga picha sole kwa ajili ya kujipatia pesa.

Katika mahojiano aliyofanya na Amani, Sanchi alisema kuwa kuna watu wengi wanafikiri akipiga picha vile labda anatafuta wanaume ili wampatie fedha, kitu ambacho sio cha kweli kwani yeye ana mtu wake na anamuelewa anachofanya.

Watu wengi sana wananifikiria tofauti labda napiga picha kujiuza au kuwateka wanaume kumbe mimi nafanya kitu ambacho nakipenda toka moyoni na si vinginevyo”.

 

BASATA Wahaidi Kumshughulikia Sanchi

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limehaidi kumshughulikia Socialite maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Janey Rimoy maarufu kama Sanchi kutokana na picha zake zenye utata.

BASATA wametoa tamko hilo baada ya kupokea malalamiko kwa Watu wengi za kwanini Mrembo huyo amekuwa akiposti picha za nusu uyupu lakini amekuwa akiangaliwa tu.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Afisa Habari wa BASATA, Agnes Kimwande alisema kwanza hawamtambui Sanchi kama mwanamitindo na hawajui ni kazi gani maalum ambayo anaifanya ndiyo maana walisita kumchukulia hatua ila watafuatilia kama ni kweli anajihusisha na kazi za sanaa ili wamchukulie hatua mara moja na sio kwamba wanamuogopa.

Watu wengi wanatumia kivuli cha sanaa kufanya mambo ambayo kimsingi sio mazuri sio kwamba tunamuogopa kumchukulia hatua, hapana ila sisi hatumtambui huyo Sanchi kama ‘Model’, kwa sababu sisi tunamchukulia hatua mtu ambaye anafanya makosa kwenye kazi ya sanaa mfano Diamond akivua nguo akiwa anafanya shoo tutamshughulikia kwa sababu inatuhusu sisi moja kwa moja ila naahidi tutamfuatilia kama kweli anafanya sanaa ili tujiridhishe kama anatuhusu basi tutamshughulikia“.

 

BASATA Watoa Tamko Picha Chafu za Sanchi

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limetoa tamko kuwa litamshug-hulikia mwanamitindo ambaye ni gumzo mtandaoni kwa kuposti picha za nusu utupu, Jane Rimoy ‘Sanchi’ baada ya malalamiko ya watu wengi ya kwa nini baraza hilo halimchukulii hatua kama ambavyo hufanya kwa wengine.

Akizun-gumza na Showbiz XtraAfisa Habari wa Basata, Agnes Kimwande alisema kwanza hawamtambui Sanchi kama mwanamitindo na hawajui ni kazi gani maalum ambayo anaifanya ndiyo maana walisita kumchukulia hatua ila watafuatilia kama ni kweli anajihusisha na kazi za sanaa ili wamchukulie hatua mara moja na sio kwamba wanamuogopa.

“Watu wengi wanatumia kivuli cha sanaa kufanya mambo ambayo kimsingi sio mazuri sio kwamba tunamuogopa kumchukulia hatua, hapana ila sisi hatumtambui huyo Sanchi kama ‘Model’, kwa sababu sisi tunamchukulia hatua mtu ambaye anafanya makosa kwenye kazi ya sanaa mfano Diamond akivua nguo akiwa anafanya shoo tutamshughulikia kwa sababu inatuhusu sisi moja kwa moja ila naahidi tutamfuatilia kama kweli anafanya sanaa ili tujiridhishe kama anatuhusu basi tutamshughulikia,” alisema Agnes

Nimenunua Kwa Pesa Yangu Kiwanja Cha Milioni 97-Sanchi

Socialite maarufu Janey Rimoy ‘Sanchi’ aliyejizlea umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake matata na picha zake za utata amefunguka na kuanika kiwanja alichonunua kwa shilingi milioni 97.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sanchi ameweka wazi kuwa alimtumia kiwanja kile kwa pesa yake mwenyewe miaka michache iliyopita ba hata kudokeza kuwa anataka kuporomosha mjengo.

Sanchi amedai yeye ndiye kumiliki halali wa kiwanja kile ambacho kina ukubwa wa hekari kadhaa na kudai ana mpango wa kuporomosha Mjengo mara tu atakapomaliza kujenga nyumba yake ya sasa.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers Sanchi aliweka wazi kuwa kiwanja kile ni muunganiko wa viwanja viwili na bei yake ni Milioni 97.

Sanchi Adai Hakuna Mwanaume Mwenye Hadhia Ya Kuwa Naye Bongo

Socialite maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Jane Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kudai hajaona mwanaume ambaye anaweza kuwa naye Bongo licha ya kumtongoza sana.

Katika mahojiano yake na gazeti la Amani, Sanchi alisema kuwa kama  kuwa na uhusiano na mwanaume wa Kibongo angefanya hivyo lakini hajaona mwanaume wa kuwa naye na wala hawashobokei kwani kama ni wanaume wamejaa kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao humfuata kwa njia ya meseji za moja kwa moja.

Unajua mimi siwezi kuwashobokea kabisa wanaume wa Kibongo kama kunitongoza wamenitongoza sana, si hao tu hata wanaume wa nje tena mastaa Marekani, wanamuziki na wanamichezo wamekuwa wakinisumbua sana na sijawa na uhusiano nao sembuse hao wa Kibongo siwataki“.

Lakini pia Sanchi amefunguka na kujibu maswali ya watu wanaomuhoji kama ametongozwa na msanii mkubwa wa Bongo fleva:

Huyo msanii wao alishanitongoza na nikamkataa, si huyo tu wasanii karibu wote wakubwa Bongo wameshanitaka nikawakatalia, siwataki. Wenye hamu ya kumjua mtu wangu ipo siku nitamuanika”.

 

Sanchi- Ni Hobi Yangu Kuposti Picha Zangu Za Utupu

Socialite maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Jane Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kuweka wazi kuwa anapendelea sana kuposti picha zake za utupu.

Sanchi alijipatia umaarufu kutokana na umbile lake na jinsi ambavyo amekuwa akipenda kupiga picha zake za kihasara hivyo kumfanya ajulikane sana ndani na nje ya Bongo.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Sanchi amefungukia suala lake la kupiga picha hizo za utupu na kudai hiyo ni moja kati ya hobi zake na anapenda sana:

Unajua kuna mtu mwingine anaweza kudhani nafanya makusudi lakini ndiyo hobi yangu. Hata nguo ambazo navaa huwa ndiyo roho yangu inapenda nivae hivyo na siyo za nusu utupu kama watu wanavyosema.

Na ukijaribu kunifuatilia utagundua kuwa nimebadilika sana kwenye suala la uvaaji kutokana na maneno ya watu”.

Lakini pia Sanchi amekana taarifa za yeye kuendesha maisha yake kutegemea kalio na kudai anategemea akili yake:

Mimi namshukuru Mungu kwa kunipa umbo hili ambalo ni la asili kabisa. Hao wanaosema nategemea kalio kuendesha maisha yangu ni ‘mabogasi’. Akili yangu ndiyo inayoniongoza katika maisha yangu, kama ni shepu mbona wengi tu wana shepu lakini hawana mafanikio kama yangu?”.

 

Nipo Tayari Kuzaa Wakati Wowote Sasa- Sanchi

Socialite na mwanamitindo maarufu nchini mwenye umbo la aina yake Jane Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kuzaa hivi karibuni.

Sanchi ameweka wazi nia yake ya kumpa mjukuu mama yake mzazi kwani anaamini kumpa mjukuu ndio zawadi pekeee ambayo inaweza kumfurahisha mama yake.

Kwenye mahojiano  na gazeti la Ijumaa Wikienda, Sanchi alisema kuwa mama yake amekuwa na hofu kutokana na kazi yake ya uanamitindo na kuzunguka nchi mbalimbali kwamba itakuwa ngumu kwake kuweza kutulia na kubeba ujauzito mpaka kujifungua.

“Kwa kweli niko mbioni kumpa mama yangu zawadi ya mjukuu maana amekuwa na wasiwasi sana kutokana na kazi yangu ninayofanya anaona labda nitachelewa sana kumpatia mjukuu hivyo nataka kwenye hilo nisimuangushe nalifanyia kazi”.

 

Sanchi: Sina Shida Ya Kuolewa Kwa Sasa

Socialite maarufu mtandaoni Janey Ramoy maarufu kama Sanchoka Sanchi amefunguka na kutoa povu zito kuwa hahitaji kuolewa kwa sasa na kama endapo akihitaji kuolewa ataolew.

Sanchi ametoa povu hilo baada ya kudai kuchoshwa na maneno ya watu wa mitandaoni ambapo Sanchi amesema hajaolewa mpaka sahivi kwa sababu hajaamua lakini sio kwamba amekosa mwanaume wa kumuoa amekiri kuwa wanaotaka kumuoa ni mwingi wamepanga foleni msururu wanamsubiria.

Tangu msanii Ay amuoe Remmy mrembo kutoka Rwanda kumekuwa na maneno mengi sana yamezuka mtandaoni kuwa Remmy ameolewa kwa sababu ya kujiheshimu na kutokaa uchi kama wanawake wengi wakibongo kama Sanchi.

 

Sanchi ni moja kati ya mastaa wa Instagram aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na umri lake kubwa ambalo ni Mashalaah maeneo ya nyuma ( makalio) lakini kilichompa umaarufu zaidi ni kawaida yake ya kukaa wazi muda wote mtandaoni na kujiachia kinusu utupu na nguo za ndani tu.

Kutokana na tabia yake ya kuvaa nusu utupu karibu kila siku watu wengi wamekuwa wakimnyooshea kidole wakidai haolewi pamoja na kuwa na makalio mkubwa lakini hakuna mwanaume anayetaka kumuoa.

Sanchi amefunguka na kutoa neno kwa Global Publishers na kudai kuwa hana shida ya kuolewa kama watu wengi wanavyofikiria:

Jamani naomba watu wajue kabisa kuwa mimi Sihitaji kuoelewa kwa sasa ningekuwa nataka kuolewa ingekuwa zamani tu nimeshaolewa wapo wanaume wengi tu wanataka kuleta posa kwetu lakini kwa sasa nimesema hapana kwanza”

.

Sanchi:Ingekuwa Kinyume Na Maadili Nisingechumbiwa

Moja wa wanamitindo ambao wameingia katika list ya wasichana wanaovaa vibaya na kutupia picha za utupu katika mitandao ameliambia gazeti la ijumaa wikienda kuwa kuvaa uchi na kuweka picha za namna hiyo ndiko kulikomfanya apate mwanaume katika maisha yake.

Mwanadada sanchi ambae amejizolea umaarufu sana kutokana na kupiga picha za utupu zikimuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa nje amefunguka na kusema kuwa watu wanashindwa kutambua kuwa yeye ni mwanamitindo na kazi ya uanamitino inakulazima kufanya vitu kama hivyo.

Sanchi anasema kuwa amekuwa akishambuliwa sana kuwa hatoweza kupata hata mume wa kumuoa lakini ukweli utabaki kuwa kazi ya uanamitindo ndivyo ilivyo na ukweli utabaki kuwa kazi hiyo ndio iliyompa mchumba mpaka sasa.

Akiendelea kujitetea Sanchi anasema kuwa kwa kazi hiyo ya kuwa mwanamitindo ndipo alipopata mchumba ambae alimuona na aligundua kuwa anaweza kuwa mchumba na mke anaefaa.

Watu wanashindwa kuelewa maana ya kuwa mwanamitindo,ndio maana nasema bila kujua kuwa kama isingekuwa ni maadili basi hata mimi mchumba hasingejitokeza mpaka sasa.

Hata hivyo maneno ya Sanchi aliyasema kabla ya kutokea kwa tamko la mh naibu waziri Mh. Juliana Shonza ambae aliwataka wasichana wanaovaa nguo za wazi hasa zinazowaacha maungo wazi kuacha mara moja huku Sanchi akiwa katika orodha ya wasichana walitakiwa kuripoti ofisini kwa Naibu Waziri huyo

 

 

Nimeshawahi Kudate na Marco chali Lakini Kuna Wanaume Wengine Nawatamani-Sanchi

Mrembo Sanchoka ‘Sanchi World’ ambaye ni mwanamitindo na mfanyabiashara aliyepata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kutokana na urembo wake na shepu yake yakuvutia amefunguka na kutaja wanaume ambao angependa kuwa nao bongo.

Katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times FM Sanchi amefunguka kuwa anapenda mwanaume mwelewa, smple, mwenye upendo na pia awe na pesa za kutosha;

“Moja kati ya msanii wa Bongo anayenivutia ni John Makini ingawa sikuwahi kumwelezea hisia zangu lakini leo ndio atajua, lakini pia ninavutiwa na Ali kiba na Diamond na kwa nje ya nchi Nigeria ningefurahi kuwa na Davido”.

Pia Sanch alifunguka kuw hajawahi kuwa na uhusiano wa imapenzi na Idris Sultan kama watu wengi walivyodhani ila ameshawahi kuwa kimapenzi na mtu mmoja tu maarufu ambaye ni producer wa muziki Marco chali.

Sanchi pia alifunguka kuwa usumbufu mkubwa anaopata kutoka kwa wanaume mitandaoni ameshazoea kwa sasa kwani wa mara kwa mara. Lakini pia amesema havutiwi na wanaume wenye wivu na mwanaume ambaye hajiamini.