Kufungia Nyimbo Kwawaingiza Matatani BASATA.

Baraza la sanaa Tanzania limefunguka na kusema kuwa kitendo cha wao kuamua kuwawajibisha wasanii kwa kuwafungia nyimbo ambazo zimekuwa hazina maadili limekuwa baya baada ya wao kuingia matatani kwa kipindi kirefu sasa tangu wameanza zoezi hilo.

Mh Godfrey Muingereza anasema kuwa kwa mwaka 2019 wanahaidi kufanya vizuri zaidi hasa katika kuwaweka wasanii katika mstari ulionyooka kwa kufuata katiba na sheria za baraza hilo ingawa kumekuwa na cgangamoto mablimbali .

Kiongozi huyo anasema kuwa wamekuwa na wakatI mgumu sana hasa wanapoanza kutishiwa maisha, kukatwa mapanga na hata kumwagiwa tindikali wakati nia yao ni kuwawea wasanii katika mstari sawa ili kulinda na kukuza muziki na tamaduni pia.

Ikumbukwe kuwa , BASATA wamekuwa mstari wa mbele kukemea kitu chochote kinachohusu sanaa mbacho kinaweza kukiuka maadili na kupotosha jamii kupitia sanaa.

 

Diamond na Rayvanny Waomba Msamaha BASATA na Serikali Baada Ya Kufungiwa

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka Katika Label ya WCB Diamond Platnumz na Rayvanny ameibuka na kuomba Radhi kwa serikali na BASATA siku chache Baada ya kufungiwa.

Wiki iliyopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) walitangaza kuwafungia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny Baada ya kukaidi amri yao na Kuperfom wimbo wa Mwanza uliofungiwa kwenye tamasha lao la Wasafi Festival.

BASATA Walitangaza kulifungia tamasha la Wasafi Festival na pia kuwataka wasanii hao kutoperfom katika nchi nyingine yoyote pamoja na kwamba walishapanga kwenda Kuperfom Nchini Kenya.

Lakini Wasanii hao wameomba msamaha Kwa BASATA na Serikali kwa ujumla na kuomba wasemehewe adhabu yao waliyopewa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny ameposti kipande hiki cha video kinachoonyesha wasanii Hawa wakiomba radhi:

https://www.instagram.com/p/BroqbY3j9YE/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1uqh6m3umbdj1

Diamond Platnumz na Rayvanny Wafungiwa Kufanya Show Ndani na Nje Ya Nchi

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Rayvanny kutokea katika Label ya WCB wamefungiwa rasmi kutofanya show ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana.

Baraza la  Sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza kuwafungia Diamond na Rayvanny Baada wawili hao kukiuka masharti waliyopewa.

Taarifa  iliyotolewa leo Desemba 18, 2018 na BASATA,  imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wasanii hao kuonyesha dharau kwa mamlaka zinazosimamia shughuli za sanaa nchini, kwa kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.

Kwa upande mwingine, BASATA  wamefuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival linalotarajiwa kufanyika nje ya nchi baada ya kuzunguuka kwenye baadhi ya mikoa hapa Tanzania.

Imeelezwa kuwa wimbo wa Mwanza ndio uliowaingiza matatani, baada ya wasanii hao wikiendi iliyopita kuonekana jukwaani katika Tamasha la Wasafi Festival jijini Mwanza wakitumbuiza wimbo huo.

BASATA Kuwashughulikia Diamond na Rayvanny Baada Ya Kupiga ‘Mwanza’

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) linefungukia kitendo cha Wasanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Rayvanny kuperfom wimbo wao wa Mwanza ambao umefungiwa.

Mwezi uliopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) walitangaza kuufungia rasmi wimbo wa ‘Mwanza’ kwa madai kuwa wasanii hao wamekiuka maadili ya Kitanzania kwa maudhui ya wimbo huo.

Diamond aliimba wimbo huo alioshirikishwa na Rayvanny jana Desemba 15, 2018 katika tamasha la Wasafi lililofanyika jijini Mwanza jana, huku maelfu ya mashabiki wakimshangilia na kumfuatisha alivyokuwa akiimba. Mkali huyo wa Bongo Fleva aliimba wimbo huo  akiwa pamoja na Rayvanny.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Katibu mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza alifungukia ishu hiyo na kusema:

Nimepigiwa simu kuhusu hii kitu. Niko Arusha kikazi nimeshawasiliana na mwenyekiti wa bodi (ya Basata).

Basata itakuja na majibu muafaka kwani hapa (Diamond) kaonyesha kiwango cha juu cha dharau kwa baraza, bodi, wizara (Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo) na Serikali kwa ujumla”.

 

 

BASATA Waibuka na Kumpongeza Diamond Platnumz

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) wamempongeza Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz Baada ya msaada aliotoa mkoani Sumbawanga alipokuwa kwenye shoo.

Sio Siri kuwa uhusiano wa Diamond na BASATA umekuwa wenye misukosuko kwani Wiki chache tu zilizopita msanii huyo alionekana akiwasihi Baraza hilo lisifungie nyimbo yake mpya ‘Mwanza’.

Baraza hilo limeamua kumpongeza Diamond Baada ya Shughuli za kijamii alizofanya mkoani Sumbawanga ikiwemo kuhaidi kutoa zaidi ya Milioni 68 kwa ajili ya kujenga shule ya msingi.

Kipitia ukurasa wao wa Instagram, Baraza hilo limeandika ujumbe huu:

Wema Achukuliwa Hatua Kali na BASATA Baada Ya Kuvujisha Picha Chafu

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Wema Sepetu amejikuta katika upande mbaya wa sheria za nchi baada ya kuvujisha picha zake za faragha alizokuwa na mpenzi wake PCK.

Pamoja na kuomba radhi siku ya jana kuhusiana na picha hizo chafu Kwenye mitandao ya kijamii lakini tayari BASATA wameamua kumchukilia hatua kali Wema pamoja na wasanii wote walioachia picha chafu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha runinga cha EATV, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza amesema wameanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliochapisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono mitandaoni.

Kwa upande mwingine, Mhe. Shonza amesema kuwa licha ya wasanii hao kuhojiwa na Bodi ya  filamu pia watahojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Pamoja na Wema kusambaza na video zake chafu Lakini pia Gigy Money amedaiwa kuachia picha yake chafu Lakini pia video vixen Amber Rutty ameachia video yake ya ngono Mtandaoni.

BASATA Wahaidi Kumshughulikia Sanchi

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limehaidi kumshughulikia Socialite maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Janey Rimoy maarufu kama Sanchi kutokana na picha zake zenye utata.

BASATA wametoa tamko hilo baada ya kupokea malalamiko kwa Watu wengi za kwanini Mrembo huyo amekuwa akiposti picha za nusu uyupu lakini amekuwa akiangaliwa tu.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Afisa Habari wa BASATA, Agnes Kimwande alisema kwanza hawamtambui Sanchi kama mwanamitindo na hawajui ni kazi gani maalum ambayo anaifanya ndiyo maana walisita kumchukulia hatua ila watafuatilia kama ni kweli anajihusisha na kazi za sanaa ili wamchukulie hatua mara moja na sio kwamba wanamuogopa.

Watu wengi wanatumia kivuli cha sanaa kufanya mambo ambayo kimsingi sio mazuri sio kwamba tunamuogopa kumchukulia hatua, hapana ila sisi hatumtambui huyo Sanchi kama ‘Model’, kwa sababu sisi tunamchukulia hatua mtu ambaye anafanya makosa kwenye kazi ya sanaa mfano Diamond akivua nguo akiwa anafanya shoo tutamshughulikia kwa sababu inatuhusu sisi moja kwa moja ila naahidi tutamfuatilia kama kweli anafanya sanaa ili tujiridhishe kama anatuhusu basi tutamshughulikia“.

 

BASATA Wakanusha Tetesi Za Kumuita Wema Sepetu

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limekanusha tetesi za kumuita na kumhoji staa wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya kusambaza Mtandaoni picha na video zenye utata.

Wiki iliyopita Wema alizua gumzo baada ya kuachia picha na video za yeye na mpenzi wake huku video ikiwaonyesha wawili hao wakiwa wanapeana mabusu moto moto na picha ikiwaonyesha wakiwa chumbani.

Mwishoni mwa wiki iliyopita kuna tetesi zilisambaa kuwa kutokana na picha hizo chafu Wema Sepetu ameitwa na BASATA kwa ajili ya kufika katika ofisi zao taarifa ambazo kwa saaa BASATA wamezikataa.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Afisa Habari BASATA, Agness na kukanusha taarifa hizo huku akidai kama mwanadada huyo anaenda Basata ni kwa mambo yake binafsi sio kwamba aliitwa.

Sio kweli Wema ameitwa Basata, hata sisi tunasikia hizo habari na kuihusisha na mambo yake ya kwenye mitandao, sisi kama Basata atu-deal na maisha binafsi ya wasanii labda afanye tukio katika kazi ya sanaa ndio tunaweza kumuita,Kama ni mambo ya mtandaoni TCRA ndio wenye mamlaka”.

BASATA ni sehemu ya wasanii, ni wazazi wa wasanii, kama anakuja sisi tutampokea na kuzungumza naye hukusu sanaa yake na namna ya kujiweka kama msanii lakini mpaka sasa hatuna taarifa kama anakuja lakini akija sawa tutampokea”.

 

BASATA Wakanusha Kufungulia Nyimbo za Diamond.

Siku mbili zilizopita baada ya msanii diamond kukutana na waziri Mwakyembe na Naibu Waziri wake Juliana Shonza ambae alikuwa katika vita ya kurushiana maneno na msanii huyo walipokutana  na kuzungumza maswala yaliyokuwa yanaendelea  kuhusu kufungia nyimbo za wasanii zikiwemo hizo mbili za Diamond Platinumz  kuna baadhi ya mitandao walizusha kuwa nyimbo mbili za Diamond zimefunguliwa na kuruhusiwa kuchezwa kama mwanzo katika vituo vya habari.

katibu mtendaji wa BASATA amesema kuwa habari zinazosambaa wanatakiwa kuzipuuzia kwa sababu hazina ukweli wowote,lakini pia mngerza ameelezea kwanini msanii Diamond amekuta na waziri na wala sio wasanii wengine waliokuwa wamefungiwa.

katibu mtendaji wa BASATA  anasema kuwa sababu kubwa ya Diamond kukutana na waziri na Naibu ni baada ya kutokea kwa majibizano kati yao hivyo walitakiwa kukutana hili kuyamaliza matatizo hayo ambayo yalikuwa yanaendelea bila wao kukutana.

Hata hivyo Mngereza maesema kufunguliwa kwa nyimbo ya msanii yoyote ni baada ya msanii huyo kukamilisha vigezo vyote na masharti atakayotakiwa kuyatimiza.

Diamond Anafanya Makosa Kumjibu Naibu Waziri:-Mngereza.

Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania Godfrey Mngereza amefunguka na kusema kuwa anachofanya diamond cha kujibishana na naibu waziri wa habari sio kizuri na kukifananisha kitendo hicho na kitendo cha kuitukana serikali .Diamond na naibuwaziri waliingia katika mgogoro wa kurushiana maneno baada y naibu waziri kufunga nyimbo zaidi ya  15 huku nyimbo mbili zikiwa ni nyimbo za msanii Diamond.

Mngerza anasema kuwa jambo analofanya Diamond kwa sasa ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo kama atashitakiwa na serikali pia ni kosa la kimtandao.ameongezea na kusema kuwa sio lazima mtu anapofanya kosa lazima aandikiwe barua kama yeye anavyodai.

Mngerza  anasema kuwa amesikitshwa sana na maneno ya diamond , kwa sababu kama angekuwa na maalalmiko angepaswa kuandika barua ili kutoa malalamiko yake na sio kwenda katika mitandao ya kijamii.

Katika kumjibu diamond, mh juliana shonza alisema kuwa hana mamlaka ya kumjibu diamond tena kwa sababu maamuzi anayoyafanya sio yake ila ni kazi ya serikali na kama ana malalamiko aandike barua, ndipo diamond alipoamua kumjibu kuwa kama yeye alianza kuyapeleka radion na kwenye mitandao na yeye hatokaa aandike barua.

 

 

Rayvanny aisuta Basata kwa kukosa kuenda kumpokea katika uwanja wa ndege

Rayvanny alipewa mapokezi ya kirais alipowasili Tanzania kutoka Marekani. Staa huyu wa Wasafi alishinda tuza la BET na kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hilo.

Diamond, Harmonize, Babu Tale na mamia ya mashabiki walijitokeza kwa wingi kumlaki Rayvanny katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere.

Rayvanny ata hivyo ameisuta Basata kwa kukosa kuenda kumlaki katika uwanja wa ndege, alisema bodi hio ya sanaa nchini haikuonyesha picha nzuri na hatua yao.

“Kwa mafano, mimi nilivyochaguliwa kama BASATA walikuwa wameona. Wao ni wazazi walikuwa na chochote cha kusema lakini wakisema kwamba wanasubiri niende mimi mwenyewe au tunasubiri watuambie au hatuwezi kwenda kwa sababu hatujaambiwa. Wale ni wakubwa kwetu ni wazazi wetu tunategemea kwamba wanakuza sanaa yetu na sisi tunawaangalia wao walitakiwa kuwa kipaumbele sisi kutusaidia,” Rayvanny alisema.

Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza akiongea na Clouds FM alitetea bodi hilo kwa kusema kuwa Basata haikupata ratiba ya Rayvanny.

“Hakukuwa na mawasiliano mazuri alivyokuwa amekwenda na ujio wake lakini tungekuwa tunaifahamu ratiba yake Baraza kama ilivyo ada huwa hatuna budi ya kwenda kumpokea Airport, kwanza inaleta heshima. Kwa hiyo, hakuna sababu ya kusema tusingeenda kumpokea ni kwamba mawasiliano hayakuwepo tangu anaenda na pia ningependa nikumbushe wasanii wanavyokwenda nje ya mipaka ya Tanzania ni vizuri tukaagana ili tukajua ratiba ikoje hata wakirudi tuwapokee,” Godfrey Mngereza alisema.

 

Baraza la Sanaa Tanzania yatoa kauli yake kuhusu picha za utupu za Ben Pol

Ben Pol alizua uzushi katika jukwaa zote baada ya picha zake za utupu kuibuka katika mitendao za kijamii siku chache zilizopita.

Msanii huyo alionekana akiwa uchi wa mnyama katika picha za kitaalamu alizopiga. Watu wengi walikerwa na picha hizo licha ya sehemu yake nyeti kutoonekana.

Moja ya picha ambazo Ben Pol aliweka kwenye mtendao wa kijamii

Baraza la Sanaa Tanzania – BASATA limetoa kauli yake kuhusu picha za Ben Pol. Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alilaani kitendo cha Ben Pol na kusema kwamba sanaa ya Tanzania bado haijafikia zama za kufanyika kitendo kama hicho.

“Kwa tamaduni zetu bado hatujafikia hapo ni wengine huko ambao wanaruhusu. Hiyo ni moja, pili ni kitendo ambacho baraza inakilaani lakini kwa utaratibu wa baraza kama baraza tutamtafuta Ben Pol tuweze kumsikia mwenyewe kwamba zile picha kweli amepost yeye au kuna kitu kingine kwa sababu teknolojia imekwenda mbali sana siku hizi kwahiyo tutamsikiliza anahusika vipi moja kwa moja. Lakini kimsingi kwa ujumla wake baraza inakilaani na tutaendelea kumtafuta Ben Pol kuzungumza naye kwa sababu ni haki yake kusikilizwa katika hilo.

“Pia naungana na wasanii waliolaani kitendo hiko ambacho ni cha ajabu sana na baraza kwa mamlaka yake kama mzazi haiwezi kukaa kimya lazima tujue kama ana tatizo la akili au maadili limemkumba Ben Pol,”alisema Godfrey Mngereza.