“Ali Kiba Ndio Anatufundisha Muziki”- King’s Music

Wasanii waliosainiwa chini ya label ya Kings Music ambayo inamilikiwa na staa wa Bongo fleva Ali kiba wamefunguka na kuweka wazi kuwa Msanii huyo ndio anawafundisha muziki.

Kundi hilo la wasanii ambalo linaundwa na wasanii kadhaa Kama Cheed, Killy na K-2GA na akiwemo kaka wa Ali Kiba, Abdu Kiba wamesema Msanii huyo ndio mtu anayewafundisha vitu vingi kuhusu muziki ikiwemo mpangilio wa nani aanze kwenye ngoma zao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi Planet Bongo ya East Africa Radio, wakati wanatambulisha ngoma yao mpya ‘Toto’, Abdu Kiba  amekiri kuwa kwa ukongwe wa Alikiba kwenye muziki lazima awaongoze.

Anayetupanga ni Alikiba yeye anajua vitu vingi kwenye muziki na ndio maana ana nafasi hiyo ya kushauri nani aanza na nani anafuata na nani atamaliza, kwahiyo Kings Music ni chuo cha muziki”.

Msanii mwingine wa Label hiyo Killy amesema tayari kwa nyimbo mbili ambazo wamezitoa ikiwemo Sina, zimeshawaletea mashabiki wa aina mbalimbali na majina yameanza kuwa makubwa.

Abdu Kiba- Ninaweza Kufanya Kolabo na WCB Lakini Inategemea na Wimbo

Msanii wa Bongo fleva Abdul Kiba ambaye pia ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kudai kuwa yupo tayari kufanya Kolabo na mahsimu wao wakubwa WCB.

Sio siri kuwa Diamond na Ali Kiba hawapikiki chungu kimoja pamoja na kwamba wameshasema hawana bifu lolote lakini ni wazi kuwa Kumekuwa na tensions fulani baina ya makundi hayo mawili.

Lakini Abdu Kiba ameibuka na kudai kuwa kama ikitokea kuwa kuna wimbo ambao utakuwa na uhitaji wa msaniii kutoka WCB ndio ukae sawa hataona shida kumtafuta ili wafanye kazi.

Abdu Kiba amefunguka hayo Kwenye mahojiano na EFM Radio Lakini amejitetea Kuwa Mpaka sasa hajapata wimbo unaohitaji sauti kutoka kwa msanii yeyote wa WCB:

Kufanya kolabo na msanii yeyote kutoka WCB inategemeana na muziki gani ambao nimeimba, naamini kila muziki una sura ambayo inaonyesha ni nani unaweza kuimba naye, ikitokea kuna muziki ambao naona kuna haja ya msanii kutoka WCB nitafanya naye na kama sina tutabaki hivi hivi WCB na Team Kiba”.

 

Abdukiba: Ali Kiba Amenitengenezea Njia

Mwanamuziki wa Bongo fleva Abdu Kiba ambaye ni kaka wa Supastaa wa Bongo fleva, Ali Kiba amefunguka na kudai kuwa kaka yake ameshiriki katika kumtengenezea njia kwenye sanaa.

Ali Kiba alianza kufanya muziki miaka ya nyuma sana ni moja kati ya msanii mkongwe ambaye amedumu kwenye gemu mpaka leo bila kuchuja tofauti na wasanii wengine wengi waliopotea.

Abdu Kiba ameibuka na kukanusha maneno yanayoongelewa na watu wanaodai kuwa alikuwa kimya kwa muda mrefu sana kwa sababu kaka yake Ali Kiba alikuwa anamkataza kufanya mziki.

Kwenye mahohiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Abdu Kiba amedai kuwa Ali Kiba alikuwa akimtengenezea njia nzuri ya kuja kufanya mziki mzuri na ni mtu anayetakiwa kusikilizwa sana kwenye game:

Kiukweli kwanza nimshukuru Mungu kwa ukimya wote niliokaa na mpaka nimerudi mafans wamenipikea alafu tena naamini mziki Una changamoto tukisikiliza maneno ya watu wanayozungumza pembeni ni changamoto ambazo mimi napata na ndizo zilizonikuza kwenye huu mziki hivyo Alikiba na management ilivyoniambia nikae nitulie nisubiri hata mwaka ili nijipange sana ili nikirudi mambo yawe mazuri kama mnavyoona nashukuru Ali Kiba amenitengenezea njia ya kupita”.

Baada ya Abdu Kiba kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kutoa ngoma yoyote maneno Mengi yalizuka huku wait wengi wakidai kuwa Alikiba amemkataza kutoa ngoma lakini hivi karibuni ametoa nyimbo mpya inayoitwa Single aliyomshirikisha Alikiba ambayo inaendelea kufanya vizuri kwenye chati.