Ali Kiba Azindua Kinywaji Chake Siku Ya Harusi Yake

Staa wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amezindua rasmi kinywaji chake cha Energy siku ya jana katika hoteli ya Serena ambapo ndipo reception yake ya harusi ilifanyika.

Ali Kiba ametangaza Habari hiyo kuwa amekuwa balozi rasmi wa kinywaji kinachoitwa Ali Kiba Mofaya Energy Drink ambacho kimesindikizwa kwa picha yake kwenye chupa.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Ali Kiba atakuwa balozi wa bidhaa kadhaa mbali na fani yake ya muziki.

Lakini pia mashabiki zake wote waliokuwepo Kwenye ukumbi huo walipata nafasi ya kuonja kinywaji hicho kwani kilipatikana kwa kila mmoja aliyekuwa Ukumbini humo.

Tazama Picha Za Harusi Ya Alikiba na Abdu Kiba

Siku ya jana tarehe 29/04  Staa wa muziki wa Bongo fleva AliKiba na alitimiza sherehe ya mwisho ya ndoa yake na mrembo kutoka Mombasa Amina Lakini pia harusi hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Serena Hotel.

Lakini pia kilichovutia watu wengi haikuwa tu sherehe kwa ajili ya Ali Kiba na mkewe Lakini pia mdogo wa ALikiba Mwanamuziki Abdul Kiba ambaye na yeye alionekana na mke wake Ruwayda.

Harusi hiyo ilirushwa Love Kwenye chanel ya Azam na pia ilihudhuriwa na mastaa mbali mbali kama vile Mama Salma Kikwete, Ummy Mwalimu, Idris Sultan, Vanessa Mdee na Mimi Mars na wengineo.

Hizi ni baadhi ya picha za harusi hiyo:

 

Wanaume Watano Wamejitokeza Wanataka Kunioa- Wema

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kueleza jinsi wanaume wanavyomiminika kwao kutaka kutoa posa ili wamuoe.

Wema amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda ambapo amedai kuwa kuna muda wanaume watano tofauti walienda kutoa posa kwao lakini aliwakataa wote:

Walijitokeza karibu wanaume watano wanaenda, kwa mama kupeleka barua kinachotokea mama ananiita, ananiuliza mimi, sikubali kwa sababu siwezi kuolewa na mtu ambaye simjui au sijakaa naye“.

Lakini kuhusu Kuolewa hivi sasa Wema amejibu hawezi kuweka wazi lakini ana mpenzi wake ambaye anampenda lakini hawezi kumuweka wazi kwani amekuwa mtu mzima siku hizi.

Wema amefunguka na kumpongeza msanii wa Bongo fleva ambaye pia ni rafiki yake wa karibu Ali Kiba kwa kufunga ndoa hivi karibuni ambapo amesema:

Ninampongeza sana kwa mwanamuziki mkubwa kama yeye kufanya jambo hilo amejijengea heshima kubwa sana, lakini ninaamini mke yupo popote ni jinsi tu Mungu alivyokupangia wapi utampata“.

Aslay Afunguka Kuhusiana na Ndoa Ya Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Aslay amefunguka na kuongelea ndoa ya staa wa Bongo wa fleva Ali Kiba iliyofungwa wiki iliyopita ambapo amesema haoni tatizo kwa Msanii huyo kuoa nje ya nchi.

Ali Kiba amemuoa mwanamke anayeitwa Amina Rikesh mwenye asili ya Kiarabu kutoka Oman lakini anayeishi Mombasa nchini Kenya.

Mashabiki walimtolea povu Ali Kiba kwa kitendo chake cha kuamua kwenda kuoa nje ya nchi wakati Tanzania kuna wanawake kibao jambo ambalo Ali kiba alijibu kuwa macho na moyo havina pazia.

Aslay ameipongeza na kusema watu wasishangae au kulalamika mtu kuamua kuoa nje ya nchi kwani jambo hilo ni la kawaida tu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Aslay amewataka mashabiki zake wasilalamike kitendo cha yeye kwenda kuoa nje ya nchi kwani ni jambo la kawaida sana kutokea:

Kuoa ni jambo la kheri bwana na ni hatua kubwa sana nampongeza sana kaka mkubwa kwani sio jambo la mchezo hilo, lakini watu wanatakiwa kuelewa kuoa nje ya Tanzania ni jambo la kawaida tu kama mtu anavyotoka kwenye kabila lake na kuoa kabila lingine“.

 

Abdi Banda Atangaza Ndoa na Dada Yake Ali Kiba

Baraka inaendela kuzisi kuitembelea familia ya Ali Kiba Kwani Dada yake na Kiba anayejulikana kama Zabibu Kiba amesemakana kufunga ndoa hivi karibuni.

Ikiwa ni wiki tu imepita tangu kaka yake Ali Kiba Abdu Jr rekodi baada ya kufunga ndoa na mrembo anayeitwa Amina kutoka Mombasa Kenya na kutrend vibaya mno hasa pale iliporushwa live kwenye televisheni.

Lakini ni juzi tu kaka mwingine wa Zabibu ambaye na yeye ni Mwanamuziki wa Bongo fleva Abdu Kiba alipoamua kuuaga ukapera baada ya kufunga ndoa Jumapili iliyopita.

Inaelekea Zabibu anakuwa Kiba wa tatu kufunga ndoa kwa mwaka huu wa 2018 kwani inasemekana Zabibu na mpenzi wake Abdi Banda wanatarajia kufunga ndoa mwaka huu.

Tetesi za Kitaa zinasema Abdi Banda anatarajia kufunga ndoa na dada ake Kiba, Zabibu baadae mwaka huu, hii ni baada ya kaka yake kufunga ndoa. Pongezi kwake Abdi Banda

Abdi Banda kwa sasa anachezea timu moja huko South Africa,ila aliwahi kuicheze timu ya Simba.

Zabibu Kiba Amtaka Wifi Yake Awe Mvumilivu Kutokana na Kazi Ya Ali Kiba

Jana ilikuwa ni siku ya kihistoria kabisa kwani ilikuwa ni ndoa ya Ali Kiba na mpenzi wake Amina ndoa iliyokuwa gumzo jiji zima.

Ndoa hiyo ilifungwa nyumbani kwa wazazi wa  Amina huko Mombasa nchini Kenya na baadae sherehe ilifanyika usiku katika ukumbi wa Diamond Hall na kurushiana live Azam Tv.

Dada wa Alikiba amayejulikana kama Zabibu Kiba amemfungukia mazito wifi yake huyo na kumtaka kikubwa awe mvumilivu hasa kwa sababu kazi ya Ali Kiba ni Mwanamuziki kazi yenye changamoto:

Mimi namkaribisha Amina nyumbani namkaribisha kwenye familia yetu kikubwa ni uvumilivu hasa kwa sababu anakuja kazi ya mumewe na changamoto ni nyingi na nafikiri alishaanza kukutana nazo na sidhani kama zitamshinda na sisi kama familia tumemkubali na tu nampenda kama alivyopendwa na mume wake 

Ujumbe Wa Diamond Kwa Ali Kiba Baada Ya Kuoa

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameweka bifu pembeni na kumpongeza msanii mwenzake Ali Kiba baada ya kufunga ndoa siku ya jana.

Diamond na Alikiba wamekuwa kwenye bifu la muda mrefu ambapo lilisababisha kugawa mashabiki zao lakini hivi katibuni Diamond aliweka wazi kuwa hana bifu na Ali Kiba.

Jana ilikuwa siku ya shamra shamra kwa Alikiba kwani alifunga ndoa mjini Mombasa Kenya na mkewe Bi. Amina na ilikuwa ni harusi iliyozua gumzo sana Kwenye mitandao ya kijamii.

Diamond hakuona hiyana kumpongeza Ali Kiba na alimtumia ujumbe wa pongezi Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

Wadau nimeambiwa King Kiba kaoa leo mumfikishie salamu zangu za ndoa njema na maisha yenye furaha Amani na baraka tele”.

Baada ya kumtumia ujumbe huo pia Mama mzazi wa Diamond na familia yake wote walimposti Ali Kiba na kumpongeza.

Mange Amvaa Jokate Baada Ya Ali Kiba Kuoa Mwanamke Mwingine

Mwanaharakati wa siasa Mtandaoni Mange Kimambi amemvaa Jokate na kumtolea povu zito baada ya aliyekuwa mpenzi wake staa wa Bongo fleva Ali Kiba kuoa mwanamke mwingine.

Asubuhi ya Leo Ali Kiba Kumuoa mke wake Amina huko Mombasa nchini Kenya lakini Ex wake Jokate anashika headlines ambapo Mange amemjia juu Jokate huku akimcheka kuhusu hilo.

Mange amekuwa akiipinga ndoa hii kufanyika hivi sasa kwa hofu ya kwamba itazima haraka tu zake za Maandamano Lakini pia amekuwa katika vita na Jokate kutokana na Jokate kuwa chama tawala na alikuwa kiongozi.

Mange amemtolea povu zito Jokate huku akihusisha ndoa ya ALi Kiba ambapo kwenye ukurasa wa Instagram wa Jokate aliandika maneno haya: