Zabibu Kiba Afunguka Kuikacha Ndoa Yake Sauzi na Kurudi Bongo

Dada wa staa wa Bongo fleva nchini Ali Kiba, Zabibu Kiba amefunguka na kuanika sababu za kumuacha mume wake Abdi Banda nchini Afrika ya Kusini na kuamua kurudi Tanzania mwenyewe.

Zabibu na mume wake Abdi Banda walihamia SA ambako anacheza soka la kulipwa, miezi michache iliyopita Mara tu Baada ya kufunga ndoa lakini ghafla Zabibu ameonekana kurudi Tanzania na kumuacha mumewe SA.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Vibes, Zabibu alisema amekuwa akipata maswali mengi kutoka kwa watu mbalimbali kwamba imekuwaje amemwacha mumewe Afrika Kusini na kurudi Bongo ambapo alisema amerudi kwa sababu kibali cha kuishi nchini humo ‘viza’ kiliisha muda wake.

Sioni kama kuna tatizo mimi kurudi mapema Bongo maana ndiyo nyumbani kwa wazazi ila sababu kubwa ni kwamba Kusini na kurudi Bongo ambapo alisema amerudi kwa sababu kibali cha kuishi nchini humo ‘viza’ kiliisha muda wake.

Viza yangu ilikuwa hainiruhusu kuendelea kukaa Afrika Kusini kwa muda mrefu kwa hiyo kuna mambo nimerudi kuyaweka sawa kisha nitarudi tena kwa mume wangu kuendeleza mahaba kama kawaida”.

 

Alichosema Zabibu Kuhusu Shughuli ya Mumewe Uwanjani

Mwanadada zabibu kiba ambae ni dada wa Alikiba na Abdul Kiba amefunguka na kuzungumzia swala la mume wake anapokuwa uwanjani akisakata kabumbu .Zabibu anasemakuwa amefurahi sana kudhuhudia mume wake akicheza uwanjani na kwa jinsi anavyomuona anaamini kuwa atafanikiwa sana.

Zabibu kiba ameyasema hayo baada ya mechi ya ligi kuu nchini afrika kusini ambapo timu yake ya Boroka Fc ilipokuwa ikimenyana uwanjani na timu ya  Orlando pirates .

Zabibu anasema kuwa alichokiona kwa mume wake ni nidhamu ya hali ya juu kwa mchezaji huyo kitu mabacho kimekuwa  kikileta mafanikio makubwa sana kwa wachezaji wengine na kuwafanya wafike mbali sana katika mpira.

Zabibu pia amefurahi kuwepo Afrika ya Kusini huku akisema kuwa mndhari yake ni tofauti na yale ya tanzania hata viwanja vyake vya mpira viko vizuri  kwa mchezaji kujituma kufanya vizuri katika mechi.

Zabibu Kiba Asemekana Kuwa ni Mjamzito

Dada wa staa wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba, Zabibu Kiba amedaiwa kuwa wiki chache baada ya kufunga ndoa tayari Mrembo huyo amesha kikwaa kibendi na ni mjamzito.

Zabibu alifunga ndoa na mume wake Abdi Banda ambaye ni mcheza mpira wa kulipwa nchini Afrika ya Kusini mwezi uliopita na sasa kuna taarifa zinasema Zabibu anawezaakawa kashanasa ujauzito.

Global Publishers wanaripoti kuwa kuna tetesi zilianza kusambaa baada ya Picha ya Zabibu kuanza kusambaa kupitia mtandao wake wa WhatsApp ambapo wapenda ubuyu waliichukua picha hiyo na kuanza kuijadili mitandaoni.

Picha hiyo iliyomuonyesha Zabibu akiwa kama mjamzito iliibua mijadala man kupelekea watu kuamini huenda Mrembo huyo tayari ameshabeba mimba.

Baada ya picha hiyo kuzua gumzo, mwishoni mwa wiki iliyopita Gazeti la Amani lilimtafuta mrembo huyo ambaye amehamishia makazi yake ya kudumu nchini Afrika Kusini kwa mumewe Abdi anayesakata kandanda nchini humo katika timu ya Baroka ambapo alipopatikana alikanusha madai hayo na kudai kuwa amenenepa tu.

Hahaha jamani sina kitumbo ni unene tu huu“.

 

Matukio Ya Harusi Ya Zabibu Kiba Kwenye Picha

Zabibu Kiba ambaye ni dada wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba ameolewa siku ya jana na Staa wa Taifa Stars na mchezaji wa Baroka FC ya Afrika Kusini Abdi Banda.

Ndoa hiyo imefungwa katika msikiti wa Sanene Tabata jijini Dar es Salaaam baada ya shamra shamra za sherehe za wiki nzima ambapo Ali Kiba alionekana kama mtu ambaye amemuoza dada yake.

Hizi ni baadhi ya picha za matukio ya ndoa hiyo iliyofungwa alfajiri na mapema:

Jini Kabula Afungukia Ndoa Ya Zabibu Kiba na Aliyekuwa Mpenzi Wake

Muigizaji wa Bongo movie Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka na kuweka wazi kuwa hana tatizo na Zabibu Kiba kufunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake mchezaji wa mpira Abdul Banda.

Siku za nyuma Jini Kabula na mchezaji wa Timu ya Baroka iliyopo Afrika Kusini, Abdul Banda waliwahi kuwa Kwenye uhusiano wa kimapenzi lakini hivi sasa Abdul yuko na Mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba, Zabibu Kiba na wapo mbioni kufunga ndoa.

                               Jini Kabula

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Jini Kabula alisema anawashangaa baadhi ya watu wanaomshambulia kwa maneno machafu kwenye mitandao ya kijamii kisa aliwahi kuwa na uhusiano na Banda lakini hawakufanikiwa kuingia kwenye ndoa kitu ambacho ni kawaida tu katika maisha.

Kwanza nafurahi sana Zabibu kuele­kea kwenye ndoa na Banda nawaombea ifanyike salama na sina kinyongo hata kidogo lakini kuna hawa vizabizabina vya pembeni vinaleta chokochoko na kusema eti nilishindwa kuolewa mimi, niwaambie tu kwamba siyo kila mtu unapokuwa naye kwenye uhusiano lazima muoane hivyo waache kuongea mambo wasiyoyajua“.

Zabibu yupo katika shamrashamra za kuelekea Kwenye ndoa ambapo siku chache zilizopita alionekana akifanyiwa visomo mbali mbali na inasemekana kuwa harusi yaweza kuwa muda wowote.

Ndoa ya Zabibu Kiba na Abdul Banda Yanukia

Ndoa ya dada wa mastaa wawili bongo Abduli Kiba na Alikiba anaejulikana kama Zabibu Kiba imeanza kunukia huku tetesi zikidai kuwa wawili hao wanategema kufunga ndoa mwezi august mwaka huu.

Katika kitandao ya kijamii hasa katika kurasa zao za instagram za wawili hao  kumekuwa na maoni mengi sana kutoka kwa mashabiki zao huku wengi wao wakisema kuwa wamechoka kusubiri tarehe yao ya ndoa ifike ili wawaone wawili hao wakiwa pamoja.

Hata hivyo aktika ukrasa wake wa instagram, Banda aliandika maamuzi sahihi, ‘Get ready its AUGUST..Unapenda tarehe gani ‘na kuzua gumzo katika ukurasa huo huko mashabiki zao wakiona kuwa mwezi huo haufiki haraka ili kushguhudia swala hilo.

 

Abdi Banda Atangaza Ndoa na Dada Yake Ali Kiba

Baraka inaendela kuzisi kuitembelea familia ya Ali Kiba Kwani Dada yake na Kiba anayejulikana kama Zabibu Kiba amesemakana kufunga ndoa hivi karibuni.

Ikiwa ni wiki tu imepita tangu kaka yake Ali Kiba Abdu Jr rekodi baada ya kufunga ndoa na mrembo anayeitwa Amina kutoka Mombasa Kenya na kutrend vibaya mno hasa pale iliporushwa live kwenye televisheni.

Lakini ni juzi tu kaka mwingine wa Zabibu ambaye na yeye ni Mwanamuziki wa Bongo fleva Abdu Kiba alipoamua kuuaga ukapera baada ya kufunga ndoa Jumapili iliyopita.

Inaelekea Zabibu anakuwa Kiba wa tatu kufunga ndoa kwa mwaka huu wa 2018 kwani inasemekana Zabibu na mpenzi wake Abdi Banda wanatarajia kufunga ndoa mwaka huu.

Tetesi za Kitaa zinasema Abdi Banda anatarajia kufunga ndoa na dada ake Kiba, Zabibu baadae mwaka huu, hii ni baada ya kaka yake kufunga ndoa. Pongezi kwake Abdi Banda

Abdi Banda kwa sasa anachezea timu moja huko South Africa,ila aliwahi kuicheze timu ya Simba.

Zabibu Kiba Afunguka Mahusiano Yake na Star wa Taifa Stars

Dada wa wasanii alikiba na abdul kiba, zabibu kiba amefunguka mahusiano yake ya kimapezni na mwanasoka kutoka katika kikosi cha timu ya taifa, Abdi Banda na kusema kuwa wamekuwa katika mahusiano kwa muda wa miaka minne sasa kwa hiyo kama mwanasoka huyo ameamua kumtambulisha hadharani basi kwake haina shida kabisa.

Akielezea kukutana kwao, Zabibu kiba anasema kuwa walivyoanza mapenzi , Abdi Banda ndio alianza kumtafuta yeye kwa njia ya simu bila hata yeye kujua amepata wapi namba yake lakini alimpigia na kumuomba wazungumze kwa kuwa alikuwa na shida.

Yeye ndo alinitafuta mimi sasa sijui aliniona wapi,au nani alimuunganisha lakini alianza kunipigia simu.

Akiongelea kuhusu mwanaume huyo kufanya makala katika moja ya magazeti pendwa hapa nchini na kumtaja yeye kama mpezni wake, zabibu alisema kuwa kwake ni jambo la kherikama aliamua kuweka wazi swala a mahusiano yake na kwake halina shida lakini hawezi kwa sasa kuzngumzia swala la ndoa kwa kuwa hilo anajua yeye.

kama alinitaja sawa lakini kuhusu swala landoa siwezi kuliongelea,kwa sababu banda bado hajaja nyumbani kutoa posa.

Mdogo wa Alikiba Katika Penzi Nzito na Star wa Taifa Stars

Ndugu wa kike wa msaini alikiba , Zabibu Kiba amejikuta katika penzi zito na mchezaji wa mpira nchini tanzania kutoka katika timu kubwa nchi ya Taifa Star anaejulikana kama  Abdi Banda .katika ukurasa wake wa instagram , mcheza mpira huyo amekuwa akimpost na kuweka picha za mwanadada huyo mara kwa mara na hata kufanya watu waanze kuingilia mahusiano yao kwa kuwasahauri kuoana kabisa.

                                               

                                    Abdi Banda mchezaji wa Taifa Stars.

Kwa muda mrefu haikuwahi kufahamika mtu wa karibu wa mwanadada huyo  lakini kadri siku inavyozidi kwenda mambo yanazidi kuwa mambo kwa sababu mapenzi ni kama kikohozi huwa hayajifichi kabisa.

Katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanadada huyo, Star huyo aliandika na kuweka picha yake kwa ajili ya kumatakia kheri ya siku hiyo ya kuzaliwa kwake.