Batuli Afungukia Ukimya Wake Bongo Movie

Msanii wa filamu za kibongo, Yobnesh Yusuf maarufu kwa Jina la usanii kama Batuli amefunguka na kuweka wazi sababu za kukaa kimya kwa muda mrefu.

Batulia amefunguka na kudai kuwa kukaa kwake kimya na kutosikika mara kwa mara hasa Kwenye skendo za mitandao ya kijamii kutawapa hamu mashabiki zake za kuona filamu zake na kumtunzia heshima.

Kwenye mahojiano yake na gazeti la  Ijumaa Wikienda, Batuli alisema alikaa kimya kwa muda mrefu kwa sababu kuna vitu alikuwa anaviweka sawa kisha arudi tena kwenye ulingo wa filamu na anashukuru Mungu amevikamilisha.

Kutoonekana mara kwa mara kumeniletea heshima hata kwa mashabiki wangu. Kuonekana kila wakati inasababisha watu wanakuchoka, ni bora ukae kimya, ukiwa na kitu ndiyo unaibuka tena na ndivyo wanavyofanya hata wenzetu wa nje”.

Wasanii wengi wa Bongo movie wamekuwa wako takes kwa kutawala vichwa vya habari kwa skendo zao kuliko kazi zao.

Batuli: Nitairudishia Heshima Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie Yobnesh Yusuf maarufu kama Batuli amefungka na kusema ana mipango ya kuirudisha tasnia hii ya Bongo movie kwenye chati.

Kiuweli kabisa Bongo movie imepoa sana kwani ni tofauti na miaka mitano nyuma ambapo kila mtu alikuwa anatazama filamu za Bongo movie lakini hivi sasa hakuna kitu.

Lakini Batuli amekiri kuwa pamoja na Tasnia ya Bongo movie kupoteza muelekea yupo tayari Kupiga na kufanya na kupona kwa ajili ya kuifufua na kuhakikisha anaitudisha pale ilipokuwepo kwenye chati.

Batuli amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambapo amekiri Bongo movie imepoteza mwelekeo kutokana na kazi mbovu walizokuwa wanazitoq ambazo hazikuwa na viwango sahihi na baada ya kufanya uchunguzi wamejipanga kuwaletea Watanzania kazi bora kabisa.

Filamu au tamthiliya ni biashara kama zilivyo nyingine na biashara yoyote lazima uangalie soko linataka nini kwa sababu wakati tulionao sasa ni tofauti na ule wa zamani, mashabiki wanataka kazi bora na siyo uchafu kwenye runinga zao hivyo nitarudisha heshima ya Bongo Muvi kutokana na kazi ninazokuja nazo”.

Kumekuwa na jitihada nyingi za wasanii mbali mbali wa Bongo movie kuongea kuhusiana na mipango ya kuhakikisha Bongo movie inarudi pale ilipokuwepo na mashabiki pia ni muhimu kutoa sapoti kwa kazi nzuri.

Batuli Afunguka Kuwa Wanaorusha Picha za Utupu Mtandaoni Sio Wasanii

Muigizaji na msanii wa Bongo movie Batuli the actress amefunguka na kudai kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni wasanii wanaokaa uchi Mara nyingi wanakuwa sio wasanii bali watu waliojipatia umaarufu kwa njia hiyo ya kukaa uchi mtandaoni.

Siku chache zilizopita Naibu waziri wa Habari Juliana Shonza aliuwasha moto baada ya kukemea wasanii kuvaa mavazi ya nusu uchi mtandaoni ambapo alimtaja msanii kama Pretty Kind ambaye alijulikana kwa kuvaa uchi kwenye mitandao ya kijamii ambapo aliishia kufungiwa kufanya sanaa yoyote kwa muda wa miezi sita.

Lakini msanii mwingine aliyeingia kwenye maji ya moto ni Gigy Money ambapo alitakiwa kuripoti Basata kwa mavazi yake ya nusu uchi lakini pia wimbo wake wa Nampa papa uliosemekana kukosa maadili.

Batuli amefunguka kwenye ukurasa wake Instagram na kudai kuwa tasnia ya filamu na muziki inachafuliwa na watu wanaojifanya kuwa wao ni wasanii wakati sio wasanii.

Asilimia kubwa ya wanaotupia picha chafu kwenye mitandao ya kijamii hawapo kwenye makundi haya mawili muziki na filamu umaarufu wao wameupata kwa kupiga picha za utupu na kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii na watanzania wasio kuwa na maadili kuwapokea kwa shangwe #Sanaa ipewe heshima yake”.

Wasanii wengi kama Gigy Money na Pretty Kind walianzia umaarufu wao kwa kurusha picha za utupu mtandaoni na baada walijiingiza kwenye sanaa ya muziki.

Bifu Jipya Laibuka Kati ya Wema Sepetu na Batuli

Waigizaji wa Bongo movie nchini Wema Sepetu na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ waliowahi kuwa marafiki wazuri hapo zamani na kisha kutibuana kisa fedha za kampeni za CCM walizopiga kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, wameibuka tena na bifu hilo jipya.

Warembo hao waliokuwa na ukaribu na urafiki uliopitiliza hadi kufikia hatua ya kuvaa nguo sare urafiki wao uliingiwa na dosari mapema mwaka huu na kupelekea urafiki huo kuvunjika. Lakini toka wamemaliza urafiki huo kumekuwa na maneno ya chini chini ambayo wamekuwa wakirushiana.

Batuli aliyekuwa kimya kidogo kwa miezi hii aliibuka na kusema kuwa Wema Sepetu hawezi kutamba kwenye filamu pasipo kuwepo marehemu Kanumba. Batuli ameyasema hayo mara baada tu ya Wema kuachia filamu yake mpya inayoitwa ‘Heaven sent’ aliyoifanya na mwigizaji mwenzake Gabo. Wema aliyeingizwa na kwenye sanaa na marehemu Kanumba na kutoanaye  filamu kadhaa zilizofanya vizuri sokoni.

Wema ni moja kati ya supastaa anayeongoza kwa kubadilisha marafiki kwani amekuwa na urafiki na wasanii wengi kama Kajala ambaye aligombana naye baada ya Kajala kumuibia Wema mwanaume, Kuna Auntyezekiel ambaye urafiki wao uliisha baada ya Aunty kuanzisha urafiki na Zari ambaye ni hasimu wa Wema na rafiki yake wa mwishoni alikuwa Munalove lakini naye pia walitifuana baada kumkamata uchawi na kumtuhumu kuwa alikuwa anamuonea wivu.