Ben Pol aweka wazi kwa nini hataki kuongelelea maisha yake ya kibinafsi kwa sasa

Muimbaji wa bongo, Ben Pol amefunguka kudai kuwa kwa sasa hataki watu wamuulize kuhusu maisha yake ya kibinafsi wala mahusiano yake, Ebitoke na mtoto.

Hii ni kwa sababu ya kazi anayoifanya kwa sasa. Akizungumza kwenye mahojiano, Ben Pol alisema;

“Kwa series ya kazi zangu zinazokuja ningependa sana vitu binafsi nisiviongelee zaidi au hadi pale nitakapokuwa tayari kuzungumzia Ben Pol anafanya nini sasa hivi nianze kuzungumzia,”

Akaendelea kwa kusema;

“kwa hiyo sipo comfortable sana kusema vitu binafsi mahusiano, sijui mtoto nataka kupunguza kuvizungumzia hivyo vitu kwa sasa hivi kusema kweli,”

 

Ben Pol aeleza sababu mahusiano yake huwa hayadumu

Msanii mkali wa Bongo Ben Pol ni mmoja wa wanaume ambao mashabiki hutamani. Yeye ni mwanaume ambaye anajitambua ila kulingana na yeye mahusiano yake huwa hayadumu.

Ben Pol alifunguka kwa mara ya kwanza kudai kuwa mahusiano yake ambayo yalidumu sana ni pale ambapo alikaa na mwanamke kwa miezi 9 lakini wakaachana.

Kulingana na yeye warembo wengi huja na matarajio ambayo yeye hawezi fikia. Ben Pol ameiambia Choice FM.

“Miezi tisa ndio longest relationship kwa sababu unajua yaani nimekutana na watu wa aina tofauti, watu ambao wanaokuwa na expectation kubwa zaidi kuhusu mtu flani, kwa hiyo akiingia kwenye maisha yako anakuwa ana vitu tayari ali-picture kwamba Ben Pol tutakuwa tunakula bata every weekend, tunakula bata milioni, tunaenda huku na kule. Kwa hiyo mtu anaingia kwenye maisha yako anakuta si mtu wa hivyo ni staa ndio lakini we don’t go to club mara kwa mara, we don’t do this, we don’t do that, kwa hiyo mtu anakuwa disappointed anatoka kwenye mahusiano ndio hicho nime-experience zaidi kwenye mahusiano yangu yaliyopita,”

Barakah the Prince amjibu Ben Pol baada ya kudai walimpunguza kwenye show

Msanii kutoka Tanzania Barakah the Prince amefunguka kwa mara ya kwanza kumjibu Ben Pol ambaye alidai hivi karibuni kuwa msanii huyu alipunguzwa kwenye show ambayo alitakiwa kutokea na wasanii wenzake Kama Juma Jux.

Akizungumza kwenye interview mpya na kipindi cha XXL cha Clouds FM Barakah alisema kuwa wake Ben Pol alichozumgumzia kwenye interview yake ni uongo, huku alisema;


“Mimi sipunguzwi, nilijitoa nikawaambia nina menejiment ambayo ina utaratibu wake, ninapofanya kazi lazima kuwe na makubaliano na mkataba kwa sababu wao walishindwa kufuata utartibu nikajitoa kwenye hiyo show yao.”

Aliendelea kwa kusema,

“Hatukuwa na muungano wowote kusema kwamba tulikuwa na tour, tulifanya show moja tu ile, show iliyofuata uongozi wangu ukataka utaratibu wa hizo show waliposhindwa nikawaambia mimi sitaweza kufanya. Sema nyimbo yake ni mbaya asitafute sababu ya kujitetetea… utovu wa nidhamu yule (Ben Pol) baba yangu?”

Ben Pol amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu picha zake za uchi mitandaoni

Ben Pol ambaye aliachia picha kadhaa akionekana uchi amefunguka kwa Mara ya kwanza kuelezea kilichomkuta ili kufanya jambo kama hili.

Kupitia kwa mtandao wake wa Instagram Ben Pol aliweza kuweka video mpya ambayo aliambatanisha na wimbo wake mpya utakao achiliwa hivi karibuni na kuandika, “Usi-judge kitabu kama hujakisoma ndani ?.”

Japo hajakuwa akiwajibu mashabiki wake, inaonekana kuwa Ben Pol ameamua kuchukua mpya ambayo kwa hivi sasa inampa kiki ya kutosha.