Wanawake na Wanaume Siku Hizi Wote Miyeyusho tu :-Billnass

Mwanamuziki Billnass amefunguka na kutoa falsafa yake anayojua kuhusu wanawake na wanaume huku akisema kuwa kumekuwa na tabia kuwa ukikaa ukaongea na mwanamke atakuwa kila wakati akimlalamikia mwanaume kuwa ni miyeyusho, lakini ndivyo inavyokuwa hata kwa wanaume unapokaa kuwauliza kuhusu wanawake wanakwambia wao ndio miyeyusho.

Hata hivyo baada yakusema hivyo, Billnass anakuja na kumalizia kuwa basi kama owte wamekuwa wakisema kwa upande wao basi wanawake na wanaume wote lao moja tu ingawa kila mmoja anavutia upande wake.

ukituuliza wanaume kuhusu mapenzi tutakwambai wanawaek ndio miyeyesho, na ukiwauliza wanawake kuhusu mapenzi watakwambia kuwa wanaume ndio miyeyusho, ila kitu ambacho ukijua ni kuwa wanawake wanafanya miyeyusho yao na wanaume wanafanya miyeyusho yao, hivyo owte ni miyeyusho.

Billnass na Whozu Kuja na Kundi Lao la Muziki.

Wasanii Billnass na Whozu wanaweza kujikuta wakiunda kundi kubwa nazuri la muziki hasa baada ya kufanya kazi pamoja iliyofanya vizuri na kuamini kuwa wanaweza kufanya kazi pamoja na kuwafurahisha mashabiki.

Wasanii hao waliotoa wimo hivi karibuni uaojulikana kama kwa leo, wanweza kuuunda kundi kwa mujibu wa billnass aliyekuwa akiongea na waandishi wa habari.Billnass anasema kuwa maneno hayo yanakuja baada ya kukaa na whozu kwa muda sasa na kugundua kuwa whozu ana kitu kikubwa cha muziki ndani yake.

‘Bado mapema sana kuzngumzia swala hilo la kuungana kama kundi kwa sababu ni kitu ambacho kinawezekan kibiashara hakuna kinachotuzuia”

Akiongelea pia picha zinazosamba katika mitandao wakiwa yeye na Barnaba na Dogo janja, Billnass anasema kuwa hakuna ujio wa project yoyote isipokuwa wamekuwa wakikutana sehemu mbalimbali zinazowakutananisha kikazi na ndio maana wameuwa pamoja na hata kukaa pamoja ni baada ya kujiona kuwa wamekuwa na interest zinazofananamuda mwingine.

Alichoongea Billnass Kuhusu Msimamo Wake Kwenye Ndoa.

Msanii wa bongo fleva Billnass amefunguka na kusema kuwa msimamo wake kuhusu ndoa ni kuwa kama wale wanaotoa michang kwa ajili ya kufanikisha harusi wangekuwa wanafatilia sana michango yao na kama harusi inavunjika basi watu hao wanaonjiwa basi isingetokea ndoa kuvunjika hata siku moja lakini kwa sababu ya kuzembea na ndio maana ndoa zinavunjika sana.

Katika ukurasa wake wa twitter, billnass aliandika “NDOA NYINGI ZA SIKU HIZI HAZIDUMU KWA SABABUWATU HAWANA HURUMA NA MICHANGO YETU, INGEKUEPO SHERIA KUWA MAHARUSI WAKIACHANA BIBI HARUSI AOLEWE NA ALIYETOA MCHANGO MKUBWA, NDOA ZINGEDUMU, ..akili za usiku.”

Billnass amekuwa siku zote akiandika baadhi ya mambo ya kijamii kwa njia ya utani lakini mwisho wa siku anakuwa akifikisha ujumbe kwa jamii anayoizunguka.

Billnass Alia na Mafisadi wa Mitandaoni.

Mwanamuziki Billnass ameonyeshwa kusikitika kwake na tabia ya baadhi ya watu wanaoharibu muziki wa nchini kwa kuwahujumu katika mitandao, hayo yamekuja baada ya billnass kuachia ngoma yake mabayo kwa upande wake anasema kwamba hakuwa hata na masaa mengi katika mtandao wa you tube lakini kitu cha ajabu ni baada ya ngoma hiyo kufutwa kabia katika mtandao huo.

Billnass ambae ametoa wimbo wa LABDA hivi karibuni na ulikuwa umeanza kupendwa na mashabiki anasema kwamba umefutwa katika akaunti ya you tube na kumfanya akose amani na imani na muziki wa tanzania.

Bilnass amabe anasema kuwa hakuwahi kufanya kazi ya muziki kwa mashindani na amekuwa akisapoti kazi za wengne inamuuma  sana anapoona kuwa watu wamekaa kwa ajili  kuangamiza soko la muziki.

kitendo cha video yangu ku0hackiwa na kufutwa you tube kimeniuzi sana,video yangu hata haikuwa na umri wa masaa mengi na viewers wenyewe wala sio wengi kiivyo , ndio imeanza kuingia katika trending lakini watu wenye roho mbaya wamefanya hivyo.sijawahi kufanya muziki kwa mashindano namuda wote nimekuwa nikifanya kazi za wenzangu  na pia nimekuwa nikitoa nyimbo kwa muda mrefu sana nikiamini kiloa mtu ana muda wake …nafanya kazi ya kujikwamua na umasikini wangu na kukuza karama yangu aliyonipa mwenyezi Mungu ,…sidhani kama roho kama hizi zinzweza kukuza tasnia…imeniumiza sana , imetisha sana kama muziki wetu umefikia huku.

Billnas -“Nandy Ana Sifa Zaidi Ya 60% Za Mwanamke Wa Kuoa”

Ikiwa ni  muda sasa tangu kuwepo kwa  tetesi za wasanii wa Bongo Fleva Nandy na Billnass kusemekana kuwa wapo katika mahusiano ya kimapenzi, Billnass nae ameamua kusema yaliyopo moyoni kuhusu mrembo huyo ambae amekuwa akifanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva.

Msanii huyo wa kiume alipokuwa katika mahojiano na BongoSwaggz alisema kuwa katika mipango yake ya kimaisha kwa sasa bado hana mpango wa kuoa ingawa atategemea kuoa hapo baadae, lakini bado alisema kuwa hata muda wa yeye kuoa ukifika bado kuna vigezo ambavyo anavizingatia hivyo muda ukifika laziamataangalia vile vigezo vya kumfanya aoe.

Billnass ambae amekuwa akifanya vizuri katika game la muziki kwa muda mrefu sasa huku nyimbo zake nyimbo zake karibia zote zikipokelewa vizuri na mashabiki,kwa sasa Billnass anatamba na vibao vyake vya  ‘mazoea’ na ‘sina jambo’ ambayo imetolewa hivi karibuni.”sijakaa nikafikiria  kwa sababu na mimi nina vigezo vyangu  ambavyo nataka , najua namtaka  .Najua namtaka mwanamke wa aina gani .Kwanza swala la kuoa kwangu linapita mbali,sio kwamba ninafikiria sana” ameongea Bilinass

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu msanii  mwenzie wa kike wa Bongo Fleva  ambae kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa wapo katika mahusiano naye na wamekuwa wakionekana baadhi ya sehemu pamoja msanii Billnass anasema kuwa Nandy ni mmoja wa wanawake anaowapa zaidi ya 60% kwamba anasifa na vigezo ambae yeye anavihitaji  kwa mwanamke wa kuoa.

Nandy ni mwanadada ambae anafanya vizuri sana kwa sasa katika game akiwa ni msanii chipukizi aliechukua nafasi kubwa sana hasa mwaka 2016, lakini bado anaendelea kufanya vizuri kutokana na nyimbo zake kupendwa na mashabiki pia,Nandy kwa muda sasa amekuwa  akifanya vizuri na nyimbo zake kama ‘nagusagusa’ , ‘one day ‘na huo mpya wa ‘wasikudanganye’,pia amepata bahati ya kuwepo katika tamasha la Cokestudio kwa mwaka 2017.Lakini pia Nandy ni mjasiriamali ambae ana Lebel yake ya ushonaji wa nguo inayojulikana kama Nandy African Print. Kwa sifa za kujituma na kufanya kazi inawezekani ndipo aslimia 60 ya billnass inapokuja kwa nandy.