Wasanii Wakubwa Bongo Wanaosikilizwa Sana Nchini Kenya.

Wapo wasanii wanaofanya vizuri sana bongo na kazi zao imekuwa zikionekana mpaka nje ya nchi.wapo wanaoendelea kufanya vizuri ili kukuza muziki huona kuufanya upendwe nje ya nchi.Msanii mkongwe kutoka Kenya amewataja wasanii wakubwa tanzania ambao wamekuwa wakisikilizwa sana katika radio na kila mkona nchini kwao Kenya.

Diamond Platinumz.

Diamond ni msanii mkubwa na mwenye kujituma sana.ukiachana drama na skendo nyingi anazokumbana nazo Diamond lakini ni msanii ambae kwa kipindi cha muda mfupi aliweza kupata mafanikio makubwa na kuweza kusaidia wengine kimuziki.kwake yeye mafanikio yake na ya wengine kumuziki ndio kipaumbele kuliko kitu kingine chochote.

Ali kiba.

Amekuja ni mmoja wa wasanii wanaopendwa sana kwa manjonjo na sauti yake anapokuwa jukwani.alikiba ni msanii anaependwa sana na wakina dada kutokana na mvuto alionao.Alikiba amekuwa ni moja ya wasanii wakubwa tanzania kwa miaka mingi tangu aanze muziki.yeye ni moja ya wasanii wakongwe wasiochuja Afrika Mashariki.

Vannesa Mdee

Ukiongelea wasanii wa kike wakubwa waliopata mafanikio kwa  juhudi zao yeye ni namba moja.vannesa amekuwa msichana hasikuwa na aibu katika kusimama na kuitetea kazi yake.siku zote amekuwa ni mtu wa kuthubutu kufanya jambo lolote lifanikiwe.Hajawahi kukata tamaa lakin i pia amekuwa anajituma ili kuendeleza muziki wake.Sasa hivi ameta album yake na amekuwa akizunguka nchi mbalimbali kwa ajili ya kusambaza nyimbo zake.

Wasanii wengine aliowataja ni pamoja na Ben Pol, Chegge na Chin Beez.

 

Wanaonyoa Kiduku Kusakwa na Polisi,Je hii Itahusu Wasanii.

Ilianza kwa kuwafungua wasanii hasa wa kike wanaovaa vibaya ili kulinda maadili ya taifa na wale wote wanaochapisha picha za utupu mitandaoni.zoezi limegeukia upande wa pili na sasa ni watu wote wanaonyoa mtindo unaojulikana kama kiduku ambao mtu hunyoa nywele za pembenina kuacha zilizopo katikati.

katika moja ya magezo yanayotoka kila siku, gazeti la nipashe ya leo imeweka habari kuwa mapolisi jijini dar es salaam wameanza kamata kamata ya vijana wote wanaonyoa style ya nywele inayojulikana kama kiduku na kuweka ndani mara moja.Msako huu utawahusu watu waote wanaonyoa hivyo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa kutunza na kulinda maadili ya Taifa.Baada ya kufanya uchunguzi gazeti hilo limebaini kuwa vijana hao wanakamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kuvunja maadili ya kitanzania.

swala la kujiuliza ni kwamba je kamata kamata hii inahusu vijana wa mitanai tu au hata wasanii wengi ambao sasa hivi style hii ya nywele imeshakuwa ni kama ya kawaida kwao.Na kama ukamataji huu unamhusu kila kijana mtanzania basi kamata kamata hii itakuwa inawahusu wasanii wengi wakubwa na wadogo wakiwemo Diamond Platinumz.

Ingawa bado haijabainika tamko la kukamtwa kwa vijana wanaonyoa viduku limetoka wapi lakini,lengo kubwa ni kulinda maadili ya TaIfa ingawa pia watu wengi katika mitandao wameonyeshwa kukerwa na ukamataji huo wa vijana.

 

Honeymoon Amuandikia Barua Mh.Juliana Shonza Kuhusu Maadili ya Wasanii

Mtanzania anayeishi Marekani , ambae pia ni  mtengenezaji wa filamu nchini humo, anaejulikana kwa jina la Honeymoon Aljabir ameandika barua ndefu kwa Naibu Waziri wa Habari na Michezo kuhusu kitendo alichokifanya kuhusu kuwafungia wasanii ambao wanavaa utupu na kuchafua maadili.

Honeymoon ambae inasemekana ni dada yake na mwanadada Faiza Ally, ametengeneza filamu kama   Forgotten hero,The king without a crown, na Daddy’s wedding aliigiza monalisa.

Amemshukuru sana Naibu Waziri kwa kuteuliwa na anaamini kuwa ataisaida sana sanaa ya tanzania kukua  na takuwa mstari wa mble katika kusaidia wanawake wenzie katika sanaa.

furaha kwangu ni kwamba mwanamama mwenzangu umechanguliwa utaweza kutusaidia sana wanawake wenzio  katika sanaa ambayo hasa inamilikiwa na wanaume.

Hata hivyo Honeymoon amesema kuwa anashangaa sana kuona kuwa badala  kusaidia wenzake katika  sanaa, ameanza kwa kuwakomoa wasanii wa kike kwa  kuwafungia na kuwakataza bila kujali maslahi yao.hata hivyo mwanadada huyo ameishia kuhoji kuwa kama anataka watu wasivae nguo za kuua maadili , je kabla ya kuja kwa wazungu asili ya mwafika ilikuwa ni nini kama sio kukaa uchi kabisa.

Honeymoon,ameendelea kuhoji kwa nini kuataza kuuliwa kwa maadili kwa wasanii kumejikita zaidi katika kuwakataza wasanii wa kike tu na sio wasanii wa kiume huku akimtolea mfano Idris Sultani ambe hivi karibuni alipiga picha za kutangaza nguo za ndani za Calvin Klein.

By the way malengo yako  ni kwa wasanii wa kike,idrisa amepiga picha za  chupi akini mbona hamjamfungia,na kama kweli una nia nzuri kwanini usichunguze unyanyasaji wa kijinsia ambao wanapitia wasanii wa kike.

Honeymoon anaonyesha hisia zake za huzuni kwa kitendo cha naibu waziri kumfungia gigy money ambae kwa sasa ni mjamzito na anahitaji kufanya kazi ili kupata kipato kitakachomsaidia klea mimba lakini pia kwa mtoto wake anaekuja.

Fikiria huyo mtoto wa kike mjamzito ambae umemfungia , unataka mtoto wake aishi vipi,kama kwlei wewe ni mwanamke unataka kulinda heshima ya wasanii kwanini usitafute wanaojiuza.

Maneno ya mtayarishaji huyo wa filamu yanakuja baada ya msako wa kuwatafuta wasanii ambao wanaharibu maadili ya kitanzania kwa kutupia picha za uchi katika mitandao.

Matukio Makubwa Yaliyotikisa Mwaka 2017, Upande Wa Burudani.

Kila kitu kina historia Duniani, pia kwa upande wa burudani Tanzania kuna matukio makubwa yaliyotokea ambayo utakapo wauliza wahusiaka lazima watakwambia kuwa hawawezi kusahau swala hilo.

Lulu Kufungwa Jela.

Mnamo tarehe 13 November, mwanadada mrembo kutoka bongo movies, alipokea kifungo chake cha kutumikia miaka miwili gerezani baaba ya kukutwa na hatia ya kuuua bila kukusudia.Kesi hiyo ya mauaji ilitokea mwak 2012 baada ya Lulu na aliyekuwa mpenzi wake Kanumba kugombana na kusababisha umauti wa mwanaume huyo.

Tukio ilo lilitikisa Tanzania nzima hasa wapenzi wa sanaa , kwa sababu wengi walikuwa wakimpenda Lulu na kazi zake pia.

 

Kutekwa Kwa Roma  na Wenzake.

usiku wa april 26, wasanii wawili roma mkatoliki na moni centrozone walitekwa na kwenda kusikojulikana huku kukiwa na kigugumizi cha kutokujua wapi walipokuwa.baada ya kupotea kwa wasanii hao wasanii wengi waliungana kwa pamoja na kuanzisha kampeni ya ‘Free Roma’ ili kumsaidia mkewe na familia kujua wapi alipo.

kama baada ya siku 3, roma na wenzake waliachi wa huru na watekaji hao huku wakiwa na majeraha mengi katika miili yao, cha ajabu na kushangaza hakuna anaejua siri ya kutekwa kwao mpaka sasa kwa sababu msanii huyo hakutaka kulizungumzia hilo.

Babu Seya   na Papi Kocha kutoka gerezanai.

Tarehe 9 Desemba mwaka huu Rais Magufuli aliweka tena historia kwa kitendo cha kuwatoa na kuwapa uhuru  wasanii wakongwe Babu Seya na Papi Kocha, hii ilikuwa ndoto ya wasanii na wananchi wengi kutokana na maombi ya wasanii hao kutoka.Tarehe hiyo ilikuwa ni moja ya siku kubwa na yenye furaha sana kwa watanzania wengi sana baada ya wasanii hao wakongwe kutoka.

Hamisa kuzaa na diamond Platinumz

Timbwili lilianza pale ambapoa hamisa alianza kusema kuwa ana mahusiano na msanii mkubwa Tanzania Diamond Platinumz ambapo Diamond alikana taarifa hizo lakini baadae Hamisa alijulikana kuwa ni mjamzito na kufanya watu kaamini kitendo hicho lakini kwa Diamond mwenyewe ilikuwa tofauti kwa sababu alikana katika vyombo vya habari na kusema mimba ya Hamisa sio ya kwake.Hamisa aliamau kuvujisha picha za mahusiano yake na Diamond na kufanya mtandao wa instagram kuzizima na hatimaye Diamond aliamua kuweka wazi na kukubali taarifa hizo katika vyombo vya habari na kuiomba radhi familia yake.

Wasanii na kashfa za madawa ya kulevya

Mh.Makonda  aliibuka na kuanza kupiga vita ya madawa ya kulevya ambapo wasanii wengi walizolewa na kusweka Lumande .Hakuna aliyetegema kuwa wasanii wakubwa na wanaopendwa wanaweza kuwa katika list ya watumiaji wa madawa ya kulevya.Wasanii kama Wema Sepetu, TID, Vannesa Mdee, Mr Blue, Lulu Diva,Tunda na Rommy Jones.Ambapo baada ya kesi na mahojiano, Agness Masogange walikutwa na hatia na mpaka sasa kesi zao ziko mahakamani.

Swala la Wema  Sepetu na vyama vya siasa.

tarehe 24 february wema sepetu aliahama kutoka CCM kwenda CHADEMA, hii ni moja ya headline kubwa katika vyombo vya habari kwa mwaka huu.hii ilitokea siku chache baada ya wema kutajwa kuwa katika list ya wasanii waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya.

Lakini tena Deseba 1 , mwaka huu huu tena wema sepetu alitangaza kuhamia kutoka CHADEMA na kurudi tena CCM.

Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja

Hii i moja ya mambo yaliyowaacha watu maneno ya kuongea sana katika mitandao ya kijamii, irene uwoya na Dogo janja walifunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu.Watu wengi walishangaa kutokana na umri wa Dogo Janja kuwa mdogo zaidi ya mwanamke aliyemuoa.

Penzi la Jux na Vannesa Mdee.

Vannesa Mdee na Jux waliingia katika trending ya mitandaoni mwaka huu baada ya kuwa moja ya couple nzuri na pendwa Tanzania kwa upande wa wasanii, lakini baadae hakuna sababu iliyokuwa wazi ambayo ilisababisha wawili hao kuachana, mashabiki wao walipiga kelele sna na kutaka warudiane.Tamasha kubwa la FIESTA linalozunguka karibia kila mikoa liliwafanya wawili hao kurudiana na kuendelea na mapenzi yao mwishoni mwa mwezi November.

 

 

 

 

Ndoa 5 Za Mastaa Zilizo-kiki Kwa Mwaka 2017

Mwaka 2017 umekuwa mwaka wa kila jambo na matukio mbali mbali kwa mastaa wetu wa Bongo mojawapo kati ya matukio yaliyochukua nafasi ya kutrend sana ni ndoa za mastaa mbali mbali.

Ndoa zilizo fungwa na mastaa mbali mbali zilitawala nakushika headlines na leo tutaangalia Ndoa tano za mastaa zilizotrend sana mitandaoni na hata mitaani ambazo kila mtu alikuwa anaziongelea.

1. Shilole na Uchebe

Ndoa ya Shilole na Uchebe ilikuwa ndoa yenye utata sana ambao ulianzia kwenye familia kwani habari zinadai kuwa familia ya Shiloke haikutaka aolewe na Uchebe hadi kufikia hatua ya kupelekana polisi na hadi siku ya harusi ilifanywa kwa siri na kuhudhuriwa na watu kumi.

2. Rommy Jones na Kay Jord

Ndoa hii ilikiki kwa staili ya kipekee kwani bwana harusi ni kaka Wa mwanamuziki maarufu Diamond Platnumz kilichowavutia watu wengi ni Diamond na Zari kuwa wasimamizi lakini pia familia ya Diamond kutoa zawadi za mamilioni kwa maharusi.

3.Ndoa Ya  Proffesor Jay

Ndoa ya mbunfe wa Mikumi Proffesor Jay iliwavutiwa watu wengi keani ni harusi iliyowakutanisha Wasanii wakongwe wanasiasa na watu mbali mbali lakini pia ndoa hiyo ilisindikizwa na sherehe tatu.

4. Joti na Tumaini

Harusi ya Joti ilizungumziwa sana kwanza kwa sababu hakuna mtu aliyeamini Kama kweli anafunga ndoa watu wengi walijua ni utani tu au litakuwa tangazo lakini ilikuwa ni ndoa kweli na ilikiki sana.

5. Irene Uwoya na Dogo Janja

Hii ndio ndoa ambayo inaweza ikawa imefunika mwaka 2017 kwani ndoa hii ilizungumziwa sana kupita kiasi yote ikisababishwa na tofauti ya umri wa Dogo Janja na mrembo Uwoya.

 

Waliozoea Kuvaa Vichupi Sasa Basi,JPM Kula Nao Sahani Moja

Jana katika kikao cha wazazi CCM kilichofanyika mkoani Dodoma , Mh. Raisi Magufuli aliongea na wazazi kuhusu maadili ya wasanii hasa wa kike ambao wamekuwa wakivaa nguo fupi na kuwaacha miili yao wazi.Raisi Magufuli amesema kuwa amekuwa akishangazwa sana pale anapowasha tv na kuona wanaume wakiwa wamevaa vizuri lakini jinsia ya kike wakiwa uchi kabisa na ni kitu ambacho akimpendezi kabisa.

M. Raisi amesema kuwa anazitaka maamlaka husika hasa TCRA, kuwachukulia hatua wote ambao wamekuwa wakipiga picha za utupu  na kutupia katika mitandao ya kijamii na kama wanataka kukaa uchi basi wakae huku huko katika club lakini sio kuwka katika mitandao.

Mh Raisi alisema kuwa ni aibu kwa wazazi kuangalia katika televisheni watoto hasa wa kike wakiwa uchi na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na mamlaka husika.

Baadhi ya maadili yameanza kupotea na nyinyi wazazi , na mmeshindwa kuyakemea , unapofungulia muziki  ukitaka kuwaona wanaocheza utakuwa ni wanawake tu ndo wako uchi,lakini wanaume hapana baadhi ya wanawake wanaachia viungo vyao.

kwanini uwavulie hata wasiotaka kuoona huo uchi,tena kwa wakati ambao sio muafaka ,nyie kama jumuiya ya wazazi inafika wakati inapaswa  kuyakemea haya , tunaelekea wapi sasa?tunawafundisha nini watoto?kwani akicheza amevaa nguo hatafurahisha?

vyombo vyetu vya habari viko wapi, vyombo vinavyosiamamia hayao wako wapi,je TCRA ambao wana mamlaka ya kufungia hata vyombo vya habari ambavyo vinarusha video za utupu iko wapi?

Ujumbe huu wa mh raisi unaenda moja kwa moja kwa wasanii wengi tanzania hasa wa kike ambao wamekuwa na tabia hii ya kuvaa nguo zinazoonyesha utupu wao, Gigy Money, Sanchoka,Amber Lulu, Pretty kindy , Kidoa na wengine wengi.

Fiesta Kuisha Saa Sita Itaathiri Ndoto Za Wasanii Wengi

Tamasha la Fiesta inasemekana kuwa ni moja ya tamasha kubwa nchini na ikiwezekana hata ikawa ndio tamasha kubwa afrika kufanyika kwa kutembea mikoa karibia nchini nzima.tamasha ilo lililoanza mnamo mwezi september, lilitembea zaidi ya mikoa 15 na fainali ya tamasha ilo limepangwa kufanyika tareh 25 Novemba  mkoa Dar Es  Salaam.

Hata hivyo tamasha ili linaweza kuwa tofauti na vile ambavyo watu wengi wamekuwa wakizoea linavyokuwa katika miaka yote kwa sababu , kwa kawaida show ya tamasha ilo uisha alfajiri lakini kutokana na tamko la mhshimu  mkuu wa mkoa husika anasema kuwa kwa mkoa wa Dar Es Salam starehe na matamasha katika sehemu za wazi mwisho wake huwa ni saa sita husika , hivyo basi hata tamsha ilo litalazimika kusiha saa sita husika kama sheria inavyosema.

Akiongea na vyombo vya habari, mkurugenzi wa Clouds Medai ambae pia ndie muhandaaji wa tamasha ilo Ruge Mutahaba anasema kuwa wamepokea tarifa hizo na kama sheria inavyosema hivyo hawawezi kupingana na sheria kwaio tamasha kweli litaishia saa siata lakini kama uongozi inawabidi kupunguza  idadi ya wasanii watakao perfom katika tamsaha ilo ili kufukia muda uliopangwa.Akiendelea kuongelea hilo anasema kuwa bado hata hivyo wanaendelea kufanya utaratibu wa kupata kibali cha kuongeza muda li kuweza kupata list ndefu ya wasanii ili waweze kuwaridhisha mashabiki lakini pia hii ni moja ya njia nyingi zinazowaongizia kipato wasanii na kuwaongezea fanbase.

Swala la kufika saa sita kama ndio utaratibu na sheria iliyowekwa basi  tuko tayari, tumeshajiandaa kwa sababu tunajua  na tutabadilisha ratiba, ila kwa bahati mbaya tu ni kwamba  inabidi tupunguze baadhi yawasanii , lakini bado tunafanya utaratibu ili kupata kibali ili tuweze kuongeza muda kwa sabau huwa kuna kibali maarum cha kufanya tamasha kama ilo.-Aliongea Ruge Mutahaba

Hivyo basi kwa wasanii ambao bado walikuwa wakichipukia na wamekuwa na hamu kubwa ya kuonyesha vipaji vyao katika tamsha ilo itakuwa ni moja ya kukatika kwa ndoto zao kwa sababu katika list ya wasanii watakao onyesha umahiri wao itawalazimu kuondoa wasanii wengi zaidi.

 

Kidoa Amtetea Hamisa Mobeto Mitandaoni

Moja ya wauza nyago wanaofanya vizuri kwa sasa katika video za wasanii bongo  Ssha salumu mwenye jina la umaarufu kama Kidoa amefunguka na kumtetea mwanamitindo na video queen Hamisa Mobeto kwa wasanii wengine wa kike ambao wamekuwa wakimsema na kumsimanga kutokaa na nyingi  skendo   anazopitia hasa hili kubwa la kuzaa na msanii mkubwa Diamond Platinumz na mambo yote yanayoendelea kuhusu kesi iliyokuwa imepelekwa mahakamani kuhusu malezi ya mtoto huyo.

Mwanadada huyo anasema kuwa anakuwa anachukizwa na kuumiza na baadhi ya wasanii wenzie wa kike ambao kutwa kukaaa katika mitandao na kuwa wanamsema Hamisa bila kujua ni kitu gani mwenzao anapitia katika kipindi hiki kigumu na badala yake walitakiwa wamsaidia na kumpa sapoti ya ushauri na sio kumsema kila kukicha katika mitandao ya kijamii.

Kidoa ambae alishinda taji la  Ijumaa Sexiest Girl kwa mwaka 2015 anasema kuwa kinachomshangaza ni jinsi wadada wamekuwa wakimsaidia Zari katika kumkandamiza Hamisa bila kujua kuwa maneno yao yanamwathiri mwanadada huyo kisaikolojia ukizingtia ni mbongo mwenzao.

Sio sawa wasanii wenzangu wanavyokaa wakimnyanyapaa hamisa hata kidogo, kutwa kumoiga vijembe wanatakiwa kukaa wakikumbuka kuwa hakuna ajuae kesha yake ,huenda  hata yeye mwenyewe hakuwaza kama yanaweza kumfika hayo yote. -Alisema Kidoa

Hamisa amekuwa ni moja ya wanadada gumzo katika mtandao kwa kipindi cha takribani miezi mitatu sasa tangu mtoto wake wa pili kuzaliwa na hii yote ni kutokana na kujulikana kwa baba wa mtoto kuwa ni wa Diamond Platinumz ambae tayari anafamilia nyingine yenye watoto wawili na Zari The Bossy Lady mwanamama tajiri kutoka Uganda.Hata hivyo Hamisa amekuwa akitajwa karibia kila kona katika mitandao huku wengine wakimkashifu kwa kujitegesha na kufanya makusudi kuzaa na msanii huyo ili aweze kupata pesa

Mastaa Wazidi Kumlilia Lulu Baada Ya Kutupwa Jela Kwa Miaka Miwili

Asubuhi ya leo msanii wa Bongo movie, Elizabeth Lulu Michael amefungwa na mahakama kuu kifungo cha miaka minne jela.

Mastaa mbalimbali wa Bongo movie na Bongo fleva wamejitokeza ili kumfariji Lulu na familia yake katika kipindi hiki kigumu.

Hawa ndio mastaa kwa kupitia mtandao wa YouTube waliojitokeza kumpa moyo na kumfariji Lulu;

1. Diamond Platnumz

2. Wema Sepetu

3. Dr. Cheni

4. Irene Uwoya

5. Dogo Janja

6. shilole

7. Aunty Ezekiel

 

8. Linah Sanga

9. Shilole

.

Hawa Ndio Mastaa Wa Kike Wanaopenda Wanaume Wenye Umri Mdogo (Viben-10)

Moja kati ya vitu vilivyo zoeleka kwenye jamii zetu kwenye masuala ya mahusiano kati ya mwanaume na mwanamke ni umri, tumezoea siku zote kuwa ni lazima mwanamke awe na umri mdogo na kuliko mwanaume yaani mwanaume lazima awe na umri mkubwa kwenye mahusiano.

Kitokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia na ujio wa wazungu basi hilo limebadilika hivi sasa unaambiwa umri  sio kitu bali ni namba tu cha maana mapenzi tu baina ya wawili haijalishi una umri gani.

Hilo pia linatokea pia kwa mastaa wetu ambao wadada wengi sahivi wanapenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wadogo kiumri kwa sababu wanazozijua wao wanawake hao wanaitwa masugar mama na vijana wanaolelewa wanaitwa viben-10, serengetiboys au maryoo.

Hawa ni baadhi tu ya mastaa waliowahi kuwa na uhusiano wakimapenzi na wavulana wadogo au mpaka sasa bado wana uhusiano nao.

1. Wema Sepetu na Idris Sultan

Wema Kazaliwa Mwaka 1988 na Idris Kazaliwa Mwaka 1993

2. Zarinah na Diamond

Zari Kazaliwa Mwaka 1980 na Diamond Kazaliwa Mwaka 1989

3. Irene Uwoya na Dogo Janja

Uwoya Kazaliwa Mwaka 1988 na Do go Janja Kazaliwa Mwaka 1994

4. Shilole na Nuh Mziwanda

5. Nisha na Baraka Da Prince

6. Irene Uwoya na Msami Baby

7. Jacqueline Wolper na Brown

 

Je unahisi ni staa gani mwingine anafaa kuingia kwenye orodha hii?

Magari Ya Kifahari Yanayoendeshwa Na Mastaa Tanzania

Hii ni moja ya rekodi iliyotolewa kwa mwaka 2016-2017 kutoka Tanzania.Haya ni baadhi ya magari ya kifahari  yanayomilikiwa au yaliyowahi kumilikiwa na baadhi ya mastaa wa bongo.

1.Masoud Kipanya (Hummer H3)

Amepitia vitu vingi katika jamii, amekuwa akisaidia vijana kwa namna tofauti tofauti kadri vile anavyoweza.ukiachana na utangazaji kama kazi yake , Masoud ni mchoraji wa katuni maarufu Tanzania.

Ndiye mwanzilishi na muhasisi wa mashindano ya Maisha Plus Tanzania.

2.Masanja Mkandamizaji(BMW x6 na Toyota landcruiser)

Ni mchekeshaji maarufu, lakini pia ni mjasiriamali alijikita katika sekta ya kilimo. pia ni mtumishi wa Mungu

 3.Wema Sepetu(Range Rover e Vogue)

Mwanadada anependwa Tanzania, aliwahi kuwa miss tanzania laini kwa sasa ni muingizaji maarufu.Aliamua kijizawadia gari hili siku yake ya kumbukumbu ya kuazaliwa.

4.Quick Rocka(Range Rover Spot)

Amekuwa na mambo ya kimyakimya na hapendi kujionyesha sana, yuko vizuri katika muziki.

5.Gadner G Habash(Discovery 3)

Ni mtangazaji maarufu wa radio Tanzania, alishawahi kuwa mum wa mwanamuzii mkongwe Lady Jay Dee.

6.Alikiba BMW X5)

Anafanya vizuri kwenye game,ingawa ni msanii asiyependa sana kuonyesha nini anamiliki.

7.Diamond Platinumz(BMW X6)

Msanii wa bongo fleva anaefanya vizuri tanzania , pia ni mmoja kati wa wasnii matajiri Tanzania.

 

 

 

 

Bifu Za Wasanii Zinazoendelea Bongo Zinaua Muziki

Kumekuwa na mifarakano mingi inayoendelea katika tasnia ya muziki tanzania, mara nyingine ugomvi unaokuwa unatokea unaweza kusababishwa na kitu kidogo tu ambacho inawezekana wasanii wenyewe wangekaa bila kufuata hisia za mashabiki wasimgefikia hatua ya kugombana kwa muda mrefu, wapo wanaogombana kwa sababu ya mambo binafsi yasiyohusiana na muziki.Kwa mwaka 2016-2017 zimezuka bifu nyingi na zingine zikiendelea kuongezea kadri siku zinavyozidi kwenda.Na hizi ni baadhi ya bifu za wasanii kwa mwaka 2016-2017.

1.Alikiba na Diamond Platinumz

Hakuna anaeweza kukujibu chanzo cha ugomvi wao ambao kila kukicha unachukua sura  mpya, ni ugomvi mkubwa ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kuumaliza wangeweza kukusanya mashabiki wengi kwa pamoja.

2.Diamond na Ommy dimpoz

Ni moja kati ya watu walikuwa na umoja sana walipoanza muziki, baade walikuja kutengana.Lakini bifu lilizidi kuw akubwa baada ya ommy kuungana na alikiba katika kazi hivyo Ommy akaanza kuwa upande wa Alikiba.bifu hili limeingiza hadi watu wa familia ya Diamond na inasemekana kuna kesi mahakamani kutokana na ugomvi wa wasanii hawa.

3.Young Dee,Young killer na Dogo Janja

Bifu lilianza kiutani utani lakini likazidi kukua, wasanii hao wanaona kuwa kila mmoja ni bora zaidi ya mwingine,kila mmoja hataki kufananishwa na mwingine, lakini kama wasanii wadogo wanaofanya vizuri katika sanaa walitakiwa kuungana ili kuendelea kuongeza idadi ya mashabiki.

4.Bob Junior na Diamond Platinumz

Kumekuwa tu na malalmiko ya upande wa Bob Junior kuhusu wawili hao kutokuwa na ushirikiano, ingawa anasema kuna mengi yanaendelea hapo katikati ikiwemo la wao kushindwa kukaa pamoja na kutatua tofauti zao kutokana na Diamond kutokuwa tayari, Diamond amekuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu ili ingawa Bob Juniour ndie amekuwa akifunguka kila mara kuhusu Diamond.

5.Man Fongo na Sholo Mwamba

Bifu lilianza pale man fongo alipomtuhumu Sholo Mwamba kufiksha habari za umbea kuhusu Wema Sepetu, ni mambo flani binafsi ambayo yaliwezekana kutatuliwa kimya kimya.Singeli ni muziki unaoshikakwa kasi kwa sasa Tanzania hivyo wasanii hawa walipaswa kuwa ndugu ili kukuza muziki huu.

Fahamu Warembo Waliofanikiwa Zaidi Katika Nyanja Mbalimbali Tanzania

1.Jokate mwegelo

Safari yake ya mafanikio ilianza kwa kushiriki mashindano ya u-miss .Ni mrembo  mjasiriamali anayeingia katika kundi la watu waliofanikwa hasa kupitia kampuni yake ya Kidoti,amekuwa akirudisha fadhila katika jamii kupitia sekta mbalimbali, kwanza alianza na kutoa misaada kwa wasusu mitaani, lakini pia alikuja na kampeni ya kusaidia utoaji wa vifaa vya shule kwa wasichana wanaoishi katika mazingira magumu.Jokate pia alishawahi kutoa msaada wa kujenga kiwanja cha mpira katika shule ya Jangwani.

2.Faraja Nyalandu

Amekuwa ni mfano wa kuigwa wa wasichana wengi katika jamii, Faraja ametoa mchango mkubwa sana katika sekta ya elimu kupitia project yake ya Shule Direct

3.Doris mollel

Amekuwa akitoa msaada mkubwa sana katika sekta ya afya hasa kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya umri wao(NJITI), chini ya Dorris Mollel Foundation, ameweza kutoa mashine pamoja na vitanda kwa wahitaji hao.Alianza kama Miss Singida mwaka 2014, na baadae Miss Tanzania namba tatu.

4.Flaviana matata

Mwanamitindo anayeishi nje ya nchi, safari yake ya mafanikio ilianza pale aliposhiriki Miss Universr mwaka 2007,amekuwa akisaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu chini ya Flaviana Matata Foundation.

5.Jenniffer Bash

Mrembo aliyeamua kuangalia fursa katika sekta ya kilimo, wengi wanamjua kaka mama Alaska, ikiwa Alaska ni jina la kampuni yake.aliona ni bora kushirikianana wakulima wa mashambani ili kuweza kuagawana faida na kunufaisha jamii pia.Kwa sasa kampuni yake inauza mayai, mchele na mafuta.

6.Nasreen Kareem

Alikuwa mshindi wa Miss Tanzania mwaka 2008,kwa sasa amejikita zaidi katika maswala ya urembo hasa wa asili akishirikia na wanawake wa jamii za kimasai katika utengenezaji wa bidhaa za shanga.Duka lake limekuwa ni moja ya maduka makubwa yanyotangaza bidhaa za asili.

7.Jackline Ntuyabaliwe

Ni mrembo aliyepitia vipaji vingi mpaka kufika hapa, alianza na kushirki U-misss mwaka 2000, na kuwakirisha Tanzania Miss World. Alishapita kwenye kuimba ,kwa sasa amejikita katika ubunifu.Ameshashinda tuzo ya designer bora wa vitu vya thamani.

 

Serikali Kuingilia Kati Swala La Mavazi Kwa Wasanii Hasa Wa Kike

Naibu waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na michezo Mh. Juliana  Shonza,ametangaza kuwa kuanzia sasa serikali itaanza kazi ya kuwabana wasanii ambao wamekuwa wakivaa vibaya katika kufanya kazi za za kisanii, na kutumia lugha mbaya zikiwemo lugha za matusi katika nyimbo zao.

Mh Juliana Shonza amesema kuwa kwa muda sasa wasanii wamekuwa na mchango mkubwa wa mmomonyoko wa maadili kutokana na nguo mbaya wanazovaa na lugha za matusi wanazotumia katika nyimbo zao.Akiongea alipokuwa akipokelewa ofisini hapo , Naibu Waziri huyo amesema kuwa moja ya vitu alivyoviona katika sanaa ni jinsi wasanii wanavyovaa vibaya katika kazi zao, na ilo ni swala analotaka kuanza kulishughulikia lakini pia lugha  mbaya zinazotumika katika nyimbo nalo inabidi kufuatiliwa.

“Nilipoteuliwa swala la kwanza kabisa kuliangalia lilikuwa ni mmomonyoko wa maadili kwakweli imekuwa ni changamoto kubwa sana nimeshuhudia saizi hata ukiangalia  kwenye nyimbo na kazi za wasnii  lugha ambayo inatumika  siyo nzuri,lakini kama haitoshi  kuna nyimbo zinaimbwa ukifuatalia kwa ndani unakuta  siyo mazuri,lakini hata ktika mavazi  nitawaambia wasanii wa kike  wajitahidi kuvaa vizuri,kwa sababu hatuwezi kuacha hivi vitu hivihivi vinaendelea tu , kila taifa lina  misingi yake na tamaduni zake”

Labda ni kutokana na utandazi na maendeleo yanayoendelea, wasanii hasa wa kike wamekuwa wanavaaa nguo  zinazowaacha nusu uchi swala ambalo limekuwa likichangia mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa, na baadhi  ya nyimbo zimekuwa na maneno makali ambayo inakuwa vigumu wazazi kusikiliza mbele ya watoto wake.

Lakini pia Naibu Waziri huyo amedai kuwa swala la kuulinda na kuutunza utamaduni wa taifa ni jukumu la viongozi na watu wote kwa ujumla.hivyo basi wasanii  wanapofanya kazi pia inabidi kuzingatia kuwa kazi zao zinalenga pia kutunza na kutangaza utamaduni wa taifa lakini pia lugha wanazotumika katika kazi zao zilenge kusikilzwa na watu wa rika zote na sio kubagua kundi fulani, kuna baadhi ya nyimbo zinaweza kuwa na maneno makali kiasi kwamba ni aibu mzazi kusikiliza na mtoto.

Picha 5 za Wasanii Na Watoto Wao

Wasanii wa filamu na wanamuziki wa Bongo movies kama ilivyo watu wengine wana familia na wana watoto kupitia mitandao ya kijamii mashabiki wanapenda kuangalia na kuwafatilia watoto wao na familia zao.

Leo tutaangalia wasanii watano wakiwa na watoto wao:

1. Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba ana watoto watatu wanaoitwa Kiba junior, Amiya na Sameera ambao anapenda kuwaweka kwenye kurasa yake ya instagram , hizi ni baadhi ya picha za watoto.

.

 

2. Diamond Platnumz

Mwanamuziki Diamond ni moja Kati ya wasanii ambao ni kivutio kwa watu, Ana watoto watatu wawili aliozaa na Zari ambao ni Nillan na Tiffah na mtoto mmoja aliyezaa na Hamisa Mobetto anayeitwa Dyllan.

 

3. Master Jay

Mtayarishaji wa muziki Master Jay ni moja kati ya staa mwenye watoto watatu ambao ni Catherine, Nuru na Silvia.

 

4. Aunty Ezekiel

Mwigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amezaa mtoto na mcheza shoo wa Diamond Moses Iyobo, cookie ana miaka miwili.

5. Hamisa Mobetto

Mwigizaji Hamisa Mobetto ana watoto wawili binti yake Fantansy aliyezaa na Majizo mkurugenzi wa EFM na Diamond Platnumz aliyezaa nae mtoto mdogo Dylan.

 

 

 

Mastaa Wa Kike Maarufu Na Muonekano Wa Nywele Fupi

Imekuwa fashion kwa  wanadada wengi kuwa na muonekano wa nywele fupi , tena wakionekana maridadi kabisa kuliko hata nywele za bandia wanazosuka wakati mwingine.Hawa ni baadhi ya mastaa na watu maarufu  wa kike bongo wenye muonekano wa nywele fupi na bado wanaonekana maridadi na kupendeza vizuri kabisa.

1.Nancy sumary.

Amekuwa akionekana na muonekano huu kwa muda mrefu sasa, ni mwanadada mjasirimali, muandishi wa vitabu lakini pia ni meneja wa Bongo5 Media.Ni mama wa familia lakini muonekano wake siku zote umfanya kuonekana mrembo bila kuchuja.

2.Elizabeth Lulu Michael

Amekuwa na muonekano wa kubadilika badilika katika nywele , lakini akiwa na nywele fupi uonekana vizuri zaid.ni mmmoja wa mastaa wa bongo movies anaeongozwa kwa kupendeza na kuvaa nguo ikamkaa vizuri kabisa.Huyu ndio Lulu Michael.

3.Jackline wolper

Jacky ni mmoja wa wasichana wanaovaa sana katika mastaa wa  bongo, amekuwa ni mtu anaejipenda.Kuwa na duka la mavazi pia linazidi kumfanya aonekane maridadi.yeye pia anamuonekeano wa nywele fupi ila za kwake amezitia nakshi, hii inamfanya azidi kung’ara kwa sababu ya rangi yake pia.

3.Faraja Nyalandu

Ingawa ni muda sasa tangu ashiriki mashindano ya ulimwende, lakini amekuwa ni mmoja wa wanawake wanaotunza umaridadi wao sana.Akiwa kama  mama wa familia pia Faraja amekuwa akivaa nguo za heshima, zenye kumfanya haonekane binti muda wote na kuonekana nadhifu na muonekano wake wa nywele fupi.She is always perfect!!!!!

5.Jackline Ntuyabaliwe

Ni moja wa mwanadada mwenye vipaji vingi, alianza na urembo, baadae akaingia kwenye muziki lakini sasa amejikita katika ubunifu zaidi na kampuni yake ya kutengeza vitu vya thamani chini ya kampuni ya Amorette.amekuwa na muonekano mzuri sana hasa katika nywele fupi. Huvaa simple but always looks stunning!!!

6.Shamimu Mwasha(8020 Fashion)

Inawezekana labda na kazi yake inamfanya aonekane maridani zaidi, amekuwa mwanamitindo na pia mtu ameweza kushauri wengine na kutoka kimaisha.shamimu ni mama wa familia,Mwanamitindo na mjasiriamali pia  lakini hii haifanyi yeye kuonekana toauti na wasichana warembo na wanaojipenda.