Maua Sama ,Diamond Ndani ya Afrima 2018, Vannesa na Alikiba Wakatwa.

Tuzo za afrima nchini nigeria imetoa list ya wasani watakaoshindanishwa katika vipengele mbalimbali katika mashindano hayo.

Huku wasanii kutoka katika lebel  ya WCB wakiongoza katika vipengele mbalimbali huku wasanii wengine wakishindwa kuonekana katika vipengele vyovyote .

kwa upande wa wasanii wa kike, ni msanii Maua Sama pekee aliyeweza kuingia katika mashindano hayo katika kipengele cha  Best Female of Eastern Africa.

Wasanii Wakongwe Wakataa Kuitwa “Legends’

Kumekuwa na ile heshima wanayoitoa baadhi ya wasanii wachanga kwa wasanii waliotangulia kwa kuwaia ma-legends  ikiwa kama njia ya kuonyesha kuwa wanamchnago mkubwa sana katika tasnia ya muziki ukizingatia muziki ulivyo sasa sio kama ulivyokuwa miaka ya nyuma.

Lakini hii inapokelewa tofauti nan wasanii wenyewe kwa sababu sio wote wanaotaka kuitwa hivyo lakini pia sababu yao kubwa ikiwa kuna sifa bza msanii kuitwa legends na sio wanaitwa tu kwa sababu yeye amekaa katika game kwa muda mrefu kuliko wengine.

Nikki Mbishi alishawahi kusema “wasanii weng wa tanzania wanaoitwa legends hawana hata miaka 40 katika game,ila wanaitwa hivyo ili kuzeeshwa na kujiona kuwa hawana kasi yakuendana na watoto wa 98′, sasa kama Dully sykes mkongwe na R.kelly je:

Siku kadhaa kupita , msanii wakazi pia alisema kuwa wasanii wakongwe wanakuwa na tabia ya kwenda katika media kuomba msaada li kusimamaisha muziki wao huku akisema “kama nyie mkilia je wale wasanii wachanga (who look up to you) na hawajawahi kutoka wafanyaje, ebu jaribuni kuwa greatful  for glorious past nad cherish it”

Hata hivyo Tid nae alifunguka na kusema kuwa wasanii wa zamani kidogo wamekuwa wakiitwa wakongwe ili tu ku-step down kutaka kudai maslahi yao huku wakipewa jina la kuwa wakongwe ili kuachana na hai zaoza msingi , Tid anasema”

“legends ni mtu mwenye miaka kuanzia 50 katika game,mimi unaniita legends gani wakati nimeanza muziki miaka 19 tu iliyopita, hata miaka 40 sijafikisha unaniita hivyo, sisi ndio tunatakiwa tule matunda ya muziki,huko ni kutoka kwenye line tu na kuwaweka watu wao kwa sababu sisis tunawadai na wanatuzulumu sana.so diamond was me lakini wakasema wanamleta diamond ili tukushushe.

lakini pia hata Jay Dee aliwahi kuwpasha watu katika mtandao wa Twitter kwa kuandika”mnikome , mkongwe ni Bi Chuka na Khadija Kopa tea mnikome kabisa mimi bado mbichi.”

 

Diamond na Vannesa Kuwania Tuzo Uingereza Tena

Wasanii wanaofanya vizuri sana tanzania katika kutangaza muzikiwa bongo ndani na nje ya nchi mabo kwa sasa wamekuwa kama kaka na dada wa bongo fleva Vannesa Mdee na Diamond Platinumz wameingia katika  headlines tena baada ya kuwekwa tena katika tuzo za huko uingereza wakiwa na wasanii wengi wakubwa.

Tuzo hizo za African Pride 2018 zitakazo fanyika June 3 mwaka huu kutakuwa na wasanii wengine wangi kutoka afrika ambao watachuana vikali na wasanii wetu kutoka Tanzania.

Wasanii kama Tiwa Sawage, Yamei Alade, Kiss Daniel , Patoranking, Davido, Wizkid na wengine wengiwatakuwepo kutafuta msanii vora wa muziki afrika kwa upande wa kike na upande wa kiume.

Vannesa na Diamond sio mara yao ya kwanza kuwania tuzo mbalimbali za nje ya nchi na kutoka na ushindi wa kuwapa tanzania hshima juu ya muziki, hivyo kila la kheri kwa wasanii hawa lakini pia pale wanapohitaji sapoti mashabiki wawe mstari wa mbele kufanya hivyo.

Steve Nyerere Kuwaombea Viongozi Waliofariki.

Kiongozi  wa bongo movies Steve Nyerere  pamoja na team yake ya uzalendo ameanda siku maarumu ya jumamosi hii kwa ajili ya kuwaombea wasanii na viongozi walitangulia mbele ya haki na kuwaenzi watu hao., maombezi ambayo yatafanyika jijini Dar katika viwanja vya Leaders club.

Steve Nyerere amesema kuwa tukio ilo la maombezi litafanyika sambamba na kuwafutulisha watu wote watakaokuwepo ambao watakuwa katika kuendeleza mfungo wa Ramadhan.

tunataka kuwakumbuka ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki,sisi tuliobaki tunatakiwa kuwakumbuka na kuwaombea ndugu zetu.sis tupo nyuma yao kwaio kama wazalendo kwanza tumeona tuanda e tukio la aina hiyo kila staa na kiongozi aliyetangulkia mbele ya haki tutamuombea.

Steve Nyerere pia ansema kuwa maombezi haya yatawagusa watu  wote katika tasnia ya sanaa bula kubagua kuwa ni muziki au filamu hivyo itakuwa ni waimbaji, waandaaji wa muziki, waandaaji wa filamu, watayarishaji, waigizaji , nahata waandishi wa habari ambao wamekuwa wakiandika habari za wasanii lakini ndio hivyo wametangulia mbele za haki.

 

Ray C Awapa Moyo Wasanii Wakongwe

Mwanadada aliwahi kuvuma sana katika tasnia ya bongo fleva mwenye kiuno chake bila mfupa amefunguka na kusema kuwa kuna jini limekuwa likiwasumbua sana wasanii wa muziki hasa wakongwe  na kushindwa kuendelea na muziki wao.Ray C aliyasema hayo baada ya shoo wa Lady Jay Dee kubadlishiwa ukumbi  siku anazindua project yake ya anaweza ambayo ilifanyika wikiendi iliyopiata jijin Dar Es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Ray c aliongea hayo baada ya kubadilika kwa ukumbi alitakiwa kufanyia shoo lady jay dee na kisha kuhoji yuko wapi mtu kama Marlow, Mandojo na Domo Kaya, juma nature , anasema kuwa anahisi kuna jini anawavuruga wasanii wakongwe.

Kuna nini bongo fleva, wasanii wapya ni wengi, ooh yes nalijua hilo lakini ukweli ni kwamba nchi yote hapa afrika mashariki nikienda nasikia tu nyimbo za zamani,mimi mwenyewe pamoja na mahanjumat ya pepo la ahera lakini bado sauti ipo nje.nasikia kuna jini mmoja ambae amekuwa akiwafanya wasanii wajione kuwa ndio basi tena.point yake ni moja kuwa anauwezo wa kukujenga na kukumaliza mara moja , jini huyo ni promota.

Ray c anaendelea kuwapa moyo wasanii kwa kuwaambia kuwa hata ingekuwaje lakini wanapaswa kujua kuwa kipaji ndio kila kitu na wala hawana haja ya kuhofia kuhusu watu wengien kama mapromota.

wasanii mna kazi kubwa ya kujiamini kwanza kabla ya kumuamini mtu mwingine,mkishajua aliyewapa viapaji basi mtasimama tena.maana mashabiki wenu bado wapo,kinachohitajika ni kipaji na wala sio promota.

 

 

Wasanii Wahaswa Kuwa Makini Katika Kusaini Mikataba ya Kazi

Wakili wa kampuni ya Selta Tanzania Noeli  Chikwindo amfanya mazungumzo na wasanii mbalimbali nchini na kuwashauri kuwa makini sana wanapokuwa wanasaini mikataba ya kufanya kazi na kampuni au menejiment mbalimbali kwa sababu wanapozingatia sheria ndipo wanapoweza kujitetea na kulinda haki zao.

Wakili huyo anasema kuwa katika mikataba ya kazi za wasanii kuna sheria kama saba ambazo wanatakiwa kuzifuata kabla ya kusaini mkabata wowote ule na wanapaswa kuzijua na kuzifatilia kila mara.

ni vema kbala ya kuweka sahihi katika mkataba ni bora kujua ni kitu gani kwanza unakuwa unasaini,lakini pia uangalia lugha inayotumika katika mikataba iyo na kama unaielewa  kuepuka matatizo yanayweza kujitokeza.

Wakili huyo anasema kuwa wasanii ni kazima watambue haki zao kwanza na ndipo watambue kuwa wanaweza kufanya  kazi na watu wengine hii itasaidia sana kuepuka wasanii kuwa wanalalamika kuwa wanaonewa au kuutapeliwa.

Ma-Miss Kuajiriwa Kufanya Kazi Shirika la Ndege La Taifa

Waziri wa habari m sanaa na michezo mh harrison mwakyembe amependekeza kuwa wanaoshiriki mashindano ya urembo wa ma-miss waajiriwe katika shirika la ndege la taifa kwa sababu wana vigezo vya kutosha.Mh Harrison Mwakyembe aliyasema hyo katika uzinduzi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 yatakayofanyika chini ya kampuni ya The Look baada ya ile ya Lino kuachia ngazi hiyo.

Mh Waziri amesema kuwa wshiriki wengi wa mashindano hayo wanakuwa na uwezo na sifa nyingi za kuwa katka cabin crew ila tu kabla ya kuajiriwa wanapaswakupelekwa kozi fupi ya miezi mitatu katika chuo cha anga kabla ya kuanza kazi na hii itapunguza tatioz la ajira kwa warembo hao.

Hii pia inaweza kusaidia baadhi ya wasichana kwa sababu kuna warembo wamekuwa wakishiriki mashindano hayo na baadae dirazao za maisha kupotea na kujikuta wakiishi maisha magumu sana.

 

Tiko Awasahauri Wasanii wa Bongo Kuwa Watiifu kwa Serikali.

Msanii wa bongo movies nchini Tiko Hasssan amefunguka na kuwataka wasanii wa bongo kuwa watiifu pale wanapoambiwa kutekeleza jambo na serikali ili wasiweze kupatwa na madhara maengine yanayoweza kutokea baada ya kukiuka sheria hizo.

Tiko amesema kuwa kuna baadhi ya wasanii unakuta wanahitajika kufika mahali flani na mamalaka inayohusiana na sanaa lakini wanakiuka maagizo hayo alafu ukifika muda wa kuipoea adhabu anakuwa mkali na wa kuanza kulalamika wakati picdi wanapokuwa wanaitwa inakuwa ni kwa manufaa ya kazi zao wenyewe za sanaa .

Akitolea mfano kutoka kwa wasanii wa muziki, Tiko anasema kuwa serikali kupitia Baraza la habari, sanaa , tamaduni na michezo wamekuwa wakiwaita wasanii ili kukaaa nao chini kuzungumza nao kuhusu marekebisho ya kazi zao hasa wasanii wa muziki lakini wanakuwa wanapuuzia na kushinwa kufika kwa kudharau.

Jamani mastaa tunatakiwa kuheshimu serikali , aple unapoitwa  wito unatakiwa kutii wito huo. kwa sababu hiyo ndo inayosaidia katika kazi za sanaa.- Alifunguka Tiko Hassan alipokuwa akiongea na  za moto moto news.

Haya yote yanakuja baada ya wki moja iliyopita wasanii wengine kukumbwa na sakata la kufungiwa kwa kazi zao na serikali kwa madai ya kwenda kinyume na maadili ya Tanzania katika utoaji wa kazi zao na mavazi yao kitu ambacho kimewaumiza wasanii wengi huku baraza la sanaa likisema kuwa wasanii hao wamekuwa wakipuuzia wito na barua za mazungumzo wanazotumiwa.

 

Baraza Kutoa list Nyingine ya Wasanii na Nyimbo Zisizokuwa na Maadili

Ikiwa bado wasanii mbalimbali wakiendelea kulalamika na kusema kuwa baraza la sanaa limekuwa likiwafungia bila kutoa sababu za kufungiwa kwa nyimbo nyingi za wasanii, baraza la sanaa linajiandaa kutoa nyimbo nyingine ambazo zitachunguzwa na  zikaonekana kuwa na tatizo la kuwa zimeenda  kinyume na maadili ya Tanzania.

Wiki iliyopita baraza la sanaa lilitoa list ya nyimbozaidi ya 10  ambazo zilitakiwa kufungiwa kuchezwa katika vituo mbalimbali vya habari kwa madai kuwa zimekiuka vigezo na masharti na maadili ya tanzania huku msaii wa hip-hop roma mkatoliki akifungiwa miezi sita kutokujihusisha na kazi za sanaa zozote kwa muda wote huo kutokana na kuwepo kwa  baadhi ya maneno yenye matusi katika wimbo wake wa kiba100 aliomshirikisha Stamina na Maua Sama.

Hata hivyo baraza la sanaa linaendelea kuchunguza nyimbo nyingine zilizopo katika muziki na hata zinazoendelea kutoka ili kujiridhisha na maadili yanayopatikana katika nyimbo hizo  na kama kutakuwa na ukiukwaji wa taratibu pia baraza haliwezi kusita kufungia nyimbo hizo au wasanii.

Baraza linawataka wasanii wote kupeleka nyimbo zao katika mamlaka husika kablya ya nyimbo hizo kutolewa na kusambazwa kwa mashabiki ili kuondoa usumbufu unaojitokeza sasa hivi wa kufungiwa.

Huu ni muendelezo na utekelezaji alioanzishwa Mh Naibu Waziri wa habari, tamaduni sanaa na michezo alipoanza kwa kuwafungia wasanii wa kike ambao wamekuwa wakiweka picha za uchi katika mitandao hivyo zoezi ili litakuwa ni kwa ajili ya wae tu wanaokiuka taratibu na kuvunja maadili ya watu katika jamii.

TCRA Yazifungia Nyimbo 13, Diamond na Nay wa Mitego Walizwa Zaidi

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imefungia kuchezwa kwa nyimbo kumi na tatu za wasanii mbali mbali huku Nay wa Mitego na Diamond wakiwa na zaidi ya nyimbo moja kwenye orodha hiyo.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha kuchezwa kwa nyimbo 13 zisizokuwa na maadili zikiwemo mbili za Msanii Diamond Platnumz.

TCRA waliandika maelezo haya na kuorodhesha nyimbo hizo:

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania imepokea nyimbo zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Nyimbo hizo zilitolewa na wasanii na kusambazwa katika vyombo mbalimbali vya utangazaji na mitandao ya kijamii. Nyimbo hizo zina maudhui ambayo ni kinyume na maadili na kanuni za huduma za utangazaji (maudhui) 2005”.

Hii ndio listi kamili ya nyimbo zilizotolewa na Mamlaka ya mawasiliano;

 

Mamlaka ya mawasiliano imetuma kopi hiyo ya barua kwa vyombo vyote vya habari na kuvitaka kusitisha kucheza nyimbo hizo mara moja na pia vyombo hivyo vimehaidi kuchukua hatua kali za kisheria kwa chombo chochote kitaendelea kucheza nyimbo hizo.

Wasanii Walioguswa na Hukumu ya Mh. Sugu

Kutokana na hukumu aliyoipokea jana mh joseph mbilinyi ambae jina lake la usanii ni Mr. Sugu siku ya jana February 26  baada ya kukutwa na hatia ya kutoa maneno makali ya kumkashifu Rais wa tanzania, wasanii wemeonekana kuumizwa na hukumu hiyo ambayo imemkabili msanii mwenzeo.

Wasanii hao walijitahidi kutoa maneno ya faraja kwa msanii huyo na familia yake pia kwa sababu hata msanii huyo alipokuwa mbungeni mara nyingi amekuwa akitetea sana swala la muziki na sanaa.

Ikumbukwe kuwa ni kwa mara ya kwanza Sugu alipoingia bungeni aliweza kuomba kulipwa kwa wasanii ili kuweza kunufaika na kazi zao pale wanapokuwa wanafanya kazi zao sehemu mbalimbali.

Baadhi ya wasani ambao waliguswa na tukio hilo ni pamoja na :

Nikki wa Pili;Nguvu ya Mungu ikapate kuwa pamoja na familia yako, gerezani  sio kaburini ,stay strong Jongwe.

Nay wa Mitego;Stay strong brother Sugu.

Rama Dee;Nasikitika sana kama msanii pia na kama rafiki wa karibu wa Sugu, hii picha sio nzuri.

Izzo Bizzness;Stay strong Big Brother Jongwe.

Kala Jeremiah;Stay Strong Jongwe.

Roma Mkatoliki;Hata hili nalo litapita, stay strong  Joseph Zaburi 35:1-28

Hata hivyo wakili mtetezi wa kesi hiyo Bw Peter Kibatala anasema kuwa wanafanya mpango wa kukata rufaa ya kesi hiyo kwa sababu hawajaridhika na mahamuzi ya kesi hiyo.

 

 

 

Wako Wapi Wasanii Walioumizwa na Kifo cha Akwilina Akwilini

Ikiwa jana ndio siku ambayo mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji kuagwa mwili wake na kusafirishwa kwenda nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi watu wengine wameonekana kusikitishwa na kuhoji wako wapi wale wasanii ambao walipata mshtuko mkubwa siku ya tukio.

Mategemeo makubwa ya mashabiki ilikwa  ni kuona wingi wa wasanii katika kuaga mwili huo siku ya jana ikiwa siku ya kifo chake wengi walionekana kuguswa lakini kitu cha ajabu  wasanii waliojitokeza ni wachache tena wanahesabika.

Acha tuone sababu, je ni kweli wasanii hao waliguswa na msiba lakini kila mtu alikuwa busy na shughuli zake akashindwa kutoa heshima za mwisho kwa mwanafunzi huyo ambae kifo chake kimeumiza watu wengi.

Je ni kweli kuwa wasanii walishindwa kujua kuwa jamii ya wanafunzi wa chuo pia ni  jamii kubwa inayosikiliza muziki wao hivyo kutokea katika msiba kungewafariji wafiwa na wanafunzi lakini pia kungewafanya wanafunzi na wafiwa kuona kuwa hata wao pia  sehemu ya maisha ya wasanii.

Je uwepo wao katika msiba na kuagwa kwa mwili huo sio kuwa ndio fursa ya wasanii kukutana na mashabiki wao hata kama wapo katika hali ya uzuni.

Yako wapi yale majonzi waliyokuwa nayo wasanii hao katika page zao za instagram siku mwanadada huyo anapoteza maisha.

Hapa tunajifunza kuwa wasanii wengi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii katika kuonyesha hayo yote lakini wanashindwa kutambua kuwa mashabiki wao pia wanawahitaji sana katika kujumuika nao katika matatizo kama hayo.

Hata hivyo, wapo waliojitokeza  kama Bilnass ambae alionekana kwenye misiba na akapata nafasi ya kuongelea masikitiko yake juu ya msiba huo na kusema “kazi ya mungu haina makosa, kikubwa ni kumuombea tu.natoa pole kwa wanafamilia, wanafunzi na wafiwa wote kwa ujumla.

Mwisho wa yote tunatoa pole kwa wafiwa  hasa ndugu wa marehemu na Mungu awatie moyo katika kipindi hiki kigumu.

Mastaa wa Kiume na Muonekano Mpya wa Rangi za Nywele Kichwani

Inaweza kuwa ni fashion mpya iliyoingia mjini kwa sasa wasanii wengi wa bongo wameanza ku-trend nayo sasa, ni upakaji wa rangi nywele.Sio mbaya kubadilisha muonekano wako hasa kwa watu maarufu ili watu wasiweze kukuzoea na muonekano ule ule kila siku lakini pia katika upakaji wa rangi hizo inabidi pia kuzingatia sana rangi yako binafsi ili uweze kutokea.

Hivi karibuni kumezuka wasanii kadhaa wa kiume wameanza ku-trend na stykle hii ya nywele kama:

                                                 

.Huu ni muonekano mpya kwa Alikiba alioamua kutoka nao hivi karibuni.

BEN POL

Wengi walizoea kuona watu wakipaka rangi ya brown. lakini Ben Pol alikuja na muonekano tofauti wa rangi ya kijani kichwani mwake ambayo pia ilimfanya aonekane poa inawa mara ya kwanza wengi walimsema.

Harmonize.

                                  

Harmonize aliamua kutoka na muonekano wa kuweka breach katika nywele zake kica kizima ingawa ilizoeleka kuwa wanaume wamezoea kuweka katikati.

LAVALAVA.

Muonekano huu wa Lavalava unataka kufanana kidogo na ule wa alikiba , ambapo juzi baada ya Alikiba kuachia picha zake watu walianza kuzua gumzo kuwa kuna aliyemuig mwenzie.

OMMY DIMPOZ

                                                 

Ommy Dimpoz ni moja ya wasanii wanaojali sana muonekano wao wa nje hasa katika mavazi na kila kitu kinachomfanya aonekane nadhifu na mwenye kuvutia, yeye pia alitoka na style mpya ya nywele juzi, akiwa ameweka breach.

 

 

Vazi la Suti Kwa Wanawake Lilivyowatoa Mastaa Hawa

Imezoeleka kuwa vazi la suti ni kwa ajili ya wanaume tu na sio vazi lililozoeleka sana kuvaliwa na wanawake lakini sio kwa dunia ya sasa ya usawa.

Vazi la suti linaweza likamtoa vizuri mwanamke endapo tu atalivaa kwa usahihi na kushonwa kwa ufundi zaidi.

Baadhi ya mastaa kama Zari, Jokate, Amber Lulu Irene na Fahyma wamelivaa vazi hili la suti na naomba niseme tu nimevutiwa na uthubutu wao kwani kama tunavyojua fashion is all about taking risks na kuangalia kama utapendeza.

Hawa ni baadhi tu ya mastaa wa kike wakiwa katika mavazi yao ya suti:

1. Jokate Mwegelo

 

2. Amber Lulu

 

 

3. Zari the Bosslady 

 

4. Irene

 

 

5. Fahyma

Kurasa za Wasanii Mbalimbali Zilivyopambwa na ‘Post’ za Valentine.

Ikiwa jana ni siku ya kusherekea sikukuu ya wapendanao, wasanii mbalimbali walikuwa wakiweka posts katika kurasa zao za instagram wakionyesha jinsi walivyokuwa wakishrekea sikukuu hiyo ya wapendanao, inawa wapo walioumia  na pia wao waliokuwa wanapost wapenzi wao na pia wapo walikuwa wakijua uwepo wa siku hiyo lakini wakionyesha kuendelea na kazi kama kawaida.baadhi ya kurasa za wasanii hao ni pamoja na :

RayVany:

Aliweka picha akiwa na mama wa mtoto wake fayhma.

MONI CENTRO ZONE

Aliamua kuweka picha ya mpenzi wake @officilanai ambae ni msanii mwenzake na kumsifia sana.

MOSE IYOBO.

Yeye aliweka picha ya mwanamke aliyeweza kumzalia mtoto wa kike Aunty Ezekiel na kuweka utenzi wa mapenzi wenye hisia kali.

                                         

ZARI THE BOSSY.

Siku yake ilianza kwa kusema kuwa siku ya valentine imekuwa ni ya kawaida sana kwake na anaendelea na kutafuta pesa.

                                        

Lakini ilipofika usiku zari the bossy aliamua kutoa tamko rasmi kuwa hayuko tena katika uhusiano wa kimapenzi na mzazi mwenzie Diamond Platinumz.

                                         

SHILOLEH.

Yeye aliweka picha na mwanaume wake aliefunga nae ndoa hivi karibuni huku wakionyesha wapo Igunga kwa ajili ya kutoa burudani kwa masgabiki zake.

DAYNA NYANGE

Dayna Nyange aliamua kuweka picha ikimuonyesha akiwa ameshika tumbo lake likionekana kama ni mjamzito na kuandika “HAPPY VALNTINES’. Hii iliibua hisia tofauti kwa mashabiki wakitaka kujua na kuhoji ni nani mhusika wa kitumbo hicho.msanii huyo mara ya mwisho alikuwa akisemekana yupo katika mahusino na Dax Cruz.

Vanessa:Muziki wa Afrika Mashariki Haujulikani Sana Nigeria.

Msani wa muziki anaefanya vizuri na album yake ya Money Monday,Vannesa Mdee amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa afrika mashariki hawajulikana sana Nigeria kama vile ambavyo inadhaniwa au kama ambavyo nyimbo za nigeria zinavyosikika sana Tanzania.

Vannesa ambae alikuwa Nigeria kwa ajili ya kutangaz album yake ya money monday ameiambia Cloud fm kuwa pamoja na kwamba watu wanahisi nyimbo zetu zinachezawa sana huko, lakini ukweli ni kwamba hata katika club alizokuwa amekwenda wimbo uliokuwa ukipoigwa sana ni wa diamond na Patoranking wa love u die na wa kwake alioimba na Reekado .

hapa Nigeria huo muziki wetu haupo kabisa kwa nguvu zile unavyopaswa kuwepo kwa sababu muziki wetu ni mkali lakini pia hata wasanii wetu ni wakali na wakubwa.

Lakini pia vannesa anasema kuwa nigeria kuna wasanii wengi sana ambao wanajitahidi kukuza muziki wao kwa kuwasapoti sana wasanii wao.

Hii sio mara ya kwanza wasanii kutoka tanzania wamekuwa wakisema kuwa ingawa Tanzania kuna wasanii wakubwa lakini wngi hawajulikana sana nje, Bright alishawahi kuongelea hilo.