Chemical Atangazaa Kujioa

Mwanadada mwenye sifa na muonekano wa kiume amefunguka na kutangaza rasmi katika mitandao na ukurasa wake wa instagram kuwa ana mango wa kujioa , huku mara zote mwanadada huyo akiisiwa kuwa hana mahusiano kutoka  na kutokuwa na muonekano wa kike.

Mwanadada huyo alitangaza nia yake iyo katika ukurasa wa instagram na kuweka icha yenye caption ya NTAJIOA , kitu mbacho kimezua gumzo kwanini  amekuwa akisema hivyo.

Chemical amekuwa akisemwa kama msanii mwenye muonekano wa kike pamoja na kwamba jinsia yake ni tofauti na kile kinachoonekana ndani yake.

 

Chemical Amwaga Povu Zito Baada Ya Kuvaa Gauni

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Claudia Lubao maarufu Kama Chemical amejikuta anawatolea povu zito watu ambao wamediss baada ya kuonekana akiwa amevaa gauni.

Chemical amejizolea umaarufu kwenye muziki wa hi hop Kama mwanadada mgumu ambaye mara amekuwa akitinga mavazi ya kiume pekee lakini Siku chache zilizopita Chemical aliposti picha akiwa amevaa gauni.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers baada ya sakata hilo,Chemical aliyekuwa amevaa kigauni hicho na kutokelezea kwenye ukurasa wake wa Instagram alisema kuwa, haoni kama ni tatizo kuvaa nguo hizo japokuwa wengi wameshazoea kumuona akiwa katika mavazi ya kiume mara kwa mara.

Wengi walishazoea kuniona na nguo za kiume muda wote, wakati ninavaa lile gauni nilijua tu kwamba wataiongelea kwa sababu kuongea ni kawaida yao, kwa hiyo hawaniumizi kichwa, ninachojua mimi ni mtoto wa kike hivyo nina uamuzi wa kuvaa nguo yoyote ninayoona kwangu inafaa ilimradi tu nisivunje maadili yetu ya Kitanzania“.

 

Chemical- Nina Bahati Ya Kutongozwa Sana na Wanaume

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa michano yake ya rap, Chemical amefunguka na kuweka wazi kuwa anatongozwa sana na wanaume tofauti na watu wanavyodhania.

Katika Interview yake  aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Chemical amesema ana Bahati ya kukutana na wanaume kibao na anatongozwa kuliko watu wanavyomfikiria kwamba ana swagga za kiume.

Mimi Nina Bahati ya kukutana na wanaume wengi ambao wananitongoza kwa sababu unakutana na mwanaume mwingine anasema kabisa kuwa anapenda mwanamke ambaye anaonekana kama mpambanaji ambaye mnaweza kufight wote katika maisha watu wa namna hiyo wapo wengi.

Kuna watu wanaamini Chemical hatongozwi, Mimi natongozwa sana huko kwenye DM kwa sababu pamoja na vyote hivi mimi bado ni mwanamke na nina Boyfriend ambaye anavutiwa na hivi nilivyo kaa kiume kwa sababu sio kila mwanaume anapenda mwanamke anayeweka makucha marefu na kuvaa mawigi”.

Chemical amewataka watu waondoe dhana ya kwamba mwanamke akivaa kiume basi ndio anataka kuwa mwanaume Hapana hayo yanakuwa ni mavazi tu.

Hakuna Wasanii Wenye Vipaji kwa Sasa, Wanatengenezwa -Chemical

Msanii wa kike, Chemical amefunguka na kutoa maoni yake kuhusu vipaji vya sanaavilivyopo bong na kusema kuwa vipaji  vya kutoka moyoni vilikuwepo zamani lakini sio sasa hivi kwa sababu kwa sasa wengi wamekuwa wakitengenezwa.

Chemical anasema kuwa kuna watu wamekuwa wakijifanya wanajua kuimba lakini hakuna kitu na hii inamfanya awaonee  huruma sana wasanii chipukizi ambao wana vipaji lakini hawawezi kusaidiwa mpaka watoe pesa ili kukuza na kuendeleza vipaji vyao.

kuna watu wanaharibu sana sanaa sasa hivi, unakuta mtu hajui kuimba nakaa studio wiki nzima anarecodi nene moja lakini mwisho wa siku ana mlipa producer na producer hasemi chochote tofauti na zamani msanii akiingia studio anaimba wimbo wote  bila kuogopa chochote lakini sasa hivi imekuwa changamoto sana. -Alisema Chmeical alipokuwa akiongea na EATV

Chemical anawaomba wadau wa muziki kuangali hillo hasa kwa sababu wasanii wengi wanaozalishwa sasa hivi ni wabovu sana na ndio wanaoharibu sanaa.

 

Napenda Sana Mapenzi

Mwanadada Chemical amefunguka na kusema kuwa sababu kubwa ya yeye kuamua kuimba style tofauti na ile aliyozoea kuimba hapo awali ni kwa sababu anapenda sana kusikiliza nyimbo za mapenzi kwa sasa.

Chemical ameyasema hayo alipokuwa akitambulisha wimbo wake wa tila lila ambao kwa kiasi flani jina lake limefanana na lile la Mr blue lakini anasema kuwa haina ufanano wowote hata kama limekuwa na jina sawa kwa sababu hata maneno yake hayafanani kabisa.

Chemical anasema kuwa kbala ya kutoa wimbo huu alimuomba Mr blue kusikiliza kazi hiyo na kutoa ruhusa ya ktumia jina la wimbo wake katika wimbo huo, na hata hivyo anasema kuwa anapenda sana kuimba mapenzi na ndio maana kila anapopata nafasi huimba kwa hisia sana.

Hata hivyo Chemical anasema kuwa sababu kubwa ya yeye kukaa kimya ni kwa sababu alikuwa shule kwa sababu  ameamua kurudi shule kwa sasa.

Chemical Awatolea Povu Wanaomsema Kuhusu Mavazi.

Msanii raper wa kike nchini Chemical amejikuta akiwatolea povu kali mashabiki zake katika kurasa mbalimbali za instagram na mitandao ya kijamii kutokana na kuwa wanamsema jinsi  anavyovaa haiendani na jinsia yake.

Chemical amejikuta akiingia katika wakati mgumu na kuwajibu mashabiki zake kuhusu swala hilo huko akisema kuwa hakuna mwanaume anaeweza kuvaa nguo zake.

kama kuna mwanaume anavaaa nguo zangu basi ajijue kabisa kuwa yeye sio mwanaume , na wewe ambae kila siku unakaa ku-judge nguo zangu basi ujue kabisa kuwa huna kazi ya kufanya , mimi ninavaa ninavyojisikia kuvaa na uanamke wangu haupo katika mavazi.

 

Wanaume Wawili Walisaidiana Kutoa Bikra Yangu kwa Wakati Mmoja:-Chemical

Mwanadada Chemical amefunguka na kuweka wazi kuwa hata siku moja hawajwahi kujutia swala la yeye kutolewa bikra na wanaume aliwaohi kutembea nao kwa sababu hata kipindi anaanza mahusiano hakuwahi kuwaza kuwa mwanaume anaeingia nae katika mahusiano ndio atakae muoa kwa sababu anajua kabisa kuwa wanaume wa sasa ni waongo na wanabadilika muda wowote.

Sijasema  kama naingia kwenye ndoa baada ya miaka mitano  hapana,anaweza akakupenda mtu leo kesho alafu wakabadilika  na ahasikupende tena kwangu mimi hiyo iko fresh tu wala sina tatizo.sijaingia katika mahusinao  na kusema kuwa huyo ndo atakuwa mwanaume wangu wa ndoa.

Hata hivyo, chemical anasema kuwa pamoja na yote lakini swala la kutoloewa bikra kwake ilikuwa kazi sana kwa sababu kwa miaka 20 alikua bikra hivyo ilikuwa ngumu sana kwa w mtu mmoja kumtoa hivyo ilibidi watu wawi;i wasaidiane.

unajua nimekaa miaka 20 kwaio sio midogo, hivyo ilibbidi wasaidianae,na yote hayo yalifanyika nikiwa na akili zangu  kwa sababu nilikuwa nimepanga itolewe lakini sasa kwa sababu ilikuwa ngumu ilibidi aje wa kwanza aliposhindwa akaja wa pili.

Chemical- Sipendi Kabisa Kutumia Kinga

Msanii wa Bongo fleva Claudia Lubalo maarufu kwa Jina la usanii kama Chemical amefunguka na kudai kuwa yeye sio mpenzi kabisa wa kutumia kinga.

Chemical amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv ambapo amesema wazi akishriki Kwenye tendo la ndoa huwa hapendi kutumia kondomu.

Mara ya mwisho kutumia kinga wakati nafanya mapenzi ni muda kidogo, Ilan kiukweli mimi huwa sio shabiki wa kinga kabisa. Mambo ya kinga kinga mimi Hapana ndiyo maana napenda sana kuwa na mtu aliyetulia”.

Chemical alifunguka hayo alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hiko Ataje mara ya mwisho ametumia kondomu.

Lakini pia Chemical alisisitiza kuwa kwa kuwa hapendi kutumia kinga hivyo njia yake pekee ya kujihahakikishia usalama wake ni kuwa na mpenzi mmoj mwaminifu.

Chemical ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpenzi kwani ameamua kuwa mwenyewe na kuyajenga maisha yake kwanza.

Chemical Ataja Vigezo Anavyotaka Kwa Mwanaume

Msanii wa Bongo fleva Claudia Lubalo maarufu kama Chemical  amefunguka na kutaja vigezo anavyoangalia kwa mwanaume ambaye anataka kuwa naye.

Chemical amefunguka na kuweka wazi kuwa anapendelea kuwa na Mahusiano na wanaume tofauti na tetesi ambazo zimekuwepo juu ya jinsia yake kutokana na kuoenda kuvaa kiume.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Chemical ametaja vigezo ambavyo anaviangalia kwa mwanaume kabla ya kuwa Kwenye Mahusiano naye:

Sitaki mwanaume mfupi maana akiwa kashakua mfupi hatweza kunikiss na wala sitaki mwanaume mnene wala mwembamba awe wa kawaida tu na wala asiwe anabeba vyuma”.

Lakini pia Chemical amesema anapenda mwanaume ambaye atamkubali yeye kama yeye na jinsi alivyo hataki mwanaume ambaye atataka abadili maisha yake kwa ajili yake.

 

Nilipotangaza Kuwa Bikra Nilitongozwa Sana;-Chemical

Msanii wa muziki wa hip -hop nchini, Chemical amefunguka na kusema kuwa amekuwa akiwashangaa sana wanaoshangaa wasichana wenye bikra hasa wanaoamua kusema ukweli kuhusu swala hilo wakati kwake ni jambo la kawaida kama ilivyo vitu vingine.

Chemical amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo katika kipindi cha kikaangono live  cha EATV.

Kuna wasichana mpaka leo wanemda kuolewa wakiwa na bikra zao na wanafanya vizuri kabisa na ni wazuri tu,kwaio kuwa na bikra sio ushamba na kutokuwa na bikra ukubwani pia sio ushamba, inategemea tu umekulia wapi na mazingira uliyopitia hapo awali.

Hata hivyo chemical anasema kuwa alipotangaza katika vyombo vya habari kuwa yeye ni bikra alitongozwa sana na watu wa rika tofauti tofauti ingawa pia wapo waliomshangaa na kumuona mshamba.

mimi nilitongozwa sana niliposema mimi ni bikra , tena na wengi wakiwa watu wazima kabisa,na nikaona kumbe kuwa bikra ni dili sana.

Chemical, Wema Ndani ya Movie Moja.

Wasanii wa tasnia ya muziki na filamu nchi kwa pamoja Wema Sepetu na Chemical wameamua kuungana na kufanya kitu cha tofauti na kukileta kwa mashabiki wao ili kuendelea kutoa burudani lakini pia kufanya baishara yao upande wa sanaa kuweza kuwalipa.

Akiongelea swala hilo , Chemical amesema kuwa yeye na Wema Sepetu watafanya kazi katika movie moja lakini sababu kubwa ni baada ya kufanya wimbo wa mary mary ndipo walipoamua kumchagua  Wema kuvaa uhusika na kuto muvi yenye  jina la wimbo huo  kwa sababu za kibiashara.

Aliipenda story na kuna watu  wa karibu yake waliongea  nae kibiashara , kwaio sio kwamba tumeangalia tu jina kubwa la msanii hapana,kwaio tuliamua kumfuata Wema Sepetu kibiashara tu.

mimi sio msanii wa bongo movie ila mimi ni msanii wa muziki kwaio mimi nimefanyatu kama by the way.

Muvi hiyo ya mary mary itakuwa ni toleo la wimbo wa Chemicaal unaoitwa Mary Mary ambao unaelezea maisha ya msichana na mapito anayopitia.Ambapo Chemical aliamua kumchagua wema kuvaa uhusika huo kwa sababu za kibiashara kama alivyosema mwenyewe.

Chemical Asema, Rosa Ree Hayupo Kwenye Anga Zake,Hasifananishwe Nae.

Msanii anaetamba na nyimbo za ku-rap nchini mwanadada Chemical amekataa kufananishwa na mtu yoyote hata kama  ni Rosa Ree kwa sababu kipindi yeye anaanza kufanya muziki alikuwa pekee yake kama msanii wa kike rapper  hivyo anga zake haziwezi kufanana kabisa na anga za Rosa Ree.

Chemical anasema kuwa. ni  muda sasa kumekuwa na tabia ya mashabiki   kumfananishwa na Rosa Ree lakini swala la kufananishwa lilitkiwa liwe  ni kile  kipindi alichotoa ngoma yake kama Sielewi na VIP lakini sio sasa ambapo ameshafika mbali kimuziki tayari.

Sio Rosa Ree tu mimi sitaki kufananishwa na msanii yoyote, mimi nafanya muziki wangu mwenyewe.Ukitaka kufanya muziki na mimi maana yake unakuwa unaingia katika anga zangu, na ukiingia katika anga la mtu manake unakuwa tayari huwezi kwa sababu kila mtu anakuwa na namna yake ya kufanya muziki.

Nilishatoa sielewi mkaniona, nishatoa VIP mkaniona  kabla hata ya huyo rosa ree, nilitoka kipindi hiko hakuna hata female rapper bongo.

Watu wengi wamekuwa wakitaka kuwashindanisha wasanii katika game la muziki  bila kuwa na vigezo muhimu vya kuwashindanisha wasanii , hii inafanya hata muda mwingine wasanii kujenga ushindani na chuki kwa sababu ya maoni ya mashabiki wao.

Chemical Ajitapa na Umbile Lake, Asema Hata hasipoji-edit Yuko Hivyo.

Msanii wa hip-hop Claudia Lubao maaarufu kama Chemical amefunguka na kuongelea picha yake inayosambaa katika mitandao ikimuonyesha akiwa amejiongeza maumbile yake ya nyuma na kuonekana yuko tofauti sana na vile alivyo kwa kawaidai.

Mwanadada huyo mwenye muonekanao wa kiume tofauti na asili yake ameshangaza watu wengi baada ya picha hiyo ku-trend sana katika mitandoa kwa sababu picha hiyo ni tofauti na vile alivyo huku wengi wakijiuliza ni kwa nini ameamua kujiedit ilhali muda mwingi anapenda kuonekana kama mwanaume.

Akijibu kwa kujinadi , Chemicala nasema kuwa yeye ni mtoto wa Kihaya na wahaya wana maumbo mazuri sana hivyo hata hasipofanya editing ya picha hizo lakini yeye yuko hivyo na umbo lake linamruhusu kujinadi.

Hata nisipojiedit mimi bado nina wowoowo kabisa, unajua mimi ni mtoto wa kihaya bwana ,fresh-Alifunguka Chemical alipokuwa akiongea na  Bongo Dot Home  ya time fme kuhusu umbile lake hilo.

Pia Chemical amesema kuwa kuna kazi kubwa ya filamu ataiachia ambayo ameifanya akiwa na Wema Sepetu na ndio itakuwa kazi yake ya mwisho kufanya akiwa chini ya menejimenti yake mpya ya kazi kwanza hivyo watu wakae kusubiria kazi nzuri.

Chemical ambae kwa muda mfupi uliopita alikumbwa na tetesi za kutoka  kimapenzi na Maximaizer ambae ni producer wake ingawa yeye mwenyewe alikanusha kutoka na mtu huyo.Kwa sasa mwanadada huyo anatamba na kibao chake cha Asali.

Chemical Akubali Kushushwa na Singeli.

Baada ya mashabiki kumtupia maneno na kumwambia kuwa amekaa kipindi kirefu bila kutoa nyimbo mpya hivyo kusemekana kuwa amefulia aliamua kuja na kujinadi kuwa hata siku moja yeye hawezi kufulia kwa sababu kwake ni kama kiwanda cha muziki kila siku zinatengenezwa nyimbo mpya.

Msanii wa kike wa Rapper Claudia Lubao maarufu kama Chemical amesema kuwa tangu ameanza kuimba singeli ndipo ameanza kuona kama muziki wake umeshuka kwa sababu muziki aliokuwa akiufanya ulikuwa ni mkubwa sana.

Chemical anasema kuwa heshima yake kwa mashabiki imeanza kushuka tangu alipoanza kujiingiza katika singeli kwa sababu kupitia muziki wake wa kuchana alikuwa tayari ameshawaaminisha mashabiki kuwa anaweza kukaa kwenye game.Hata hivyo Chemical anasema kuwa ingawa singeli inamleta mashabiki wapya ambao ni wapenzi wa singeli lakini wale waliokuwa wakipenda muziki wake wa kuchana wamemshusha thamani ana na wengine atakuwa amewapoteza.

Ukweli ni kwamba siamini sana kupitia muziki wa singeli,ninaamini kuwa muziki niliokuwa naufanya hapo awali ulikuwa mkubwa sana kuliko hata huu wa singeli wa sasa.-Alifunguka Chemical.

Kwa kuongea kuhusu muziki huo wa singeli na hisia za mashabiki wake , Chemical anasema kuwa kwa sasa hajafikiria kabisa kuufanya tena muziki huo labda baadae sana kwa sasa anataka kurudi kwa mwanzo ili kuwaridhisha mashabiki wake wa mwanzo.

Mwaka uliopita Chemical aliamua kufanya singeli ya wimbo uliojulikana kwa jina la kama ipo ipo tu ambao sasa hivi anakiri kuwa uamuzi wake huo umefanya hshima ya muziki wake ishuke na kupoteza baadhi ya mashabiki.

 

Chemical Akanusha Taarifa za Kufulia Kimuziki

Msanii wa kike wa hip-hop nchi chemical amekanusha tetesi zinazosambaa zidi yake kuwa kwa sasa amefulia kumizki na ndio maana amekuwa kimya kwa muda mrefu bila kutoa wimbo wowote.tetesi za kufulia kwa Chemical zinakuja baada ya kuwa kwa kpindi hiki kifupi kuna wasani wengi wa kike wanaofanya muziki kama wake wameibuka na wamekuwa wakifanya vizuri hivyo Chemical amewekwa chini na wanadada wenzake.

Lakini hata hivo akijibu tetesi hizo , Chemical anasema kuwa mashabiki wake wengi wamekuwa wakihisi kama amefulia kwa sababu ya kuwa amejikita sana katika kufanya muziki wa singeli  na kuacha muziki uliomfanya ajulikane sana kwa mashabiki wake.Hata hivyo akiongea kwa kujitetea Chemical amesema kuwa kufanya singeli kwake sio kufulia bali alifanya ili kuwaonyesha mashabiki kuwa anauweoz wa kufanya muziki tofauti tofauti.

Siwezi kufulia hata siku moja kwa sababu mimi chemical ni kiwanda kwa sababu kinajitosheleza kwa uzalishaji wa muziki wa muziki, kwaio watu wanaodhani kuwa nimefulia  wanakosea sana  na kiukweli wategemee kuona mambo makubwa na mazuri kutoka kwangu.-Alisema Chemical huku akiwaahidi mashabiki kuwa anakuja vizuri kimuziki.

Chemical ambae kwa hivi karibuni amekuwa akifanya vizuri na wimbo wao mpya alioshirikishwa na mwana hip-hop mwenzie Pink ambao umekuwa ukifanya vizuri sana katika vyombo mbalimbali.

 

 

Picha Za Chemical na Maxmizer Zaleta Utata.

Kwa muda mrefu msanii wa hip-hop nchini Chemical, amekuwa akijitapa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari  kuwa yeye ni single na hana mpango wa kujiingiza katika mahusiano hivi karibuni,huku akisema kuwa tangu utoto wake hakuwahi kujiingiza katika maswala ya mapenzi na hii ni kutokana na malezi mazuri aliyokulia kutoka nyumbani kwao.

Ilishawahi pia kusikika kuwa mwanandada huyo aliwahi kutamka kuwa yeye ni bikra(hajawahi kushiriki tendo la ndoa) na hii inawezekana iliwavutia wanaume wengi kwa sababu baada ya hapo watu wengi walikuwa wakisikia wakituma maombi kwake na hata yeye alikiri kuwa amekuwa akisumbuliwa sana na wanaume.

Lakini hivi karibuni mwanadada Chemical na Maxmizer walipiga picha na kusambaa katika mitandao ya kijamiiwakionekana wakiwa katika hali flani ya kimahaba, ambapo picha hzio zilizua utata na kuwafanya watu waamini kuwa sasa hivi Chemical ameamua kuachia baada ya kukaza kwa  muda mrefu na kuamua kujiingiza katika mahusiano.

Msanii mwenzie Stereo aliwahi kusikika katikia baadhi ya mahojiano akimuomba kumuoa Chemical lakini alikataa  na kusema kuwa kwa muda ule hakutaka kuwa katika mahusiano, lakini kwa picha zilizoanza kusambaa hivi karibuni zikimuonyesha wana-kiss na Maxmizer zinathibitihsa kuwa mwanadada huyo yuko tayari kwa sasa na amepata yule anaehisi ndie anaemfaa.

Chemical ni moja ya wasanii wa kike chipukizi wanaofanya vizuri katika muziki wa hip-hop , huku mara nyingi akiwa anajiwka katika muonekano wa kiume.