Chini Bees amjibu Chid Benz baada ya kumchana

Baada ya Chid Benz kumwambia msanii mwenzake Chin Bees awembunifu na kutafuta jina lingine…. Chin Bees ameamua kumjibu mwenzake.

Wawili hawa ambao wanaonekana kuwa na beef kutokana na kufanana kwa majina yao, uenda wakakosana baada ya Chin Bees kusema kuwa hawezi kubadilisha jina ili kumkwepa Chid Benz.

 

Akizungumza kwenye mahojiano na E-News ya EATV, Chin Bees ambaye ni mmoja wa wasanii wanaotamba kupiti nyimbo zake za bongo Fleva aliweka wazi kuwa hana mipango ya kubadilisha jina kwa kuwa hata yafanani. Chin Bees alisema,

“Mimi siwezi kubadilisha jina kwa sababu ya Chid Benz kwa sababu halifananini, very different. Mimi nafanya muziki wangu, siwezi nikakaa nipiganie jina, hivyo bro kama anahitaji jina dah!, sidhani kama jina langu linaendana na lake  me am do my thing.”

Haya basi tutazame tuone watakachafanya sasa!

Hii ndiyo sababu ya Chid Benz kumchana Chin Bees

Chid Benz ambaye ni mmoja wa wasanii wa hip hop walioanza kuachia nyimbo zao kitambo ameonelea kumkanya Chin Bees ambaye anatumia jina linalokaribiana na staa huyu.

Sababu za Chidi Benz kumwambia Chin Bees atafute jina lingine ni kwa sababu majina hayo yanafanana na kunauwezekano wa kuwakanganya mashabiki wake.

Ingawa wawili hawa wanafanya nyimbo tofauti Chid Benz anamtaka Chin kuwa mbunifu na kutafuta jina ambalo halifanani na lake. Msanii huyo alisema,

“Siku moja nimeona Shetta anamuangalia Instagram nikamuuliza huyo ni nini?, akaniambia ni Chin Bees, nikamuuliza anafanya muziki gani, akaniambia Bongo Fleva!. Sisemi kwa ubaya ila sikuelewa ile style anayofanya yeye ni tofauti sana na mimi mtu mzima mwenye hit kama 32 najua nikiingia kwenye stage nachapa tu,”

Akipiga stori na Planet Bongo ya EA Radio aliendelea kusema;

“Huyo Chin Bees ana single hata saba kweli?, atafute jina lingine,”