Mh Mwakyembe Aagiza Dudubaya Kukamatwa

Waziri anaeshughulikia maswala ya michezo nchini amefunguka na kutoa amri kukamatwa kwa msanii Dudubaya ambae alianza kutoa maneno ya kashaf kwa marehemu Ruge Mutahaba ambae amefariki siku ya jana jioni,.

Marehemu Ruge alifariki akiwa katika matibabu yake nchi Afrika ya Kusini , huku msanii Dudubaya akiwa ameanza kurusha maneno ya kejeli na matuzi kwa mkurugenzi huyo ambae  alikuwa akipigania afya yake tangu akiwa hai.

Hata baada ya kifo, msanii dudubaya aliendelea kutuma maneno ya kejeli katika mitandao ya kijamii na kukwaza watu wengi na hata kuanza kumlili awaziri mwenye  dhamana hiyo kutaka kumchukulia hatau msanii huyo.

Hata hivyo baada ya saa chache tangu kuripotiwa kwa msanii huyo , tayari msanii huyo ameamuriwa kukamatwa na kuwekwa ndani ili  kuthibiti hali hiyo.

Taarifa hiyo ambayo imetolewa na naibu waziri wa habari ,sanaa na micheoz mh juliana shonza anasema kuwa kwa kushirikiana na BASATA  na polisi wanatakiwa kumkamata msanii DUDUBAYA.

Dudu Baya Aongea na Chid

Msanii Dudu baya amefunguka na kumpa ushauri msanii mwenzake Chid Benz kuwa aache kuendelea  kutumia madawa ya kulevya kwa sababu hayatampeleka kokote zaidi ya kumsababishia kifo kama ilivyowahi kuwasababisia kifo baadhi ya watu aliowahi kuwaona na kuwajua.

Dudu Baya abasema kuwa kwa moyo wake mmoja inabidi chid akatae kutumia dawa za kulevya la siovyo hakuna atakae weza kusaidia zaidi ya kujisaidia yeye mwenyewe.Dudu baya ansema kuwa aanatakiwa kwanza kuogopa kifo ambacho aliwahi kukishuhudia kwa wenzake na ndipo amua kuachana nayo kwa sababu hakuna anayeweza kusaidia hali yake kama atotaka kuanza mwenyewe.

Namshauri Chid benz aache madawa ya kulevya na kinachoniuma ni kwamba aliwahi kushuhudia kabisa kifo cha rafiki yake mangweah lakii bado haoni kama iyo ni hatari, kuna langa pia alishakufa na yeye pia aliwashuhusia watu hao, hakuna mtu anayeweza kusaidia hata kama ni rais magufuli kama yeye mwenyewe na moyo wake haujataka kufanya hivyo. inabidi kwanza akatae kutumia madawa ya kulevya ndipo atarud kwenye level zake.Akiendelea na staili hii wakati tanzania tuna ardhi kubwa , tunachimba tunazika tu.

 

Diamond Ampa Shavu Dudu Baya Kwenye Wasafi Festival

Msanii mahiri wa muziki wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz amempa shavu Nono msanii mkongwe  wa Bongo fleva Dudubaya baada kumtaja kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye taamasha la Wasafi Festival 2018.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Diamond ameweka wazi kuwa kuna wasanii wengi wakubwa ambao hawapati nafasi ya kutumbuiza kwenye matamasha makubwa kwa kisingizio kuwa hawajatoa nyimbo mpya.

Kaka yetu Dudu Baya muda mrefu watu hawajamuona kwenye show ya steji, sasa nawambia kwamba nitafurahi sana akiwepo kwenye show ya Wasafi Festival. Unajua sio tu Dudu Baya peke yake unajua kuna wasanii wengi wana sauti kubwa lakini sometimes hawapewi nafasi kwenye matamasha kwa sababu tu hawajatoa wimbo mwaka huu lakini kuna watu wanawapenda.

so wanaoandaa Wasafi Festival nitaongea nao na Dudu Baya pia wamuweke kwenye tamasha, nitafurahi kwa sababu nilikuwa tu namuonaga kipindi kabla sijatoka namuona anaimba”.

Dudu Baya au maarufu Kama Konki Konki Konki master amejizolea umaarufu Baada ya kendo yake inayoendelea kusambaa ya ushoga na bifu lake na Mange Kimambi.

Dudu baya Amtupia Dongo Ney wa Mitego na Kumwita Mwanamke.

Msanii mkongwe wa bongo felva, Dudu baya amezungumza nawaandishi wa habari na kutoa maodongo yake kwa msanii mweznie ney wa mitego kutokana na kile alichokifanya cha kuingilia ugomvi kati ya Shiloleh na Muna lov ulioibuka siku za hivi karibuni.

Hapa awali kulikuwa na maneno aliyoyatoa sishi baada ya Muna kuongelea swala la mtoto wake aliyefariki na kumtaja baba wa mtoto huku akikana kujua peter ambae wengi walikuwa wakijua kuwa ndie baba wa mtoto, hata hivyo Shiloleh alikwazwa na amneo ya muna na kitendo cha kuita waandisi wakati msiba bado haujaisha na kumwita mnafiki na kwamba anatafuta kiki.

Baada ya maneno ya Shisi, Nay wa mitego nae aliiibuka na kusema kuwa Shiloleh anatafuta kiki ya wimbo mpya kupitia Muna na ndipo dudu baya bae kaibuka na kusema kuwa ukimuona mwanaume kama nay anaingilia maswala ya kike huyo aakuwa na homoni mbili zinamsumbua.

Dudu baya anasema “Ukiona mwanaume yeyote amekurupukia jambo la wanawake na wamezozana na yeye akaegemea upande mmoja, ujue huyo ni mwanamke mwenye homoni mbili yaan ya kiume na ya kike , na ndio maana watu wa hivyo wanaingiliaga  sana mambo ya wanwake , mimi sijawahi kuona hata nicki minaj anaingiliwa na bosi wake, waangalia wakina lily wyne, wakina p.diddy hawaingiliagi hayo mambo wanajua kabisa kuwa ni ya wanawake.

Wasanii Wanamuogopa Dudu Baya Kumsaidia Mtoto Wake

Mtoto wa msanii Dudubaya amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wamekuwa wakitaka kumsaidia lakini wanakuwa wanaogopa kutokana na ukorofi wa baba yake mzazi kwa wasanii wenzake.

Mtoto huyo ambae amekuwa akionekana mitaa ya Coco Beach akifanya kazi anasema kuwa wasanii tofauti kama madee pamoja na Dully sykes wamekuwa wanataka kumsaidia lakini wanakuwa kama wana uoga ambao hata yeye anauona kutoka kwao kutokana na ukorofi wa baba yake.

Hapo nyuma iliwahi kuzka tetesi kuwa mtoto huyo amekataa shule na kutaka kujiingiza katika muziki   ambapo dudu baya mwenyewe alitokwa na povu zito na kusema kuwa ameshindwa kumlea mtoto huyo kutokana na ujinga anaokuwa anauonyesha wa kukataa kusoma na kutaka kuimba muziki.

Alichokiongea Dudubaya Kuhusu BASATA na Wasanii Kufungiwa

Msanii wa bongo fleva Dudubaya amefunguka na kusema kuwa amekuwa akikerwa na tabia ya baraza la sanaa kwa wanawafungia wasanii kazi zao kwa sababu za kuvuja maadili .Kwa kitendo hicho Dudubaya amekiita ni ukurupukaji kwa sababu wanafanya vitu hivyo  bila  kuwa na muongozo maalumu.

Hata hivyo Dudubaya anasema kuwa inakuwa haina maana kuufungia wimbo ambao tayari ulishasambaa katika mitandao na kwenye simu za watu hivyo inakuwa haina maana ya kuufumgia kwa sabau watu nwalishauona.dudubaya anasema kuwa kitendo wanachofanya ni kukurupuka na kufuata mihemuko ya mashabiki lakini lengo lao sio kurekebisha maadili.

Lakini pia Dudubaya alisema kuwa kama BASATA wanataka kufanya lengo lao liweze kufanikiwa ni lazima waweke mkakati wa kufanikisha hilo kwa kuandaa blog ambayo itabidi kazi zote za sanaa zitapitia hapo kabla ya kutolewa kwa mashabiki wao.

Nampongeza sana naibu waizri kuwa nafanya jitihada katika kukuza na kufanya tasnia ikiue lakini pia kutunza maadili ya wasanii,lakini nimekuwa nikikerwa sana na swala la kufungiwa kwa wasanii hasa audio na video za wasanii kwa sababu hazina maadili wakati tayari zilishatapakaa mitaani na katika simu za watu.wanachofanya ni kukurupuka tu kama mtu aliyekuwa amezama kwenye maji.

Dudu baya anasema kuwa watakapo anzisha blog wa ajili ya kuweka nyimbo na audio za wasanii itakuwa ni vizuri na itasaidia kutangaza kazi za wasanii kwa sababu kila wimbo utakapitia hapo na wao watakuwa ndio watu wa mwisho kutoa go-ahead kuwa nyimbo hiyo ipo sawa na imekaguliwa na kuthibitishwa kuwa inafaa kusikilizwa na watu, akitolea mfano anasema kuwa mbona vyakula vinakaguliwa na TFDA.

 

Dudu Baya Ataja Wasanii Wenye Tabia Mbaya

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Dudu Baya amezidi kutawala vichwa vya habari kwa mwaka 2017 na hajatawala vichwa vya habari kwa ajili ya mziki wake hapana bali ni bifu lake la siku nyingi na msanii mwenzake Mr. Nice na skendo ya kumtelekeza mtoto wake Wille ndivyo vitu vinavyozidi kumuweka kwenye chati.

Kama kawaida yake Dudu Baya ni mmoja wa wasanii wababe ambaye anaweza akasema kitu chochote bila kumuogopa mtu yoyote na kwa kutambua hilo Dudu Baya ameibuka na kutaja wasanii watano wenye tabia mbaya.

Dudu Baya akifunguka kuhusu listi hiyo alipofanya mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa kupitia kipindi cha Enews ambapo alifungukaa mengi kama yafuatayo:

Kuna mambo mengi yanaendelea kwenye industry hii ya Bongo fleva na kusema kuna vitu vinakera kwa kweli lakini tunashukuru wakati sisi tunaanza mziki vyombo vya habari havikuwepo pia social media hazikuwepo leo hii zipo lakini hizi instagram zimetokea ughaibuni lakini wenzetu waliozileta hawazitumii kujizalilisha kama wasanii wetu wanavyofanya”.

Hawa ni wasanii ambao Dudu Baya amewataja kama wasanii wenye tabia mbaya:

1. Nuhu Mziwanda na Shilole

Nuh Mziwanda na Shilole walikuwa wanaongoza kwa kupiga picha za uchi kipindi kile wako wote na wanazirusha mtandaoni na pia walikuwa wanaweka video wanaoga bafuni kwani nani asiyeoga hapa duniani?

2. Young Dee

Huwa namkubali huyu mdogo wangu Paka rapa lakini aliharibu ,waka huu pale aiporushia mapicha mtandaoni akiwa uchi na Amber Lulu akimshika makalioni akijua kabisa yeye ni baba.

3. Nuh Mziwanda

Nuhu aliposti mistari ya wimbo eti “aliyelala na bibi harusi siku moja kabla ya harusi na wala sio bwana harusi wakati sio bwana harusi?” huo ni ujinga aliofanya akijua wazi kabisa kuwa mwenzake amefunga ndoa

4. Gigy Money na Amber Lulu 

Haw ndio wameongoza mwaka 2017 kwa picha zao za chi mitandao ni hawa wote ni wadogo zangu nawaheshimu lakini lazima.

Dudu Baya Amwagia Povu Kali Mwanaye Wille Baada ya Tuhuma za Kumtelekeza

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Dudu Baya ambaye kwa muda sasa amekuwa akishutumiwa kupitia mitandao ya kijamii kwa kumtelekeza mtoto wake wa kiume mwenye miaka 17 anayeitwa wille ambapo inasemekana kuwa Dudu Baya alikataa kumsomesha mtoto huyo.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5 Dudu Baya alikataa tuhuma hizo na kudai kuwa alimlea mwanaye huyo kwa miaka kumi na tatu hivyo hawezi kumtelekeza;

“Mara ya mwisho nilimtafuta Wille akaja Mikocheni tukalala mpaka kesho yake nikampa zawadi zake zilikuwa pea mbili za raba tukaaga kuwa anarudi shule lakini hapo kuna tetesi nilisikia kuwa na yeye anaimba muziki anaimba maskani huko Mwananyamala kwaiyo kama mzazi nikajiuliza kama mzazi na mtoto wamekutana halafu humwambii baba ako kuwa unaimba na baba ako ni star, baadae napita mitaani naambiwa Wille anapatikana tu hapa maskani hayupo shule wala nini na shule ameshaacha Dah! kiukweli kama mzazi nilishtuka kwa sababu nampenda sana mwanangu na mi nimeishi tangu mdogo mwaka 2013 ndo mama yake alimuomba nikampa lakini nilikuwa naclear kila kitu lakini nimekuja kusikia ameacha shule kwa miezi tisa wakati nilikuwa nalipa ada kama kawaida na matumizi mengine lakini kinachonishangaza zaidi mama yake anajua haya yote lakini nasikia na mama yake yupo upande wake na wanagawana pesa za shule”.

Dudu Baya aliishia kwa kumwagia povu mwanaye;

“Lakini kwa kitendo alichofanya cha kuacha shule kuwa anakamatwa na polisi akalala ndani  Mimi kama Dudu Baya na baba yake sina kinyongo naye wala sina chuki naye japo amenidanganya anasoma shule kwa miezi tisa na haendi shule na anipiga hela kwa hilo nimemsamehe kwa kuwa ngamia huwezi ukampeleka kisimani ukamchapa anywe maji kama kaamua kuacha shule ni kijana wa miaka 17 siwezi kumlazimisha kwani anajitambua kama mi nilimwambia twende kulia kataka kwenda kushoto kila lakheri huko kushoto kwani maandiko matakatifu mwenyezi Mungu aliandika ‘mtoto mwenye hekima na busara humfurahisha babaye’ na toto jinga shenzi na pumbavu ni mzigo kwa mama na sio zigo kwa baba kwaiyo kwangu mimi simtafuti akiwa tayari anitafute aniombe msamaha kwani milango kwangu iko wazi.

Dudu Baya awaonya wanaopiga picha za uchi

Imekuwa kama ni desturi kwa  hivi karibuni kwa baadhi ya kina dada tena hasa wasanii wa kike chipukizi  kupiga picha za uchi na kuzipost katika mitandao ya kijamii, tena wengine wakiwa hawana nguo kabisa hata moja  huku wakijitetea kuwa iyo ni sehemu ya kazi zao zinazowaingizia kipato.Wakati hali inakuwa tofauti kwa wakaka ambao kazi zao huwa ni za heshima na huwezi kukuta mwanaume anapiga picha za uchi na kuzirusha mitandaoni.

Msanii mkongwe wa muziki nwa Bongo Fleva alikuwepo toka kitambo ambae alikuwa ni mmoja kati ya walioinua muziki wa Tanzania  Dud baya aamua kuongelea swala hilo.

Alipokuwa akiongea na Bongo5 na kuojiwa maoni yake kuhusu wadada wanaopiga picha za uchi mitandaoni Dudu baya alionyeshwa kukerwa sana na tabia hiyo na kulaani vibaya, Dudu baya anasema kuwa mwanamke wa dizaini iyo si mcha Mungu na hana heshima katika jamii anayoishi kwa sbabau siku zote biashara yoyote ile nzuri huwa inanunulika yenyewe.

katika maongezi yake na bongo 5 Dudu baya anasema kuwa “dunia imekuwa kama Sodoma na Gomora saivi, na ikifikia hataua ya kuweka matangazo ya biashara mitandaoni inamaana biashara imekuwa ngumu” akimaanisha kuwa wadada wa aina iyo basi kuna biashara wanaifanya ivyo wanapopost picha basi wanaitangaza biashara iyo.

Dudu baya ametolea mfano wa waganga wa kienyeji kuwa waganga wa ukweli ni wale ambao wapo kijijini na hawajitangazi, lakini unapoona bango la mganga wa kienyeji basi huyo ni muongo ,hivyo wanaopiga picha za uchi hawana uhalisia wowote.

“kama wewe ni mkali, hata ukivaa buibui utaonekana tu, uzuri wa mwanamke hauwezi kwa kutumia carolite,uzuri wa mwanamke sio kwa kuongeza makalio, wala sio kwa kujichubua ,bali ni tabia njema, nidhamu, heshima, na kumcha Mungu ndio maana hao wanaangaika mitandaoni”

Dudubaba ameishauri serikali kuhusu nini cha kuwafanya wakina dada hao wanaowekaa  picha za uchi , anasema “serikali wajaribu kuwakamata hao wanaopiga picha za uchi ,wasiseme wanaume hatujui kutongoza”