Eric Shigongo Asema Menejiment ya Daimond Ndio Sababu ya Kugombana Kwao

Mjasiramali na mtunzi wa vitabu kutoka nchini  Tanzania Eric shigongo amefunguka mazito kuhusu bifu lililokuwepo kati yake na msanii Diamond Platinumz na kusema kuwa sababu kubwa ya kutokupatana kwao ilikuwa ni uongozi wa Diamond ambao haukuwa unamuongoza kama alivyotakiwa kuongozwa.

Katika makala yake ndefu aliyoiandika, Eric alianza kwa kumpongeza lakini hku akisema kuwa alichokifanya mwaka huu ndicho kilichowagombanisha miaka kadhaa iliyopita na menejiment yake kwa sababu ya tamasha aliloliandaa ambalo lilikuwa la wazi kwa wananchi wa Tandale.

eric anasema kuwa aliamua kuwaalikia wsanii mbalimbali katika moja ya matamsha makubwa aliyoamua kufanya tandale na kwa sababu aliamini kuwa diamond ametokea huko basi tamasha linaweza kuwa lenye mafanikio kwa sababu lengo lilikuwa ni kuwarudishia maskini fadhila na kuwa nao karibu.

Eric anasema kuwa kutokana na uongozi wake unaomshauri sana Diamond wamekuwa wakimshauri sana kufanya shoo nje ya nchi kuliko za humu ndani bila kujali kuwa kuna watu wengi sana wanaompenda msanii huyo nchini na hata kufikia kuiga baadhi ya vitu vyake kama kutengeneza nywele na kuvaa mashati yenye jina lake.

Hata hivyo Eric aanasema baada ya kuyaona hayo yote, aliamua kundika makala ya kumhusu diamond huku akitaka kumshauri kwa baadhi ya mambo kama hayo lakini cha ajabu viongozi wake akiwemo Babu tale aliamua kumchambua sana Eric na mpaka akuhojiwa katika kipindi cha shilawadu huku akiogea maneno yasiyo na busara kumhusu.

Hata hivyo Eric anasema kuwa baada ya hapo hakupata kuwasiliana tena na WCB mpaka wiki iliyopita alipopigiwa simu na Babu tale tena akimtaka kuhudhuria tukio ambalo siku zote yeye amaekuwa akiomba wasanii walifanye na ndo maana hata hakukataa kwa sababu aliamini ni jambo muhimu.

Kwa kumalizia Eric anaona kuwa alichokifanya Diamond ni kitu chema na ameona jinsi gani wasanii wamekuwa na faida kubwa katika jamii inayowazunguka ,

 

Eric Shigongo: Diamond Asipoangalia Atapotezwa na Mameneja Wake

Mkurugenzi mtendaji wa Global Publishers na Mjasiriamali Eric James Shigongo amefunguka kuhusu supastaa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kudai kuwa pamoja na kipaji chake lakini anaweza akaja kupotezwa na uongozi wake.

Shigongo aliyejipatia umaarufu kwa kichapisha vitabu na magazeti amekiri kuwa anavutiwa na Diamond kwa sababu anaona kama wote wana historia sawa ambapo wote wametokea kwenye familia au maisha ya hali duni ambapo amekiri amekua katika maisha magumu maana mama yake alikuwa anauza vitumbua lakini amekuja kujikwamua na kujitengenezea maisha mazuri kama Diamond.

Shigongo alifunguka hayo kwenye barua ya wazi aliyomuandikia kwenye mtandao wa Instagram siku za nyuma kidogo, ambapo aliandika:

Nampenda Diamond sana tena sana (sina uhakika kama analijua hili)  I am too proud of him ni fighter (mpiganaji) kutoka Tandale mpaka Beverly Hills with Neyo kwenye video ya wimbo wa Marry you ambao nimetoka kuuangalia    Kwenye YouTube hakika sio kitu kidogo.

Nafahamu kwa sababu niameanzia chini sana kimaisha, Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania.  Bila elimu kubwa bila connection bila fedha, ameweza kuvuta vizingiti vyote hadi kufika hapo alipo leo hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. Bravo!

Lakini nina machache ya kusema naomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi kama kaka na Mtanzania mwenzake niseme huko anakoelekea kuna shimo asiporuka atatumbukia na huo utakuwa mwisho wake. 

Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu nao ni Naseeb Abdul, Babu Tale na Salaam Sk. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti”.

 

 

Meneja wa Diamond Babu Tale amrarua mmiliki wa kampuni ya Global Publishers Eric Shigongo

Eric Shigongo alianza mgogoro na Wafasi alipodai kuwa Diamond anaingizwa shimoni na Naseeb Abdul, Babu Tale na Salaam.

Soma pia: “Diamond anapelekwa kwa shimo na watu watatu” Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers aonya

Babu Tale amemjibu Eric Shigongo kwa Instagram:

“Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kwenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya… baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo insyagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako…

“Siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata..ila kesho ukawaambie vizuri waamdishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wengine na watu mbalimbali…

Babu Tale

“Tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu… Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond… ila sie kaa kimya… na kujifanya unazungaa eti unatushauri… kweli mtu unasema unampenda unamshauri instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?… Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini?…na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya Harmonize DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi “kupost tumepost… ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilika na kutak asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa…tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa…

“Hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na mashabiki zao hii ndio kuwaeka wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe… mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula madawa…yote kutafuta sababu msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kumbomoa msanii kupitia magazeti yako…tafadhali heshimu heshima yetu kwako…”Mh Magufuli tafadhali ulipo kaza legeza, ona wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoot vidogo vyao….”

Eric Shigongo na Diamond

 

 

“Diamond anapelekwa kwa shimo na watu watatu” Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers aonya

Eric Shigongo, mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, amekiri kuwa Diamond ni mfano mwema wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi Tanzania na ata duniani kote.

Shigogo amesema hit maker huyo ameweza kuvuka vizingiti vyote maishani na kuwa msanii wa kutajika nchini Tanzania na ata barani.

Lakini Shigogo ameonya kuwa Diamond anaelekea shimoni. Mmiliki huyo wa Global Publishers aliandika barua yenye ujumbe kwa Diamond kupitia mtandao wa Instagram;

“Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo.

“ Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha. Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania. Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. BRAVO! LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake. Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE. Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti.”

Eric Shigongo na Diamond