Aikah Afunguka Mpango Wa Kuzaa Mtoto Mwingine

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika kundi la Navy Kenzo Aikah Mareale amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kuzaa mtoto mwingine na mpenzi wake Nahreel.

Aikah alijifungua mtoto wake wa kwanza anayeitwa Gold Navykenzo mapema mwaka huu na mpenzi wake wa siku nyingi Emmanuel Mkono maarufu kama Nahreel.

Lakini Gold akiwa na Miezi michache tu Aikah amefunguka na kusema yupo mbioni kutaka kuongeza mtoto mwa pili.

Kwenye mahojiano na Risasi Vibes, Aika amesema kuwa tangu amezaa mtoto mmoja ameona raha kuwa mama hivyo basi hana muda wa kujishauri tena bali ni kumleta mdogo wa Gold, mapema wala hana muda wa kupoteza.

Najisikia furaha sana kuwa mama hata wa watoto watano hivi nimeona raha ya kuzaa na hivi sasa niko njiani kuleta mtoto mwingine mambo ya kupishana muda mrefu sio sawa kabisa”.

Aikah na Nahreel wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka zaidi ya kumi Lakini hivi karibuni walisema hawana haraka ya kufunga ndoa kwani kuwa na bond ni muhimu zaidi.

“Nipo Tayari Kuzaa Mtoto Mwingine”- Aikah

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka kundi la Navykenzo, Aikah Navykenzo amefunguka kuhusu mipango yake ya kuzaa mtoto mwingine hivi karibuni.

Aikah ambaye alijifungua mtoto wake wa kwanza miezi miwili iliyopita na  mpenzi wake wa miaka mingi Nahreel amekiri kuwa ana mpango wa ‘kutengeneza’ wengine zaidi ya huyu aliyenaye sasa.

Gold Navykenzo

Tarehe 9 December mwaka jana Aikah alijifungua mtoto wake wa kwanza waliyemuita Gold Navykenzo lakini siku ya jana miezi miwili baadae Aikah kashasema anataka kuzaa mtoto mwingine.

Gold akiwa na Baba yake Nahreel

Siku ya jana ilikuwa ni sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaa kwa Aikah na kupitia ukurasa wake wa Instagram Aikah alifunguka kuhusiana na mipango yake ya kuzaaa mtoto mwingine ambapo aliandika maneno haya machache:

Najisikia msichana mbichi zaidi na nipo huru zaidi kwenye mwili wangu mwenyewe niko tayari kufanya kazi kwa nguvu zaidi, kutengeneza muziki mzuri, kusafiri na kuzunguka duniani na hata nipo tayari kwa ajili ya kuzaa watoto wengine… Nashukuru kwa kunitakieni heri katika siku yangu ya kuzaliwa nawapenda wote”.

Tangu ajifungue Aikah na Nahreel wamerudi kwenye jitihada zao za kutengeneza mziki kwani ni wiki chache zilizopita walienda nchini South Africa kurekodi video ya nyimbo yao mpya lakini inasemekana kuwa walisafiri na mtoto wao Gold.