Navy Kenzo Watangaza Ndoa hivi Karibuni.

Wasanii wa zamani wanaounda kundi la Navy kenzo Aika na Nahreel wametangaza ndoa yao inayotarajiwa kufungwa hivi karibuni huku ndoa iyo ikionekana kutarajiwa kufanyika huko kijijini kwao moshi,

Katika ukurasa wa instagram wa nahreel aliweka picha inayowaonyesha wakiwa Egypt wakisherekea siku  ya kumbukumbu ya kuzaliwa na Nahreel huku wakiandika kuwa ndoa coming soon na kufuatiwa na comments za wasanii mbalimbali akiwepo vannesa mdee.

Katika picha hiyo aliandika ” more life, more love , love you @aikanavykenzo  soon wedding... ”

Hata baada ya maneno hayo wasanii walianza kuwapongeza na kuwatakia kheri katika maamuzi hayo wanayotaka kuyachukua.

Kwa zaidi ya miaka kumi wawili hao wamekuwa pamona na kufanikiwa kupata mtoto mmoja anaitwa GOLD

Aikah Afunguka Kuhamia WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Kutoka katika kundi la Navy Kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuongolea taarifa za kuhamia WCB.

Baada ya kutoa hit single ambayo inaendelea kufanya vyema mpaka sasa ‘Katika’ waliomshirikisha Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuliibuka tetesi kuwa Nahreel na Aika wamehamia chini ya WCB.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers , Aika  amesema kuwa, amekuwa akisikia kwa watu wengi juu ya kuhamia WCB mara baada ya kuachia wimbo wao  na Diamond jambo ambalo halina ukweli.

Yaani watu wengi wanasema nimehamia WCB lakini ukweli ni kwamba tuna meneja anayetokea huko anaitwa Sallam na amekuwa akitusimamia sasa sijui hayo mengine yanatokea wapi.

Nilikaa na mwenzangu tukatunga Wimbo wa Katika tukaona ni vizuri tukamshirikisha Diamond ndiyo ikawa hivyo sasa nashangaa hao wanaoungaunga maneno”.

Tetesi hizo za Kuhamia WCB zilipamba moto mara baada ya Msanii kutoka WCB Harmonize kusema wazi kuwa wasanii hao wanahamia Kwenye Label yao taarifa ambazo Navykenzo walidai ulikuwa ni utani.

Aikah Aandaa Navykenzocup Kwa Ajili Ya Watoto Wa Mitaani

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika kundi la Navykenzo, Aikah Mareale amefunguka na kuelezea jinsi alivyosaidia watoto wa mitaani baada ya kuwakusanya na kutengeneza Navykenzo Cup.

Aikah ameeleza hayo wakati akiwa anatamba kuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja na si kutegemea muziki tu.

Katika mahojiano na Ijumaa Wikienda, Aika alisema kwa sasa anafanya kazi tofauti za kijamii kama kuwakusanya watoto wa mitaani ambao wanaweza kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu.

Pamoja na kuwa mimi ni mwanamuziki na mama pia namuomba Mwenyezi Mungu anisaidie jukumu hili lingine la kuchukua watoto wa mitaani na kuunda timu ili waweze kushindana na kuonesha vipaji ili baadaye wacheze kwenye timu kubwa“.

 

Aikah Afunguka Mpango Wa Kuzaa Mtoto Mwingine

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika kundi la Navy Kenzo Aikah Mareale amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kuzaa mtoto mwingine na mpenzi wake Nahreel.

Aikah alijifungua mtoto wake wa kwanza anayeitwa Gold Navykenzo mapema mwaka huu na mpenzi wake wa siku nyingi Emmanuel Mkono maarufu kama Nahreel.

Lakini Gold akiwa na Miezi michache tu Aikah amefunguka na kusema yupo mbioni kutaka kuongeza mtoto mwa pili.

Kwenye mahojiano na Risasi Vibes, Aika amesema kuwa tangu amezaa mtoto mmoja ameona raha kuwa mama hivyo basi hana muda wa kujishauri tena bali ni kumleta mdogo wa Gold, mapema wala hana muda wa kupoteza.

Najisikia furaha sana kuwa mama hata wa watoto watano hivi nimeona raha ya kuzaa na hivi sasa niko njiani kuleta mtoto mwingine mambo ya kupishana muda mrefu sio sawa kabisa”.

Aikah na Nahreel wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka zaidi ya kumi Lakini hivi karibuni walisema hawana haraka ya kufunga ndoa kwani kuwa na bond ni muhimu zaidi.

Navykenzo Watia Msisitizo Kuwa ‘Fela’ Haijabuma

Wasanii kutoka kundi la Muziki la Navykenzo Nahreel na Aikah Marealle wamekana maneno maneno yanayosemwa dhidi ya single yao mpya inayoitwa ‘Fela’ kudaiwa kubuma.

Navykenzo walitoa Fela siku chache zilizopita lakini kuna tetesi kuwapatanisha wimbo huo umebuma kwani haujapata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Vibes Aikah ameweka wazi kuwa wimbo wao mpya wa Fella, haujabuma bali unafanya vizuri na kipimo cha wimbo kufanya vizuri kwao si ‘views’ za Mtandao wa YouTube pekee.

Wimbo wa Fella unafanya vizuri, kwenye media mbalimbali, anayesema umebuma atakuwa si mfuatiliaji mzuri wa muziki na ‘trend’ ya muziki kwa jumla”.

Navykenzo ambao wamekuwa na kawaida ya kutoa nyimbo ambazo siku zote zimekuwa zikifanyavizuri kama vile Kamatia chini na game na nyinginezo wamesisitiza na Fela ipo kwenye kundi hilo.

NavyKenzo Kutoa Shilingi Milioni Mbili Kwa Shabiki Mmoja

Kikundi cha muziki wa Bongo fleva cha NavyKenzo kinachoundwa na wasanii wawili ambao ni Nahreel na Aikah wamekuja na zawadi ya pesa taslimu kwa ajili ya mashabiki zao.

NavyKenzo wametangaza zawadi hiyo nono baada ya kuachia ngoma yao mpya inayoitwa ‘Fella’ ambapo shabiki atajinyakulia kitita hicho cha pesa kama atacheza wimbo huo.

NavyKenzo wametangaza zawadi hiyo nono Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo wameandika:

Fella Dance challenge, Winner get 1000usd, Tunatoa dola 1000 ambayo ni  sawa na milioni 2 na lakini 2 kwa mshindi tuma clip yako”.

Fella ni wimbo wa kwanza kwa Navy Kenzo kutoa mwaka huu tangu pale walipomshirikisha Patoranking katika wimbo wao unaokwenda kwa jina la Bajaj uliotoka June 19, 2017.

“Nipo Tayari Kuzaa Mtoto Mwingine”- Aikah

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka kundi la Navykenzo, Aikah Navykenzo amefunguka kuhusu mipango yake ya kuzaa mtoto mwingine hivi karibuni.

Aikah ambaye alijifungua mtoto wake wa kwanza miezi miwili iliyopita na  mpenzi wake wa miaka mingi Nahreel amekiri kuwa ana mpango wa ‘kutengeneza’ wengine zaidi ya huyu aliyenaye sasa.

Gold Navykenzo

Tarehe 9 December mwaka jana Aikah alijifungua mtoto wake wa kwanza waliyemuita Gold Navykenzo lakini siku ya jana miezi miwili baadae Aikah kashasema anataka kuzaa mtoto mwingine.

Gold akiwa na Baba yake Nahreel

Siku ya jana ilikuwa ni sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaa kwa Aikah na kupitia ukurasa wake wa Instagram Aikah alifunguka kuhusiana na mipango yake ya kuzaaa mtoto mwingine ambapo aliandika maneno haya machache:

Najisikia msichana mbichi zaidi na nipo huru zaidi kwenye mwili wangu mwenyewe niko tayari kufanya kazi kwa nguvu zaidi, kutengeneza muziki mzuri, kusafiri na kuzunguka duniani na hata nipo tayari kwa ajili ya kuzaa watoto wengine… Nashukuru kwa kunitakieni heri katika siku yangu ya kuzaliwa nawapenda wote”.

Tangu ajifungue Aikah na Nahreel wamerudi kwenye jitihada zao za kutengeneza mziki kwani ni wiki chache zilizopita walienda nchini South Africa kurekodi video ya nyimbo yao mpya lakini inasemekana kuwa walisafiri na mtoto wao Gold.

 

Angalia Picha na Video za Mtoto wa Aikah na Nahreel Navykenzo

Wanamuziki wanaounda kundi la Navykenzo, Aikah na Nahreel waliotamba na vibao kama kamatia chini, game, bajaji na nyinginezo wamemkaribisha mtoto wao wa kwanza wiki chache zilizopita.

Wapenzi hawa ambao wana sifa nzuri ya kuweka mahusiano yao mbali na mitandao ya kijamii na kwenye mitandao wanachoweka ni kazi tu, walitangaza kuwa Aikah ni mjamzito wakati tayari mrembo huyo ana mimba ya miezi saba.

Wamepata mtoto wa kiume anayeitwa Gold Navykenzo ambaye mpaka sasa Gold ni balozi Wa duka la nguo za watoto la Kids shopping center.

Hizi ni baadhi ya picha na video za Gold akiwa na wazazi wake Nahreel na Aikah.

                   Gold Navykenzo
                    Gold Navykenzo

 

Gold akiwa na baba yake

Angalia Jinsi Nahreel na Aika Walivyotangaza Ujauzito Wa Aika (picha)

Wanamuziki Nahreel na Aika au kwa pamoja maarufu kama ‘Navykenzo’ wameweka wazi ujio wa mtoto wao jana usiku kwa kupitia kurasa zao za Instagram.

Wawili hao ambao  sio tu wanamuziki toka kundi moja la Navykenzo bali pia wamekuwa wapenzi kwa miaka zaidi ya tisa wametangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto hivi karibuni ingawa hawajatoa taarifa za zaidi lakini kilichovutia wengi ni staili waliyotumia kutangaza jambo hili la baraka.

Aika na Nahreel waliweka picha ya chumba cha mtoto kwenye nyumba yao wanayopenda kuiita Casadekenzo baada ya muda watu mbalimbali walianza kuwapongeza.

Nahreel aliweka picha hii kwenye ukurasa wake wa Instagram
Aika aliweka picha hii kwenye ukurasa wake wa Instagram

Nahisi wametimiza maneno yao kwani mapema mwaka huu kwenye mahojiano aliyoyafanya na East Africa tv, waliweka wazi wanategemea kuhamia kwenye jumba lao la kifahari walilo jenga lakini pia wanataka mtoto maana nyumba ni kubwa sana.

NavyKenzo ni kundi la mziki wa kizazi kipya ambao wametamba na vibao vyao kama ‘game’ ‘kamatia chini’ na hivi sasa wanafanya vizuri na wimbo wao wa ‘bajaji’.