Aika Afungukia Skendo Za Diamond Kuwadhalilisha Wanawake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetokea katika kundi la Navykenzo, Aikah Marealle ambaye hivi sasa pamoja na mpenzi wake Nahreel wanafanya vizuri na ngoma yao ya ‘Katika’ amefunguka na kumuongelea Diamond Platnumz.

Aikah na Nahreel wameonekana kuwa na ukaribu mkubwa na Diamond hii ni baada ya kumshirikisha katika ngoma yao ya Katika lakini kuna tetesi zilisambaa kuwa kundi hilo Lina mpango wa kusainiwa chini ya WCB tetesi zilizokataliwa na Navykenzo.

Lakini pia siku za hivi Karibuni Diamond amekuwa akinyoshewa sana vidole kwa tabia yake anayo tuhuma ya kumdhalilisha wanawake ambapo mashabiki walimjia juu kwa vitendo ambavyo vilimuonyesha kama hawaheshimu wanawake waliomzalia ambao ni Mobetto na Zari.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Aikah alihojiwa kuhusu tuhuma hizo za Diamond kudhalilisha wanawake ambapo alifunguka kwa kusema:

Mimi huwa siwezi kumhukumu mtu na maisha yake na kila anachoamua kukifanya, ila ni mtu ambaye nimekaa na Diamond kwa nyuma ya pazia ambapo naona jinsi anavyoishi na watu vizuri, hao wanawake wote mnaosema anawadhalilisha anaishi nao vizuri na anawajali“.

Lakini pia Aikah aliulizwa kuhusu mstari ambao umesikika Kwenye wimbo huo ambapo Diamond alimtaja Hamisa kuhusu uchawi na matunguli:

Tena huo ndio ubunifu ambao unatakiwa katika muziki maana kitu kinapokuwa kinaongelewa halafu ukakiweka katika muziki ili kuburudisha watu inakuwa sio kitu kibaya sisi tuliona kawaida na ni njia ya kufanyabiashara na nina uhakika hata muhusika mwenyewe alipokisikia alikifurahia”.

Aika amesisitiza kuwa hana tatizo na Hamisa na ni mtu wake ambaye anachat naye mara kwa mara.

Aikah Afungukia Miaka 10 Ya Mahusiano na Nahreel

Msanii kutoka kundi la Navy Kenzo, Aikah Mareale amefungukia na kuongelea Mahusiano Yake yaliyodumu kwa miaka 10 na mpenzi wake Msanii na mtayarishaji wa muziki Nahreel.

Wiki iliyopita Nahreel na Aikah walisheherekea miaka kumi ya kuwa pamoja tangu walipokutana kwa mara ya kwanza nchini India walipokuwa kimasomo.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers , Aika alifunguka kwamba ndani ya miaka hiyo waliyoishi pamoja kama marafiki wakubwa, wapenzi na watu wanaosi-kilizana, imeweza kuwafundisha vitu vingi kwa sababu wamepitia changamoto nyingi hadi kufika hapo.

Ulishawahi kukaa na mtu miaka 10, lakini unaona ni kama jana tu? Hii ni kutokana na jinsi mlivyoishi katika upendo na urafiki mkubwa, ndivyo tulivyo mimi na Nahreel na tunaunganishwa zaidi na mtoto wetu, Gold“.

Pamoja na kwamba Aikah na Nahreel wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Gold lakini wameweka wazi hawana papara ya kuoana kwa sasa endapo muda Ukiwa tayari watafunga ndoa.

Aikah na Nahreel Washeherekea Miaka Kumi Ya Mahusiano

Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo ambao wamehusika kutoa hit songs kama Game na Kamatia chini,Producer Nahreel na Aikah Mareale wanasheherekea miaka kumi ya Mahusiano.

Baada ya kuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka kumi Nahreel na Aikah  tayari wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume mapema mwaka huu anayeitwa Gold.

Wasanii hao walikutana miaka kumi iliyopita nchini India ambapo wote walikuwa wameenda kimasomo na kuanzisha Safari yao ya mapenzi pamoja na kufanya Muziki pamoja.

Pamoja na kuwa wote kwa miaka kumi sasa wasanii hao wameweka wazi kuwa hawana haraka ya kufunga ndoa kwa sababu tu maneno ya watu bali watafunga ndoa pale watakapokuwa tayari.

Wapendanao hao wameonekana wakila bata katika viwanja mbali mbali katika visiwa vya Zanzibar na hata kuandikiana posti za kimahaba Kwenye mitandao ya kijamii:

https://www.instagram.com/p/BnTQZxIARXF/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=rwp3x59l4rn8

https://www.instagram.com/p/BnUCar7nctO/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=167fp4g7z53ei

“Nipo Tayari Kuzaa Mtoto Mwingine”- Aikah

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka kundi la Navykenzo, Aikah Navykenzo amefunguka kuhusu mipango yake ya kuzaa mtoto mwingine hivi karibuni.

Aikah ambaye alijifungua mtoto wake wa kwanza miezi miwili iliyopita na  mpenzi wake wa miaka mingi Nahreel amekiri kuwa ana mpango wa ‘kutengeneza’ wengine zaidi ya huyu aliyenaye sasa.

Gold Navykenzo

Tarehe 9 December mwaka jana Aikah alijifungua mtoto wake wa kwanza waliyemuita Gold Navykenzo lakini siku ya jana miezi miwili baadae Aikah kashasema anataka kuzaa mtoto mwingine.

Gold akiwa na Baba yake Nahreel

Siku ya jana ilikuwa ni sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaa kwa Aikah na kupitia ukurasa wake wa Instagram Aikah alifunguka kuhusiana na mipango yake ya kuzaaa mtoto mwingine ambapo aliandika maneno haya machache:

Najisikia msichana mbichi zaidi na nipo huru zaidi kwenye mwili wangu mwenyewe niko tayari kufanya kazi kwa nguvu zaidi, kutengeneza muziki mzuri, kusafiri na kuzunguka duniani na hata nipo tayari kwa ajili ya kuzaa watoto wengine… Nashukuru kwa kunitakieni heri katika siku yangu ya kuzaliwa nawapenda wote”.

Tangu ajifungue Aikah na Nahreel wamerudi kwenye jitihada zao za kutengeneza mziki kwani ni wiki chache zilizopita walienda nchini South Africa kurekodi video ya nyimbo yao mpya lakini inasemekana kuwa walisafiri na mtoto wao Gold.