“Uwoya Chaguo Lake Lilikuwa Ndikumana Sio Dogo Janja”-H.Baba

Msanii wa muziki wa Dansi nchini Hamisa Ramadhan maarufu kama H. Baba ameibuka na kutoa Nemo kuhusu mahusiano ya msanii wa Bongo fleva Dogo Janja na Alice Kuwa mke wake msanii wa Bongo movie Wema Sepetu.

H. Baba ambaye aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Uwoya miaka ya nyuma amedai Dogo Janja hakuwa type ya Uwoya Baya kidogo kwani yeye huwa anapendelea wanaume aina ya Marehemu mumewe Ndikumana.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, H. Baba alifunguka kuwa Dogo Janja na Uwoya  wasingeweza kudumu kwenye ndoa kwa sababu mwanamama huyo chaguo lake lilikuwa ni Ndikumana pia anapenda wanaume warefu wenye nguvu na miili ya mazoezi.

Unajua Uwoya chaguo lake lilikuwa ni Ndikumana ila Mungu alimpenda zaidi, kwa Janjaro sidhani kama atamuweza maana Uwoya anapenda wanaume warefu wenye nguvu na miili ya mazoezi.

Lakini pia H. Baba amemshauri Dogo Janja akomae kumuomba msamaha mrembo huyo kwani no mke wake halali wa ndoa:

Uwoya angenitema kama Dogo Janja ningeumia sana yaani ningeandamana kutoka Dar mpaka Mwanza kwa miguu maana mke anauma sana lakini  Namshauri Dogo Janja akomae kama ataweza ukomavu kurudisha penzi ila Uwoya ana maamuzi yake binafsi akisema sikutaki ndiyo kamaliza”.

 

 

H.Baba Aongea na Diamond kwa Kilichotokea kwa Mavoko.

Msanii wa muziki wa dansi nchini H.Baba  amefunguka na kelezea mtazamo wake kuhusu kile kinachoendelea kwa sasa kati ya rich mavoko na WCB huku akisema kuwa haiwezekani WCB wakawa wanyonyaji lakini kama kuna kitu chochote pande hizo mbili wanapaswa kukaa chii na kuongea tofauti zao na kuzimaliza.

katika ukurasa wake wa instagra, H.baba aliandika ” Diamond platinumz pole sana , nadhani sasa ni muda wako wa kujifunza maisha na watu na kuzingatia vitu viwili, umakini wako wewe sio kila mwanadamu ana umakini kama wako.kujitambua wewe, kujipambanua na kumheshimu Mungu sio kwa kila mdharau mwiba.

kama kuna tofauti kati yako na mr mavoko ni bora kulimaliza kistaarabu,maana mnajuana kwa muda huo mliokaa pamoja.mimi nimetoka mwanza nimewakuta kwenye game, inagwa siku ya kutoboa huwa ni siri kubwa kutoka  kwa Mungu.

WCb hawana uwezo wa kumnyonya msanii lakini msanii ana uweoz mkubwa sana wa kumnyonya WCB, waangalie kina Mbosso na lava lava utakugundua kuwa WCB wana Utu sana , ni wapambanaji sana na kama kila upambanaji ikienda kwa kasi ya diamond basi mtaomba pooh.

 

H.Baba- Wasanii Wanaishi Maisha Ya Uongo Ya Kuigiza Wana Pesa

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba miaka ya nyuma na kibao chake cha mpenzi bubu, H.Baba amewachana wasanii wenzake na kusema wanaishi maisha ya uongo.

H. Baba amedai kuwa wasanii wengi sana wanatumia mitandao ya kijamii kufanganya mashabiki kwa pesa za kuazima kwa watu ili tu kuwaaminisha wako vizuri lakini kumbe kiukweli wanaishi maisha magumu sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, H. Baba ametoa povu hilo zito kabisa dhidi ya Wasanii Wenzake ingawa hakutaja majina:

Wasanii wanaishi maisha ya uongo, anapost picha ana pesa kumbe ameomba kwa jirani apige nazo picha tu lakini ukija kuangalia maisha yake unakuta maisha yake ni magumu sana“.

Hii sio mara ya kwanza kwa wasanii kunyoosheana vidole kuwa wanaigiza maisha kwa watu lakini kiuhalisia hali zao ni mbaya.

H.Baba- Hakuna Msanii Wa Kushindana na Mziki Wangu

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva H.baba amefunguka na kudai mpaka hivi sasa hajaona bado msanii ambaye anaweza kushindana naye.

H.baba ameweka wazi kuwa ukimya wake Kwenye gemu unatokana na yeye kukosa msanii ambayr anaweza kushindana naye kwani mziki wake ni wa kipekee.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, H.baba  amesema ameona akae pembeni kwa muda kuwa muziki wa BongoFleva unaenda kupotea kabisa kwenye ramani nchini Tanzania.

Mimi binafsi naona muziki unaelekea ukingoni, wasanii wameacha kufanya muziki wanafanya kiki kila kukicha.

Sisi tulipendwa kutokana na muziki wetu na sio makiki yasio na mpango ndio maana baada ya kuona sina mshindani tena nikaamua nikae pembeni siku akitokea mshindani wangu mtaona fujo zangu”.

H.Baba amedai kwa sasa anashindwa kuweka wazi ni lini ataachia wimbo wake mpya kwa madai anaogopa kulogwa kwani wasanii wa siku hizi wanatumia ndumba kuwashusha kimuziki wasanii wenzao.

H.Kaba kumaliza Beef Lake Na Diamond.

Msanii mkongwe alikuwa katika miondoka ya dansi H.Baba, ameamua kumaliza beef alilokuwa nalo na msanii mkubwa na anayefanya vizuri   kwa sasa bongo Diamond Platinumz kwa kuweka picha ya msanii huyo mkubwa akiwa na mzazi mwenzie Zari The Bossy hivi karibuni na kuandika maneno yenye kuonyesha kuwa hana chuki na wawili hao.

H.baba amesema kuwa amekuwa akivutiwa sana na mahusiano ya Diamond na Zari kwa muda mrefu na kwa sasa anawashauri waweze kuoana kwa kufunga ndoa na kama msanii mwenzie atatoa ngombe watano kwa ajili ya harusi hiyo.

H.baba ameongezea na kusema kuwa hawezi kuficha hisia zake kwa couple hiyo kwa sababu amekuwa akivutiwa nayo kila anapoiona ana amekataa kuwa kaa kwa kutaka kurudisha nyuma mahusiano hayo kwa sababu watu hao wanapendana na wamekuwa wakiendana sana.

Kinyama mnapendezana sana na mnaendnana sana , Mungu awasimamaie na kuwaongoza mfunge ndoa awe wako katika hesabu ya mwenyezo mungu,natoa ngombe watono kabisa wakubwa wa kisukuma waletwe Dar, huo nduo uwezo wangu  na hicho ndicho ntaajaliwa na Mwenyezi mungu.nakutakia maandalizi mema ya ndoa yako na hongera kwa kupendana……ninaheshimu mahusino yamtanzania mwenzangu#MIMINIMZALENDONANIMEKATAAKUWAKAA #Usinilazimishekwamanenoyakokuwakaa #Natudiatenanimekataakuwakaa.

Hii inakuja baada ya muda mrefu msanii h.baba kuwa katika beef zito na msanii diamond kutokana na kile kuwa msanii huyo alikuwa ni team alikiba kwa kuwa alikuwa akipost na kumsapoti alikiba huku akiweka vijembe vya kumkandia Diamond Platinumz.Hii inaongeza na kuwafariji mashabiki pale wasanii wanapokuwa wanapendana na kuungana ili kufanya kazi pamoja kwa sababu hii inaleta hamasa ya mashabiki kuzidi kuwapenda ,ashabiki.