Post ya Wema Ilivyozua Utata Mtandaoni

Staa wa bongo movies wema sepetu amewaacha watu katika mshangao na kuchanganyikiwa baaada ya kuweka posti ya kusikitisha inayohusu mwanamke ambae alipata tatizo la kuharibika kwa mimba.

Watu wamekuwa wakijiuliza je post hiyo inamkumbusha mimba iliyoharika kipindi cha nyuma au ni mimba nyingine imeharibika tena.Watu wengi wameonekana kuguswa na jambo hilo na kusema kuwa Wema anapitia kipindi kigumu sana kwa sasa kutokana na hamu yake kubwa ya kutaka kuwa na mtoto lakini inashindikana.

wema aliweka picha hiyo katika ukurasa wake wa instagram na kuandika “Story of my life

                                                           

Yawezekana Hizi Ni Sababu Za Wema Kutaka Kufa

Siku kadhaa zilizopita mrembo Wema Sepetu aliandika katika ukurasa wake wa instagram kwamba anataka kufa kutokana na kuchoshwa kwa maneno ya watu katika mitandao ya kijamii wakimsema vibaya, lakini hii haitakuwa mara yake ya kwanza kwa mwanadada huyo kusema katika mitandao ya kijamii, lakini  je inawezekana sasa ikawa ndio imezidi na kujikuta anachoka ndio maana ameamua kutamka maneno hayo ambayo kwa kawaida sio vizuri  kujitabilia kifo.

Kuna tetesi zimekuwa zikisambaa kuwa inawezekana kutokana na mambo mengi ambayo Wema amekumbana nayo kwa muda mfupi ndio yaliyomfanya aseme hayo yote hii ni pamoja na ;

Kesi yake ya madawa ya kulevya ambayo imekuwa ikimkabili na imekuwa haiishi tangu ianzwe kusikilizwa, mwanadada huyo amekuwa akienda mahakamani kila kukicha na kesi yake imekuwa ikihairishwa karibia kila inapoenda kusikilizwa.mara ya mwisho kesi hiyo ilitajwa kusomwa tena Desemba 14.kutokana na kesi hiyomwandada Wema amekuwa akiandamwa sana na maneno katika mitandao kutokana na kesi hiyo.

Sababu nyingine inawezekana kuwa ni swala la kisiasa linaloendelea ambapo katika mitandao wamekuwa wakikisia kuwa anakaribia kurudi CCM kutokana na mambo yake na familia yake kuwa magumu huko alikoamia hapo awali.Inasemekana kuwa Wema na mama yake walitegemea kuwa kuhamia Chadema kutakuwa na manufaa kwao lakini kitu cha ajabu ni kwamba wasiasa wengi wamekuwa wakiendelea kuhamia CCM wakitokea walipoamia wao.

Swala lingine ni mapenzi ambayo tamekuwa yakimtesa Wema kila kukicha lakini mwaka huu alipoanzisha mahusiano na mwanaume mmoja aliejulikana kama Bakari ambae Wema alihisi kuwa atakuwa amemfuta machoz na kutulia nae katika mapenzi lakini kitu cha kushangaza na cha kumuhurumia ni kwamba mwanaume huyo alikamatwa Mombasa kwa kosa la madawa ya kulevya.

Swala la kupata mtoto nalo limekuwa likimpa Wema huzuni kila kukicha tena wengi wamekuwa wakimsema vibaya na kwamba amekuwa aki-feki kubeba mimba wakati hakuwahi kupata mimba.Wema amekuwa akitamani sana kupata mtoto lakini bado hajafanikiwa kwa hilo.

Lakini pia hivi karibuni kuna wimbo ulitoka ambao uliongelea mahusiano ya msanii mkubwa nchi na yeye alitajwa kati ya wasichana waliotembea na msanii huyo na kumuumiza .

“Nisipobahatika kupata mtoto nitafunga uzazi” Wema Sepetu asema

Tanzanian sweetheart Wema Sepetu hi karibuni alifunguka kuhusu suala la kupata mtoto katika mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa Wikienda hivi karibuni.

Mrembo huyu ambaye ni mmoja wa waigizaji ambao wamefanya vizuri kwenye industry ya Tanzania amedai kuwa kwa sasa akona mpenzi ambaye wametulia pamoja na pia wanajaribu kupata mtoto pamoja.

Wema Sepetu

Aliendelea kwa kudai kuwa baada ya kupoteza mapacha wake imemchukua muda kuwasahau lakini kila kitu hufanyika kwa nguvu za mwenyezi mungu.

Hata hivyo aliweka wazi kuwa asipopata mtoto kabla ya kufikia miaka 32 basi atafunga kizazi. Lakini akona uhakika kuwa atapata mtoto kwani amepata ufumbuzi wa kitaalam na kujua tatizo lake ni lipi. Alisema;

Ndiyo na tena safari hii nisipobahatika kupata mtoto hadi ninafikisha umri wa miaka 32 (kwa sasa ana 29), nitafunga kizazi.

 

Wema Sepetu afunguka kueleza kinachomkera kuhusu Tanzania ya sasa

Mrembo wa filamu Wema Sepetu ameonekana kukasirishwa na alichofanyiwa mtu mmoja aliyekutana na yeye mahakamani hivi karibuni.

Wema Sepetu aliweka tweet kadhaa kupitia mtandao wa Twitter huku akionekana kama amekasirika kwa kilichomtokea mtu huyo wakati wa kusikiliza wa kesi ya Mh.Tundu Lissu.

Aliandika tweet hizo akisema;