Ni kweli Hamisa Mobetto anaujauzito wa Diamond Platnumz?

Hamisa Mobetto amejipata tena akisingiziwa kuwa yeye na baba Tiffah wanatoka kimapenzi. Kuzidisha mara hii mrembo huyu anasemekana kuwa anamtarajia mtoto na mkali huyo wa Wasafi records.

Hamisa, Diamond na Zari
Hamisa, Diamond na Zari

Kulingana na fununu mitandaoni hii ndio shida ambayo imemfanya Diamond Platnumz na Zari Hassan kutosikilizana. Hapo awali ilisemekana kuwa wapenzi hao walikosana baada ya Diamond Platnumz kutohudhuria mazishi ya Ivan Don lakini inaonekana kuwa kuna taarifa ambazo mashabiki hawajui kwa sasa.

Hata hivyo hakuna anayejua ikiwa Hamisa Mobetto anamtarajia mtoto wake wa pili na kama ni kweli, hatujui ikiwa mtoto huyu ni wa Diamond Platnumz.

Mamake Diamond Platnumz pia anasemekana kuwa ameridhia mwanae kuwa na Hamisa Mobetto na iwapo hii ni kweli basi Nillan akokaribu kupata mdogo wake!

Picha ya Hamisa Mobetto akiwa amevaa suruali ya Diamond Platnumz

Kuna riporti zimekuwa zikianaa mitandaoni kuwa Diamond Platnumz ashawai kuwa na mahusiano ya ndani na Hamisa Mobetto, video vixen ambaye alishirikisha kwenye video yake ya Salome.

Hivi majuzi kuna picha iliyoebuka mitandaoni ikimuonesha Hamisa Mobetto kama amevaa suruali ya Diamond Platnumz.

Picha hii imewawacha mashabiki wakiamini kuwa wawili hawa washiakuwa pamoja na hivi ndivyo Hamisa aliweza kuipata suruali hii.

Ingawa hakuna kitu kinachodhibitisha kuwa Hamisa alitoa trouser hii kwa Diamond Platnumz, wengi bado wanaamini kuwa uvumi uliokuwa ukiwafuata Diamond na Hamisa Mobetto ni wa ukweli.

Pia Wengi wanadai kuwa hii ndio maana Zari Hassan and Mobetto hawajaweza kupatana kwa muda sasa.

Hamisa Mobetto hajazungumzia kuhusu picha hii inayoenea mitandaoni lakini mashabiki wa team Diamond Platnumz wamekuwa wakimtag mrembo huyu kwa hiyo picha kuona kama ataweza kusema kitu kuihusu.

Hata hivyo, Tazama hiyo picha hapa chini.

Hamisa na Diamond Platnumz kavaa suruali zinazo fanana
Hamisa na Diamond Platnumz kavaa suruali zinazo fanana