Mange Amtaka Wolper Asirudi Kwa Harmonize Maana Ameachwa na Mzungu

Mange Kimambi ameibuka na kumfungukia Staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper kuhusu kurudiana na Ex Wake Msanii wa Bongo fleva Harmonize na kumtaka asijaribu.

Mange ameongea hayo Baada ya kuwepo kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wolper na Harmonize wamerudiana Baada ya kuonekana pamoja wakiwa beneti kwenye tamasha la Wasafi Festival.

Mange amemchana Wolper na kumtaka kutorudi kwa Harmonize kwa sababu hana mapenzi ya kweli kwake kwani amerudi Baada ya kuachwa na Sarah ambaye amemtimua Nyumba waliokuwa wanaishi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika:

https://www.instagram.com/p/Bq8-aiHAvPK/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=wwhqlwlkrzki

Harmonize na Wolper Mapenzi Moto Moto

Msanii wa Bongo fleva nchini kutoka WCB Harmonize na msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper wamezidi kutengeneza headline kwa tetesi za kurudisha Penzi Lao Kama zamani.

Wawili hao wameendelea kuzua gumzo baada ya Harmonize kutangaza kurudi kwa Wolper wake ambaye alimwagana naye miezi kadhaa iliyopita. Ishu nzima ilijiri usiku wa kuamkia juzi Jumamosi katika shoo ya Wasafi Festival iliyofanyika mjini Iringa na kusababisha mji huo kutikisika.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Wikiend iliyopita katika Uwanja wa Samora, Harmonize alimpandisha stejini Wolper kama ‘sapraizi’ na kumwangukia akimuomba warudiane, jambo ambalo Wolper alilikubali mbele ya maelfu ya mashabiki wao.

Naomba niseme wazi hapa hadharani kuwa nimerudi kwa Wolper wangu”.

Kufuatia kile kilichojiri mjini Mtwara ambapo Wolper alieleza nia yake ya kumrudisha Harmonize kwenye himaya yake ambapo wengi waliamini kuwa wawili hao wamerudiana maana wahenga walisema kiporo hakihitaji kupashwa na moto mwingi.

Pamoja na kuwepo kwa tetesi za wawili kurudiana Mpenzi wa siku nyingi wa Harmonize, Sarah ambaye kwa sasa yupo nyumbani kwao nchini Italy lakini amesema wazi kuwa yeye na mpenzi wake Harmonize bado wako wote na anategemea kurudi Tanzania muda wowote.

Wolper afunguka kuhusu uhusiano wake na Harmonize, hii ndio maana hawezi muacha!

Harmonize na Wolper wamekuwa pamoja kwa muda sasa na ingiwa wapenzi hawa pia hupitia mashida kama watu wengine, wawili hawa hawana mipango ya kuachana hivi karibuni.

Miezi kadhaa iliyopita wengi waliacha wakijiuliza kilichotokea kati ya hawa wawili na kuachana kwenye mitandaoni hata hivyo hakuna anayejua lakini kwa sasa wamerudiana na wawili hawa wanapanga kuanza maisha yao pamoja.

Hata hivyo Wolper alifunguka kwa mara ya kwanza kudai kuwa hakuna kitu kibaya ambacho Harmonize hashawai kumfanyia. Wolper alidai kuwa  hajuti kuwa na msanii huyu kwa sababu anamuelewa na pia kwa sababu wanapendana.

Harmonize akashifu madai kwamba wolper aliwai kufanya mapenzi na boss wake Diamond Platnumz

Mwanamuziki Harmonize amejitokeza kukashifu madai ya kwamba mpenzi wake wa hapo awali Wolper alikua na uhusiano wa kimapenzi na boss wake Diamond Platnumz.

I DON’T KNOW ABOUT THAT, SIJUI KAMA JACKIE ALISHAWAHI KUDATE NA CHIBU D. SIJUI NA SIJAWAHI KUSIKIA. MIMI MWANAKIJIJI BRO MJINI SIJAFIKA SIKU NYINGI, SO SIJUI NA SIJAWAHI KUSIKIA NDIO KWANZA UNANISUPRISE. KUMBE ILISHAWAHI KUTOKEA HIVYO?,” Alijibu wakati aliulizwa hilo swali.

Mwamuziki ametoa wimbo mpya alowakilisha Wolper kama video vixen na uvumi ukaanza kusambaa kwamba alimwandikia wimbo hiyo jambo ambalo amelikana.

Also read:Msanii kutoka Wasafi Harmonize azungumza mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na Wolper

Jambo la kutisha ni kwamba lazima angeomba mdosi wake Diamond ruhusa la kuingia na uwasiliano wowote na Wolper.

“CONFIRMATION NILIYOKUWA NAIHITAJI SIO HIYO BRO, NILIKUWA NATAKA CONFIRMATION KUTOKA KWA DIAMOND KWAMBA ANAONAJE MIMI NIKIKAA PALE KWA WOLPER. ALINIJIBU KUWA NI MWANAMKE MZURI LAKINI HAKUNIAMBIA KAMA ALISHAWAHI KUDATE NAYE NA WALA JACKIE HAJAWAHI KUNIAMBIA KAMA ALISHAWAHI KUDATE NA DIAMOND,” Alikamilisha jambo hilo.