Prezzo na Jaguar Wakubali Kulizika Bifu Lao

Mastaa wa Muziki kutoka 254 Kenya, Prezzo na Jaguar wametangaza kulizika bifu lao la muda mrefu.

Kwa kipindi kirefu Prezzo alikuwa akiponda jina la Jaguar kwa kueleza Jaguar anayoifahamu yeye ni aina ya gari, Jaguar naye hakuwa nyuma kujibu hilo, kuna kipindi alimpa Prezzo ofa ya kutibiwa rehab bure.

Wasanii hao wawili walitangaza kumalizika kwa bifu hiko huku kila mmoja akiweka katika ukurasa wake wa Instagram:

Jaguar aliandika maneno haya:

Prezzo naye aliweka picha yao na Jaguar na kusindikiza na ujumbe huu kuonyesha wako safi:

 

 

Lulu Diva aeleza ukweli kuhusu madai kuwa anashiriki mapenzi na Jaguar

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva anadaiwa kushiriki mapenzi na msanii Jaguar kutoke nchi jirani ya Kenya.

Jaguar ni meneja wa mrembo huyo kutoka Tanzania lakini kuna wale wanaodai kuwa wasanii hao wawili wanashiriki mapenzi chini ya maji.

Jaguar

Lulu Diva hata hivyo aliambia Star Mix kuwa wambeya wametunga tu hadhiti kuwa yeye na Jaguar ni wapenzi ilhali wao wanahusiana tu kikazi.

“Ni uzushi kama unavyojua Wabongo, Jaguar ni meneja wangu tu ambaye ananisaidia katika kunisimamia katika muziki na si vinginevyo,” Lulu Diva aliambia Star Mix.

Lulu Diva