Jini Kabula Afungukia Ndoa Ya Zabibu Kiba na Aliyekuwa Mpenzi Wake

Muigizaji wa Bongo movie Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka na kuweka wazi kuwa hana tatizo na Zabibu Kiba kufunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake mchezaji wa mpira Abdul Banda.

Siku za nyuma Jini Kabula na mchezaji wa Timu ya Baroka iliyopo Afrika Kusini, Abdul Banda waliwahi kuwa Kwenye uhusiano wa kimapenzi lakini hivi sasa Abdul yuko na Mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba, Zabibu Kiba na wapo mbioni kufunga ndoa.

                               Jini Kabula

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Jini Kabula alisema anawashangaa baadhi ya watu wanaomshambulia kwa maneno machafu kwenye mitandao ya kijamii kisa aliwahi kuwa na uhusiano na Banda lakini hawakufanikiwa kuingia kwenye ndoa kitu ambacho ni kawaida tu katika maisha.

Kwanza nafurahi sana Zabibu kuele­kea kwenye ndoa na Banda nawaombea ifanyike salama na sina kinyongo hata kidogo lakini kuna hawa vizabizabina vya pembeni vinaleta chokochoko na kusema eti nilishindwa kuolewa mimi, niwaambie tu kwamba siyo kila mtu unapokuwa naye kwenye uhusiano lazima muoane hivyo waache kuongea mambo wasiyoyajua“.

Zabibu yupo katika shamrashamra za kuelekea Kwenye ndoa ambapo siku chache zilizopita alionekana akifanyiwa visomo mbali mbali na inasemekana kuwa harusi yaweza kuwa muda wowote.

Kabula Amwagia Sifa Kiba Q Chillah Amuita Dhahabu

Muigizaji wa Bongo movie aliyewahi kutamba katika filamu ya Jumba la dhahabu Jini Kabula amefunguka na kuonyesha kuumizwa na Kitendo Cha Q Chief kutangaza kuacha mziki.

Mwezi uliopita msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Q Chillah aliweka wazi kuwa anataka kuachana na muziki baada ya kukata tamaa baada ya kushindwa kurudi kwenye chati kama zamani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kabula ameamua kutoa ushauri juu ya maamuzi aliyoyafanya Q Chillah kuhusiana na kuachana na muziki.

Wee unaanzaje kumuacha mtu kama huyu apotee kizembe ifike mahali Taifa lipaze sauti kwa vijana nguvu kazi Chilla ni dhahabu ya Tanzania alipotangaza kuacha mziki roho ilipasuka nikasema No bado anauwezo mkubwa wa kuipeperusha bendera ya Taifa letu.

Wewe ni dhahabu kaka na dhahabu haiwezi ngaa bila kupita kwenye moto huwezi kuwa shujaa mpaka ukutane na mengi ya kukuumiza moyo na kukukatisha tamaa lazima udharauliwe ukataliwe na wakati mwingine kunenewa maneno ya uwongo ila ukiweza kutobowa hakuna anaweza kukushusha chini tena.

Sisi ni mashujaa wa Taifa ata tukiondoka leo tutaacha histolia ktk vizazi vijavyo acha ya zamani yaende simama ukainuliwe kaka…Watanzania tunakupenda tuko pamoja Maisha na mziki Go chilla”.

Skendo:Jini Kabula Adaiwa Kuiba Nguo

Muigizaji wa Bongo movie Miriam Jolwa maarufu kama Jini Kabula aliyejizolea umaarufu miaka ya nyuma baada ya kuonekana kwenye mchezo wa Jumba la dhahabu, amekumbwa na skendo nyingine ya kuiba nguo kwa rafiki yake aliyempa hifadhi.

Habari zilizosambaa zimedai kuwa mwanadada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Candy alidai kuwa alimpa hifadhi Jini Kabula nyumbani kwake huko mkoani Mwanza lakini amedai  kamuibia nguo mpya za thamani na kisha kuondoka na kutimkia nchini Oman.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Soudy Brown Kupitia kipindi cha XXL, Candy amedai kuwa ameshangazwa na kitendo hiko kwani alimfanyia we na kumkaribisha kwake lakini amedai tangu ameandoka amemblock Kwenye WhatsApp na Instagram akijua wazi ameiba.

Baada ya tuhuma hizo Jini Kabula aliulizwa na kutokea nchini Oman alifunguka yafuatayo:

Kwanza simjui huyo Candy alafu kama anatafuta kiki aseme halafu isitoshe mimi nimeshazoea hayo mambo kwaiyo hayaniumizi kichwa  na sahivi nimeshachoka na habari za watanzania  ngoja nile bata alafu kama hamjui huyo Candy mshamba anavaa malonya malonya kwaiyo siwezi kumuibia kitu kila mtu apambane na hali yake”.

 

Hali ya Jini Kabula Yaimarika,Amshukuru Esha Buheti

Msanii wabongo movies Jini Kabula amekairi kuwa  kwa sasa hali yake ya kiafya imehimarika sana na yupo mwanza kwa kaka yake ambapo bado anajitazamia hali yake. Msanii huyo ambae alikuwa kama mtu aaliyeugua uchizi baaada ya kusemekana ni athari za matumizi ya madawa ya kulevya alipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi .

Hata hivyo Jini Kabula amekuwa akilalamika kwa wale ambao wamesambaza taarifa kuwa yeye ni muathirika wa Ukimwi, na kusema kuwa watu hao hawamtakii mema na habari hizo hazina ukweli wowote zaidi ya kuwa anachukiwa na  baadhi ya watu.

Jini Kabula anamshukuru Esha Buheti kwa wema alimfanyia  kipindi chote alichokuwa akiumwa na kwa msaada mkubwa aliompa huku akisema kuwa kipindi anaumwa kuna baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wamemtenga kabisa na hawakutaka hata kujua hali yake.

Ni kweli kuna watu walikuwa mbali na mimikabisa, lakini ni kawaidasana hasa kwa ugonjwa kama niliougua mimi nivigumu sana watu kutaka kuwa karibu na mimi kwakweli  lakinibado nina washukuru sana baadhi ya wasanii wachache waliopambana sana katika kuokoa maisha yangu hasa dada yangu Esha Buheti , Mungu ambariki sana na hakika maisha yake yamebalikiwa sana, ni mwanamke mwenye roho ya utu na uungwana wa  kupitiliza.

Hata hivyo Jini Kabula anasema kuwa kwa sasa ameshaachana na hanasa zote na amekuwa mtu wa Mungu kwa sababu matatizo yaliyompata ni makubwa na atakuwa mjinga kama atarudi kule kwasababu aliteseka sana.

Wasanii wengi wamekuwa wakilalalmika kuwa wanapopata matatizo ni wasanii wenzao wachache wanaosimama nao na kuwashika mkono katika matatizo hayo, wengi uendelea na shughuli zao na kusahahu kuwa mtu  huyo aliepata matatizo walikuwanae wote katika starehe kipindi hayuko na matatizo.