Jini Kabula aeleza familia yake ilivyomtemga baada ya kuugua ugonjwa wa akili

Miriam Jolwa anayetambulika Kama Jini Kabula ni muigizaji aliyepata umaruufu kupitia tamthiliya ya Jumba la Dhahabu. Hata hivyo kwa hivi sasa anaonekana hali ya akili haiko sawa.

Baada ya Wolper kujitokeza na kuwaomba wasanii wenzake kumsaidia Jini, Global TV online iliweza kukutana na yeye Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo walizungumza na yeye na kulingana na walichotangaza, ni kweli Jini anapitia wakati mgumu.

Mrembo huyu alifunguka kudai kuwa wetu ana tatizo kwenye akili yake na akaendelea kukiri kuwa ndugu zake walimpeleka Muhimbili ambako alilazwa kwenye wodi ya wagonjwa akili kwa zaidi ya mwezi mmoja na kumtenga.

Kwa Sasa hana sehemu ya kuishi na ndugu, jamaa na marafiki zake, wamemtenga kutokana na matatizo aliyonayo na kumbidi kutangatanga mitaani.

Tazama mahojiano yao hapa;

Wolper awasihi raia na wasanii wa Bongo movie kumsaidia Jini Kabula anaye Ugua

Jackline Wolper ambaye ni malkia wa bongo movie amejitokeza kuwaomba wasanii wenzake na raia pia kumsaidia Mariam Jolwa anayejulikana kama Jini Kabula aneyeugua ugonjwa wa akili.

Kupitia mtandao wake Wa a Instagram Wolper aliandika kusema;

Natamani niongee mambo mengi sana juu yako lakini natamani ata kukusaidia urudishe akili yako swali ni kwamba nimechelewa??nakama nimewahi je nitafanikiwa kweli. sasa tuzungumze jambo jamani maana siju hizi tarfa tunazipata insta naona nalangu niliongelee insta wanatasnia wenzangu tunamsaidiaje mwenzetu nini kimekuta kipi je nayoyasikia ndio hayo????nakama ndio mbona kuna wataalam wakusena nae naakakaaa sawa. Basi watanzania wenzangu naombeni tuchangie maoni yenu hapa nakama nim2 uwezi toa ushauri hapa basi tuma msg kwakupitia cm hii 0765776776 basi tuweze kumrudisha kabula jamani. naandika msg hii huku nalia namoyo mdogo sana usiweza kuvumilia naumivu nakumbuka nimishawahi kumwambia kabula we nimwanamke mzuri sana bongo movie lkn natamani kujua tatizo nini kacheka tuu akachukua nguo akaondoka sikupata muda wakuzungunza nae ….sasa npo safarini hope kesho au kesho kutwa nikijaliwa tukutane kwaoamoja .. Bongo movie tumfwate alipo jamani tujue tunamsaidiaje nimeona vdio anaongea sjui niamechanganyikiwa masikn me ata nashindwa kuandika jamani ….