“Muna ni Mwanamke Shupavu Sana”- Joyce Kiria

Mtangazaji wa kipindi cha ‘Wanawake Live’ na mpiganaji wa haki za wanawake Joyce Kiria amemkingia kifua Muna Love na kumtaja kama mwanamke shupavu.

Siku chache zilizopita Muna amekuwa akikosolewa sana baada ya kuonekana amerudi Kwenye maisha yake kama kawaida baada ya Kifo Cha mwanaye Ikiwa zimepita wiki chache tu.

Mashabiki wamemjia juu Muna kutokana na mavazi yake ambayo amekuwa akivaa na hata kuposti picha Kwenye mitandao ya kijamii na kuendelea na maisha yake kama kawaida.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Joyce Kiria amedai Muna yuko sahihi kwa hivi sasa anavyotoka na kuonekana kwenye mitandao kabla ya kumaliza 40 ya mtoto wake aliyefariki kwa sababu hana sababu ya kuendelea kulia na kujifungia ndani kama watu wanavyomtaka.

Mimi binafsi nampongeza sana kwa kile anachokifanya sasa hivi, inaonekana jinsi gani alivyo shupavu maana bila hivyo basi angekuwa anaishi kwa maumivu makali tena ya kumsababishia athari ndani ya moyo”.

Mashabiki walimjia juu Muna baada ya kuamua kuongea na waandishi wa habari siku chache baada ya Kifo Cha mwanaye na sasa ameonekana nchini Kenya na kuendelea na maisha yake kama kawaida wakati mtoto wake hjafikisha siku 40 tangu afariki.

 

Joyce Kiria Azidi Kufunguka Mazito Kuhusu Ndoa Yake

Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na Kituo cha East Africa Tv, Joyce Kiria amezidi kufunguka Mazito Kuhusu ndoa yake na Mwanasiasa wa Chadema Henry Kilewo.

Joyce aliweka wazi hali ya ndoa yake Miezi michache iliyopita ambaoo amedai kuwa Mumewe alikuwa anamnyanyasa na kumtesa na hata kumpa kichapo wakati wa ndoa yao.

Lakini Joyce amedai kuwa tangu ameanika maovu hayo ya mume wake amekuwa akipokea matusi na lugha za kebehi kutoka kwa watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii.

Joyce amesema kuwa matusi hayo na lugha za kebehi kwake anaona ni jambo la kawaida na ni afadhali kwake lakini sio kuvumilia maumivu aliyokuwa akiyapata kwenye ndoa yake na mumewe Henry Kilewo.

Nachotaka kusema ni kwamba kwa vile nilichangua hii kazi  ya kuwa sauti za wanawake najua gharama zipo, na gharama kubwa kabisa ni kutukanwa lakini sio kwamba mimi sioni hayo matusi nayaona lakini navumilia. Kwahiyo sio kwamba siumii naumia!! na kuna wengine wananikosesha dili za matangazo kwenye kipindi changu kwa kuona nimejiharibia na mambo ya kisiasa.

Pamoja na machungu yote ninayoyapitia ya kutukanwa na kukosa wadhamini kwenye kipindi changu nikilinganisha na maumivu ya kwenye ndoa ni bora nitukanwe na jamii  lakini sio kuvumilia ukatili na machungu ya ndoa yangu“.

 

Baadhi Wamshambulia Joyce , ni Baada ya Kujitokeza Kwa Waliotelekezwa.

Baadhi ya watu wamejikuta wakimtolea povu mwanamama ambae alianza kama utani katika tasnia ya filamu kwa kuwainua wasanii na mpaka kuja kuwa na kipindi chake ambacho kilikuwa kikiwatetea wanawake kilichojulikana kama wanawake live.

Siku ya jana wanawake wengi walijitokeza katika ofisi za Mh mkuu wa mkoa baada ya mkuu wa mkoa kujitolea kuwasaidia wanawake wote walio na shida ya kutelekezwa na wanaume wa kwa kuwazalisha na kushindwa kulea watoto.

Kuna picha zilisambaa sana baaada ya mwana dada Joyce Kiria kujitokeza katika umati huo wa wanawake akiwa ni mmoja wa waliokwenda kwa ajili ya kutaka msaada.

Hata hivyo bado hakuna haja ya watu kubaki mdomo wazi kumuona Joyce Kiria katika eneo hilo kwa sababu kipindi cha nyumba joyce alishawahi kuweka wazi maisha yake ya ndoa na kusema kuwa ameshindwa kukaa kwenye ndoa hivyo ameamua kuachana na mwanaume wake. inawezekana pia uwepo wake ni kwa ajili ya kutaka msaada lakini pia inawezekana yuko pale lwa sababu yeye pia ni mwanaharakati wa akina mama hivyo bado anamchnago mkubwa katika jamii.

Baadhi ya mashabiki wamemtukana sana na hata kumshambuia katika mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwake pale, lakini akiwa kama mmoja wa wanawake jasiri Joyce siku zote amekuwa akisema haogopi kuonekana kituko mbele za watu kwa yale anayoyafanya ilimradi yanampa nguvu na kumuinua.

Joyce Kiria Amefunguka Mazito Kuhusu Ndoa Yake

Mtangazaji maarufu wa kipindi cha ‘Wanawake Live’ cha East Africa Tv, Joyce Kiria amefunguka na kueleza mazito yanayoikabili ndoa yake na Mh. Henry Kilewo ambaye ni katibu wa Chadema Mkoa wa Kinondoni.

Joyce alitumia mtandao wa kijamii kueleza matatizo yanayomsibu ambapo alifunguka na kueleza jinsi ndoa yake ilivyomharibua maisha yake baada ya kuolewa na mwanasiasa na kupelekea kugawa mashabiki zake wa vyama tofauti na alichopo mume wake lakini pia amedai kuwa mume wake amekuwa mzigo kwenye maisha yake kwasababu yeye ndio anamuhudumia na mpaka analipa kodi ya nyumba.

Lakini Joyce amekiri kuwa mume wake amekuwa Ana tabia ya kumpiga kipigo ambacho kina msababishia maumivu makubwa ambapo amesisitiza hiyo haikuwa mara moja au mara mbili mume wake akainua mkono wake na kumpiga.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka yafuatayo kuhusu changamoto na matatizo ya kwenye ndoa yake :

Yaani maisha yangu yanashuka kwa sababu yake kwa kweli sikutegemea Mimi ni mfanyabiashara, mimi ni mjasiriamali wa siku nyingi tu kwaiyo kufikia hatua ile ya kujitoa mhanga vile kumpigania mpaka kugawa mashabiki zangu siku huzi nafanya biashara zangu kwa shida sana na ndio maana nasali sana namuomba Mungu anipiganie kwa ajili yake na hili ambalo nalifanya yaani sasa hivi mimi ndio nalipa kodi ya nyumba”.

Joyce alijipatia umaarufu kwa historian yake ambapo alianza maisha kama house girl/ Mfanyakazi wa ndani mpaka kuwa mtangazaji wa kipindi maarufu cha Wanawake Live ambacho kinazungumzia changamoto mbali mbali ambazo wanawake wanakutana nazo katika maisha yao ya kila siku na amesaidia wanawake wengi sana kupata haki zao za msingi.