Kajala Amchagua Wema kwa Zari, Asema Hawezi Kujitolea Kumsaidia Zari

Kajala anasema kuwa kamwe hawezi kumsaidia Zari bali kama itatokea shida  na wapo Zari na Wema Sepetu basi anaweza kumchagua Wema kwa ajili ya kumsaidia kwa sababu anamjua wema na pia ameishi na wema na amekuwa wakimsaidia sana .

Kajala ameyasema hayo alipoulizwa kama kitatokea kitu kibaya na anatakiwa kumchagua mmoja wa kumsaidia ndipo aliposema kuwa kamwe hatomsaidia Zari kwa sababu aliwahi kusaidiwa na Wema na anaamini .

sijui niongeeje lakini ukweli ni kwamba siwezi kumsaidia zari kwa sababu simjui na wala sijawahi kuwa nae karibu lakini ninaweza kumsaidia wema kwa sababu aliwahi kunisaidia sana.

Ingawa jibu hilo la kajala limewashtua mashabiki wengi wa zari na inawezekana hilo linaweza kuleta kinyongo kwa  mashabiki kuacha kusapoti kazi za kajala.

Agness Aliniambia Ana Mchumba Amwemwambia Atulie:-Kajala

Kuna kuwa na stori nyingi sana hasa mtu maarufu anapofariki kwa sababu kila mmoja anataka kuongea kile alichowahi kushare na marehemu, moja ya watu waliofunguka na kuguswa na msiba huu ni msanii wa bongo movies ni  kajala ambae anasema kuwa pamoja na kwamba Aggy alikuwa kama alivyo lakini hakuwahi kulinga na mtu.

Kajala anasema kuwa mara ya mwisho kuongea na aggy ilikuwa ni mwezi watatu  na walikuwa waitaniana mambo mengi sana

ni mtu ambae alikuwa unaweza kutaniana nae na kuongea na mtu yoyote yule, alikuwa hana majivuni pamoja na kwamba alikuwa vile alivyo. mara ya mwisho kuchart na aggy ilikuwa mwezi wa tatu nakumbuka na alinitania kuwa sasa hivi nimenenepa sana nikamwambia sawa lakini mbona siku hizi huonekani , akanijibu kuwa sasa hivi ametulia amepata mchumba amemuomba atulie.

 

Kajala Akumbwa na Skendo ya Kubeba Ujauzto na Kurudiana na Majani

Mwanadada kajala masanja amejikuta aksema tena katika mitandao kwa kile kinachodaiwa kuwa amerudiana na baba ya mtoto wake wa kwanza paula , mwanaume huyo ambae alikuwa katika industry ya muziki tangu zamani na kujipatia umaarufu wake kutokana na kazi anaejulikana kama majani alishawai kukaa na kajala na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike.

katika ukurasa wake wa instagram ,siku chachezilizopiata kajala aliweka picha na baba yake na aula na aula mwenyewe huku akimtakiwa kheri ya sikukuu ya kuzaliwa kwa Majani.

 

Katika ukurasa wa Kajala aliweka picha hii siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Majani

hata hivyo baaadhia ya kurasa katika mitandao ya kijamii imekuwa ikisema kuwa wawili hao kwa sasa wapo pamoja na kwamba kajala kwa sasa ni mjamzito.

 

Moja ya watu wanaomfahamu kajala akitoa taarifa hiyo

Kajala, Wolper na Harmonize Waingia Katika Bifu Zito

Mastaa wawili wa Bongo movies Kajala Masanja na Jacqueline Wolper wameingia katika bifu zito baada ya maongezi kwa njia ya video ‘video call’ baina ya Kajala na mpenzi wa zamani wa Wolper mwanamuziki Harmonize kuvuja mtandaoni na kuibua makubwa.

Kajala alikuwa akizungumza kwa njia hiyo ya kisasa na Harmonize ambae alionekana akila tunda aina ya apple kitandani kwake huku na Kajala akiwa kitandani kwake, baadaye Harmonize aliirusha picha hiyo mtandaoni na kusababisha minong’ono ya chini chini kusambaa. Picha ile ilimkera Wolper ambaye ametoka kuachana na Harmonize miezi si mingi na Kajala pia ni rafiki yake hivyo ilipelekea Wolper kuandika maneno yafuatayo kwenye picha ile: “Yaani nimekaa hapa mwenyewe nimewaza mapenzi ya siku hizi yana drama mno, mara leo huyu mara kesho yule”. Akijua wazi Kajala ameumizwa na kitendo hicho. 

Wema Sepetu naye aliingilia kati ishu hiyo na kuandika maneno chini ya picha hiyo “Be carefully my baby huyo nyakunyaku asije akapita maana keshaambiwa mlango uko wazi”. Maneno hayo yalionekana kumuuma Kajala ambaye mara moja alikimbilia mabatini kituo cha polisi kwenda kumshtaki Harmonize kwa kitendo chake cha kuweka picha hiyo mtandaoni na kuleta tafsiri kuwa huenda wawili hao ni wapenzi kitu ambacho sio cha kweli, na yeye amepewa RB No/ KJN/ 73/2017 Jalada la uchunguzi

Kajala amesema;

“Nimemshtaki Harmonize ili ajue mimi sio mtu wa mchezo  kila wakati, maana ile video tulikuwa tukizungumza kawaida kwa nini aisambaze ili iweje kama sio kuchafuana huko”.

Kajala aliongeza kuwa anawashangaa wasanii wenzake Wolper na Wema kuingilia vitu kama hivyo kwa sababu wanaona kama yeye ni wakula mizoga yao. “Mimi nashangaa hivi wamenionaje, wanafikiri mimi ni wakula  mizoga yao nini wanayoiacha, wamenishangaza sana”.

Harmonize aliwasili kituoni hapo na kwa mujibu wa chanzo kinachoaminika kutoka kituoni hapo, Mwanamuziki huyo alijitetea kuwa sio yeye aliyeweka picha hizo mtandaoni bali ni mwanamke wake wa kizungu ndo aliyemtumia mtu mwingine kwa nia ya kutaka kumjua Kajala.