Ray C na Rostam Wala Shavu Kutoka Kwa Msanii Wa Kenya

Raper wa muziki kutoka Kenya Khaligraph Jones siku ya jana aliachia rasmi albamu yake.

Albamu hiyo aliyoipa jina la Testimony 1990 ina nyimbo zipatazo kumi na saba na habari njema ni kwamba ndani ya nyimbo hizo kuna wasanii watatu wa Bongo fleva walioweka mkono humo.

Wasanii wa Bongo fleva ambao watasikika Kwenye Albamu hiyo ni pamoja na Msanii mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila ‘Ray c’ aliyeimba wimbo unaoitwa ‘Aisee’ na kundi la Rostam linalounda na Stamina na Roma.

Roma na Stamina watasikika katika albamu hiyo Kupitia kibao chao cha ‘Now you know’.

Hii inaonyesha ni jinsi gani muziki wetu wa Bongo fleva unavyozidi kukua kila siku na hata kufika kabisa mbele na kimataifa zaidi.

Rapa kutoka Kenya -Khaligraph aondoa video yake na Rayvanny kwa YouTube

Rapa Khaligraph Jones kutoka Kenya alimshirikisha Rayvanny kwa wimbo unaoitwa ‘Chali Ya Ghetto’ ambao uliwekwa YouTube mwezi moja uliopita.

Kutolewa kwa wimbo huo YouTube kumewashangaza watu wengi kwani ‘Chali Ya Ghetto’ ulikuwa na zaidi ya views laki moja.

Akiongea na Mseto East Africa, Khaligraph alieleza kuwa alitoa wimbo huo ile aiweke kwenye channel nyingine ya YouTube.

“Yes it’s true I pulled it down but it will be uploaded on another channel” Khaligraph Jones alisema.

 

Rayvanny aachia wimbo mpya aliyoshirikiana na mfalme wa rap kutoka Kenya (Video)

Hii ni mara ya pili Rayvanny kufanya kolaba na msanii kutoka Kenya. Mwimbaji huyo wa Wasafi alishirikiana na Bahati kuachia wimbo unayoitwa ‘Nikumbushe’ ambayo ni hit kubwa Kenya.

Rayvanny tena ameshirikiana na msanii mwingine kutoka Kenya anayeitwa Khaligraph Jones. Wawili hao wametoa wimbo unaoitwa ‘Chali Ya Ghetto’.

Khaligraph hudai kuwa yeye ndiye mfalme wa hip hop nchini Kenya. Tazama video ya wimbo wao mpya hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=9pIYpVNeNfQ