Maua Sama Afuata Nyayo Za Rostam Kwa Hili

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini aliyofanya vyema na ngoma yake ya ‘Iokote’ Maua Sama amefunguka na kuweka wazi anaunga mkono msemo wa wakali wa Hip Hop Roma na Stamina (Rostam).

Roma na Stamina Wameunda msemo wao wa ‘Tunafunga Jumla jumla’ kwa ajili ya kuufungia mwaka 2018 kikazi zaidi kwa njia ya Sanaa ya muziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Maua Sama anayetamba na Ngoma ya Iokote alisema kuwa, ametokea kuvutiwa na msemo huo baada ya kuusikia na kwamba anatamani kuja na wimbo wenye jina hilo.

Nimependa kwa kweli, kwa sababu msemo kama huu kutumika mwishoni mwa mwaka huwa mzuri, unaweza kuta mtu umefanya biashara zako sasa unafunga jumla jumla ili ufungue mwaka mwingine.

Nitajaribu kuongea na Rostam ikiwezekana nitatoka na wimbo wa tunafunga jumla jumla baada ya hii ya Iokote”.

Maua Sama licha tu ya kuvutiwa na msemo wa Roma na Stamina ‘Tunafunga jumla jumla’ na kutaka kufanya wimbo Lakini pia wasanii hao wametangaza kufanya baadhi ya shoo pamoja.

Rostam na Maua Sama Wawasanua Mashabiki Zao

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva wanaounda kundi la Rostam Roma na Stamina pamoja Maua Sama Wake wateja Mashabiki zao Baada ya kuanzisha msemo wa Tunafunga Jumla jumla.

Katika kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wamekuwa wakiposti picha zao na wakati mwingine wa tukio fulani wa­kiambatanisha na maneno Tunafun­ga Jumla Jumla, jam­bo ambalo mashabiki wengi wamekuwa wak­ishindwa kung’amua maana yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Roma alisema neno hilo alianza kuliona kwa Stamina lakini anashangaa wengine wameanza kuliiga huku wengi wakiomba ufafanuzi.

Ukiniuliza maana yake sielewi ila ni misemo kama ilivyo misemo mingine. Mfano Mangi anaweza kufunga duka akasema nafunga jumla jumla, au mama n’tilie, muuza maji, karanga na wengine wengi kwa hiyo suala la biashara kuna kufunga jumla jumla”.

 

ROSTAM Wamkana Lulu Michael.

Wasanii wa hip hop nchini Roma na Stamina  wamekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa  wimbo wao mpya mabo ulitambulishwa wiki hii na wake zao kuwa uliimbwa ukimlenga msanii wa maigizo Lulu Michael kwa sababu ya mambo yanayoendelea katika mahusiano yake kwa sasa.

Kama utakumbuka, wikiendi iliyipota mwanadada Lulu Michael amevalishwa pete ya uchumba na mwanaume aliyakaa na katika mahusiano kwa muda mrefu ambae ni meneja ya EFM Majizo.

Hapana sisi hatujamzungumzia lulu , mwajuma ni mwanamke mcharuko na pia mtata sana na watu wengi walisema kuwa hatoolewa lakini mwisho wa siku aliolewa na sidhani kama lulu ana tabia hizo.-Alisema stamina alipokuwa akiongea na palnet bongo ya EATV.

Hata hivyo roma anakazia na kusema kuwa katika video hiyo walitaka kumchukua wema kama vieo Queen lakini mke wake alikataa swala hilo kwa sababu wema hana tabia za uswahilini.

pia tulikuwa na nia ya kumchukua wema sepetu , lakini mke wangu akasema kuwa wema hawezi kufit na ndio maana tumemchukua nisha na amefanya kitu tulikuwa tunataka.japo wengi walijua kuwa tungemchukua Rimaya , au hata shiloleh pia angefaa lakini sasa yeye alishaolewa.

Nilipiga Stop Kitendo Cha Wema Kuwepo Kwenye Video Ya Roma-Mke Wa Roma

Wasanii wa hip hop wanaounda kundi la Rostam Roma Mkatoliki na Stamina wameachia kazi yao mpya “Kaolewa” ambayo mpaka sasa inafanya vizuri kwa hewa.

Kwenye video hiyo yupo msanii wa Bongo movie Nisha ambaye amecheza uhusika wa Mwajuma lakini inadaiwa uhusika huo alitakiwa acheze Wema Sepetu lakini Mke wa Roma alikataza kitendo hiko.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Mke wa Roma amefunguka na kuweka wazi kuwa alimkataza mume wake kumtumia Wema Sepetu kwa sababu aliamini Nisha angefanya kazi nzuri zaidi na kuvaa uhusika:

Wakati wanaenda kushoot video nililetewa option ya video Queen wenyewe walikuwa wanataka kumchukua Wema Sepetu nikawaambia Hapana Wema hayupo Kwenye uhusika wa hiyo nyimbo yenu nikawaambia kama mnataka Msanii atakayevaa uhusika vyema basi mchukueni Nisha, na kweli Nisha amevaa uhusika vizuri sana na video imependeza”.

Wema Sepetu ameshawahi kuonekana kwenye video ya wimbo wa Diamond tu na alishawahi kusema hawezi kufanya video za wasanii wengi.

Video ya wimbo wa Rostam ‘Kaolewa’ inaendelea kufanya vyema na sasa inashika chati kwa kutrend namba 3.

“BASATA Mnaua Sanaa, Ubunifu na Vipaji”- Roma

Msanii wa muzili kutoka kundi la ROSTAM, Toma Mkatoliki amewatolea uvivu Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) baada ya kufungiwa nyimbo yao mpya.

Roma Mkatoliki amemwaga povu hilo baada ya ya yeye na msanii mwenzake Stamina kufikishwa BASATA siku ya jana baada ya kuachia wimbo wao wa Parapanda.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Roma ameandika na kudai kuhuzunishwa na jinsi BASATA wamekuwa wakifanya maamuzi yao juu ya kazi za wasanii.

Roma ameandika kuwa BASATA inaua Sanaa, Ubunifu na vipaji na kudai hachukizwi na BASATA bali anachukizwa na utendaji kazi wao pia akawataka mashabiki zake watoe maoni huku akisisitiza haoni kama wimbo wao wa parapanda ulikuwa na sababu za kufungiwa.

ROSTAM Waipania Fiesta 2018

Wasanii wanaounda kundi la rostam, Roma na Stamina wameonyesha manjonjonyao na jinsi walivyojipana katika kufunika tena fiesta ya mwaka 2018 kama walivyofanya hapo mwaka uliopita kwa mashabiki zao kwa show zao za kibabe.

Wasanii hao wameongea hivyo walipokuwa wakitambuisha wimbo wao mpya katika vituo vya clouds media na kusema kuwa mashabiki hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu ukimya wao walikuwa wakijipanga jinsi ya kuendelea kuwaburudisha  na wala kundi halijavunjika.

Hatukuwa kimya tu bila kuwa na sababu, tulikaa kimya ili kuja na kitu tofauti na kweli tumekuja na kitu tifauti.watu wasiubiri tu waone jinsi tutakavyo wapagawisha katika fiesta ni zaidi ya mwaka jana.

Kundi hili limeanza kufanya kazi zake mwaka uliopita lakini walikumbwa na misukosuko ya BASATA hapo katikati baada ya kutoa wimbo usiokuwa na maadili kwa jamii, hata hivyo kundi hili linafanya vizuri na wameanza kufanya kazi na wasanii wa nje.

Ray C na Rostam Wala Shavu Kutoka Kwa Msanii Wa Kenya

Raper wa muziki kutoka Kenya Khaligraph Jones siku ya jana aliachia rasmi albamu yake.

Albamu hiyo aliyoipa jina la Testimony 1990 ina nyimbo zipatazo kumi na saba na habari njema ni kwamba ndani ya nyimbo hizo kuna wasanii watatu wa Bongo fleva walioweka mkono humo.

Wasanii wa Bongo fleva ambao watasikika Kwenye Albamu hiyo ni pamoja na Msanii mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila ‘Ray c’ aliyeimba wimbo unaoitwa ‘Aisee’ na kundi la Rostam linalounda na Stamina na Roma.

Roma na Stamina watasikika katika albamu hiyo Kupitia kibao chao cha ‘Now you know’.

Hii inaonyesha ni jinsi gani muziki wetu wa Bongo fleva unavyozidi kukua kila siku na hata kufika kabisa mbele na kimataifa zaidi.

Umoja Wa Roma Na Stamina Kuvunjika Kabla ya Mwakani

Wasanii wawili waliokuwa wakiunda kundi la Rostam (Roma na Stamina), ambao wameanza kufanya vizuri kabisa katika muziki huku sasa hivi waki-hit na kibao chao chao cha kiba100 wanaweza kuvunjika na kutokufanya kazi tena pamoja kutokana na wawili hao kuwa  na upishani sana hasa kwenye swala la ratiba.

Akiongea na chombo kimoja cha habari , mmoja wa wanaunda kundi hilo anaefahamika kama Roma amaesma kuwa wamekuwa wakipishana sana na mwenzie Stamina kutoakana na kuwa busy sana na hata kuna muda wanashindwa kufanya baadhi ya mahojiano muhimu katika radio stations kwa sababu ya safari zake zisizokuwa na msingi.

Roma anasema kuwa Stamina amekuwa ni mtu wa kupoteza ratiba nyinhi sanahasa kutokana na kuangalia mpira muda mrefu huku yeye hawezi kufanya kitu kama hicho, hata hivyo roma anasema kuwa kuna kipindi wanaweza kukwaruzana akatamani hata kumpiga vibao kutokana  na kumpotezea madili yake mengi.

Roma anaendelea kusema kuwa kuna wakati alipigiwa simu anahitajika katika interview lakini mwenzie alipomjulisha alimjibu yuko njiani anakwenda mMrogoro ilhali yeye hakuwa na taarifa hizo wakati wapo katika muunganiko wa kikazi.hata hivyo msanii huyo alio ngea katika kipindi cha now you know kwamba hajui kama kundi ili litaweza kutoboza mwezi desemba na kuvuka mwaka kabla halijavunjika.

Roma na Stamina walianza kufanya kazi pamoja mwaka huu, wakiamua kuunda kundi hili kutokana na aina ya muziki wanaofanya kuendana lakini upishani wao unakuja pale ambapo kila mmoja anakuwa na interest tofauti.