“Siwezi kumfurahisha kila mtu” Linah awajibu wanaotaka afunike tumbo lake

Linah ambaye anamtarajia mtoto wake wa kwanza hivi karibuni ameamua kuwajibu mashabiki ambao wameonesha kuwa na shida na picha ambazo aliweka kwenye mtandao wake wa Instagram kuonesha tumbo lake.

Msanii huyu wa Bongo alisema haya baada ya mashabiki kadhaa kuacha maoni ambayo yalikuwa ya kuudhi kwenye picha zake ambazo aliweza kuonesha ujauzito wake.

Linah aonesha Ujauzito wake
Linah aonesha Ujauzito wake

Hata hivyo Linah haoni ubaya wa picha hizi na ndio maana amewajibu mashabiki hawa. Kulingana na alichosema, Linah haoni kwamba anaweza kufurahisha kila mtu na kwa upande wake haoni kama kuna shida yoyote.

“Siwezi kumfurahisha kila mmoja ndio maana anafanya kile ambacho anahisi kipo sahihi kwa upande wangu pia wakosoaji wapo wengi tu”

Linah achanwa mitandaoni baada ya kuachia picha hii

Linah ambaye akokaribu kumkaribisha mtoto wake wa kwanza hivi karibuni amewacha wengi wakiongea mitandaoni baada ya kuachia picha ambazo zinaonyesha uchi wa tumbo lake.

Muimbaji huyo aliwaacha wengi kama wamechanganikiwa baada ya rangi yake iligeuzwa na kuwekwa nyeusi huku akikaa nikama amepakwa mafuta mingi mwilini. Mmoja wa mashabiki wake aliandika kusema,

jumalokole2Kwanza najuwaga linna ni mweupe sasa sijui kapakwa nini na tarick,, pili aya mafuta ni ya kula au ya Nazi? . Maana umekandikwa ukakandikika haswaa. Kwani ukivaa dera tumbo alionekani? ?

Ingawa huu ndio mtindo ambao wanawake wengi wanaiga siku hizi, inaonekana Linah akufanya inavyotakikana. Tazama picha hiyo hapa.

Linah aonyesha muonekano wa kitanda cha mwanae anayemtarijia hivi karibuni

Linah bado hajataja jinsia ya mtoto wake mtarajiwa ila anaonekana ameanza kujipanga mapema kwani amebakisha wiki kadhaa ajifungue.

Muimbaji huyo wa Bongo amekuwa akiposti picha kuonyesha ujauzito wake huku akiwa na furaha ya kuwa mama kwa mara ya kwanza maishani yake. Hata hivyo hajamtambulisha baba ya mtoto anayemtarajia lakini hapo mbeleni aliweza kufunguka kwa kusema kuwa ni mtu wa dini ya Kislamu.

Hata hivyo amebakisha wiki kadhaa ajifungue na kulingana na mtandao wake wa Instagram, Linah ameanza kujipanga kwa kumnunulia mwanae kitanda na doli kadhaa alizoziweka mtandaoni wake.

Tazama picha aliyoiweka hivi karibuni.

Linah adai wazazi wake walimkataa mpenzi wake kwa sababu ya dini

Linah ambaye ni muimbaji maarufu Tanzania amefunguka mara ya kwanza kuhusu mchumba wake na baba ya mtoto anayemtarajia hivi karibuni.

Akizungumza na kipindi cha XXL cha Clouds Fm alisema kuwa dini iliwafanya wazazi wake kumkataa mchumba wake mara ya kwanza. Muimbaji huyo alisema kuwa amelelewa katika misingi ya dini ya kikristo na alipopata mimba ya mwanaume wa dini nyingine iliwafanya wazazi wake kuwa na ugumu wa kumkubali mwanaume huyo.

“Mwanzoni wazazi wangu walimkataa mpenzi wangu kisa ni dini tofauti na mimi, lakini sasa hawana pingamizi. Tumeunganisha damu na kwenye mahusiano naamini upendo, nisingependa mtu anipangie, lakini jambo la wazazi kwa familia za kiafrika ni tofauti.”

Aliendelea kusema kuwa hajuti kubeba mimba hiyo kwani aliipata at the right time.

Nimebeba ujauzito katika right time kwangu na mwenzangu yupo tayari. Mashabiki wategemee ndoa kabisa muda wowote.