Hii ndio sababu Linex hajaweza kuachia nyimbo mpya

Linex ambaye ni msanii wa Bongo ameweza kuachia nyimbo kadhaa ambazo zimetamba Afrika Mashariki kwa muda sasa. Lakini inaonekana kuwa ameweza kuwa kimya kwa miezi kadhaa bila kuachia nyimbo yoyote hata hivyo msanii huyu amefunguka kuelezea sababu zake za kutoweka mambo mpya.

Akizungumza kwenye kipindi cha Twenzetu Linex alisema kuwa alijipa muda wa kupumzika kwa sababu tangu aanze kuimba miaka 7 iliyopita hajapata saa ya kukaa nyumbani na kutulia na familia yake. Alisema,

“Kwa hiyo ninaweza kurudi muda wowote, sisemi kuwa nitakaa muda mrefu bila kutoa wimbo kwa sababu kuna vitu nilitakiwa kuvifanya lakini sikuvifanya ambavyo ni mapumziko, nimefanya kazi zaidi ya miaka saba sijawahi kukaa nyumbani hata siku mmoja,”

Aliendelea kwa kuongeza,

“Kwa hiyo nimejipa mapumziko huu ni mwezi karibia wannne sasa, nimekaa nyumbani nimepumzika, nimeandika kazi, kwa hiyo any time nitafanya kitu ambacho ni kikubwa.”

 

Msanii wa Bongo Fleva Linex adai kuwa kiki inaua muziki

Linex, msanii maarufu wa bongo amefunguka na kusema kuwa mtindo wa kupa mziki kiki unapoteza ladha na focus ya mziki nchini Tanzania.

Akiongea na waandishi wa global punlishers Tz nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es Salaam, Linex amesema kuwa imekuwa kama trend ya wasanii wa Bongo kutokea na skendo wakati wanpotaka kuachilia mziki siku hizi. Kulingana na yeye vitendo kama hivi havina maana kama msanii anaamini kazi yake ni nzuri.

Msanii huyu aliendelea kusema kuwa mashabiki ndio wanaoamua kama projects za wasanii ni za kuvutia au la. Linex alisema,

“Nachoweza kusema turudi kushabikia muziki mzuri, tuache kushabikia skendo. Nachokiona hapa muziki unapotea kabisa”

Ata hivyo hit maker huyo wa Kiherehere aliwasihi mashabiki kuwa makini na kufuatilia muziki wa maana badala ya kushabikia skendo za watu maarufu.