Lulu Diva- Siwezi Kuachana na Mavoko Kisa Kuondoka WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kudai hawezi Kuvunja Bongo Penzi lake na msanii wa Bongo fleva Richard Mavoko kisa tu amejitoa WCB.

Lulu Diva ambaye amekuwa Kwenye Mahusiano ya muda mrefu na Rich Mavoko ameongea juu suala hili kutokana na sakata linaloendelea hivi sasa kati ya Mavoko na uongozi wake WCB.

Kwenye na Global Publishers, Lulu Diva amesema kuwa amekutana na maswali ya wengi ambayo yame-fanya afahamu kwamba wanahofu na penzi lao kwamba linaweza kuwa ni mwisho kwa sababu uhusiano wao ulianza wote wakiwa wapo kwenye lebo hiyo, lakini wafahamu kwamba penzi lao haliwezi kukatishwa na WCB.

Watu wanahofia kwamba nitaachana na Mavoko kwa sababu ya kutoka WCB, hilo ni jambo lisilowezekana kwani tunapendana kweli na penzi letu halishikiliwi na lebo“.

Lulu diva pia alikataa kuongelea tetesi ambazo zimekuwa zikienea kuwania hivi sasa ana ujauzito wa Mavoko.

Rich Mavoko na Lulu Diva Waanika Penzi lao Hadharani

Msanii wa Bongo fleva kutoka label maarufu kabisa Tanzania Wasafi Classic Group (WCB), Rich Mavoko amejikuta anashindwa kujizuia na kuanika penzi lake na msanii mwenzake wa Bongo fleva Lulu diva.

Rich Mavoko na Lulu Diva wamekataa mara kwa mara habari za wao kuwa na uhusiano wa kimapenzi ingawa habari hizo zimekuwa hazichezi mbali nao kila uchao.

Habari za wawili hawa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi zilianza kusikika tangu mwaka jana ingawa kila mmoja wao amekuwa akikwepa tuhuma hizo na kudai hawana ukaribu wowote bali ni watu walio katika tasnia nyingine.

Siku ya Jumapili kampuni nzima ya WCB walikuwa wanamtambulisha rasmi msanii wao mpya ambaye wamemsaini ambaye ni Maromboso au Mbosso katika hafla hiyo matukio mbali mbali yalikuwa yanaendelea moja ya tukio lililowavutia watu wengi ni ukaribu uliokuwepo baina ya Lulu diva na Mavoko.

Wawili hao walionekana wakiwa wamekaa karibu sana (zero distance) huku mara chache chache walikuwa wakiwekeana mikono kama ishara ya kukumbatiana na kwa wakati huo wakiwa ndani ya maongezi mazito.

Wiki iliyopita habari zilisambaa kuwa Lulu diva kaachwa na sponsor wake anaye muweka mjini kisa ni mahusiano yake na Rich Mavoko lakini kama kawaida yao wawili hao walikataa tetesi hizo na Lulu diva kudai yeye ana mpenzi wake na wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Hizi baadhi ya picha walizopigwa Rich Mavoko na Lulu diva siku ya tukio:

 

 

Lulu Diva Adaiwa Kulitema Penzi la Mwanaume Anayemuweka Mjini Kisa Rich Mavoko

Mwanamuziki wa Bongo fleva Lulu Diva amedaiwa kulitema penzi la mwanaume aliyekuwa anamuweka mjini ‘Sponsa’ kisa na mkasa ni penzi la mwanamuziki mwenzake kutoka WCB Rich Mavoko.

Mambo yanasemekana sio mambo kwani Lulu Diva anadaiwa kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye ndiye aliyekuwa anamuweka mjini msanii huyo mrembo au wenyewe wadada wa mini wanawaita ‘Sponsa’.

Tetesi za Lulu diva kuwa na uhusiano na mkali wa Bongo fleva Rich Mavoko zilanza kuenea kitambo kirefu kweli ingawa inajulikana wazi kuwa Lulu Diva ana mpenzi wake mwingine ambaye mwenyewe amekiri kumpenda.

Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na habari za Lulu Diva kuolewa na mwanaume huyo ambaye habari za chini ya kapeti zinasema mwanaume huyo anaishi nchini South Africa lakini ndiye anaye mwezesha Lulu Diva yaani anamuweka mjini.

Inhawa mwenyewe Lulu mara kwa mara amesisitiza kuwa hana uhusiano wowote na mavoko zaidi ya kazi za kisanaa lakini picha zao zilisambaa mtandaoni miezi michache iliyopita zilisema vinginevyo kwani walikuwa wamekaa mikao ya kimahaba sana.

Pia chanzo cha habari hii kilidai kuwa picha zile zilizowaonyesha Luludiva wakiwa pamoja club pia zilimkasirisha mpenzi huyo wa Lulu diva hali iliyompelekea kumpiga kibuti lakini kwa sasa penzi la Lulu Diva na Mavoko linasemekana kuwa moto moto.

Baada ya habari hizi za kimbea kusambaa gazeti la GPL lilijaribu kumtafuta Lulu diva lakini baada tu ya kusikia alichoulizwa alikatiwa Simu lakini pia baada ya Mavoko kutafutwa alisema hawezi kuongea chochote kwani hajaruhusiwa kusema chochote na uongozi wake wa WCB.