Maimartha Atia Neno Mavazi ya Tanasha

Mwanadad maimartha ametia neno kuhusu mavazi ya mwanadada Tanasha ambae kwa sasa amekuwa ndio habari ya mjini kutokana na mahusiano yake ya kimapenzi na msanii Diamond pltainumz.

Maimartha anasema kuwa amekuwa akimuona mwanadada huyo akivaa nguo za ajabu ambazo zimekuwa hazieleweki lakii pia haziendani na hadhi ya mwna uema anaetembea nae akitokea madale.

maimartaha ambae kila siku amekuwa haachi kutoa comments kuhusu wanawake wanaokuwa katika mahusiano na msanii diamond platinums anasema kuwa tanasha amekuwa na tabia ya kuvaa malonya lonya mabayo hayana uelekeo wa mbele wala nyuma.

katika ukurasa wake maimartha aliandika ‘Mrs chibu…ni macho yangu au naona….mavazi yako saiayelewi…mbona kama unavaa maronya… au ni macho yangu tu..samahani lakini….sisi tunataka uvae kimadale madale…madale bwana…”

Ikumbukwe kuwa hata mama mzazi wa msanii Diamond Platinumz aliwahi kupata kigugumizi kutaka kuongelea swala la mavazi ya mwanadada huyo.

Sabby Angel Amtaka Maimartha Kutoingilia Mambo ya Hamisa Na Zari

Mwanadada Sabby Angel ameamua kumpa ushauri wa bure mwanamke mwenzie maimartha wa jesse kufuatia migogoro inayoendelea katika mitandao kati ya Hamisa Mobeto na Zari The Bossy kila siku katika mitandao ya kijamii.

Sabby anamwambia maimartha kuwa ni bora kukaa kimya na kuwaangalia wawili hao wakifanya wanayoyafanya kuliko kukaa na kuingilia kwa sababu wao ni wanawake wa mwanaume mmoja ambae kila mtu anamtoto na mwanaume huyo ( Diamond).

Maimartha asiiingilie kati ya hamisa na zari kwa sababu wote ni wazazi wenzie na DIAMOND ,  na hata yeye mwenyewe haonekani kuwa na  msimamo na mwanamke yoyote kati yao kwaio kuingilia ni kujichoresha tu.

Maimartha ambae hapo wali alikuwa akimshambulia sana Hamisa lakini sasa hivi anaonekana kuwa na chuki na zari na amekuwa akimsema katika ukurasa wake wa instagram.

Hamisa Akataa Darasa Alilopewa Na Maimartha Wa Jesse

Mwanamitindo Hamisa Mobeto amemjibu kwa kashfa mwanadada Maimartha wa Jesse ambae alimshauri Hamisa kuachana na kutukanana na kushindana na Zari katika mitandao bali ajiwekeze zaidi katika swala zima la kufanya maisha yake na kuacha kusikiliza maneno ya watu katika mitandao.

Katika darasa ambalo Maimartha alimpa Hamisa kupitia ukurasa wake wa instagram, alimwambia kuwa Hamisa hapaswi kabisa kusikiliza  maneno ya team yake kwa sababu wanamuharibia sana yeye na familia yake , lakini pia swala la kuwa na  team linafanya familia yake kudharirika pia.

ZKatika ushauri huo Maimartha alimwambia Hamisa kuwa ni bora kuungana  na Zari na kuwa nae kitu kimoja na kwa sababu  wote ni wazazi ni bora kuwe na mahusiano mazuri kati ya Mama Mobeto na Mama Diamond ili kuileta familia pamoja na pia awapende  watoto wa Nassibu na kuwachukulia kama watoto wake.Pamoja na yote Maimartha alitoa pia tathmini ya show aliyoifanya Zari Uganda na kumwambia Hamisa kuwa show yake ilikuwa ni kama alienda kujidharirisha tu kwa sababu show yake haikuendana na hadhi yake.

Katika ukurasa wa maoni, Hamisa alimua kumjibu Maimartha na kumwambia kuwa ushauri huo yeye wala hauitaji labda angeufanyia kazi yeye mwenyewe na familia yake ungemsaidia.

Huu ushauri un gejishauri wewe dada yangu na kizazi chako ungekusaidia sana lakini ndo hivyo tena.