Mkubwa Fella Awajibu Wanaomtukana Kisa Kifo cha Ruge

Moja wa wadau wakubwa katika tasnia ya sanaa nchini amefunguka na kuwajibu watu wanaomsema kuhusu kukaa kwake kimya bila kufanya chochote tangu ulipotokea msiba wa Ruge na hata kabla ya kifo chake.

Mkubwa fela amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakisema  hajali kitu kuhusu msiba huo bila hata kujua kuwa yeye na Ruge wametoka mbali sana na hata msiba huo umemgusa sana lakini hana cha kufanya kwa sasa kwa sababu na yeye ni mgonjwa.

katika ukurasa wake, mkubwa fella amefunguka na kusema ”

Mkubwa Fella Adai Hana Kinyongo na Juma Jux

Mdau mkubwa wa  muziki Bongo Mkubwa Fella ambaye alikuwa Meneja wa wasanii kama Wanaume TMK, Mkubwa  wanawe  Yamoto Band na amesema hana kinyongo na aliyekuwa msanii wake Jux.

Mkubwa Fella amesema pamoja na kulea hafanyi kazi za kimuziki na Jux kama ilivyokuwa zamani lakini sio kusema kinyongo na yeye Hapana bali bado anamkubali sana na kazi zake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mkubwa Fella amesema kwa sasa Jux ni mtu wake wakaribu zaidi kwa kuwa anaukubali muziki wake.

Bwana Jux amebaki kama shabiki yangu, kwa sababu tayari ameshakuwa lakini akitaka mawazo nitampatia kwa sababu sasa hivi anafanya kazi na watu wengine lakini kwangu ametoka ameshatoboa.

Yule ni mwanangu wa dhahabu, kwanza mimi ni shabiki yake namba moja kuliko mtu yoyote“.

Jux amesema ameendelea kufanya vizuri na kila ngoma ambayo amekuwa akitoa ambapo kwa sasa anategemea kuanza Tour yake na mpya na mpenzi wake Vanessa Mdee inayoitwa ‘In Love and Money”.

 

Aslay kakua Maswala ya Mapenzi Muachieni Mwenyewe.-Fela

Mkubwa fella amefunguka kwa mara ya kwanza na kuongelea  kuhusu mahusiano ya Aslay na aliyekuwa mpenzi wake na kupata naeo mtoto mmoja kuachana na kwamba wawili hao kwa sasa wanaishi mbalimbali.

Mkubwa Felaa anasema kuwa kwa sasa aslay ameshakuwa kwaio anauwezo wa kuamua kufanya yale anayoweza kufanya kwa kuamua mwenyewe lakini kuhusu swala la ndoa yake Aslay mwenyewe hajamfata na kumuelezea kuhusu kitu icho kwaio hawezi kusema kitu juu ya swala  hilo.

mkubwa Fela anasema kuwa kwa sasa aslay amekuwa ‘ mtoto kakua , huu ni mwezi wa ramadhani kwaio ingekuwa mwezi wa kawaida tungeongea lakini yeye kakua na anajua kuna ubaya, kuna mazuri kuna nini,angekuwa na akili angekuja angenifuata na kusema baba kuna hili na hili ningejua tunamrekebisha wapi.

Mkubwa Fela- Wanaopenda Kuona Diamond na Ali Kiba Wana Ugomvi Wameumbuka

Sio jambo la siri kuwa Wasanii wakubwa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Ali Kiba hawaivi chungu kimoja ingawa wenyewe kila mmoja kwa wakati wake amesisitiza  kuwa hana bifu na mwenzake.

Siku ya jana Diamond na Ali Kiba walizua gumzo baada ya kuonekana wakipeana mikono na kusalimiana Kwenye msiba wa marehemu Agnes Masogange.

Meneja wa Diamond na mdau wa muziki wa Bongo fleva Saidi Fella maarufu kama Mkubwa Fela amefunguka na kuweka wazi kufurahishwa na kitrndo cha Diamond kusalimiana na Ali Kiba.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Mkubwa Fela alifunguka haya:

Naomba nirudie tena niseme kama ninavyosemaga siku zote watu hawa hawanaga matatizo wala ugomvi kwaiyo hiyo ni baraka kwa nchi yetu na hata muziki wetu wa Bongo fleva kwaiyo cha msingi sisi tuombe dua watu waishi kwa usalama na amani tusipende ile watu wachukiane wapende kugombana sawa ni biashara maana mashabiki wanapenda ushabiki lakini haina maana wasanii hawa wachukiane”.

Lakini pia Mkubwa Fella ameongelea umuhimu wa wasanii hao kuonyeshana ushirikiano kwenye matatizo pale walipokutana Kwenye msiba wa Masogange Lakini pia Mkubwa Fela amewashangaa wachochea bifu na kudai wanaumbuka.

 

Fella Hamiliki Muziki,-Chambuso Aongea.

Ya Moto Band ni moja ya kundi kubwa la muziki lililokuwa limeteka sana hisia za mashabiki wa Bongo Fleva nchini kutokanana kazi nzuri waliyokuwa wakiifanya  katika muziki , kundi hilo  ambalo liliundwa na vijana wadogo waliokuwa wanachipukia kimuziki lakini walikuwa wakifanya vizuri. kKwa bahati mbaya kundi ilo lilikuja kusambaratika na vijana wote kuanza kufanya kazi kwa kujitegemea huku Aslay akiwa chini ya menejenti mpya  ya Chambuso.

Kabla ya kundi ilo kuvunjika lilikuwa likiongozwa na Chambuso pamoja na Mkubwa Fela na kuunda lebel iliyokuwa ikijulikana kama Mkubwa na wanawe  na moja kati ya kundi lililoundwa lilikuwa ni Ya Moto Band, ambalo hivi sasa limekufa.Hata hivyo baada ya kundi kuvunjika Chambuso aliamua kuanzisha lebel yake mpya  na  alipomchukia Aslay kama msanii wake.

Kumekuwa na  tetesi zinazoendelea  kwa baaadhi ya watu wakisema kwa endapo msanii akitoka kwa Mkubwa Fellla basi na muziki wake umekufa, Chambuso anakanusa maneno hayo na kusema kuwa“Wanaosema kwamba muziki upo kwa  peke yake, kwamba ukianzia kwake na ukatoka basi hautaweza kufanya vizuri tena, wanakosea na hakuna kitu kama hicho”

Chambuso anasema kuwa mfano mkubwa ni kutoka kwa aslay ambae ametoka kwa mkubwa fella na sasa hivi anafanua vizuri na kazi zake za kimuziki “Mbona Aslay  anafanya vizuri sana na hayupo kwa Fella? Msisahau kwamba hata yeye huu muziki alizaliwa na akaukuta, kivipi ishindikane msanii kutoboa  kisa hafanyi kazi naye, hicho kitu sikiamini.”anaongezea Chambuso

Hata hivyo maneno ya meneja mpya wa Aslay yanaweza kuthibitika kwa sababu tangu aslay amekuwa na menejiment mpya amekuwa akifanya vizuri na kila siku amekuwa akitoa nyimbo mpya ambazo zinapendwa sana na mashabiki, hivyo kufanikiwa kimuziki kwa msanii itategemea na nidhamu na juhudi anazokuwa nazo msanii binafsi katika kuifanya kazi yake ya sanaa.Tangu kuvunjika kwa kundi ilo Aslay ndio anayesikika sana katika muziki akifatiwa na  Beka ambae pia ametoa wimbo mpya wa Libebe na  Sikinai hivi karibuni.

 

Meneja wa Diamond: Wasanii wanaibiwa kazi zao, wananyonywa bila kujua

Mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz amelalamika kuhusu jinsi ambavyo wasanii wa Bongo wanavyo nyanyaswa na makampuni.

Diamond ako na meneja watatu; Sallam SK maarufu kama Mendez, Babu Tale na Mkubwa Fella ambaye pia ni muanzilishi wa kundi la TMK Wanaume Family na Yamoto Band.

Diamond na mameneja wake

Mkubwa amedai kuwa muziki wa Bongo umechelewa kuwanufaisha wasanii kwa kipindi kirefu kutokana na kukosa mlezi wa kuuongoza.

Mkubwa amedai kuwa makampuni zinazidi kupata faida nyingi kupitia kazi za wasanii ilhali wasanii wenyewe hawanufaiki pa kubwa.

“Muziki wetu umekosa mlezi wa kuuongoza ndiyo maana unakuta Wasanii wanaibiwa kazi zao, wananyonywa bila kujua pa kwenda kupeleka malalamiko yao, Unaona watu wanauza kazi za wasanii kiholela,” Mkubwa Fella aliambia Bongo 5.

Aslay ampaka tope Saidi Fella

Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella maarufu pia kama Mkubwa Fella amekosolewa hadharani na msanii Aslay.

Akiongea katika kipindi cha Zero Planet cha Ice Fm, Aslay alisema kuwa Mkubwa hamsaidii msanii anayefanya kazi yake binafsi.

“Ni kweli Mkubwa yeye anasimamia Yamoto Band, Mkubwa hasimamii msanii mmoja mmoja, kwahiyo unatakiwa ufanye kitu cha ziada ilimradi ngoma zako zifike. Wenzangu wanaandaa vitu vinakuja lakini mimi nimefanya kama nimewahi kuwaonesha njia,”Aslay alisema.

Aliyosema Aslay yanapinga maneno Mkubwa Fella alisema hapo nyuma kuhusu kusupport wasanii wa Yamoto Bend wanaofanya miradi zao za kibinafsi.

Soma pia: Mkubwa Fella: Hakuna msanii aliyekatazwa kuondoka ndani ya kundi ya Yamoto Band

Mkubwa Fella: Hakuna msanii aliyekatazwa kuondoka ndani ya kundi ya Yamoto Band

Mkurugenzi wa Yamoto Band Mkubwa Fella amefunguka kuhusu utata ambayo umekumba bendi hio baada ya Aslay kutoa wimbo wake binafsi.

Uvumi ulienea kuwa Aslay alizuiliwa kuondoka kundi hilo baada ya kufanya project yake ya muziki ya kibinafsi bila kushirikisha bendi ya Yamoto.

Akiongea na Bongo5, Mkubwa Fella alieleza kuwa wanabendi wa Yamoto wako na uhuru wa kuondoka ndani ya kundi hilo wakati wowote.

Mkubwa Fella

Fella pia alisema wasanii wa Yamoto wako na uhuru wa kufanya project zao binafsi za muziki.

“Hakuna msanii ambaye amekatazwa kuondoka Yamoto Band hata Mkubwa na Wanawe ila ukiondoka bila kuaga haufiki sehemu yoyote.

“Mimi nawasaidia kuwaonyesha njia wafike sehemu fulani, mtu akijiona amekuwa kwanini nimzuie?. Hakuna aliyefungwa kwa namna yoyote, sema ni vyema mtu kufuata taratibu hata za makuliano yetu ya mdomo.

“Aslay hivi karibuni ameachia kazi yake mpya na sisi tunamsupport kwa sababu kabla ya Yamoto Band, Aslay alikuwa msanii ila sisi tulimtumia yeye kuwainua wenzake na kweli tumefanikiwa leo hii vijana wanapata makate wao wa kila siku. Kwa hiyo hata wasanii wenzake wanaweza kufanya hivyo pia lakini kama wanamakubaliano yao binafsi siwezi kuyaingilia,” Mkubwa Fella alisema.