“Wote Wanaomkejeli Ruge Hawatamaliza Mwaka”- Mwijaku

Muigizaji maarufu wa Bongo movie Mwijaku amewajia juu watu wote ambao wamekuwa wakimkejeli aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi Ruge Mutahaba.

Baada ya Ruge kufariki siku mbili zilizopita maneno Mengi yaliibuka kwenye Mitandao ya kijamii ikiwemo Msanii kama Dudubaya ambaye alianza kumuongelea vibaya Marehemu.

Baada ya watu Mbali Mbali kukemea Suala hilo Serikali imeingilia kati na sasa Hivi Msanii Dudubaya amewekwa chini ya ulinzi wa Polisi kwa muda usiojulikana.

Mwijaku amewajia juu watu wote wanaomsema vibaya Marehemu Ruge na kusema wazi kuwa yeye binafsi ana mpango wa kusali na kuwaombea dua watu wote ambao wanafanya matendo hayo na kuhakikisha kuwa watu hao hawatamaliza mwaka:

Naomba niseme kuwa mimi binafsi nitafunga na kusali na kufanya dua kwa ajili ya wote ambao wamekuwa wakimdhihaki Boss Ruge.

Mimi Ruge ni Kaka yangu kwaiyo hiyo Dua naapa itawafikia hao watu na ninawahakikishia hao watu kuwa huu mwaka hawataumaliza “.

 

Maneno ya Mwijaku Kuhusu Mke Wake Yachafua Mitandao

Moja kati ya watu wanaongelewa sana katika mitandao kwa sasa ni msanii Mwijaku ambae amekuwa akitumbua majipu ya watu mbalimbali hasa wasanii wanaopenda drama katika mitandao ya kijamii.

Mwijaku ambae kwa sasa amekuwa akisemea kila kinachotoka katika mitandao kuhusu wasanii wenzake amewaacha watu hoi baada ya kusema kuwa katika wanawake wote Tanzania, mke wake pekee ndo mwanamke mzuri kuliko watu wote,

Msanii huyo aliamua kumsiafia mke wake na kuwapnda wanawake wengine huku akiamini kuwa wanawake wengi wa bongo wanakosa uhalisia wa maisha na ndio maana kutwa kushinda katika mitandao ya kijamii na wanashindwa kukaa katika ndoa zao na wengine hawabahatiki kabisa kupata ndoa.

Msanii huyo aliwaacha watu midomo wazi huku wengine wakihjaribu kufanya uchunguzi na mlinganishao wa mwanamke wake na wanawake wengine waki kibongo hasa wasanii.

Mwijaku Awaonea Wivu Jacquline na Mume Wake

Moja ya waigzaji na wasemaji sana ktaika mitandao ya kijamii Mwijaku amefunguka na kusema kuwa moja ya vitu anavyotamanisana katika maisha yake ni kuwa na familia bora kama ile ya mengi na mke wake.

Mwijaku anasema kuwa  mke wabwana mengi ni moja kati  ya wanawke wachache sana wenye pesa nyingi lakini pia na heshima kubwa sana katika jamii na hata mitandaoni., pamoja na umri wake kuwa mkubwa lakini amekuwa moja kati ya wanawake wachache sana walioweza kutunza heshima zao kwa muda mrefu bila kuwa na skendo mbya ambapo kwa mijaku hii anaita ni ubora wa mwanamke.

Mwijaku anasema kuwa ifike mahali, mwanamke anatakiwa kujua idaid na kiwango cha wanaume wa kuwa nao katika mahusiano kabla ya kuoa au kuolewa lakini pia sio kila mwanamke ni wa kumtongoza vivyo hivyo kwa mwanamke sio kila mwanaume ni wa kumpa namba.

Mwijaku anasema kuwa anachoona wivu kwa mengi ni kuwa amekuwa moja kati ya wazee wachache sana wenye bahati ya kuzeeka akiwa kama brother men , kitu ambacho sio rahisi kila mtu kukipata.

Mc pilipili Amewadhalilisha Wanaume Wote :-Mwijaku

msanii wa maigizo maarufu kama mwijaku amefunguka na kumtupia lawama msanii mwenzake upande wa vichekesho mc pilipili kwa kitendo alichokifanya wikiend hii na kumuita kuwa ni zuzu.

Mc pilipili ambae aliweza kumvalisha pete mchumba wake phinomena wikiendi iliyopita na kuzua gumzo sana kutoka katika mitandao ya kijamii kwa sababu alimwaga machozi kipindi akimvalisha pete mwanamke huyo kitu ambacho hakikuwa cha kawaida katika matendo hayo.

Mwijaku anasema kuwa alichokifanya MC pilipili ni kuwa zuzu kwa sababu huwezi kulia mbele za watu kwa sababu ya mwanamke na kwmaba amewadhalilisha wanaume wote wa dar kutokana na kitendo icho.

Mwijaku anasema kuwa kulia sio dhambi lakini dhambi ni pale unapolia mbele ya watu lkwa sababu ya mwanamke.

Sio dhambi kulia, dhambi ni kulia mbele za watu kwa sababu ya mwanamke .

Hata hivyo Mwijaku anasema kuwa amekuwa akimfahamu sana Mc pilipili naamekuwa akimueleza mengi kuhusu yake anayoyapitia katika mahusiano yake.

 

“Wema Anasumbuliwa na Pepo La Ngono”- Mwijaku

Muigizaji maarufu wa Bongo movie anayejulikana kama Mwijaku ameibuka na kudai kwamba Msanii mwenzake Madam Wema Sepetu anasumbuliwa na pepo la ngono.

Mwijaku amefunguka hayo alipokuwa anaongelea skendo inayomuandama Wema Sepetu hivi sasa ya kusambaa kwa picha na video akiwa faragha chumbani na mpenzi wake anayeitwa PCK.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo, Mwijaku ameibuka na kudai anaamini kabisa Wema atakuwa na pepo la ngono kwa sababu mambo anayofany sio ya kawaida kabisa:

Wema inawezekana sio umaarufu wake unaomsumbua kuna kitu kingine tu kinamsumbua nacho ni pepo la ngono, nisikufiche naongea leo niko hai mpaka nakufa kama hatatibiwa pepo la ngono tutaona anaenda vizuri kesho anaaibika.

Lakini pia leo hii mambo anayefanya Wema hawezi kupata investor serious aka invest Kwenye Wema Sepetu Brand   Kwa sababu hakuna mtu anayeweza kuwekeza kwa mtu ambaye anakuaibisha yaani endorsement zote atapoteza na kuishia kujirudisha nyuma”.

Tangu kusahau kwa video hizo chafu Wema Siku ya jana ameita mkutano na waandishi wa habari na kuomba radhi kwa yote aliyofanya.

Alichoandika Mwijaku Kuhusu Anachoweza Kumfanyia Mwanamke Wake.

Mwigizaji mfanyakazi wa Clouds Media mwijaku amefunguka na kusema kuwa kwake mwanamke ni kama malaika na anaweza kumfanyika kila kitu anachotaka kwa kuwa mwanamke wake anastahili kufanyiwa hivyo.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram , Mwijaku anasema hata kama kuna kitu hataki kufanyiwa lakini ana stahili kufanyiwa basi yeye atafanya kwa sababu anastahili na kikubwa zaidi ni kwamba haoni shida kuonekana kuwa mwanaume wa kizamani kwa sababu ya mwanamke anayempenda.

Mimi Ni aina ya Boyfriend ambae siogopi kufanya lolote kwa mwanamke ninaempenda. Anahitaji pedi? Nitamnunulia. Anataka nimsaidie kubeba mkoba? Nitambebea. Anataka nimpake rangi kucha? Nitampaka. Nimfumue nywele? Nitajaribu. :

Hataki zawadi yoyote kutoka kwangu? I don’t care nitampa tu..anahamu ya chocolate? Nitamnunulia…anajihisi maumivu ya mgongo? Nitamfanyia massage ya mgongo!

Anataka kwenda dinner date sehemu nzuri nzuri, she shuldn’t worry…we will go there babe!

Haujisikii poa, umechoka mishe mishe za kazini? Asijali nitampikia chakula kitamu…ni mwanamke wangu, msaidizi wangu…nitafanya kila kitu chochote kile kuhakikisha naliona tabasamu lake. :

Naamini mwanamke bora anahitaji kila kitu.

I do forever staffs! Saved, Smart and Straight!! That’s me…the old fashioned me

 

 

 

“Irene Hana Marafiki Wa Kweli, Shamsa Ford ni Mnafki” Mwijaku Amchana Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie maarufu kama Mwijaku amemwagia povu zito msanii mwenzake Irene Uwoya baada ya picha yake kusambaa siku ya jana.

Siku ya jana Irene aliposti picha iliyozua utata Kwenye mitandao ya kijamii na mara moja Mwijaku alimwandikia posti nzito ambayo alimsema sana kwa vazi lile hasa kwa sababu ni mke wa mtu.

Lakini Mwijaku hakuishia hapo kwani Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Mwijaku alionekana akiweka wazi Kuwa marafiki zake na a Uwoya wanaomsapoti kwa picha zile ni wanafiki wakubwa kwani wanamshauri vibaya wakijua wazi kabisa picha ile siyo nzuri:

Irene ni mtu mzima na mke wa mtu na hii ni ndoa yake ya pili kwa nini aposti picha kama ile? Nikajiuliza Marehemu Ndikumana angekuwepo wakati amemuoa angeweza kuposti kitu kama kile? Asingeweza kuposti Ndikumana alikuwa mkali ila kwa sababu mume wake Dogo Janja ni mdogo basi anamuonea.

Halafu na marafiki wanaomzunguka Irene ni wanafiki siku akija kufa atakuwa peke yake halafu na Shamsa Ford anaenda kumwambia hivyo hivyo umependeza ishi utakavyo! Tuongee ukweli Shamsa Ford ni mnafki na anampoteza mwenzake”.

Dogo Janja aliweka wazi kuwa hakukerwa na picha ile zaidi alimpa sapoti mke wake.