Chege awashirikisha Ray C na Sanaipei kwenye wimbo wake mpya-Najiuliza

Chege ameamua kuwachia nyimbo mpya ambayo inawazingua mashabiki wake baada ya kuwashirikisha warembo, Ray C na Sanaipei Tande kutoka Kenya.

Watatu hao wamejiunga kwenye wimbo unaozungumzia mapenzi huku Ray C na Sanaipei wakiomuomba Chege achungue mrembo anayemtaka.

Wimbo huu unalenga mambo ambayo wanaume na wanawaka wengi hupitia. Video hiyo imetengenezwa na Kwetu Studio. Itazame hapa

“Mimi sina mpenzi” Ray C asema

Ingawa Ray C ni mrembo na mwanamke mwenye umbo la malkia bado hajaweza kuanza familia yake kwani hivi sasa hana mpenzi wala hana haraka ya kutafuta mtu wa kumpenda.

Muimbaji huyu amesema kuwa sasa hivi mawazo yake yote yako kwenye muziki na siyo mapenzi. Ray C ambaye alikuwa amepotelea kwenye madawa ya kulevya amejipa muda kufanya kazi yake ambayo aliiwacha baada ya haijakamilika baada ya kuzidiwa na raha ya madawa ya kulevya.

Ray C
Ray C

Hata hivyo akizungumza katika interview Ray C aliweza kusema kuwa hivi sasa anaonelea kuachilia nyimbo ambazo mashabiki wake watafurahia kabla ya kufikiria ikiwa atatafuta mpenzi wa kutulia na yeye. Alisema,

“Mimi sina mpenzi. Kwa sasa nafikiria kuhusu muziki wangu sitaki kujichanganya na mambo mengine. Mashabiki wangu wamenipambania kwa muda mrefu siyo kwaajili ya mpenzi wangu, wao wanataka kazi, muziki mzuri.”

Diamond Platnumz amuandikia Ray C ujumbe kumpa moyo wa kutokata tamaa katika muziki wake

Ni wengi ambao hawakudhania kuwa Ray C atarudi kufanya muziki tena baada ya kupotea ndani ya madawa ya kulevya. Hata hivyo mrembo huyu amewafurahisha wengi ambao hawakuwa wamekata tamaa kwake.

Mmoja wa hawa ni Diamond Platnumz ambaye amemwandikia ujumbe wa kumtia moyo huku akimsihi kuendelea na muziki wake japo ya kukawia sana bila kutoa nyimbo.

Kupitia mtandao wa Instagram Diamond aliandika kusema…

Ray C

Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali…. Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya….

Diamond aliendelea kwa kusema,

Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku? @rayctanzania

Hata hivyo Ray C ameonyesha kuwa hanamipango ya kuacha muziki tena na kuna uwezekano wa kuenda mbali hivi karibuni.