Rich Mavoko Ashinda Kesi Dhidi Ya WCB BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko ameripotiwa kushinda kesi dhidi ya Label yake ya zamani WCB na kufanikiwa kuvunja mkataba na kutoka.

Rich Mavoko ambaye alijizolea umaarufu miaka ya nyuma kwa vibao vyake vikali  alisainiwa na kujiunga na WCB siku za nyuma kidogo na kutoa nyimbo kadhaa zilizomrudisha Kwenye chati.

Lakini mapema mwaka huu kulikuwa na tetesi nyingi Baada ya Rich MAvoko kutoonekana Kwenye shughuli mbali mbali za WCB na hata kutoonekana kwenye trailer ya shoo mpya ya Wasafi.

Rich Mavoko pamoja na uongozi wake WCB wamekuwa kimya juu ya Tetesi za Rich Mavoko kuondoka WCB Mpaka sasa ambapo kuna taarifa kuwa Mavoko kajitoa rasmi.

Kituo cha Televisheni cha TV E  wanaripoti kuwa siku ya leo Mavoko amefanikiwa kushinda kesi dhidi ya WCB rasmi na inasemekana amejitoa Kwenye Label hiyo Lakini pia mkataba alikuwa nao umevunjwa.

Mpaka hivi sasa Rich Mavoko hajatoa tamko lolote kuhusu  nini kinachoendelea Mpaka sasa Uongozi wa WCB haujatoa tamko juu ya tuhuma hizo.

Mashabiki Wampongeza Mavoko Kuondoka WCB

Baada ya msanii  Rich mavoko ,aliyewahi kuwa   katika kundi la wcb kutoa ngoma mpya na  baadhi ya mashabiki kumpongeza kwa uamuzi huo mkubwa aliuamua. hata hivyo utata unakuja pale ambapo wengi wa mashabiki wake wanaamua kutoa pongezi kuwa  bora alivyoondoka WCB ,

Hakuna mtu yoyote aliyethibitisha kufukuzwa kwa Rich mavoko lakini kuna  baadhi yaishara tu zimekuwa zikionyesha kuwa  msanii huyo ametoka wcb kama vile kufuta baadhi ya picha alizowahi kupiga akiwa na wasanii wenzake wa wcb lakini pia hata kutoa bo ya wcb katika ukurasa wake wa instagram.

Kubwa zaidi ni kwamba Rich Mavoko ameshaamua kum-unfollow bosi wa wcb ambae ni diamond platinumz.

Swala la wasanii wa wcb kuondoka au kuacha kazi limekuwa likifanywa kimya kimya na hii inaweza kuangalia hata katika mifano ya nyuma kama kwa Q-boy, kwa kifesi na hata bodyguard wao ambae mpaka sasa hakuna ana ejua hatima yake mpaka pale yanapowafika shingoni ndio wanaanza kusema ukweli.

Hata hivyo mashabiki wamefurahi sana ujio mpya wa rich mavoko na huku wengi wakiamini kuwa kuwepo kwake WCB ndiko kuliko sababibsha ukimywa wake siku zote bila kutoa ngoma.

Mavoko Athitisha Kujitoa WCB

Kumekuwa na mambo mengi yakizunguka kuhusu ukweli wa  msanii rich mavokokuwepo ndani ya wcb au hayupo tena, kila mtu amekuwa akiongea lake uku wengine wasitake kusema moja kwa moja kuusu swala hilo.

Hata hivyo katika akaunti za wasanii wa WCB wote kumekuwa na alama inayoashiria kuwa msanii huyo anatoka katika lebo ya WCB, lakini hii imeonekana tofauti kwa akaunti ya instagram ya Rich mavoko kwa sasa kwa sababu kiashiria icho hakipo  tena kama hapo awali,

Lakini pia kama kunakuwa na ushirikiano kati ya wasnaii basi wanaweza kuwa wanafuatana katika kurasa zao lakini, rich mavoko  amemu-unfollow bosi huyo ya lebo hiyo hivyo kwa sasa hawana mahusiano mazuri katika mitandao.

Hivyo vinaweza kuwa ni viashiria vicaheche vinavyoweza kumfanya mtu aamini kuwa rich hayupo tena katika kundi hilo, na kwa kusthibitisha hilo zaidi, mwanamuziki huo ametoa wimbo mpya  ambao haonyeshi kuwa na mahusiano yoyote ya uzalishaji na wcb.

Babu Tale Aanika Ukweli Kuhusu Rich Mavoko Kutimuliwa WCB

Meneja wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Babu Tale amefungukia kwa mara ya kwanza tetesi zinazoendelea kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rich Mavoko katimuliwa.

Tetesi hizi zilianza wiki chache zilizopita baada ya Mavoko kutoonekana Kwenye tangazo jipya la Trailer ya Wasafi reality show lililowaonyesha wasanii wote wa WCB na familia ya Diamond.

Kwenye mahojiano  na Ijumaa kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp akiwa Marekani, Babu Tale alisema kwamba tetesi hizo siyo za kweli na Mavoko bado yupo WCB ila kipindi ambacho walikuwa wanachukua video ya Reality Show aliyoiposti Diamond ambayo ndiyo iliyozua maneno mwanamuziki huyo hakuwepo alikuwa kwao Mahenge, Morogoro kwenye msiba kwani alifiwa na dada yake.

Wakati tunarekodi hiyo video ya Reality Show, Mavoko alikuwa Mahenge kwao, alifiwa na dada yake kwa hiyo alikuwa kwenye msiba, lakini hizi siku zote yupo bize anashuti wimbo wake mpya na zamu inayokuja ni yake kuachia wimbo kwani sisi huwa tunaachiana muda wa kutoa nyimbo kwa hiyo sioni haja ya kuongopa kwamba hayupo WCB, kwa sababu hata asipokuwepo lazima itajulikana tu”.

Baada ya habari kuanza kusambaa Mavoko alimtafuta ili kuthibitisha taarifa hizo lakini alikataa kabisa kuongea na kutaka uongozi wake utoe majibu ya maswali hayo.

Rayvanny Afungukia Suala la Rich Mavoko Kutimuliwa WCB

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Rayvanny amefunguka kuhusu Tetesi za Msanii mwenzake Rich Mavoko kutimuliwa kutoka katika label hiyo.

Tetesi za Mavoko kutimuliwa WCB zilianza kusambaa mwezi uliopita baada ya kutoonekana Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na WCB ambao ulijumuisha wasanii wote wa label Lakini pia Mavoko hajaonekana Kwenye trailer ya shoo mpya ya Wasafi.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Rayvanny amesema hawezi kuliongelea sana suala hilo kwa sababu sio msemaji lakini amesema Rich Mavoko bado yupo na huwa wanawasiliana naye mara kwa mara:

Ujue sisi tunachekiwa kwenye group, leo kuna tukio hili na hili, so ukiona huyo kakosa ni masuala ya uongozi sana labda angekuwepo Diamond au Babu Tale angeweza kuongea sana lakini Mavoko yupo Wasafi kila siku.

Anakuja, anajiunga kwenye vitu lakini yeye kutokuja siku ile sijui sababu, kama kuna vitu vinavyoendelea ni yeye na uongozi. Mimi siwezi kuongea sana kwa sababu Mavoko ni mwanangu tunaongea tunachati, tunarekodi ngoma zetu“.

Lakini Hata hiyo Babu Tale alieleza kuwa siku hiyo Rich Mavoko alikuwa aki-shoot video ya wimbo wake mpya na kushindwa kuhudhuria.

Rich mavoko aeleza kwa ukamilifu kwa nini aliamua kuumpa mwanawe jina la babake Dokii

Hii leo, 19th April 2017, Rich Mavoko alikuwa mgeni kwenye Clouds FM ambapo alizungumzia mambo mbali mbali ikiwemo mtoto wake.

Alieleza kwa ukamilifu aliwita mwanawe Wency, jina la babake Dokii na akaeleza ya kwamba yeye na Dokii ni Ndugu na ilifaa kumpea babake heshima.

Pia soma: Huu ndio ujumbe Rich Mavoko alioutoa kwa wasanii wote wa Tanzania…mpaka bosi wake Diamond

Pia alizungumzia wimbo wake mpya Show me ambao ameshirikiana na Harmonize na akaeleza ya kwamba ana matumaini ya kubadili style yake ya muziki na pia image yake kama msanii.

”Nimeamua mwenyewe nibadilishe muonekano wangu wa nywele. Kuhusu cheti nilichopata kwenye Jiwe La Mwezi, kwangu ni kitu kikubwa sana na asanteni kwa kutupa thamani wasanii.” Alieleza.

 

Kuna nini? Rich Mavoko na Nay wa Mitego wakijibizana mitandaoni

Kuna dalili za Rich Mavoko na Nay Wa Mitego kuanza beef baada ya majibizano yao mitandaoni ya kijamii hivi karibuni.

Hii ilianza baada ya Mavoko kuposti picha na maneno ya kuwajulisha mashabiki wake kuwa anatarajia kuachia nyimbo mpya hivi karibuni kwa kuandika.

Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii ? #Showme

Lakini baada ya masaa kadha Nay wa Mitego alirepost picha hiyo ya Mavoko na kumchana kwa kumwambia kuwa ngoma yake mpya WAPO ndio inapaswa kutiliwa maanani na wananchi. Aliandika kusema,

Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii ? #ShowmeNAOMBA MUENDELEE KUSUBILI, MAY BE MPAKA MWAKANI 2018, NDO MTAANZA KUJISHUGHULISHA NA MASWALA YA KUWAIMBIA WANA NCHI. MWAMBIENI NA BABA YENU PIA AWE MPOLE KWASASA ALEE WATOTO. KAZI TULIYO NAYO IKIENDA SAWA TUTA WARUHUSU MUENDELEE KUBURUDISHA WANA NCHI. TUNATAKA MAMBO YAENDA SAWA KWANZA✊?.
Wimbo wetu wa TAIFA ni #Wapo LINK ON MY BIO☝?️

Huu ndio ujumbe Rich Mavoko alioutoa kwa wasanii wote wa Tanzania…mpaka bosi wake Diamond

Rich Mavoko ana ujumbe na ni ujumbe ambao anaelekeza kwa wasanii wote Tanzania na pia mashabiki wake.

Na ni ujumbe ya kwamba anawachilia wimbo wake mpya na ina maana watu waache siasa na washughulike na kueneza wimbo huo.

Tunafikiri alikuwa akimweleza bosi wake Diamond ambaye amekuwa akihusika na mambo ya siasa sana Tanzania.

Huu ujumbe ulikuja pia na picha tunayo tumaini ni wimbo mpya aliotoa. Itakuwa wimbo wake mwingine baada ya Kokoro.

Hivi ndivo alivyoandika mitandaoni:

“Hapana, siasa ipo kila siku ila now naona wasanii wengi wanaliongelea hilo, ila mie sidhani kama ngoma nzuri inashindwa kwenda kwaajili ya siasa,” amesema.

Kuhusu muda wa kuachia wimbo wake Mavoko amesema, “Wiki hii naweza kufanya hivyo, au wiki ijayo mwanzoni.”

Na pia kutupa picha hii:

Rich Mavoko