Rommy Jones Adai Mwanamke Pekee Anayemfaa Diamond ni Zari

Kaka wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Rommy Jones ameibuka na kudai mwanamke pekee  anayemfaa mdogo wake ni Mpenzi wake wa zamani na mzazi mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari’.

Mahusiano ya Diamond yameendelea kutengeneza headlines Kwenye mitandao ya kijamii hasa sasa kutokana na warembo wawili ambao ni Kim Nana na Lynn kuonekana kugombani Penzi la staa huyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Rommy Jones, amefunguka kuwa mke pekee ambaye anamfaa mdogo wake huyo ni mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’.

Nasema ukweli ndani ya moyo wangu, Zari ni mwanamke ambaye anafaa kuwa mke na kuwekwa ndani kwa sababu anajielewa na anasimama kama mama kuanzia kwenye ulezi wa watoto wake na kila kitu ndani ya nyumba”.

Rommy amesema anatamani Zari awe shemeji yake wa maisha na ikiwezekana wafunge ndoa kwani ana kila sifa ya kuwa mke na ndiye mwanamke pekee anayeweza kumuweka sawa mdogo wake na akaenda kwenye njia sahihi.

Unajua kila familia ingependa sana kuona mtoto wao anapata kitu kilicho bora, yaani mke ambaye anaweza kusimama vyema kama mama hivyo mimi leo nikiamka Diamond aniambie anamuoa Zari, nitafurahi sana kwa sababu najua atakuwa amepata kilicho bora kabisa”.

Lakini pia Rommy hakusita kuwaongelea Lynn na Kimnana ambapo amesema;

Unajua Diamond kwa hao (Lynn na Kim Nana) ni kama tu zile za mwanaume kutenda kosa na kuchepuka nje, lakini akawa na msimamo na mwanamke wake, kwa hiyo kwa hao siwezi kumuongelea sana kwa sababu pia sisi hata siku moja hatukai na kujadiliana naye mambo yake ya kimapenzi, ila ukizungumzia mke, basi nitakuambia ni Zari tu”.

Romy Aongelea Kutochezwa kwa Nyimbo za Rich Mavoko Wasafi Tv

Dj maarufu wa msanii mkuwa diamond platinumz amefunguka na kuongeea swala la Wasafi Tv kutocheza nyimb za msanii rich mavoko ambae hapo awali alikuwa msanii wa lebel hiyo lakini kwa sasa wametengana baada ya kupelekana BASATA.

Rommy anasema kuwa hakuna ubaguzi wa wasanii katika tv yao lakini labda tu mzunguko wake haujafika na kama ukifika bas nyimboi zake zitachezwa kwa sababu kama zimekuwa zikipigwa za Alikiba na Ommy kwa nini sio zake.

sidhani kama kuna shida , kwa sababu tumepiga za Alikiba, na ommy dimpoz kwanini tusicheze za Rich mavoko ukiona haijachezwa basi ujue mzunguko wake haujafika tu.mzunguko wake ukifika itachezwa na itabaki kuwa ile ni ya kwetu sote.

Hivyo Rommy anathibitisha kuwa hakuna makatazo yoyote kutoka kwa uongozi wa WCB kuhusu kutopigwa kwa ngoima za Rich mavoko.

 

Rommy Akataa Kusimamamiwa na Wasafi

Dj maarufu kutoka kundi laWcb, Rommy Jones amefunguka na kusema kuwa pamja na kwamba hata yeye anatokea katika kundi la wcb, lakini hii haimaanishi kuwa hata yeye  atasimamiwa na Wcb , watu wajue klwamba yeye anajisimamia mwenyewe na project zake.

Ingawa watu wengi walitegemea kuwa kutokana na ukweli kwamba Rommy yuko Wcb na wcb imekuwa na wasanii wengi wanaofanya kazi chini ya lebel hiyo basi hata yeye na project zake za muziki itakuwa chini ya wcb lakini kumbe sio.

pale unajua mimi ni vice president na kuna record lebel ambayo ni wcb,  na inawasanii wengine tu kama kina Mbosso, Harmonize , Lavalava na Rich Mavoko ila mimi siko chini ya Wcb, kwa project zangu zote ninafanya kwa kujisimamaia mwenyewe wala sio Wcb,

Rommy Jones Kuja na Album Yenye Wasanii Kutoka Marekani.

Dj maarufu kutoka lebel ya WCB Rommy Jones ambae pa ni ndugu wa msanii Diamond amepanga kutoa album yake ya muziki mwaka huu ambapo amesema kuwa kutakuwa na wasanii wengi katika album yake hiyo huku wengine wakitokea nje ya nchi.

Rommy ambae hivi karibuni ametoa wimbo wake aliomshirikisha Baraka The Prince amaesmea kuwa mwaa hu hautaisha na atafanya kitu kikubwa cha kuzindua album yake hiyo na kusema kuwa itakuwa na radha nyingi ikiwemo raggae, Hip Hop na pia Rnb.

Album yangu nadhani mwezi wa saba nitasema inatoka lini,album yangu iko tayari na kadri siku zinavyozidi ndio na yenyewe inazidi kwenda mbele  , na kitu kizuri ni kwamba humu hakuna radha moja tu ya bong fleva kuna hip hop , kuna raggae  na radha nyingi tofauti kwa sababu hata wasanii wako wengi tofauti.

Rommy Jones ambae mara ya kwanz alikuwa amejikitakatika kazi yakuwa dj wa msaniii Diamond ameamua kuibuka na kuingia katika muziki ukizingatia amekuwa katika kazi za muziki kwa muda mrefu.

 

Baraka ni King’asti Kwa Naj;-Rommy Jones

Rommy Jones ni moja ya ma-Dj maarufu kutoka katika lebel kubwa ya wasafi chini ya mwanamuziki  nguli na anaefanya vizuri duniani kote Diamond Platinumz, amefunguka dj huyo baada ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili za kuwa amemtongoza mwanamke wa msanii Baraka the Prince anaejulikana kama Najma Datani.

                                        

Akiongea na dizzim online, Rommy anasema kuwa kwake yeye kilichokuwa kinazungumziwa ni baishara hayo maswala ya kutongozana yalikuwa yamekuzwa na Najma mwenyewe, hata hivyo rRommy anasema kuwa hawezi kukaa katika media akamzungumzia Baraka kwa sababu hana uwiano wowote wa kukaa na kumzungumzia Baraka kwa sababu Baraka ni king’asti kwa Najma.

Baraka ni kingasti kwa naj, mimi kwanza uwezi kunifafanisha na baraka hata siku moja, am paying my own bills, ninapokea mishahara kama kumi hivi, nalipwa na watu wengi wakubwa na siwezi kukaa nikaanza kuzungumzia swala la naraka aaaah sijui rommy katongoza mwanamke wa baraka .ukizungumzia maswala la kutongoza yule mwanamke ndio aliyafanya yaonekane kuwa makubwa kwa sababu mimi nilifanya kuzungumzia biashara maana mimi ninafanya biashara.

pointi ya kuongea nae ilikuwa ni kuanda shoo, Najma mimi nimemjua miaka kumi iliyopita huko kwanini sikumtongoza,nimtongoze leo.

Siku moja iliyopita baraka aliweka post yenye picha ya Rommy na kuandika kuwa andhamilia kumuumbua Rommy kwa yale anayoyafanya yasiyoendana na yeye , hata hivyo kabla hajaweka wazi kitu hicho zilivuja picha zikionesha meseji kati ya  Najma na Rommy ikionekana kama Rommy akimtongoza Najma.

Baraka The Prince Amuumbua Rommy Jones

Msanii wa bongo fleva Baraka The Prince ameshindwa kuvumilia kwa muda mrefu kitedno alichokifanya rommy jones na kuamua kumuumbua katika mitandao ya kijamii.Ingawa barak the prince hakutaka moja kwa moja kusema kile alichokifanya rommy jones lakini siri ilikuja kuvuja na kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Katika ukurasa wake wa instagram, Baraka The Prince aliweka picha ya Rommy Jones na kuandika caption hii”unaonekana mwana kumbe pimbi tu,hata hilo vazi uliovaa pia unalitia aibu tu,shenzi typ soon  nakutia aibu jamaa..next post nakutia aibu wack wewe..

hata hivyo baada ya baraka kushindwa kuweka moja kwa moja kosa la rommy, dada yake na rommy anaejulikana kama ladynaha aliamua kuweka wazi picha za meseji ambazo rommy alikuwa akichat na najdattan akiwa anamtongoza.

Picha hizo ndizo zilizosambaa sana katika mitandao na kufanya siri kuvuja na kitu gani kilifanya baraka aandike maneno yale kwa Rommy.

Mama’ake Rommy Atafuta Talaka BAKWATA

Mama mzazi wa Dj maarufu wa msanii Diamond Platinumz, Rommy Jones ambae pia ni kaka wa msanii huyo kutokana na ukaribu wao wa damu kwa sababu mama ya diamond na mama wa rommy ni mtu na dada yake, imesemekana kuwa amekuwa akienda   baraza la kiislamu (Bakwata ) kwa ajili ya kudai talaka kwa mume wake a nae ndoa miaka kadhaa iliyopita huku ikisemekana  kuwa mwanamke huyo anaejulikana kwa jina la Shani  amemzidi umri mwanaume wake,

Wakati huku ndoa ya mdogo wake ambae ni mama yake na Diamond(Sandra) ikiwa katika hatua za kuchipua huku kwa dada yake mambo ya ndoa yanaonekana kumshinda.

Dada wa mama Diamond (Shani) alionekana akiingia  Lakwata  mtaa wa lumumba jijini Dar kwa ajili ya kudai talaka kwa mwanaume wake ambae inasemekana kuwa alifunga nae ndoa miaka kadhaa iliyopitao lakini inasemekana kuwa mwanaume huyo ni mdogo kuliko Shani hivyo aliamua kuoa mwanamke mwingine anaeendana ane umri.

amekuja hapa mamaake na rommy anasema amechoka sana ,  mwanaume aliyenae amebadilika sana kwa sababu ameoa mwanamke mwingine wanaeendana nae umri,yeye ukimwangalia ni mkubwa sana kwa huyo bwana.Bakwata wamempokea na kumpa barua ya kwenda kumuita huyo mwanaume ili waje kuzungumza na ikibidi watoe talaka._Kilisema chanzo cha habari kilichokuwa kinapatikana maeneo hayo.

Hata hivyo wanahabari walifanikiwa kunasa barua hiyo ya Bakwata ambayo ilidai kuwa na muhuri na pia ilimtaka mwanaume huyo kufika ofisini hapo tarehe 27 February lakini siku ya tukio mwanaume huyo aliejulikana kwa jina la Ajazi alimuita mama huyo ofisini kwake na kumtaka wakayazungumze ili yaishe.