Ruby afunguka baada ya kusemekana anatoka kimapenzi na Alikiba

Iwapo hauna habari basi hivi karibuni muimbaji wa Bongo Ruby alisemekana kuwa ndiye mpenzi mpya wa Alikiba. Taarifa hizi zilisabaa kwenye mitandao baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja mara kadhaa.

Hata hivyo Ruby ameweza kufunguka kuhusu taarifa hizi na kukana waandishi wanachoandika mitandaoni. Kulingana na Ruby hakuna kinachoendelea kati yake na Kiba huku akiendelea kwa kusema kuwa hata hana namba ya muimbaji huyo.

Ruby
Ruby

Hii sio mara ya kwanza Ruby kusingiziwa kuwa anatoka kimapenzi na msanii wa bongo. Hapo mbeleni ilisemekana kuwa alikuwa na uhusiano na Diamond Platnumz hata hivyo sio wengi walioamini.

Akizungumza na Bongo 5 Ruby alisema,

“Na mimi taarifa hizo nimekuwa nikiziona kama wewe ulivyoziona, sioni jipya kwasababu walishawahi kusema kuwa nipo karibu sana na Diamond, sasa wamegeukia kwa Kiba ambaye hata mawasiliano yake sijawahi kuwa nayo.”

Ni nini kinachoendelea kati ya Alikiba na Ruby?

Ubuyu mtaani ni kuwa Alikiba na Ruby kuwa wamekuwa watu wa karibu sana na kuzua maswali mitandaoni ya kijamii.

Habari hii imevuma mda mchache baada ya Alikiba alisemekana kuwa alimvisha pete ya uchumba mwandani wake aitwaye Amina kutoka nchini Kenya.

Ruby
Ruby

Hata hivyo baada ya kuonekana na Ruby sana wengi wanaamini kuwa wawili hao wanauwezekano wa kuwa wapenzi ikiwa hawafanyi wimbo mpya pamoja.

Ruby ambaye aliweza kuzungumzia jambo hili aliwasihi watu hataki kuulizwa kuhusu mahusiano yake…. Ruby alisema,

“Sorry, sitaki kuulizwa kuhusiana na hayo mambo, naomba niulizwe kuhusu kazi zangu tu!”

Alikiba naye hajazungumzia jambo hili kwa sasa hata hivyo kuna uwezakano kuwa yeye na Ruby wanapanga kuachia wimbo mpya hivi karibuni.