Diamond ,Vannessa,Alikiba kuwakilisha Tanzania tuzo za MEAMA

Wasanii Diamond, Vannessa pamoja na Alikiba wamechaguliwa kuwania  katika tuzo za Middle East Africa Music Award (MEAMA) ,tuzo hizo ambazo zinapangwa kufanyika tarhe 5 Oktoba mwaka hu zina lengo la kuibua vipaji na kuonyesha amasa kwa wasanii wa africa kwa ujumla.Akiongea katika uzinduzi wa tuzo hizo kwa awamu ya pili CEO  wa FAJ GLOBAL ENT.L.T.D ,MAJESTICAL ROYAL CLUB (MRC)  na pia ni mwenyekiti wa FAJ ONLINE-RADIO Mr. Fajuyi Adeniyi Oluwaseun amesema kwamba wanaahidi kuwa kwa mwaka huu tuzo izo zitakuwa zenye ubunifu zaidi na zina kuwa na lengo la kuibua vipaji vingi zaidi ili kuendelea kuipa sifa na kuitangaza Africa.

Tuzo hizo ambazo zimejumuisha  washiriki wengi  ambao wametoka nchi mbalimbali za Africa kama Kenya,Uganda, Nigeria, South Sudan,Tanzania, Egypt na zinginezo jana tarehe 13 Septemba imeelekezwa kuwa majina ya washiriki kutoka nchi zote yanapatikana katika website ya tuzo hizo hivyo mashabiki  waweze kuwapigia kura wasanii wao wanaowapenda ili waweze kujinyakulia tuzo izo.

Kwa upande wa Tanzania msanii wa kike Vannesa Mdee ndiye   msanii pekee wa kike kutoka nchini hapa aliyewekwa katika kategoria ya msanii bora wa kike wa mwaka huku akichuana na  Victoria Kimani,Yemi Arade na Seyi Shayi, kwa upande wa wanaume yupo alikiba  katika kategoria ya msanii bora wa kium wa mwaka,pamoja na Diamond Platinumz katika kategoria ya wimbo bora ya mwaka na wimbo wa Eneka .

Wasanii wengine wanaoshiriki kuwania tuzo izo kutaka nchi tofauti na Tanzania  ni pamoja na Davido,Wizkid,Mr.Eazi katika kategoria tofauti tofauti.

Mashabiki wanahamasishwa kupigia kura msanii anaependa kushinda katika tuzo izo,na jinsi ya kupiga kula ni kuingia moja kwa moja katika website ya tuzo izo (MEAMA) ambapo upigaji wa kula umeanza mara baada ya kutangazwa kwa washiriki huku mwisho wa kupiga kula ikiwa ni tarehe 30 septemba mwaka huu na tuzo kufanyika oktoba 5 nchi Egypt.Tunawatakia mema wasanii wote waliopo katika kategoria mbalimbali , muziki wa Africa unafika mbali kwa sasa.

King Kiba atisha baada ya kuweka rekodi mpya YouTube

Alikiba ama ukipenda King Kiba ameweka rekodi mpya Afrika Mashariki kama msanii ambaye video yake imepata kutazamwa na watu milioni masaa 38 baada ya kuiwachia.

Seduce me imeweka rekodi ya kipekee ambayo hata wakalik ama Diamond Platnumz na Vanessa Mdee bado hawajaweza kufikisha. Kupitia ukurasa wake wa instagram, King Kiba aliweka post akiwashukuru mashabiki wake kwa kufanikisha kuvunja rekodi hiyo. Aliandika;

“Ahsanteni sana kwa upendo, nisingebarikiwa zaidi na kupendelewa bila nyinyi, nyinyi ni wa maana sana kwangu na nafanya haya kwa ajili yenu”,

kampuni ya Rockstar ambayo inamsimamia Kiba pia iliandika ujumbe kusema kuwa wimbo huu umevunja rekodi ya kipekee na ni video zinazotrend Tanzania na Kenya.

“Historia ya kunjwa rekodi imewekwa, Mfalme Kiba na wimbo wake mpya wa ‘Seduce me‘ umekuwa wa kwanza na kipee kwa msanii wa Afrika Mashariki kufikia kutazamwa mara milioni 1 kwenye Vevo/YouTube ndani ya masaa 38 tu, ina ‘trend’namba 1 Tanzania na namba 1 Kenya kwa ‘weekend’ nzima, rekodi imevunjwa.”

Alikiba awachia video mpya – seduce me

King Kiba ameachia video ya wimbo wake mpya Seduce me hivi leo miezi kadhaa baada ya kukawia kimya.

Msanii huyo amewachia wimbo huo wakati kuna tetesi kadhaa za kuchambuliwa na Diamond Platnumz kwenye mix ya Fresh.

Wimbo huu umewaacha mashabiki wake kama wameridhika baada ya kusubiriwa kwa hamu. Wimbo huu umetengezwa chini ya kampuni ya Rockstar4000 Music Entertainment and Rockstar Television inayommiliki.

Itazame hapa

 

 

 

“Gombaneni, roganeni mpaka muuane” Huu ndio ujumbe Nay aliowaandikia Ommy Dimpoz, King Kiba na Diamond Platnumz

Rapa wa bongo Nay wa Mitego hatimaye ameingilia vita mpya ya Ommy Dimpoz, Diamond Platnumz na King Kiba kwa kutoa maoni yake.

Kupitia mtandao wa Instagram Nay alifunguka kwa kusema kuwa hakuna anayemuunga mkono lakini jambo linalomkasirisha ni kuwahusisha wazazi kwenye vita hivi vyao vya utoto. Aliandika kusema;

Gombaneni, roganeni mpaka muuane, napenda kusikia changamoto kwenye gemu, ila tusiwaingize wazazi wetu tafadhali, tukananeni matusi yote wenyewe kwa wenyewe ikibidi piganeni kabisa atakaye kufa tutazika na itakuwa historia kama Big na Pac.

Akaendelea kwa kuongeza kuwa;

“Ila kuwaingiza wazazi ni ujinga, sipo upande wowote si kwa Kiba, Dimpoz wala Diamond, endeleeni na vita yenu kama wanawake mmechukuliana mabwana, ila suala la wazazi mnavuka mipaka,”

Alikiba asheherekea siku ya kuzaliwa ya mwana wake na ujumbe huu

Alikiba hivi karibuni alisheherekea miaka 7 tangu mtoto wake wa kwanza kuzaliwa. Msanii huyu wa Bongo aliziweka picha kadhaa akimtakia Kiba junior miaka mingi duniani anapoendelea kukua.

Kama wasanii wenzake Alikiba alimwandika Prince Sameer ujumbe wa kuvutia huku akimtakia mwanae kila laheri kupitia mtandao wake wa Instagram. Kiba aliandika,

“Haya kibaba Miaka 7 sasa @kiba_junior mwenyezi mungu akupe umri mrefu wenye faida kwake na kwako InshALLAH

Tazama picha kutoka sherehe hiyo hapa;

 

Abdu Kiba akana tetesi za kumuiga Ali Kiba

Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa Alikiba hivi karibuni alifunguka kuelezea kilichotokea baada ya mtandao wake wa Instagram kuibiwa na mtu asiyejulikana.

Msanii huyu ambae amekawia bila kuachia nyimbo mpya alisema kuwa baada ya kurudisha Instagram yake alipata kuwa amewafollow watu ambao yeye hawajui na jambo hili likamfanya kuunfollow kila mtu kama anavyofanya Alikiba.

Alisema haya kukana tetesi zinazodai kuwa anamuiga ndugu yake mkubwa. Alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Nikizungumzia akauti nakumbuka mwezi mmoja nyuma nikiwa Marekani akaunti yangu walihack kwa hiyo nilikaa karibia wiki tatu siko kwenye mtandao wa instagram, nilipoweza kuirudisha akauti yangu ndipo nilipoamua nisimfollow mtu yeyote kwa sababu watu niliowakuta mule sio watu wangu.”

Aliendelea kwa kusema,

“Kwa hiyo niliwa-unfollow nikabakia siwezi kumfollow mtu tena. Sijafuta utaratibu wake bali ni maamuzi yangu, wategemee any day naweza nikamfollow mtu yeyote,”

Msanii wa Bongo AT asimulia ugomvi wa Diamond Platnumz na Alikiba ulipoanzia

Ni wengi bado wanajiuliza ni nini kilichotokea Kati ya Diamond Platnumz na Alikiba kuwafanya wawili hao kukosana.

AT ambaye ni maarufu Bongo alisimulia tukio la Kiba na Naseebu akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muimbaji huyo maarufu wa muziki wa mduara alisema;

“Tulikuwepo tupo Oman kwenye hotel moja inaitwa Dream tulikuwa tuna show, kwa hiyo walikuwa wanacheza game, Alikiba amechagua Real Madrid na Diamond Barcelona, mimi nimekaa pembeni naangali watu wanacheza game yao. Ali akawa amefungwa mbili, akawa anataka kupiga free kiki kwenye game Diamond akamsukuma akamwambia halafu mwanangu nakutafuta siku nyingi. Alikiba akanyanyuka ikabidi na mimi ninyanyuke sasa, nikamuuliza Ali tatizo nini mbona kama mnataka kupigana halafu tupo ugenini wazee vipi?  Akaniambia huyo dogo kuna vitu anavifanya mimi sijavipenda.”

Aliendelea kwa kusema,

“Mwisho wa siku naona kama vile vitu vinaendelea halafu watu wanakurupuka wala tatizo wao hawalijui. Ebu watafute ukweli ulipo, sijui huyo kamtoa kwenye wimbo huyo, kuna jambo lingine ambalo lipo. Kiukweli kuna vitu ambavyo pengine wao wenyewe wanavijua ni vikubwa zaidi,”

Baada ya Diamond Platnumz kuzindua perfume yake, King Kiba kuingiza bidhaa moto moto sokoni

Japo King Kiba amekuwa kimya kwa muda sasa msanii huyo amefunguka na kusema kuwa sasa hivi anajiandaa kuachia bidhaa kadhaa kutoka kwa AK na sasa King Kiba.

Ali Kiba

Kwa sasa muimbaji huyo wa Aje ameachia shati na kofia ambazo zimekuwa zikiuzwa Afrika Mashariki. Lakini kwa sasa anatarajia kuachia viatu, glasses na energy drink. Alisema haya kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“AK ni brand ya Alikiba nashukuru imekuwa kubwa watu wanavaa lakini pia ipo na ya King Kiba nayo ni brand yangu na zipo official kabisa na kazi zitakapoanza watapata product zote.”

Aliongeza kwa kusema kuwa anamalengo makubwa na ndio maana bidhaa zake zinachukua muda kuachiliwa sokoni.

“Kuna malengo makubwa sana tumeyaweka lakini siwezi kusema sasa hivi ila kuna jeans, viatu na glasses tayari zishatoka soon wataziona maana hizi zitakuwa za kwanza sababu tayari zishatoka na kuna energy drink”

Ni nini kinachoendelea kati ya Alikiba na Ruby?

Ubuyu mtaani ni kuwa Alikiba na Ruby kuwa wamekuwa watu wa karibu sana na kuzua maswali mitandaoni ya kijamii.

Habari hii imevuma mda mchache baada ya Alikiba alisemekana kuwa alimvisha pete ya uchumba mwandani wake aitwaye Amina kutoka nchini Kenya.

Ruby
Ruby

Hata hivyo baada ya kuonekana na Ruby sana wengi wanaamini kuwa wawili hao wanauwezekano wa kuwa wapenzi ikiwa hawafanyi wimbo mpya pamoja.

Ruby ambaye aliweza kuzungumzia jambo hili aliwasihi watu hataki kuulizwa kuhusu mahusiano yake…. Ruby alisema,

“Sorry, sitaki kuulizwa kuhusiana na hayo mambo, naomba niulizwe kuhusu kazi zangu tu!”

Alikiba naye hajazungumzia jambo hili kwa sasa hata hivyo kuna uwezakano kuwa yeye na Ruby wanapanga kuachia wimbo mpya hivi karibuni.

Huu ndio ujumbe Alikiba aliomwandikia binti yake kusheherekea siku yake ya kuzaliwa

Alikiba ameonekana kuwa baba aliyenafuraha baada ya binti yake kusheherekea siku yake ya kuzaliwa hivi juzi. Baba huyu ambaye amekuwa akiwaeka watoto wake kipaumbele hakusita kuzipost picha za mwanae huku akimuandika ujumbe wa kupendeza.

Ingawa ni star mkubwa Tanzania, Alikiba huwa anapenda kuwaeka watoto wake off social media na anapowapost yeye huwa akisheherekea siku zake za kuzaliwa.

Mwaka huu inaonekana akumfanyie binti yake birthday kubwa kama ya mwaka uliopita. Hata hivyo haimaniishi kuwa upendo wake kwake umepungua. Muimbaji huyu siku hizi anaonekana kuwa mtu anayeshughuli mingi na career yake ambayo inaonyesha matumaini ya kugrow.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, king Kiba aliandika kusema…

Happy Birthday My Princess ? nitakupenda siku zote ❤️ @Amiyakiba #SupportedByKiba #KingKiba

Binti ya Alikiba
Binti ya Alikiba