Saida Karoli: Watu wameanza kutumia ushirikina kunipiga vita

Saida Karoli amekiri wazi kuwa suala la ushirikiana lipo na kwake si jambo la ajabu. Muimbaji huyo amedai kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanatumia ushirikina kumpiga vita ili aweze kupotea tena kwenye muziki kama ilivyotokea kipindi cha nyuma.

Karoli alifunguka na kusema kuwa kuna mtu ambaye alilipwa pesa ili amuuwe kabisa, jambo ambalo lilimlazimisha yeye kuahirisha baadhi ya show zake.

“Huyo mtu alinielekeza watu kadhaa ambao wamepanga mpango wa kuniua aliniambia, sasa mimi nimeshalipwa nikuuwe nikuondoe duniani kabisa yaani kabla ya kufika Mwanza, Geita tena bora hata hizi show zingine uvunje, kweli ramani aliyonipa nilichoka ikabidi show zingine za Bukoba tumezivunja tukasema ngoja tutulie kwanza tuone nini kitaendelea” alisema Said Karoli

Saida Karoli anadai kurejea kwake kwa muziki kumewakera watu wengine ambao wanataka kumua. Staa huyo ambaye kwa sasa anawika kwa wimbo wake mpya ‘Orugambo’ ata hivyo alisisitiza kuwa yeye anamtegemea Mungu tu.

 

Saida Karoli ampa staa wa Tottenham – Victor Wanyama zawadi kusherekea siku ya kuzaliwa kwake

Victor Wanyama alizuru Tanzania kwasababu ya mapumziko, kiungo huyo wa Tottenham Hotspur pia alihudhuria shindano la kandanda akiwa nchini humu.

Serikali ya wilaya ya Ubungo ilimpa heshima Victor Wanyama kwa kuipa moja ya barabara za Ubongo jina la nyota huyo ambaye alikuwa mgeni wa heshima kwenye mchezo wa Ndondo Cup 2017 kati ya FC Kauzu dhidi ya Faru Jeuri.

Hata hivyo serikali hio ilibadilisha hatua ya kuipa moja ya barabara jina la Wanyama wakidai kuwa utaratibu haukuzingatiwa.

Hata kama serikali ya wilaya ya Ubungo ilifuta jina la Wanyama kwa barabara, staa huyo wa Tottenham alipata zawadi nzuri kutoka wa Saida Karoli.

Wawili hao (Wanyama na Karoli) walikutana kwenye studio za Clouds FM na Wanyama alimjulisha Karoli kuwa yeye ni shabiki wake mkuu.

Na kwa bahati nzuri siku waliokuta ilikua birthday ya Wanyama ambaye alikua anatimia umri wa 26; Karoli alimpa Wanyama CDs zake kama zawadi.

“Thank you @saidakarolitz for the CDs,I’m humbled,” Wanyama aliandika.

 

Saida Karoli aeleza kilichompa nguvu mpya ya kurudi kwenye muziki baada ya kustaafu

Mwimbaji mkongwe Saida Karoli anayejulikana kwa hit yake ‘Maria ya Salome’ amerejea kwenye sanaa ya muziki baada ya kupotea kwa miaka kadhaa.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa iliopita, Saida Karoli alisema kuwa kurejea kwake kwenye muziki ulifanikishwa na Diamond na Belle 9.

Anadai kuwa Belle 9 na Diamond walimpa nguvu mpya ya kurudi kwenye muziki baada ya kuachia nyimbo zao walizotumia baadhi ya vitu kutoka kwenye wimbo wake wa ‘Maria ya Salome’.

“Nilishatamani kuacha muziki na nilishawahi kuhamisha baadhi ya vitu vyangu kurudi kijijini na ndiyo kipindi hiko hiko Belle Nine na Diamond walitoa nyimbo ya Chambua kama karanga, wakanirudisha maana ilikuwa safari kabisa,” Saida Karoli alisema.

Diamond and Saida Karoli