Diamond, Victor Wanyama wamtakia AY heri ya siku ya kuzaliwa

Rapa Ambwene Allen Yessayah maarufu kama AY anasherekea siku ya kuzaliwa kwake leo Julai 2017. AY amefikisha miaka 36 leo.

Mastaa wengi wamemtakia AY heri ya siku ya kuzaliwa kwake, rafiki wake wa karibu Victor Wanyama alikua miongoni mwa wale waliomtumia jumbe mapema.

AY na Victor Wanyama

“Happy bday big boss @aytanzania have a good one bro,” Victor Wanyama aliandika.

Diamond na Rayvanny pia walimtumia AY jumbe:

“Big Birthday wish to Msoja wange @jahprayzah and my Legend Brother @aytanzania …. Long Life!!” Diamond Platnumz

“HAPPY BIRTHDAY KAKA LAO @aytanzania Mungu Akupe maisha marefu yenye Mafanikio zaidi,” Rayvanny

 

Saida Karoli ampa staa wa Tottenham – Victor Wanyama zawadi kusherekea siku ya kuzaliwa kwake

Victor Wanyama alizuru Tanzania kwasababu ya mapumziko, kiungo huyo wa Tottenham Hotspur pia alihudhuria shindano la kandanda akiwa nchini humu.

Serikali ya wilaya ya Ubungo ilimpa heshima Victor Wanyama kwa kuipa moja ya barabara za Ubongo jina la nyota huyo ambaye alikuwa mgeni wa heshima kwenye mchezo wa Ndondo Cup 2017 kati ya FC Kauzu dhidi ya Faru Jeuri.

Hata hivyo serikali hio ilibadilisha hatua ya kuipa moja ya barabara jina la Wanyama wakidai kuwa utaratibu haukuzingatiwa.

Hata kama serikali ya wilaya ya Ubungo ilifuta jina la Wanyama kwa barabara, staa huyo wa Tottenham alipata zawadi nzuri kutoka wa Saida Karoli.

Wawili hao (Wanyama na Karoli) walikutana kwenye studio za Clouds FM na Wanyama alimjulisha Karoli kuwa yeye ni shabiki wake mkuu.

Na kwa bahati nzuri siku waliokuta ilikua birthday ya Wanyama ambaye alikua anatimia umri wa 26; Karoli alimpa Wanyama CDs zake kama zawadi.

“Thank you @saidakarolitz for the CDs,I’m humbled,” Wanyama aliandika.

 

Staa wa Tottenham Hotspur Victor Wanyama na mwenzake wa Everton – Morgan Schneiderlin waingia Tanzania (Picha)

Tanzania inazidii tu kupokea wageni mashuhuru kutoka kote ulimwenguni. Ni jana tu ndo tuliskia kuwa kiungo wa Tottenham Hotspur Christian Eriksen yuko nchini kuzuru mbuga ya wanyama la Serengeti.

Soma pia: Kiungo wa Tottenham Hotspur Christian Eriksen aingia Tanzania baada ya David Beckham kuondoka (Picha)

Sasa mwenzake kutoka Tottenham Hotspur pia amejiunga na yeye nchini, nahodha wa Harambee Stars ya Kenya na kiungo wa Tottenham Hotspur – Victor Wanyama pia ameingia Tanzania.

“Tumepokea ugeni wa superstars wa Kenya @VictorWanyama @alawiabdul pamoja na Marafiki zao. Tunawatakia Mapumziko mema. Karibuni Tanzania,” Tanzania Tourism ulitangaza kwa Twitter.

Mshambulizi wa kitambo ya Manchester United ambaye alijiunga na Everton – Morgan Schneiderlin pia yuko Tanzania kwa honeymoon yake. Staa huyo alioa mpenzi wake karibu wiki moja hivi.

Morgan Schneiderlin  na bibiake Camille Sold waliweka picha zao kwa Instagram wakiwa wakijivinjari katika mbuga ya wanayama Tanzania.