Sanchoka Aamua Kufanya Mabadiliko ya Mavazi.

.Mwanadada anaesifika kwa maumbo makubwa na kutupia picha za uchi katika mitandao maarufu kama Sanchoka amefunguka na kusema kuwa kwa sasa anaanza kufanya mabadiliko ya kuvaa nguo fupi na kuanza kuvaa ndefu kwa sababu ameona kuwa hata hizo ndefu pia zinampendeza na zinamtoa poa.

Sanchoka nasema kuwa tangu mwaka huu umeanza ameamua kufanya mabadiliko ya mavazi na kuvaa nguo ndefu kwa sababu anaona kabisa nguo ndefu pia zinamtoa poa na kuonekana maridadi zaidi.

unajua kila kitu ni mpaka ujaribu kukifanya ndo utajua.lakini kwa upande wa nguo nimeamini kuwa hata nguo ndefu pia zinanitoa poa tu na zinznipendeza tu hata nikienda kwenye hafla mbalimbali  navaa naonekana msichana wa nguvu mwenye heshima zake.

Sanchoka ni moja kati ya wanamitindo wa kike waliowahi kutajwa katika orodha ya wasichana wanaovhapisha picha katika mitandoa ya kijamii wakiwa uchi na kuvunja maadili yakitanzania kwa kufanya hivyo.wasanii wengine ni kama gigy money na susan michael.

Sanchoka aamua kubadilika sasa na kuanza kuvaa nguo za heshima na kuficha maungo yake na anaamini kuwa pia watu waliozoea kumuona nusu uchi wataanza pia kumzoe na nguo ndefu.

 

 

Mrembo Sanchoka Aweka Hisia Zake Juu Ya Dr. Shika Hadharani

Mrembo anayetingisha mitandao ya Kijamii kama Instagram kwa umbo lake matata Sanchoka au maarufu kama Sancho World amefunguka nakudai kuwa yuko tayari kuolewa na Dr. Shika ‘900 Itapendeza’.

Dr. Shika alipata umaarufu wiki chache zilizopita baada ya kwenda kwenye mnada wa nyumba za Lugumi na kuhaidi kuzinunua kwa mabilioni ya pesa lakini mara baada ya mnada kuisha Dr. Shika alishindwa kuzilipia na hivyo kuishia kupelekwa polisi. Baada ya kuachiwa huru Dr. Shika aliishia kupata umaarufu baada yakupata attention kubwa kutoka kwa waandishi wa habari iliyopelekea kupata nafasi mbalimbali za kushiriki kwenye matangazo ya kampuni nyingi ambayo yanamuingizia pesa nyingi.

Mrembo Sanchoka amejizolea umaarufu baada ya kuzoea kuweka picha za utupu ambaxo zinaonekana kuwavutia hasa wanaume kutokana na umbo lake la kuvutia.

Sanchi amemtolea macho Dr. Shika amefunguka na kudai kuwa anautamani sana umaarufu waDr. Shika kwasababu hajatumia ngumu kubwa. Sambamba na hilo Sanchi amesema kama Dr. Shika mzee wa 900 Itapendeza Kama atanunua kweli nyumba za Lugumi basi atakubali hata kufunga naye ndoa kwani Dr. Shia naye ni mwanaume, Sanchi ameyafunguka hayo baada ya kuulizwa kama yuko tayari kuolewa na Dr. Shika.

Sanchi aliweka wazi tangu mwanzoni kuwa anataka kuolewa na mwanaume mwenye hela kwani bila mahari ya miliobi kumi basi hataolewa.

 

 

Sanchoka: Makampuni Ya Kutengeneza Filamu za Ngono Yananiwinda Sana

Mrembo Jane Rimoy maarufu kama Sanchoka au Sanchiworld anayetikisa Bongo kwa sasa kutokana na umbo lake na picha zake za utupu anazopiga amefunguka na kueleza changamoto anazopata kutoka na umbo lake hilo na umaarufu alionao.

Kwenye mahojiano yake na Global Tv, Sanchoka amefunguka na kudai kuwa watu wengi wakimuona anapiga picha zake za mitego wanahisi kuwa labda anajiuza kitu ambacho si cha kweli bali anapiga vile kwa kazi zake za u-model anaofanya mara nyingi nchi kama Ghana, South Africa, Kenya na Nigeria, pia amedai watu makampuni mengine ya filamu za ngono yamefikia hatua ya kumtafuta ili akacheze filamu zao:

Unajua kama mwanamke kuna mambo mengi unaweza ukafanya tofauti na kujiuza na bado ukapata hela coz ni jinsi tu ya kucheza na akili za watu na ujue watu wanataka nini sio kwamba mtu akivaa nusu uchi akapiga picha basi anajiuza hiyo ni akili ya watu wengi wa Afrika yaani wanaona mtu kama mimi napiga picha vile nimevaa nguo za ndani tuna kuonyesha viungo vya mwili wangu basi wanajua nataka kujiuza lakini huko tunakoelekea naomba niamini tutaamini kwa sababu mwisho wa siku hao mnaosema wanajiuza ndo watakuja kufanikiwa na kufanya vitu vikubwa mshangae”.

Pia Sanchoka alielezea usumbufu anaopata kutoka kwenye makampuni ya kutengeneza filamu za ngono:

Makampuni mengi ya kutengeneza movie za ngono ya nje ya Tanzania hadi Marekani wengi tu wameshanitafuta wananiambia nitaje pesa ninayoitaka nifanye nao kazi lakini mimi sio mtu wa aina hiyo ndo maan nasikitishwa na uzushi wa watu wanaodai mimi najiuza kwa milioni moja ni kitu ambacho siwezi kabisa kwani hiyo ni pesa ndogo na isitoshe sijawahi hata kufikiria kujiuza kwa hela yoyote duniani kwani hayo sio malengo yangu wala wakati napiga hizo picha sijawahi kuwaza kutafuta wanaume”.

Sanchi aliweka wazi mwanaume anayeweza kutembea naye ni yule anayejishughulisha, anayejituma na siyo lazima awe na kipato kikubwa sana lakini awe anajitahidi awe ana malengo ya kufika mbali zaidi.