Diamond Platnumz aeleza sababu hataki Tiffah awemsanii kama yeye

Wasanii wengi duniani hawapendi kuwaonyesha Watoto wao mitandaoni na ukiwaukiza, hii ni kwa sababu wanahofia watoto wao kuishi maisha kama wanayoishi.

Mmoja wao ni Diamond Platnumz ambaye anahofia mwanawe, Tiffah Dangote kuwa msanii. Akizungumza kwenye mahojiano na Larry Madowo wa NTV Kenya Diamond alisema kuwa Tiffah akiwa msanii atatembea na wanaume wengi kitu ambacho yeye mwenyewe hataki kukiona ama kusikia. Alisema,

“Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii, watamla sana. Mtoto akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu wanaokujua wakiwa wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha. Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi kama yangu lazima wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata Zari na kweli nimetulia,”

Tazama interview hiyo hapa:

Huu ndio ujumbe Diamond Platnumz aliowaandikia watoto wake

Diamond Platnumz hivi karibuni aliwaandikia watoto wake ujumbe kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuwatania kwani wanamidomo ambayo inafanana na yake.

Hii sio mara ya kwanza kusikia muimbaji huyu akikiri kuwa wanae wanamfanana hasaa kwenye area ya mdomo. Na Kwa mara ya kwanza aliwaandikia ujumbe kuwasihi watumie midomo yao vizuri, kama alivyofanya yeye. Aliandika kusema,

Prince & Princess Lion!!!.. Midomo mkaitumie vizuri hiyo watoto….

Diamond aliambatanisha ujumbe huu na picha ya wawili hao kuonyesha wanavyofanana kisura. Kulingana na comments zilizoandikwa na mashabiki, wengi wao walipata wakati mgumu kuwatofautisha.

Hata hivyo ni kweli kuwa genes za Diamond na Zari zinatoa watoto warembo na picha hii aliyoipost inaonyesha kuwa ni ukweli.

Tiffah na Nillan
Tiffah na Nillan