Tunda- Nipo Tayari Kuwa Mke Wa Mtu

Muuza nyago maarufu mtandaoni Tunda Sebastian maarufu kama ‘Tunda the Bossbabe’ amefunguka na kudai kuwa hivi sasa ametulia na yupo tayari kuwa mke wa mtu.

Siku za hivi karibuni Tunda ameonekana kubadilika sana kwani kwa mara ya kwanza alipata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kwa vituko vyake vya kuvaa nguo za utupu na kula bata ndefu ambapo watu walikuwa wanamweka kwenye kundi moja na warembo kama Gigy Money.

Pamoja na hayo ni mara kwa mara kumekuwa na tetesi kuwa Tunda ni mjamzito ingawa mwenyewe amekuwa akikataa mwaka jana mwishoni habari zilienea kuwa Tunda ana ujauzito wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz ingawa mwenyewe alikataa tuhuma hizo na kudai kuwa watu wengi walidhani kuwa ni mjamzito kwa sababu alinenepa na kuwa na kitambi lakini sababu pekee iliyopelekea yeye kunenepa ni kula sana na si kingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Star Mix hivi karibuni Tunda amefunguka kuwa anapendezwa na muonekano alionao hivi sasa kwani angalau anaonekana mtu mzima kiasi ya lwamba mtu akimuona anaweza jua ni make wa kuia na kuweka ndani.

Nafurahia sana muonekano wangu wa sasa hivi nilivyo na kwa sasa nipo tayari kuitwa mke wa Mtu maana hata nikiwekwa ndani kama mke nafaa kabisa nilikuwa nakereka watu kunifananisha na katoto kadogo”.

 

Tunda Amefunguka Kuhusu Skendo Ya Kutoa Mimba na Uhusiano Wake na Diamond

Video queen maarufu Bongo, Tunda a.k.a the Bossbabe amefunguka kuhusu skendo inayomuandama kwa muda mrefu ya kutoa mimba mara kwa mara na hata kubeba ujauzito wa mwanamuziki Diamond Platnumz.

Tunda amezungumza kuhusu yale maneno yaliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa wiki kadhaa sasa ambapo amedaiwa pia kutoka kimapenzi na mwanamuziki Diamond baada ya kuposti picha zake mara kwa mara na kuweka picha yake kama profile picha.

Tunda amefunguka kuhusiana na skendo hizo zinazomkabili kwa sasa kwenye mahojiano aliyoyafanya na Millard Ayo Tv ambapo amesisitiza kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na Diamond kama watu wengi wanwvyozusha bali ni rafiki wa karibu na kaka yake;

Hizi stori za mimi kuwa mjamzito siyo za kweli kabisa sijawahi kubeba maishani mwangu bali nimeongeza tu nikawa tofauti, na kwa maana hivyo sijatoa mimba wala sijawahi kutoa mimba maishani mwangu mwote. Kuhusu kuweka picha za Diamond mtandaoni ni kuwa mimi namkubali sana Diamond ni kama kaka yangu nampenda. Nakubali kazi zake ni mtu wangu wa karibu kwa kweli sisi ni marafiki”.

Lakini pia Tunda amesisitiza kuwa ana mpenzi wake tayari ambaye sio staa wala msanii kwaiyo watu wengi hawamfahamu  lakini amesema siku akiwa tayari kumuweka wazi basi watu watamuona, pia Tunda amewaomba watu wasim-judge kwa kumuangalia kwenye mitandao ya kijamii kwani kila kitu sio serious kiasi hicho.

Tunda Aomba Msamaha Kwa Petitman

Tunda na Petiti Man walikuwa katika bifu zito baada ya Tunda kumwita Petit kuwa chawa wa Wcb, lakini bifu hilo halikuishia hapo liliendelea na kufikia hatua ya watu hao kutukanana katika mitandao ya kijamii na  baade kuna baadhi ya  ya sms zilivuja zikionyesha wawili hao kuwa wamekuwa wakitukanana hata katika magroup ya whatsap na katika simu zao.Hata hivyo mwanadada huyo aliamua kukubali yaishe na kuamua kujishusha kwa kuomba msamaha kwa Petitman

Hata hivyo akiongea na Clouds E ya Clouds Tv, mwanadada Tunda amesema kuwa yeye ameamua kuomba msamaha na bora aishe kwa sababu yeye ni muoga sana wa kuwa na bifu na watu na anaogopa sana kupigwa hivyo aliona bora yaishe kuliko kuanza kuangalia ni nani kamkosea nani.

Niliamua kuona bora yaishe kwa sababu sitaki kuwa na bifu na watu, mimi sitaki kujua  nani kamuanza mwenzake lakini bora tu bifu liishe kwa sababu mimi ni muoga sana wa mabifu alafu naogoapa sana kupigwa kwaiyo sitaki tu. -Alisema Tunda

Hata hivyo aliulizwa kwanini waligombana mpaka kufikia hatua ya kuyaanika katika mtandao Tunda anasema kuwa bifu hilo halikuanzia instagram lakini lilianzia private katika simu zao na baadae watu walikuja kuvujisha katika mitandao ya kijamii, bila hata  kujua nini chanzo.

Akiendelea kuongezea , mwanadada huyo anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakimjudge kutokana na maisha yake anayoishi  na kuyaweka katika ukurasa wake wa instagram lakini ukweli ni kwamba hayo sio maisha yake kuna muda huweza kujisikia akaposti   kitu chochote lakini sio kwamba ndivyo anavyoishi kila wakati.

Alipoendelea kuulizwa kuhusu tabia yake ya kuonekana katika viwanja na kula bata mwandada huyo anasema kuwa watu wamekuwa wakimsema kuwa anafanya starehe sana na hata wengine kumuiga maisha anayoishi yeye bila kujua yeye ela anatoa wapi, ni bora kila mtu akaamua kuishi maisha yake na sio kuanza kuiga maisha anayoishi yeye kwa sabau kwake yeye starehe ni kitu cha kawaida kutokana na ela anayoingiza ingawa kuna muda huwa anakaa nyumbani tu na kupika na kula lakini akiamua kutoka na kuspend kwa chakula huwezi kufika hata milioni moja na nusu.

Huwa nakaa nyumbani najifungia na kupika na kula lakini nikiamua huwa naweza kutumia hata milioni moja na nusu kwa ajili yaku-spendi kwa siku.-Alifunguka Tunda

Tunda Akumbwa Na Skendo Ya Mimba Kwa Mara Ya Pili

Sio mara ya kwanza kwa muuza nyango maarufu katika video mbalimbali kuambiwa kuwa anamimba,Tunda ambae miezi kadha iliyopita alisemekana kuwa na mimba lakini baadae ilisemekana kuwa ametoa mimba hiyo bila kuweka wazi ni nani alikuwa muhusika wa mimba hiyo.

Hata hivyo mwanadada huyo alisema kuwa hakuna na mimba ya mtu yoyote na kitendo chake cha kuwa na mwili mkubwa ni kunenepa kwa sababu amekuwa akila sana vyakula lakini alisema anaanza kufanya diet ili kupunguza mwili huo, na kusema kuwa alikuwa hajui swala lolote kuhusu mimba watu wamekuwa wakimsingizia.

Hivi karibuni tena , mwanadada huyo ameonekana akiendelea kupasuka kutokana na badahi ya sehemu za mwili wake kuendelea kuongezea kama tumbo pamoja na maziwa ambapo waatalamu wa mambo wanasema kuwa mwanadada huyo kwa sasa ana mimba na hawezi kupindua hilo.lakini kitu cha kushangaza ni kwamba mwanadada huyo amekataa na kusema kuwa hana mimba.

Lakini pia mwanadada huyo amekataa kuzushiwa kuwa mimba aliyonayo ni ya msanii wa bongo fleva  ambae alikuwa mpenzi wake wa muda mrefu kwa kipindi cha nyuma, na kusema kuwa kitendo cha yeye kumuweka katika ukurasa wake wa instagram mara nyingi ni kwa sababu anamsapoti msanii huyo kama rafiki yake na sio vinginevyo kama watu wamekuwa wakimzushia.

Ndio kwanza nasikia kwenu mimi wala sina mimba, na wala hizo taarifa sio za kweli kabisa.Huwa namuweka insta ili kusapoti kazi zake tu maana ni rafiki yangu sana sana lakini cha ajabu watu walivyoona hivyo tu ndo wakaanza kuzusha  kwamba ninatoka nae na nina mimba yake , swala la kuhusu kunenepa ni kweli nimenenepa sana kwa sababu nimeridhika na maisha ninayoishi tu.

Hata hivyo Tunda amekuwa kila siku akikana swala la yeye kuwa na ujauzito huku wataalamu wa mambo wakisem akuwa mtu mjamzito akionekana anaweza kujulikana kutokana na vile anavyokuwa.Kama ni kweli mjamzito tunamtakia afya bora yeye na kiumbe kilichopo tumbano na kama ni uzushi basi kila la kheri kwake.Maana wahenga wanasema lisemwalo lipo kama halipo linakuja.

Tunda Anapenda Sana Kufatilia Maisha Yangu Binafsi: Petit Man

Petit Man Wakuache ambaye ni mume wa dada wa Diamond, Esma Platnumz amefunguka kuhusu skendo iliyomwandama wiki chache zilizopita pale alipomtolea matusi ya nguoni mrembo Tunda.

Petit Man alipata umaarufu kwa mara ya kwanza alipokuwa na ukaribu na mrembo Wema Sepetu. Baada ya kumuoa Esma na kuwa shemeji wa Diamond ndipo pale umaarufu ulipozidi. Lakini muda wote Petit aliweka ukaribu wake zaidi na Wema kuliko na familia ya Esma, lakini hata baada ya kupatana na Wema siku za hivi karibuni Petit ameonekana kuweka ukaribu zaidi na familia ya Diamond.

Tunda ambaye amekuwa na urafiki wa siku nyingi na Petit Man alirushiwa matusi hayo na Petit baada ya kumuita Petit chawa wa Diamond baada ya Petit kusafiri na timu nzima ya Diamond kuelekea Zanzibar kwaajili ya shoo ya Diamond. Kitendo kile cha kuitwa chawa na Tunda kilimuumiza Petit na kumtukana Tunda.

Alipohojiwa na clouds tv Petit alifunguka yafuatayo kuhusiana na Tunda:

Yaani yule msichana Tunda anapenda sana kuingilia vitu vyangu binafsi yaani anachimba vitu vyangu vya ndani sana anapenda kuviingilia na kuviongelea sasa sielewi kwa nini anapenda kunizungumzia wakati mimi simzungumzii hata siku moja kwaiyo kitu kama hicho kinatokea kea binadamu yoyote unaposikia unazungumziwa kitu kibaya kupaniki kitu cha kawaida sana”.

Pia Petit alifunguka kuwa kwa sasa anasimamia wasanii wawili ambao ni Country Boy na Bill Nass ambao wanategemea kutoa kazi zao mpya hivi karibuni.

Tunda Amwita Petit Man Chawa Wa Wasafi

Mwanadada asiechuja ambae amekuwa akifanya vizuri mpaka sasa kutokana na kuuza sura katika video za wasanii mbalimbali ikiwemo video ya Diamond Platinumz  ‘Salome’, amemwita Petit Man mume halali wa Esma Platinumz kuwa ni chawa kutokana na kufatana fatana na Diamond na kundi la wasafi kila sehemu, ,Petit Man ni moja kati ya wanafamilia ya wasafi kwa sababu ni mume wa dada yake na Diamond anaejulikana kama Esma Platinumz.

Katika moja ya post katika kurasa za Dizzimonline, katika ukurasa wa instagram ambapo ilipostiwa picha ikimuonyesha Petit Man akiwa na mke wake Esma na Aunty Ezekiel akiwepo, Tunda alicoment na kumuita Petit Man kuwa ni chawa wa wasafi.

“Petiiman hatimaye amekuwa chawa wa WCB, kweli maisha yanabadilika” aliacha comment iyo katika picha, hata hivyo Petit Man na Tunda walikuwa wakionekana pamoja na hata kufanya kazi  pamoja lakini kinachshangaza mashabiki kuwa ni kwanini Tunda aandike ujumbe kama huo tena wazi katika post ambao watu wengi wangeiona au alijua kabisa kuwa lazima ujumbe utafika.

Hata hivyo , picha iyo ni moja ya picha zinazoonyesha matukio  na watu waliokuwa wameudhuria katika show mojawapo alioifanya Damond Platinumz  na Rayvanny katika uwanja wa Amani huko Zanzibar , Petit Man akiwa kama shemeji na mtu wa karibu wa familia ya Diamond alikuwepo kwa ajili ya kusapoti show hiyo.

Hata hivyo show iyo ilihudhuriwa na watu na wasanii wengi maarufu ikiwemo Aunty Ezekiel kutoka bongo movie, Zari The Bossy ambae baada ya kumaliza uzundizi wa  duka jipya Mlimani City mali ya Gsm waliondoka na kuelekea Zanzibar.

Hii sio mara ya kwanza kwa Petit Man na mkewe kutokea katika events na party za familai ya Diamond, na akiwa kama mwanafamilia na mtu anaesapoti sana muziki wa Tanzania basi anapotokea katika shughuli kama izo anakuwa pia na umuhimu wake kwa mkewe na kwa wasanii pia kwa sababu petit man alishawahi kuwa meneja wa wasanii mbalimbali wa bongo fleva na bado anaendelea kusapoti baadhi ya wasanii.

Tunda akiwa pamoja na Petit Man

Tunda akanusha tetesi za kutoa ujauzito

Yule mwanadada anaetikisa jijini Dar Es Salaam  hasa katika upande yeye  wa kuwa moja kati ya  video vixen bora na amekuwa  akionekana katika video nyingi za mastaa wakubwa nchi , Tunda Sebasita anafahamika kwa jina la umaarufu kama Tunda  leo amefunguka na kukanusha stori zilikuwa zikisambaa katika mitandao kuwa alikuwa mjamzito kipindi cha nyuma  na sasa ameitoa mimba iyo, hata hivyo kuenea kwa tetesi izo kunasababishwa na mrembo huyo  (Tunda) ambae amekuwa akipost picha huku akionyesha sehemu za  tumbo lake ambapo watu walianza kujudge na kusema  kubwa  mrembo huyo atakuwa ni mjamzito, lakini bado hata muda ulipopita bila kuona maendeleo yoyote  basi tetesi zilibadilika na kusemekana kuwa  ametoa mimba iyo.

Hata hivyo Tunda amekanusha tuhuma hizo zinazoendelea katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa kwa upande wake taarifa hizo ni ngeni, na wala hakuwa na mimba na katika maisha yake hajawahi kupata mimba kabisa.

Akizungumza na waandishi wa habari wa kituo cha EATV, Tunda anasema kuwa sababu za yeye kuwa na  tumbo ni kitambi tu kilichokuwa kinakuwa sababu ya yeye kunenenpa maana yaye ana asili ya tumbo ila kwa sasa anafanya diet na ndio maana watu wanaona tumbo linaisha.

“Sina mimba na sijawahi kupata ujauzito hilo tumbo limeongezeka tu nina asili ya tumbo nikinenepa na tumbo linaongezela hizo tetesi za kutoa mimba ndo nazisikia kwako sijawahi kupata wala kutoa mimba kabisa.”

Tunda ni moja ya video vixen maarufu hapa nchi na amekuwa akitokea katika video za wasanii wakubwa maarufu nchi.baaadhi  ya video zake ambazo ameshawahi kutokea ni pamoja na “Salome”  ya Diamond Platinumz, pamoja  na “Furaha” wa Young Dee

Tunda ni mmoja kati ya video queen mwenye drama nyingi sana za kwenye mitandao kutokana na picha anazoposti katika ukurasa wake wa instagram, na katika historia yake mrembo huyo alishawahi kutoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva Young Dee  mwenye kibao kipya cha “Utani utani”