Ni kweli Video vixen Tunda anamtarajia mtoto wake wa kwanza?

Ingawa tetesi zinazosambaa mitandaoni Ni kweli, basi Tunda anamtarajia mtoto na alikuwa mpenzi wake wa zamani, Young Dee.

Hapo awali mrembo huyu alikuwa amekanusha taarifa kuwa alikuwa mjamzito. Hata hivyo hivi karibuni aliweka picha ya Utrasound akionyesha mtoto mdogo anayeendelea kuwa kumaanisha kuwa anatarajia kupata mtoto.

Hata hivyo, hakuandika ujumbe unaodhibitosha kuwa anamtarajia mtoto lakini mashabiki wake waliacha ujumbe wa kumpa pombe mrembo huyu pamoja na Younge Dee.

Tazama picha hiyo hapa;

Tunda aeleza sababu ambazo wasanii wengi hawatoi nyimbo baada ya kufunga ndoa

Tunda ambaye ni msanii mkubwa kutoka Bongo amefunguka kuelezea sababu ambazo wasanii wengi hukawia bila kuachia muziki baada ya kuoa.

Msanii huyo aliambia Bongo 5 kuwa wasanii wengi hukawia ndio warejelee na nyimbo ambazo wake zao na jamii wanaweza kusikiza. Aliendelea kwa kusema kuwa kuna wasanii Kama Mr Blue ambao wameweza kuachia nyimbo zinazofanya vizuri hata baada ya kupata bibi.

Alisema,

“Msanii akioa eti anapotea kwenye muziki hizo ni dhana potofu, kuna wasanii wengi wameoa na bado wanafanya vizuri, wapo akina Mr Blue wanafanya vizuri. Mimi najua msanii anaweza kupotea kama anatoa nyimbo za kumuimbia mke wake, mke wako unatakiwa kumuimbia ndani mwako, na jamii inataka muziki wao,”

Tunda aeleza kwanini hatoweka mambo ya mapenzi yake kwenye mitandaoni kama zamani

Mrembo Tunda ambaye anajulikana kutokea kwenye video za wasanii wakubwa wa bongo amefunga kusema kuwa kwa hivi sasa hatamani mapenzi ya mitandaoni. Hapo mbeleni alikuwa akitoka kimapenzi na Young D lakini baada ya mambo kadhaa wawili hawa waliachana na kila mmoja kwenda njia yake.

Tunda
Tunda

Akizungumza na Uwazi Showbiz hivi karibuni mrembo huyu alisema kuwa uhusiano wake na Young D ulikuwa sana mitandaoni kitu ambacho hakuwa anajua inaweza kuleta utata.

Hata hivyo kulingana na yeye, hatorudi kufanya hivi tena kwa sababu amejua kuwa sio marafiki wake wote wanamtakia mazuri na badala ya kumueka mpenzi wake mitandaoni anaonelea kukaa kimya. Alisema,

“Kiukweli nimejifunza juu ya kuwa muwazi katika suala zima la mapenzi kuwa kuna watu wengine hawapendi kuona mnakuwa na furaha.Hawa huweza kupenyeza maneno ya kuwagombanisha ilimradi tu muweze kuachana, sasa mimi nimeamua katika uhusiano wangu wa sasa kutokuwa muwazi, mtu anayefahamu juu ya ninatoka na nani kwa sasa lazima atakuwa amefanya kazi ya ziada.”