Vanessa Mdee aonya msanii mkongwe anayemsemea maneno machafu

Vanessa Mdee anadai kuwa kuna msanii mkongwe anamchafulia jina lake kwa kumtaja katika kashfa kadha zisizoeleweka.

Vee Money hata hivyo hakuweka wazi jina lake mwanamuziki huyo mkongwe ambaye anadai  anamsemea maneno machafu.

“Inasikitisha kwamba mtu ninayemheshimu na kumtambua kwenye hii sanaa kila kukicha jina langu mdomoni mwake kwa kashfa zisizoeleweka,” Vanessa Mdee aliandika kwenya mtandao wa Twitter.

Mrembo huyo alitoa onyo kwa kusema kwamba hawezi jibishana na msanii huyo mkongwe kwasababu anampa heshima zake.

“Siwezi kujibishana na wewe itakuwa utovu wa nidhamu baba.,” Vanessa aliongezea.

 

Picha tano za Vanessa Mdee akivaa nguo ya nusu utupu akiwa Nigeria

Vee Money ameachia picha mpya ambazo zimezua utata kwenye mitendao za kijamii. Mwibaji huyo wa Bongo flava ambaye anafanya poa katika anga za kimataifa, yuko nchini Nigeria kwa sasa.

Mdee, aliyekua na show nchini humo siku ya Pasaka, alionekana akivaa mavazi hayo ambayo hayakubaliki kwa jamii.

 

Baadaye Mdee alionekana kwa beach na maceleb wawili wa kiume kutoka Marekani. Vee Money alikua amevaa nguo za nusu utupu  alipokua akijivinjari na Diplo.

Madai yachipuka mitandaoni ya kwamba Vanessa Mdee anamcheza Jux na mume wa watu

Leo, 11th April 2017 show ya Soudy Brown You Heard likuwa imeshika moto na ni kutokea madai ya kwamba Vanessa Mdee anatembea na mume wa wenyewe.

Jambo hili lilitokea wiki iliyopita wakati ujumbe recording fulani ya mwanadada anayeitwa Nicole ilianza kuenea mitandaoni akilalamika ya kwamba Vanessa Mdee ana uhusiano wa kimapenzi na mume wake na anamzuia kwenda kumuona mtoto wake aliyezaliwa hivi karibuni.

Basi leo Soudy Brown alimpigia Nicole na hivi ndivo alivyosema:

“Hiyo sauti siyo yangu, ila nilisikia story tu japo mimi najua ni watu wa karibu sana. So, siwezi kusema anatoka naye maana sijawakamata. Mimi najua wako karibu ni marafiki japo nilimuuliza akaniambia ni dada yake, na, ni kweli baba mtoto hajamuona mtoto tangu azaliwe.”

Soudy Brown hata hivyo hakuweza kumpata Vanessa Mdee azungumzie jambo hili.

 

Vanessa Mdee: Collabo za kimataifa zinafurisha akaunti yangu ya benki

Vanessa Mdee anavuna faida ya kufanya collabo na wasanii kutoka nchi zingine. Mwimbaji huyo amekiri kuwa collabo za kimataifa zinamletea pesa nyingi sana.

Akiongea na Bongo5, Mdee alisema kuwa collabo zake na wasanii kutoka Malawi na Nigeria zimemfungulia mlango kufanya shows katika nchi hizo.

Mdee anasema yeye hupata pesa nyingi kutoka kwa shows anazofanya nje ya nchi.

“Yeah collabo hizi definitely zinaamisha more money in the bank, sababu kama mimi Malawi nilikuwa sijawahi kwenda kufanya show sasa hivi nimeshakaribishwa kwenye matamasha mbalimbali so more money in the bank. Pamoja na Nigeria, kesho kutwa naenda kufanya show Gidi Fest, ni tamasha kubwa, nilishawahi kufanya lakini sasa hivi nina content nyingi zaidi ambazo zina wasanii wa Kinaijeria so nyimbo zinakuwa zinafahamika na mashabiki wengi zaidi huko so definitely more money in the bank because to me every fan is a blessing na wanaendeleza muziki wangu wanaufikisha pande ambazo hata mimi sijawahi kufika,” Vanessa Mdee alisema.

 

Video:Wimbo alioahidi Vanessa Mdee baada ya kuachiwa na Polisi umetoka

Wimbo alioahidi kuachia msanii Vanessa Mdee,baada ya kuachiwa na jeshi la polisi,kwa kuhusishwa na biashara ya mihadarati,umetoka. Kazi hii mpya iitwayo ‘Just Like That’ amemshirikishwa msanii kutoka Nigeria Orezi.

Vanessa Mdee alipitia mazito pale alipozuiliwa na polisi,akifanyiwa uchunguzi iwapo ni mmoja kati ya wahusika wa madawa ya kulevya,Tanzania.

Mistari inaenda hivi,’When I move you move, Just Like That, Just Like That… When I move you move Just Like That, Just Like That’ kama vile ya wimbo wa Ludacris, Stand Up aliomshirikisha msanii Shawnna.

Pata kusikiliza kazi hii ya Mdee na Orezi kisha utupe maoni yako? Hivi wasanii wanazembea katika utunzi wa mashairi yao au ni ubunifu unaozidi kudidimia katika fani hii za mziki kila siku?

Wakati huu wasanii wengi wachukua tu melodies na mistari ya nyimbo zilizovuma zamani,na kufanya yao.