Nimeshangazwa na Mauzo Ya Albamu Yangu Ya Money Mondays

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri kwa hivi sasa mrembo Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amefunguka na kuweka wazi kuwa mauzo ya albamu yake yanafanya vizuri sana.

Vanessa alitoa albamu yake ya ‘Money Mondays’ mapema mwezi uliopita na amekiri kuwa ameshangazwa na mauzo ya albamu hiyo na muitikio wa watu ambao ni mashabiki zake.

Vanessa alifunguka hayo kwenye Interview aliyofanya na Global Online Tv ambapo amekiri kuwa hayakuwa mategemeo yake hasa ukizingatia kutoa albamu sio kitu ambacho kimezoeleka:

Albamu yangu ina miezi miwili tangia itoke na kusema ukweli nimestaajabishwa na mapokezi watu wanadownload kwa kasi kubwa sana watu wamenunua nakala original Kupitia wakala wetu tunaendelea Kuitangaza lakini naona kuna kama muitikio fulani.

Nina furaha sana kwa sababu maisha yangu hayapo kama yalivyokuwepo mwaka jana kwani sahivi mimi ni msanii ambayr ninamiliki Albamu na ni sifa kubwa kwangu kwani sikutegemea muitikio huu na sapoti yao nashukuru sana Watanzania”.

Kwa muda mrefu wasanii wa Bongo fleva walikuwa hawatoi albamu kwa kuogopa kutopata maslahi lakini hivi sasa jambo la albamu limerudi mezani tena na wasanii Kama Vanessa, Chin Bees na Diamond wameshatoa albamu zao.

Alikiba, Darassa, Diamond na Vanessa Wang’aa Kwa Tuzo Nchini Uganda

Wanamuziki wakali wa Bongo fleva kama Diamond, Ali kiba, Vanessa Mdee na Darassa wameng’aa kimataifa zaidi baada ya kila mmoja kujishindia tuzo za Hippo nchini Uganda.

Tuzo hizo zilifanyika usiku wa jana nchini Uganda ambapo baadhi ya wasanii waliopata Tuzo kutoka Tanzania ni kama vile Diamond, Ali Kiba, Vanessa Mdee na Darassa.

Vanessa Mdee ameibuka na tuzo ya heshima katika kipengele cha ‘East Africa Best Female Artist’ na Alikiba akiibuka na tuzo ya kipengele cha ‘Song of the Year Tanzania’ kupitia wimbo wake wa Seduce Me.

 

Diamond Platnumz ameshinda tuzo mbili mbili kwenye vipengele vya ‘Africa Song of The Year’ kupitia wimbo wake wa ‘Marry U’ aliomshirikisha Ne-Yo na ‘Best East Africa Video’ kupitia wimbo wa Eneka.

Darassa ameibuka kidedea kwenye kipengele cha ‘East African Super Hit’ na wimbo wake wa Muziki ambao amemshirikisha Ben Pol.

 

Vanessa Mdee: Sina Mpango wa Kuolewa Kwa Sasa Wala Kuwa na Mtoto

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na albamu yake ya ‘Money Mondays’ Vanessa Mdee amefunguka na kuzima tetesi zote zilizo kuwa zinasambaa kuwa yeye ni mjamzito.

Kwa wiki chache sasa kumekuwa na tetesi kuwa Vanessa Mdee na mpenzi wake Jux wanategemea kupata mtoto wao wa kwanza hii ni baada ya picha ya Vanessa kusambaa mtandaoni ikimuonyesha akiwa na kitumbo ndii.

Vanessa amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo ambapo amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuolewa kwa sasa wala kupata mtoto kwani kuna mambo mengi anayohitaji kufanya kabla hajafika hatua hizo.

Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo ‘On air with Millard Ayo’ Vanessa aliulizwa endapo ana mpango wa kuolewa na kuzaa hivi karibuni na alifunguka kama ifuatavyo;

Kwanza unajua watu wananiuliza old are you? I am going to be 30 this year yah naingiza miaka thealathini kwaiyo nimesonga kiumri lakini naona bado kidogo lakini hiyo ni mipango ya Mwenyezi Mungu kwaiyo sijui nini kitatokea lakini kwa sasa kuna vitu vingi natamani kutimiza kabla ya kuzaa au kuolewa, natamani kuona wadogo zangu Brian na Mimi Mars wakifanya vizuri sana, natamani kushinda tuzo ya Grammy, natamani kuwa msanii mkubwa sana duniani yaani kuna kazi ambazo nazikamilisha za Universal na kwa sababu ya mipango yetu ya Universal siwezi kuwa na mtoto kwa sasa naona sio wakati sahihi kwa mimi kufanya hivyo”.

 

Vanessa Mdee Amwaga Povu Kwa Mashabiki Waliosema Hajapendeza na Staili Yake ya Nywele

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na albamu yake ya Money Monday’s Vanessa Mdee amejikuta akiingia kwenye trend ya mastaa iliyoingia hivi sasa ya kubleach nywele.

Vanessa ameungana na mastaa wenzake kama Ali Kiba na Ommy Dimpoz walioonyesha staili yao mpya ya nywele wiki hii mwanzoni ambapo pia walionekana rangi walizopaka kwenye nywele ambapo Ali Kiba alikuwa amepaka rangi nyekundu na Ommy Dimpoz alikuwa amepaka rangi ya njano.

 

 

Vanessa alionyesha staili yake mpya siku ya jana kupitia mtandao wa Instagram ambapo alikuwa amepaka rangi ya machungwa (orange) ambapo alisindikiza picha hiyo na ujumbe uliosema:

New hair who is this? Benpol najua utakuwa umefarijika sana”.

 

Lakini baada ya picha hizo kusambaa mtandaoni Vanessa aliwatolea povu zito mashabiki zake waliokuwa wanamsema kuwa hajapendeza na rangi ile ambapo kupitia mtandao wa Instagram alimwaga povu hili:

Tatizo la wengi mmekariri kila kitu hadi nywele mnataka kunipangia nikiwa na nywele za kuvaa mnasema nikivua mnasema sasa nasemaje Ben amefarijika”.

Vanessa Mdee: Mimi ni Shabiki wa Ali Kiba, Niliyoongea Yaligeuzwa

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri sana hivi sasa Vanessa Mdee amefunguka na kusema amesikitishwa na watu kugeuza maneno aliyoyasema na kufanya yawe negative wakati yeye hana tatizo na staa wa Bongo fleva Ali Kiba.

Wiki hii Vanessa Mdee alikamata headlines kwa maneno aliyosema kuhusu mastaa Diamond Platnumz na Ali Kiba ambapo alidai kuwa baada ya kutembelea nchini Nigeria na kuenda kwenye kumbi mbali mbali za starehe amegundua kuwa hawapigi sana nyimbo za nje ya nchi yao na alisikia nyimbo mbili tu kibongo ambazo ni za kwake na Diamond ambazo wote wameshirikishwa kwenye nyimbo hizo na Wanaigeria wenyewe.

Lakini alipoulizwa kama amesikia nyimbo za Ali Kiba zikipigwa Vanessa alisema hapana hakusikia nyimbo ya Ali Kiba basi baada ya kusema hayo mashabiki wa Ali Kiba walimjia juu Vanessa na kusema kama Ali Kiba sio maarufu Nigeria kama anavyodai mbona ameshinda tuzo nchini Nigeria?.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na mashabiki wa Ali Kiba wanazidi kumtolea povu aliandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Nilivyokuwa nazungumza hiyo ishu nilikuwa nazungumza kitu kikubwa zaidi lakini wenye akili zao wamegeuza imekuwa hivyo na ukiangalia lengo la jibu langu lilikuwa kuwahamashisha Watanzania wapromote na kuuthamini zaidi muziki wa nyumbani wenzetu Wanigeria ndivyo wanavyofanya sasa hapo wapi nimeudiss mziki wa Ali Kiba? Alafu Kiba anajua mimi shabiki yake sasa tutafika kweli kila neno linageuzwa kuwa baya na negative wakati nilikuwa nashedd light kwa hii ishu jamani?”.

Vanessa aliyaongea hayo alipokuwa nchini Nigeria ambapo yupo kwenye media tour kwa ajili ya kutangaza Albamu yake mpya inayoitwa Money Mondays.

“Afande Sele Ana Stress Zake Anatafuta Pa Kutokea”- Vanessa Mdee

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee anayefanya vizuri kwenye gemu amefunguka na kudai kuwa msanii mkongwe wa Bongo fleva Afande Sele ana stress zake binafsi ndio maana anatokwa na povu.

Wiki chsche zilizopita Afande Sele akiwa kwenye interview na kituo cha redio alimtaja msanii Vanessa mdee kama msanii anaefanikiwa sio kwa sababu ya kipaji chake au kujua kuimba bali kudai anabebwa na kiki lakini pia anabebwa na penzi lake na msanii Jux. Hii haikuwa mara ta kwanza kwa Afande Sele kumponda Vanessa ameshawahi kumtaja kwenye listi yake ya wasanii wasojua kuimba.

Vanessa alimtolea uvivu Afande Sele kwenye interview aliyofanya na Planet Bongo ya East Africa Radio ambapo alisema kuwa kitendo cha Afande Sele kumponda na kusema kuwa anabebwa alichukulia poa kwa sababu anaelewa Afande Sele alitafuta pa kutokea na stress zake.

Mimi binafsi nilimuelewa niliangalia anazungumzia kwa upande gani nikagundua in few seconds kama nimetumika kama punching bag, sikuchukulia personal, nikaona fresh kabisa, nikajua anhaa alikuwa na yeye anataka kusikika anatafuta pa kutokea kihivyo ila mimi ni shabiki yake Mkubwa akawa ameniua kihivyo yaani amenitathimini kaniona hivyo ila kiukweli yule ni legend pia”.

Lakini pia Vanessa amesema kuwa anaelewa kuwa Afande Sele ni mkongwe kwenye game ila huenda alikuwa na stress zake binafsi, hivyo alikuwa anatafuta pa kumalizia hasira zake ndipo alipoangukia kwa Vanessa.

Vanessa Mdee Amejiunga na Universal Music na Kupata Dili La Mkwanja Mrefu Haijawahi Kutokea

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee amezidi kupata mafanikio yasiyo na kipimo baada ya kupata deal jipya la mkwanja mrefu na kampuni ya Universal na Air force 1.

Mwaka 2017 umezidi kuwa mzuri kwa supastaa huyo kwani huu sio mkataba wa kwanza Vanessa amesaini na kupata mkwanja mapema mwaka huu alipata nafasi ya kuwa balozi wa Hyatt Regency.

Siku ya Jana mchana Vanessa kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza habari njema kuwa zitakuja punde na hivyo baadae aliweka wazi mafanikio hayo aliyoyapata baada ya kupata nafasi ya kipekee kabisa ya kufanya kazi na kampuni hizo kubwa duniani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vanessa Mdee alifunguka haya kuhusu deal hilo jipya:

Kama ilivyo ada tunaanza kwa kumshukuru Mungu kwa baraka zake na kibali chake cha kutufikisha siku njema ya leo . Nimeona nitumie fursa hii wapendwa mashabiki zangu mwanzoni mwa mwaka huu nilipitia changamoto nyingi sana, lakini kwa neema za Mungu nilitoka mahali pale na sio kuona baraka tu bali na maajabu mengi yaliyotokea kwenye maisha yangu. Ikiwemo kuwa mmoja wa familia ya Universal music group in a unique signing joint between #Universalmusicgermany #airforce1 #Universalmusicgroup”.

Vanessa hakuishia hapo aliendelea kufunguka kuhusiana na deal hilo litakalotengeneza historia.

 

Na hii ni mara ya kwanza kwa msanii wa Afrika kupata dili la aina hii yenye mkwanja mrefu sanaaaa. Hii ni habari njema kwa mashabiki zangu na ndio kwanza tumeanza mambo  makubwa zaidi yanakuja. Kumbuka kila mwisho wa Jumapili ndio mwanzo wa Jumatatu usiogope kuanza upya”.

Mwaka huu unaisha vizuri kwa Vanessa kwani amepata dili lenye pesa ndefu lakini kwenye maisha yake binafsi pia yamendaa vizuri kwani amerudiana na mpenzi wake Jux hivyo tunamtakia kila la Kheri na la Shari limuepuke.

 

 

Nyota Za Warembo Hawa Zazidi Kung’aa Zaidi (picha)

Katika kuonyesha kuwa kweli wanajitihada ya kazi wanazofanya warembo Elizabeth Michael ‘Lulu’,Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na Jokate Mwegelo wamekuwa mfano wa kuigwa na jamii kwa ujumla kutokana na jitihada zao na uwezo wao wa kufanya kazi na zikaonekana na jamii.

Haya ni baadhi ya mafanikio waliyofikia warembo hawa ambao wanahitaji pongezi:

  1. Vanessa Mdee
Vanessa kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram leo hii ametangaza kuwa ataungana na hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam ambapo atakuwa Balozi wa Hoteli hiyo, hayo ni mafanikio mazuri sana kwa Vanessa na anastahili pongezi. 

2. Jokate Mwegelo

Jokate Mwegelo amechaguliwa kuwania Tuzo za Vjana 100 wenye ushawishi mkubwa Africa(100 Most Influential Young Africans) kama Mfanyabiashara kupitia kampuni yake ya Kidoti. Hivi sasa Jokate yupo nchini Marekani kwaajili ya kushiriki Mkutano unaojulikana kama Forbes Under  30 Summit kwaajili ya kukutana na Vijana Wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali.

3. Elizabeth Michael

Elizabeth Michael kupitia Azam TV amechaguliwa kuwa Balozi wa Tamasha la tuzo za filamu kwa upande wa Africa Mashariki ikimaanisha kuwakilisha Tasnia ya Filamu za Bongo Movie katika Tuzo hizo.

Wanawake wote hawa warembo wamethubutu na wameweza na ni vyema kuwapongeza mara kwa mara katika Jamii Zetu.

Siwezi Kujichubua Naipenda Rangi Yangu-Vanessa Mdee

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri kitaifa na kimataifa Vanessa Mdee amedai kuwa hatokaa ajichubue rangi yake ya mwili na haamini kwenye kujibua.

Kumekuwa na kasumba kubwa ya wasanii kujibalisha rangi ya mwili kwa kudhani kuwa ndio wanakuwa warembo zaidi, huku wasanii wengi wa mziki na filamu wamenyooshewa vidole na kudhaniwa kuwa wanajichubua.

Katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni Vanessa alifunguka kuhusiana na msimamo wake juu ya swala zima la kujichubua ambapo alisema;

“Mimi kama Vanessa siamini kwenye kujikoboa, kujichubua au kujibadilisha rangi yako ya kawaida au mwili wako wa kawaida my belief is in temporary stuff, so ukaweka make up au nywele ukuongezea hiyo ni kitu temporary ambayo usiku ukiamua unatoa lakini vile vitu vya kufanya moja kwa moja siviamini”.

Pia Vanessa aliongezea kuwa;

“Na pia ile issue ya confidence, mtu ukiwa secured unaweza kufanya hivyo vitu ukiwa unataka kujiboresha au kujiridhisha mwenyewe ukadhani ukijibadilisha utakuwa bora zaidi but I don’t think I need to do that“.

Vanessa ameongeza kuwa hawezi kufanya hivyo kwasababu ni kinyume na maadili yake ya kidini na dini imekataza kufanya hayo anachofanya yeye ni kumshukuru Mungu kwa kumfikisha hapo alipo leo.

Diamond ,Vannessa,Alikiba kuwakilisha Tanzania tuzo za MEAMA

Wasanii Diamond, Vannessa pamoja na Alikiba wamechaguliwa kuwania  katika tuzo za Middle East Africa Music Award (MEAMA) ,tuzo hizo ambazo zinapangwa kufanyika tarhe 5 Oktoba mwaka hu zina lengo la kuibua vipaji na kuonyesha amasa kwa wasanii wa africa kwa ujumla.Akiongea katika uzinduzi wa tuzo hizo kwa awamu ya pili CEO  wa FAJ GLOBAL ENT.L.T.D ,MAJESTICAL ROYAL CLUB (MRC)  na pia ni mwenyekiti wa FAJ ONLINE-RADIO Mr. Fajuyi Adeniyi Oluwaseun amesema kwamba wanaahidi kuwa kwa mwaka huu tuzo izo zitakuwa zenye ubunifu zaidi na zina kuwa na lengo la kuibua vipaji vingi zaidi ili kuendelea kuipa sifa na kuitangaza Africa.

Tuzo hizo ambazo zimejumuisha  washiriki wengi  ambao wametoka nchi mbalimbali za Africa kama Kenya,Uganda, Nigeria, South Sudan,Tanzania, Egypt na zinginezo jana tarehe 13 Septemba imeelekezwa kuwa majina ya washiriki kutoka nchi zote yanapatikana katika website ya tuzo hizo hivyo mashabiki  waweze kuwapigia kura wasanii wao wanaowapenda ili waweze kujinyakulia tuzo izo.

Kwa upande wa Tanzania msanii wa kike Vannesa Mdee ndiye   msanii pekee wa kike kutoka nchini hapa aliyewekwa katika kategoria ya msanii bora wa kike wa mwaka huku akichuana na  Victoria Kimani,Yemi Arade na Seyi Shayi, kwa upande wa wanaume yupo alikiba  katika kategoria ya msanii bora wa kium wa mwaka,pamoja na Diamond Platinumz katika kategoria ya wimbo bora ya mwaka na wimbo wa Eneka .

Wasanii wengine wanaoshiriki kuwania tuzo izo kutaka nchi tofauti na Tanzania  ni pamoja na Davido,Wizkid,Mr.Eazi katika kategoria tofauti tofauti.

Mashabiki wanahamasishwa kupigia kura msanii anaependa kushinda katika tuzo izo,na jinsi ya kupiga kula ni kuingia moja kwa moja katika website ya tuzo izo (MEAMA) ambapo upigaji wa kula umeanza mara baada ya kutangazwa kwa washiriki huku mwisho wa kupiga kula ikiwa ni tarehe 30 septemba mwaka huu na tuzo kufanyika oktoba 5 nchi Egypt.Tunawatakia mema wasanii wote waliopo katika kategoria mbalimbali , muziki wa Africa unafika mbali kwa sasa.

Vanessa ana thamani kubwa kwangu- Jux

Msanii wa RnB nchini Juma Jux anayetamba na wimbo wake mpya wa “Utaniua” amefunguka juu ya uhusiano wake na mwanamuziki wa hapa nchini Vanessa Mdee, Kuwa kwake kwanza ni familia yake kisha Vanessa.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Vanessa alisema, “Nampenda Vanessa kuliko msichana yoyote niliyewahi kuwa naye kwenye mahusiano na sitegemei kumuachia aende hivi hivi hata familia yangu inajua mapenzi yangu kwa Vanessa.

“Nikiwaga mbali na Vanessa kitu cha kwanza nikiamka asubuhi naingia Instagram namuangalia halafu nampigia simu, Siwezi kumpigia Simu bila kuangalia picha zake kiufupi ninampenda sana Vanessa”.

Kuhusu kuwa na Mtoto Jux alifunguka kuwa ” Sasa hivi natamani kupata mtoto na nina mpango huo, kwa sasa najipanga vizuri Mungu akinijalia basi hivi karibuni ntapata mtoto na nitapenda kumuita Karim na si jina jingine zaidi ya hilo.

Jux na mpenzi wake huyo Vanessa waliachana miezi michache iliyopita lakini Jux ameweka wazi kuwa bado a na mp end a.

Kuhusu kutoka na msanii wcb,vannessa aongea

Ule uvumi wa muda mrefu ambao umekuwa ukiendelea sehemu mbalimbali katika mitandao unaomhusu msanii wa kike anaetamba na kibao chake ‘KISELA’ vannesa mdee kuwa kwa sasa anatoka na msanii mwenzie kutoka katika lebel ya wasafi (WCB) utakuwa sasa umeeleweka baada ya msanii huyo kutoa yaliyopo moyoni kuhusu maneno hayo.

Akiongea katika interview na ayo Tv ,Vee money anasema kuwa ‘Ninazushiwa ninatoka na watu kila sehemu mwanangu..ndio maana inaitwa ni uzushi” hivyo basi kwa maneno hayo ambayo ameongea yeye mwenyewe vannesa ni dhahiri kuwa maneno yanayosambaa mitandaoni kuhusu yeye ni uzushi mtupu hakuna ukweli ndani yake.

Hata hivyo itakuwa ni mapema sana kwa msanii huyo kuwa wazi juu ya mahusiano yake mapya kwani ni muda mchahche tu uliopita vee ametoka kuachana na mpenzi wake juma jux,hata hivyo baada ya kuulizwa na mwandishi kuhusu swala la yeye na juma jux vannesa alijibu hivi’sisi saivi tunaelewana sana na tumekuwa na maongezi kuhusu swala hilo” hivyo basi inawezekana wawili hao wapo katika harakati za kurudisha mahusiano yao kama mwanza ilihali vannesa anasema wapo katika maongezi.

Kumekuwa na comments nyingi sana kutoka kwa mashabiki kuhusu wawili hao wakiwashauriwa na kuwaomba wawili hao kurudisha mapenzi yao kama awali maana ni moja kati ya couple iliyokuwa inatrend sana na kuonekana kupendeza wanapokuwa pamoja,ivyo labda basi wasanii hao wanafata nguvu ya mashabiki na kukaa pamoja ili kumaliza tofauti zao.

Alipoulizwa kuhusu kuolewa na kuzaa ,vee money alisema kuwa yeye kuzaa bado sana na  kwa sasa  yupo single

Mahusiano ya vannesa na jux yalikuwa ni moja kati ya couple iliyovutia mashabiki wengi,hata hivyo wawili hao walikuwa wakionekana vizuri pamoja na kufikia hatua ya kutoa mpaka nyimbo pamoja,na hata baada ya mahusiano yao kuvunjika jux aliamua kumuimba wimbo mpenzi wake huyo kuonyesha ni jinsi gani bado anamuhitaji,nasi kama mashabiki tunawatakia maongezi mema na tunaimani watarudisha kile walichokuwa nacho hapo awali.

Jux: “Bado nampenda Vanessa”

Mwanamuziki Juma Jux amekiri kuwa bado anampenda mpenzi wake wake wa zamani Vanessa maarufu kama V-money , Jux na Vanessa waliachana miezi mitano iliyopita baada ya kudumu kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda wa miaka minne.  Jux aliweka wazi  kuwa wimbo wake mpya “Utaniua” aliouachia  hivi karibuni  alimuimbia Vanessa, Lakini katika mahojiano tofauti aliyofanya Vanessa alisema wimbo wake mpya wa “Kisela” ulihusu maisha yake binafsi na hisia alizopitia katika mahusiano yake na Jux.

Katika mahojiano aliyoyafanya Jux hivi karibuni alikiri kuwa bado anampenda vanessa na ataendelea kumpenda na itakuwa ngumu kwake kumsahau na itamchukua muda mrefu sana. Moja kati ya vitu mashabiki wengi wa wasaanii hawa wamekuwa wakijiuliza na wakitaka kujua ni sababu gani iliyopelekea wawili hao kufikia uamuzi huo wa kuachana, Jux aliweka wazi kuwa muda na umbali uliokuwepo baina yao  ulikuwa kikwazo kikubwa katika mahusiano yao na alisisitiza kuwa kati ya yeye na Vanessa hakuna hata mmoja wao aliyechepuka (kuwa na wapenzi wengine).

Jux amesisitiza kuwa yeye na Vanessa hawana uadui wowote na wataendelea kuwa marafiki wa karibu japokuwa saa nyingine bado ni ngumu kwake kumuona Vanessa kwenye mitandao ya kijamii mpaka kufikia hatua ya kuamua “kum-block “. Lakini amekiri kuwa “Vanessa amenifundisha vitu vingi sana na amenipa changamoto sana kwani yeye ni msanii mzuri kwaiyo nilikuwa siwezi nikaona yeye anatoa nyimbo na video nzuri alafu mimi nikabweteka bali alinipa changamoto ya kuwa mtafutaji”

Jux amemalizia kwa kusema hayupo kwenye mahusiano yoyote kwa sasa ameamua atumie muda wake kufanya muziki na pia amekiri akisikia Vanessa ana mpenzi mwingine itamuumiza sana.

Picha 4 za Vanessa Mdee and Romy Jones wakionyesha chembechembe ya mapenzi

DJ wa Diamond Platumnz – Romy Jones alisherekea siku ya kuzaliwa kwake siku ya Agosti 18. Wasanii kadhaa walijuinga naye kusherekea birthday yake.

Siku chache baada ya sherehe hio, Romy Jone na Vanessa Mdee walipigwa picha kadhaa kwa photo shoot mpya. Wawili hao walionekana kwenye pozi ya kimapenzi kwenye baadhi ya picha walizopigwa. Tazama picha hizo hapo chini:

Vanessa Mdee: Mapenzi yangu na Jux hayakuwa ya kisela

Wiki mbili zimepita sasa tangu Vanessa Mdee kuachia wimbo wake mpya wa kimapenzi ‘Kisela’ aliyomshirikisha Peter Okoye wa P Square.

Mdee, ambaye aliwachana na mpenzi wake Juma Jux, alifunguka kuhusu uhusiano wake na mwanamuziki huyo.

Mrembo huyo alieleza kuwa mapenzi yake na Jux hayakuwa ya kisela kwani walikua wako na mapenzi ya dhati ingawa iliisha katikati.

“Mapenzi yangu na Juma hayakuwa ya Kisela, lakini pia sitaki na ninakemea kwa nguvu mapenzi ya kisela. Kuhusu kuimba wimbo huu nikwamba nimewasaidia wanawake wenzangu ambao huwa wanaingia kwenye mahusiano bila kujua ni mahusiano ya aina gani waliyonayo. Lakini kwenye uhalisia mimi siishi maisha hayo,” Vanessa aliambia EATV.

Tazama wimbo wa Vanessa Mdee ‘Kisela’ hapo chini:

Mpenzi wa Vanessa Mdee amwadikia ujumbe huu kumsheherekea siku ya kuzaliwa

Msanii wa Bongo Juma Jux amewaacha wengi wakiulizana maswali baada ya kumuandikia mpenzi wake Vanessa Mdee ujumbe wa kufurahisha roho kumsheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Ujumbe huu umekuja wakati ambao mashabiki wengi walidhani kuwa wawili hao waliluwa wameachana. Kwa kufanya hivyo Juma Jux amedhibitisha kuwa mapenzi yake kwa Vanessa bado yako na kutupilia mbali fununu hizo.

Jux aliandika kusema,

Happy birthday ?#eastafricanqueen @vanessamdee more life n God bless you mama #bestfemaleartist #moneymondays,”