Ombi la Wakazi Kwa Wasanii Wenye Pesa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva  Wakazi amefunguka na kuwataka wasanii wakubwa ambao wana majina makubwa na wenye pesa wawasaidie wasanii wengien wadogo,

Wakazi amewataka wasanii kuwa na ushirikiano na kunyanyuana ambapo amesema kuwa wasanii wenye majina makubwa na pesa wawekeze kwa wasanii wachanga na wasiojiweza.

Kipitia ukurasa wake wa Instagram, Wakazi ameandika:

WAKUTUKOMBOA NI SISI WENYEWE… #Artists
Huu ni wito wangu kwa wasanii wenzangu. Wasanii Wenye majina makubwa washikeni mkono wasanii wachanga. Na Wasanii wenye hela fanyeni investment kwa Wasanii wachanga.
Ujue kuna Wasanii wana majina makubwa na wana hela, ila public interest imepungua. Wamefika kikomo cha umaarufu wa ndani. The only way they can get bigger ni kwa ku explore masoko ya nje. Sasa ukifikia hiyo level, ni bora ubadilishe jinsi unavyo attack market (focus on international one), na pia vi vyema kutoa a “helping hand” kwa upcoming Artists. Sasa hivi kujenga jina/brand hadi uwe household name ni changamoto sana regardless how talented you are. Na hakuna kitu kinauma kama kuwa Talented alafu level ya mafanikio hususan kiuchumi ni almost nothing. 

Wewe kumsaidia “underground” kunaweza kukurudisha hata wewe kwenye ramani, alafu mambo yakaenda. Let’s embrace the young artists and respect their ideas cause in reality it’s them and their peers, who are the current consumers of the music.
Ila maandaglaundi na nyie Acheni kulia lia. Onyesheni THAMANI zenu kwa washika dau, Big Artists and more importantly kwa Mashabiki, badala ya kukariri tu “naomba unisaidie”. Huhitaji kuwa signed au kupata sponsor ndio uanze ku-act ki professional au kujinadi kwenye Social Media, au ku exhibit Nidhamu ya kazi, etc. (Nitalichanganua hili swala vizuri siku za karibuni). Ila kiufupi, wakati unasubiri bahati ya kushikwa Mkono na Msanii mkubwa au yeyote yule (Media, Presenter, DJ, Mashabiki), Anza kujijenga na kujijengea mazingira ya kuonekana you are worthy and worth it!!! Only We, can save ourselves !!! 
#Workethic ”.

 

Wakazi Amhoji Steve Nyerere Kama ni Msanii Au Mwanasiasa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Wakazi Music amemjia juu msanii wa Bongo fleva na mwanaharakati wa mambo ya siasa Steve Nyerere kutokana na kauli alizotoa.

Sakata hilo limetokea siku chache zilizopita baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kuanika wasanii katika mkutano Wake na wasanii wachache kujitokeza.

Wasanii wengi waliweka wazi kuwa hawakuenda kwenye mkutano huo kutoka na kwamba hawakupata mwaliko rasmi zaidi ya kuona matangazo kwenye Mitandao ya kijamii.

Stevw Nyerere ambaye alikuwa mratibu wa Shughuli hiyo amewajia juu wasanii ambao Hawakufika kwenye mkutano huo Mpaka kufikia hatua ya Kuwaita Madodoki.

Wakazi amemjia juu Steve Nyerere kwa kauli yake hiyo na kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BtYAjLZFFpb/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=17yqbv5ow4sx6

Rapa Wakazi Kupita Njia za Nandy

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana (Rap) Wakazi ameweka wazi nia yake ya kufanya remix ya ngoma ya Msanii wa Bongo fleva Nandy.

Wakazi ameweka wazi kuwa yupo mbioni kutoa remix ya wimbo wa Nandy unaokwenda kwa jina la Aibu ambao unafanya vizuri kwa sasa kwenye chati mbalimbali za redio.

Siku za nyuma Utakumbuka Wakazi alifanya hivyo pia kwenye wimbo, Sijutii wa muimbaji Ruby ambaye anatajwa kuwa hasimu mkubwa na Nandy kimuziki kwa sasa. Pia Wakazi aliwahi kufanya refix ya wimbo wa msanii kutokea nchini Nigeria, Wizkid unaokwenda kwa jina laOjuelegba na kuipa jina la Natokea Dar .

Wakazi Awaonya Wasanii Wapenda Kiki

Msanii wa Muziki wa hip hop nchini Webiro Wassira maarufu kama Wakazi amewafungukia wasanii wote wa Bongo fleva ambao wanajulikana kwa kupenda kiki.

Wakazi amefunguka na kusema ingawa kiki inaweza  ikawa nzuri kwa biashara Lakini pia inaweza ikawa inapotosha kama kazi yenyewe inayotolewa na msanii ni mbovu.

Katika mahojiano yake na Global Publishers, Wakazi amesema hawezi kufanya kiki ili ‘kuboost’ wimbo wake ufanye vizuri, lakini atatoa kazi nzuri ambayo ni kiki tosha maana yote yanawezekana hivyo hata wasanii wengine wajitahidi kufanya kazi nzuri ili zijiuze zenyewe.

Wasanii wanaofanya kiki wanatakiwa kuwa makini sana kwa sababu pamoja na kwamba wanaona ni njia mojawapo ya kuuza kazi zao, inaweza ikawaharibia kama kazi wanazotoa ni mbovu mwisho wa siku kiki inageuka maisha badala ya muziki, wafanye kiki wakiwa na uhakika kazi zao ni nzuri”.

Wasanii wengi Bongo wamekuwa wakitengeneza ‘Kiki’ ama skendo fulani ili waweze kupata airtime kubwa ili pale wanapotoa kazi zao za kisanaa zipate coverage kubwa zaidi.

Wakazi Akiri Hakuna Msanii Kama Davido

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Wakazi Music amefunguka na kumnyanyulia mikono msanii kutoka Nigeia David Adeleke maarufu kama Davido baadae ya ushindi wake wa tuzo ya BET.

Davido aliibuka mshindi wa tuzo ya BET 2018 katika kipengele cha ‘Best International Act’, tuzo zilizofanyika katika ukumbi wa Microsoft Theater huko mjini Los Angeles, jimboni California, Marekani.

Baada ya ushindi huo Davido alitoa hotuba ambayo ilikuwa imejikita katika kutangaza soko la Muziki wa Africa na kuwataka wasanii wa Marekani kufika Africa Kutembea:

Hotuba hiyo Ikiwa huwa watu wengi na mmoja wao ni Msanii Wakazi ambaye alishindwa kujizuia na kumwagia sifa lukuki Davido kwa hotuba hiyo ambapo kipitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Hongera nyingi zimwendee Davido kwa ushindi wa “Best International Act” kwenye @betawards huko Marekani. Mwaka huu hakukuwa na mtanzania Ila pia Category ya International iliunganiswa Africa na Europe, so angechukua mwafrika yeyote tungehesabu Ushindi. Ila kikubwa ni kwamba mwaka huu ndio mara ya kwanza Tuzo za International kupokelewa on the Main Stage. Na niseme ukweli Davido hajatuangusha kwenye Speech yake. Ilikuwa Fupi and I understand maana sio mchezo (kutembea tu kwenda pale mbele unamuona kila Star, hatari) lazima utetemeke. Ila Davido alimshukuru D’banj kama Msanii aliyeanza kutufungulia milango african artists upande wa marekani (Collabo na Snoop Dogg, Signed by Kanye West) na pia alichukua Fursa kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya D’Banj Maana amefiwa na mwanae (R.I.P Daniel III). Kisha akashukuru Fans, Familia yake, Management yake. Mwisho akawasihi wanyamwezi kuja africa wajionee hali, chakula na kufanya Collabo na Wasanii wetu, pia akasema Album yake inakuja soon. Kiukweli I don’t see any other artist kufanya a better job of representing zaidi ya alivyofanya OBO.
Ila sasa hii iwe changamoto na chachu ya sisi huku kupigania muziki wetu na sisi maybe tuje kushinda na kupata fursa ya kuinadi Tanzania kikamilifu. I know I’m inspired and I’m going to the studio leo. Ikiwezekana tuongeze support ya wenyewe kwa wenyewe kama itasaidia. Tuache UMBEA na kuongelea yasiyotuhusu, Tuache Uvivu… tupige Kazi, uwe underground uwe Legend!! Wote tuna nafasi… peace #AfricaPride