Kwenye Msiba wa Zilla Mimi Niko Kwenye Kamati :-Wakazi

Msanii Wakazi amefunguka na kusema kuwa yeye kama msanii amekuwa moja kati ya watu wanaoongea sana wanapokuwa katika mikusanyiko ya watu na hii imemfanya kila siku kuwa mstari wa mbele kujichagua kama kiongozi wa sababu ya uongeaji wake hivyo anashawishi watu kwa haraka.

Wakazi ambae hapo awalia liwahi kuingia katika mgogoro wa kimuziki na Godzilla anasema kuwa hata katika msiba huo yeye ni kiongozi wa kamati ua kuandaa mazishi ya msanii huyo ambae kabla ya ufariki kwake waliweza kukaa na kumaliza tofauti zao.

Wakazi anasema kuwa yeye haoni kazi kuwatumikia wengine na hata kama hawatamchagua, kwake kuwa kiongozi katika maswala hayo haoni kazi.

huwa sichaguliiwi na mtu bali najichagua mwenyewe kwa sababu mimi ni muongeaji mbele ya wenzangu.mara nyingi matatizo yanapotokea mimi huwa ni muongeaji kwa wenzangu, nanhii unifanya kuwa mbele kuongoza wenzangu, hata kwenye msiba wa ndugu yangu Godzilla niko kwenye kamati

Alichondika Wakazi Kuhusu Kufungiwa kwa Diamond.

Baada ya kufungiwa na Basata hata kukaidi  amri hiyo na kuamua kufanya vile wanavyotaka wao BASATA  waliwaongezea adhabu msanii Diamond Platinumz pamoja na ravyanny kwa kutokufanya kazi za sanaa kabisa kwa muda usiojulikana .

Wasanii  walizua gumzo sana katika mitandao ya kijamii  hasa kwa sababu wao ni moja ya wasanii wanaochngamsha sana indusrty ya sanaa kwa sasa kutokana na nyimbo zao, lakini pia wamefungiwa muda mabao mashabiki wengi walitegemea kupata burudani kutoka kwao.

Baadhi ya wasanii waliongea kila mtu alisema hisia zake, Moja ya walioongea hivi karibuni ni msanii WAKAZI ambapo yeye anasema kuwa swala la diamond kufungiwa na BASATA itakuwa ni kwa sababu  amekuwa akihitenga sana na wasanii wenzake na hata vikundi mbalimbali vya sana nchini.

WAKAZI anasema kuwa kuna mambo ambayo wasanii waaweza kuyafanya kwa pamoja kuepuka hayo yote lakii kwa sababu yeye tayari anaingiza pesa za kumtosha anaona hata hakuna haja ya kumjuika na wenzake.

anasema “Maybe ungekuwa unakuja kushiriki nasi tungekuwa tumei vunja BASATA na kuanzisha BASATA mpya inayoelewa kuwa the society is different, kuzingatia biashara, etc. Kuwa to mkaidi (Kwa Waziri Shonza, Basata) sio solution. Kwa nguvu uliyonayo ungeweza kusaidia sana ila inaonyesha we uliridhika as long as you were making money. Well “Karma is a B”. Kuna Chama chetu cha TUMA (Tanzania Urban Music Association) hebu kuwa karibu, changia mawazo, onekana kwenye vikao. Utafanya kazi zako huru kabisa kama tutaibadilisha system, ila haitobadilika bila kujihusisha na kuungana na wenzako.”

Wakazi Awaonya Wasanii Wapenda Kiki

Msanii wa Muziki wa hip hop nchini Webiro Wassira maarufu kama Wakazi amewafungukia wasanii wote wa Bongo fleva ambao wanajulikana kwa kupenda kiki.

Wakazi amefunguka na kusema ingawa kiki inaweza  ikawa nzuri kwa biashara Lakini pia inaweza ikawa inapotosha kama kazi yenyewe inayotolewa na msanii ni mbovu.

Katika mahojiano yake na Global Publishers, Wakazi amesema hawezi kufanya kiki ili ‘kuboost’ wimbo wake ufanye vizuri, lakini atatoa kazi nzuri ambayo ni kiki tosha maana yote yanawezekana hivyo hata wasanii wengine wajitahidi kufanya kazi nzuri ili zijiuze zenyewe.

Wasanii wanaofanya kiki wanatakiwa kuwa makini sana kwa sababu pamoja na kwamba wanaona ni njia mojawapo ya kuuza kazi zao, inaweza ikawaharibia kama kazi wanazotoa ni mbovu mwisho wa siku kiki inageuka maisha badala ya muziki, wafanye kiki wakiwa na uhakika kazi zao ni nzuri”.

Wasanii wengi Bongo wamekuwa wakitengeneza ‘Kiki’ ama skendo fulani ili waweze kupata airtime kubwa ili pale wanapotoa kazi zao za kisanaa zipate coverage kubwa zaidi.

Wakazi-Mashabiki Wamechoka na akili Za Wasanii Wanataka Kazi

Mwanamuziki wa muziki wa Bongo fleva Wakazi amewatolea povu wasanii wenzake na kuwataka waachane na mambo ya kutengeneza kiki badala yake wafanye kazi.

Wakazi ambaye anafanya sana miondoko ya kuchana (Kurap) ameweka wazi kuwa haoni kama kiki zinajenga mziki kama wasanii wengi wanavyojiaminisha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm Kupitia kipindi cha The Playlist, Wakazi amesema kuwa kwa sasa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wanafanya vioja kiasi kwamba hata mashabiki wanajua ni kiki kuna wimbo unatoka.

Tuweke kiki pembeni tufanye muziki, nadhani muziki ndiko unakoelekea hata raia wanaosikiliza muziki na kuufuatilia wameanza kuchoka sasa. Kwa sababu unakuta mtu kafanya vioja hadi unajua kuwa hii sasa single inakuja“.

Lakini pia Wakazi aliendelea kuongelea suala la wasanii kupenda kutengeneza kiki:

Halafu angalia sometimes mambo ya kiki yanavyokuwaga mabaya, inawezekana ikaleta shop value ile unayohitaji ili watu wasikilize bidhaa yako halafu baadae unakuta watu wanaizungumzia kiki yako kuliko hata wimbo wako, wakati wewe unataka wimbo uzungumziwe ili upate show“.

 

Wasanii Wakongwe Acheni Kulia Kwenye Media- Wakazi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya hip hop Wakazi amewatolea povu zito wasanii wakongwe wanaoenda kulia kwenye media waakiomba wasaidiwe na kazi zao.

Msanii huyo amemwagia povu lake Kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amewachana wasanii hao wakongwe na kusema kitendo hivho sio kizuri na hakiwezi kukuza muziki huo.

Hamna kitu kinaniboa kama Wasanii wakongwe ambao kila kukicha wanaenda kulia kwenye media ili wapewe support na career zao. Kama nyie mkilia, je Wasanii wachanga (who look up to you) na hawajawahi kutoka wafanyaje?

Kuna Wasanii wachanga wanalilia airplay, alafu na Veteran wa 15 years nae analilia airplay?! Wakati veteran ilitakiwa awe amemuweka the new artist under his/her wing na kumsaidia aweze ku flourish. And maybe y’all can shine together,”

Wakazi amewataka wasanii kuacha kulalamika na kuanza kufanya muziki kibiashara.

Siku za hivi karibuni tumeona wasanii wengi wakongwe wakiibuka na kujaribu kurudi kwenye gemu jambo ambalo limekuwa sio rahisi kwani mambo yamebadilika kwaiyo wamejikuta wakifeli na kusababisha wengi wao kuishia kukata tamaa.